JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MBUNGE FRANK MWAKAJOKA (CHADEMA) MBARONI

- Mbunge huyo wa Tunduma amekamatwa na Polisi leo ikielezwa atafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma za kumpiga Mtu mwaka 2018

- Inadaiwa amekamatwa kwa madai ya kumpiga Afisa Mtendaji, Deus Mwampashe

Zaidi, soma https://jamii.app/MwakajokaMbaroniTuhuma2018
AFCON2019: Timu ya Taifa ya Ivory Coast imetoshana nguvu na timu ya Taifa ya Algeria katika dakika 90 za mchezo wa robo fainali kwa kufungana goli 1-1

- Timu hizo zinaenda katika dakika 30 za nyongeza na zikitoka suluhu mshindi atatafutwa kwa mikwaju ya penati
DAR: WATU 7 WATUHUMIWA WA UJAMBAZI WAKAMATWA

- Walivunja maduka matatu na kuiba bidhaa mbalimbali, fedha na bajaji mbili huko Ukonga

- Polisi imesema Watuhumiwa hao walikuwa wakitumia gari aina ya Toyota Harrier nyeusi yenye namba T 666 DJG

Zaidi, soma https://jamii.app/Majambazi7Mbaroni-DarJul2019
AFCON2019: Algeria imefuzu kucheza nusu fainali baada ya kuiondosha Ivory Coast kwa penati 4-3

- Mchezo huo umeamuliwa kwa penati baada ya timu hizo kutoka sare ya goli 1-1 ndani ya dakika 120

- Algeria itakutana na Nigeria Julai 14, 2019 katika nusu fainali
TFF IMEMCHAGUA KOCHA WA AZAM KUKAIMU UKOCHA WA TAIFA STARS

- Ndayiragije Etienne anakaimu ukocha na ataiongoza Stars kufuzu CHAN

- Kocha wa Coastal Union, Juma Mgunda na Kocha Msaidizi wa Polisi Tanzania, Suleiman Matola wapo benchi la ufundi

Zaidi, soma https://jamii.app/NdiyaragijeKaimuStars
AFCON2019: Timu ya Taifa ya Tunisia 🇹🇳 imefanikiwa kufuzu kucheza hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo baada ya kuifunga timu ya Taifa ya Madagascar 🇲🇬 goli 3-0

- Tunisia itapambana na timu ya Taifa ya Senegal 🇸🇳 katika mchezo wa nusu fainali mnamo Julai 14, 2019
MAREKANI: R. KELLY AKAMATWA TENA KWA TUHUMA ZA UNYANYASAJI WA KINGONO

> Akamatwa na Idara ya Polisi ya New York kwa tuhuma za kuwasafirisha Wanawake kwa ajili ya kuwatumikisha kingono

> Ametiwa nguvuni wakati akiwa katika Jimbo la Chicago

Soma > https://jamii.app/RKellyArrested
KENYA: AUA WATOTO WAKE NA KUWATUPA CHOONI

- Polisi katika Kaunti ya Nandi inamtafuta Mwanamke, Floxy Cheptoo(32) anayedaiwa kumuua Mtoto wake wa Kike(7) na wa Kiume(11)

- Miili iligundulika baada ya Mwanakijiji kubaini alama za damu chooni

Zaidi, soma https://jamii.app/AuaWatotoChooni-KE
RAIS WA UGANDA KUFANYA ZIARA BINAFSI, NCHINI

- Rais Yoweri Museveni Kesho, Julai 13, 2019 atafanya ziara binafsi ya siku moja kwa kumtembelea Rais Magufuli

- Atamtembelea Rais Magufuli Kijijini kwake, Mlimani katika Wilaya ya Chato, Mkoani Geita

Zaidi, soma https://jamii.app/MuseveniZiaraBinafsi-TZ
UINGEREZA YADAI IRAN ILITAKA KUIZUIA MELI YAKE YA MAFUTA. IRAN YAKANUSHA

- Imedai tukio limetokea katika mlango bahari wa Hormuz, ila meli yake ya Kivita iliinda meli ya mafuta

- Iran imesema haikuwa na makabiliano na meli yoyote ya kigeni

Zaidi, soma https://jamii.app/Iran-UK-Hormuz
MENEJA MAABARA TUME YA MADINI AKAMATWA KWA WIZI WA DHAHABU

> Donald Njonjo anatuhumiwa kuiba kilo 6.244 za dhahabu yenye thamani ya zaidi ya Tsh. milioni 507

> Dhahabu hiyo ilikuwa imehifadhiwa katika Ofisi za Wakala wa Madini Masaki, Dar

Soma > https://jamii.app/DhahabuYaibwa
MAREKANI: AISHI NA MAITI YA MAMAYE NDANI KWA MIAKA MITATU

- Mwanamke mmoja(47) huko Texas, amekamatwa baada ya maiti ya mamaye iliyooza kugunduliwa nyumbani

- Polisi inaamini Mwanamke huyo(71) alifariki kutokana na kuanguka mnamo mwaka 2016

Zaidi, soma https://jamii.app/MaitiMamaChumbani-USA
PETER CROUCH ASTAAFU KUCHEZA SOKA

- Mchezaji huyo wa zamani wa timu ya Taifa ya England mwenye miaka 38 amechukua uamuzi huo akiwa amecheza soka la kulipwa kwa miaka 21

- Amevitumikia vilabu 11 vikiwemo Portsmouth, Tottenham, Aston Villa, Liverpool, Stoke na Burnley
KENYA: WANAWAKE 11 WAKAMATWA WAKIREKODI VIDEO ZA NGONO

- Wamekamatwa kwenye nyumba moja iliyopo Nyali, Mombasa na wanatarajiwa kufikishwa Mahakamani leo

- ‘Midoli ya kufanyia ngono’ imekutwa katika nyumba hiyo walimokuwa wakirekodi video

Zaidi, soma https://jamii.app/WaigizaNgonoMbaroni-KE
MWENYEKITI WA ZAMANI WA UWT KIZIMBANI WA KUGHUSHI CHETI CHA NDOA

- Aliyekuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT) Wilaya ya Ilala, Norah Waziri maarufu ‘Norah Mzeru’ amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni leo Julai 12

Zaidi, soma https://jamii.app/MwktUWTKizimbaniChetiNdoa
KIZIMBANI KWA KUSAMBAZA PICHA YA RAIS MAGUFULI KAVAA HIJAB

- Ni Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kampala(KIU), Amenitha Konga(19), Mariam Tweve(20) na Agnes Gabriel(21) wanaodaiwa kusambaza picha hiyo kwa kutumia WhatsApp mnamo Juni 9, 2016

Zaidi, soma https://jamii.app/KizimbaniMagufuliHijab
BoT YAIPIGA FAINI BENKI YA DTB YA TSH. BILIONI 1

- Imeipiga faini benki ya DTB kwa kushindwa kuwa na Kituo cha Data (Data Center) nchini

- Imeanisha kuwa imebaini DTB haina kituo hicho licha ya kuthibitisha kuanzisha ‘Secondary Data Center’

Zaidi, soma https://jamii.app/BoTYaipigaFainiDTB
SUDAN: JESHI LADAI KUZIMA JARIBIO LA MAPINDUZI

- Baraza la Kijeshi la nchi hiyo limesema limezima jaribio la mapinduzi ambapo kwa mujibu wa Jenerali Jamal Omar, Maafisa 12 na Askari wanne wamekamatwa wakihusishwa na jaribio hilo

Zaidi, soma https://jamii.app/MapinduziYakwamaSudan
SOMALIA: HOTELI YASHAMBULIWA KWA ZAIDI YA SAA MOJA

- Hoteli ya Kismayo imeshambuliwa na Al-Shabaab na kusababisha vifo vya watu 26 hadi sasa na majeruhi 50

- Waathirika wapo Watanzania, Wakenya, Wamarekani na raia wa Canada pamoja na Briton

- Taarifa zinadai Miongoni mwa waliofariki ni pamoja na Mahad Abdulahi Nur, Mkurugenzi Mtendaji wa Paradise Holiday Resort ya Bagamoyo

Zaidi, soma https://jamii.app/KismayoAttackSomalia
SIMIYU: BAWACHA WATAWANYWA KWA MABOMU

- CHADEMA imeripoti Wanachama wa Baraza la Wanawake wa CHADEMA wametawanywa kwa mabomu ya machozi

- Polisi wa Bariadi, wamevamia kikao cha ndani kilichokuwa kinaongozwa na Mwenyekiti wao, Halima Mdee

Zaidi, soma https://jamii.app/BawachaWatawanywaMabomu-SMY