JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MSHIRIKI WA ‘MISS SHINYANGA’ APIGWA NA WAANDAAJI

- Nicole Emmanuel(19) amepigwa na Mkurugenzi, Richard Luhende na Meneja George, wote kutoka Makumbusho Intertainment

- Nicole amedai kuwa amepigwa wakati akidai fedha zake za nauli Tsh. 70,000

Zaidi, soma https://jamii.app/MshirikiMissShinyangaApigwa
HOJA: UKITAKA KUOA, MCHUNGUZE PIA MAMA MKWE KWANI TABIA ZAKE NDIO ZA MKEO

- Mdau kutoka JamiiForums anadai tabia za Mama Mkwe zinarandana kwa asilimia kubwa na tabia za atakaye kuwa Mke wako, hivyo mchunguze pia Mama Mkwe kumjua Mchumba wako

- Amedai sababu kubwa ni kwamba Mwanamke anapoolewa Mshauri mkuu ni mama yake mzazi, kwa hiyo maisha yake kwenye ndoa yatategemea ushauri wa mamaye

Kushiriki mjadala, tembelea https://jamii.app/TabiaMamaMkweMchumba
BREAKING: Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imesitisha uteuzi wa Bw. Frank Nyabundege kama Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TIB Corporate
JULIUS MTATIRO ATEULIWA KUWA DC WA TUNDURU

> Rais Magufuli amemteua Ndg. Julius S. Mtatiro kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma

> Mtatiro anachukua nafasi ya Juma Z. Homera ambaye ameteuliwa kuwa RC wa Katavi

Zaidi, soma https://jamii.app/MtatiroDCTunduru
INDONESIA: AHUKUMIWA KWA KUREKODI SIMU ZA BOSI WAKE AKIMTAKA KIMAPENZI

- Baiq Maknun(41) amehukumiwa miezi 6 jela na faini ya Tshs. 82,257,200 kwa kusambaa kwa sauti aliyomrekodi bosi wake

- Rais nchi hiyo, Jokowi aahidi kufuatilia hukumu hiyo kuona uwezekano wa kumpa msamaha

Soma https://jamii.app/BaiqNurilSentence
LUGOLA: WANAOJITEKA NA WANAOSAMBAZA TAARIFA ZAO WASHITAKIWE

> Waziri wa Mambo ya Ndani amesema kuna taarifa za uongo za utekaji na kupotea zinazolenga kumchonganisha Rais na wananchi

> Asema Serikali kamwe haiwezi kuwateka wananchi wake

Soma https://jamii.app/LugolaUtekajiBunda
BURUNDI: KIONGOZI WA ‘IMBONERAKURE’ APEWA UONGOZI SHIRIKA LA HABARI LA TAIFA

> Imbonerakure ni kikundi cha vijana cha chama tawala, CNDD-FDD wanaotuhumiwa kwa mauaji, ubakaji kwa Wapinzani hususani mwaka 2015 wakati wa jaribio la mapinduzi

Soma https://jamii.app/NshimirimanaHeadRTNB
#JFLeo
HALIMA MDEE AKAMATWA NA JESHI LA POLISI AKIWA BUKOBA

- Jeshi la Polisi limezingira ukumbi wa kikao cha Semina ya kuwajengea Uwezo BAWACHA, na kumkamata Mbunge wa Kawe

- Aidha, jana akiwa Simiyu, Jeshi la Polisi lilizuia kikao chao cha ndani

Soma https://jamii.app/MdeeAkamatwaBukoba
#AFCON2019: Dakika 90 za Mchezo wa nusu fainali kati ya #Senegal 🇸🇳 na #Tusinia 🇹🇳 zimemalizika kwa timu hizo kutoshana nguvu kwa kutofungana

- Mchezo huo unaenda katika dakika 30 za nyongeza na timu hizo zikitoka suluhu tena, mshindi atapatikana kwa penati
TENNIS: NOVAK DJOKOVIC ASHINDA TAJI LA WIMBLEDON DHIDI YA ROGER FEDERER

- Amefanikiwa kutetea taji hilo kwa kumfunga Federer seti 7-6, 1-6, 7-6, 4-6, 7-6 katika fainali iliyoweka historia ya kuchezwa kwa muda mrefu

- Hili ni taji lake la 5 la Wimbledon
#AFCON2019: Timu ya Taifa ya #Senegal 🇸🇳 imefanikiwa kutinga fainali ya michuano hiyo baada ya kuifunga timu ya Taifa ya #Tunisia 🇹🇳 goli 1-0

- Senegal inasubiri kucheza fainali na mshindi wa mechi kati ya #Algeria 🇩🇿 na #Nigeria 🇳🇬 itakayoaanza saa nne usiku huu
#AFCON2019: Timu ya Taifa ya #Algeria🇩🇿 imefanikiwa kufuzu kucheza fainali ya michuano hiyo baada ya kuifunga timu ya Taifa ya #Nigeria🇳🇬 goli 2-1 katika mchezo wa nusu fainali

- Algeria itakutana na #Senegal🇸🇳 katika fainali ya michuano hiyo mnamo Julai 19, 2019

#JFLeo #ALGNGA
SAKATA LA MUSIBA: WAZEE NDANI YA CCM WACHEFUKWA

> Mzee Makamba, Kinana waandika waraka mzito kwa niaba ya Wazee

> Wakerwa na tabia yake kuwachafua watu bila kuchukuliwa hatua

> Wadai anatumiwa na watu wenye uwezo wa kumlinda

Soma zaidi > https://jamii.app/WarakaWazeeCCM
KAHAMA: KAKA AMUUA DADA YAKE BAADA YA KUMKUTA NA MPENZI NYUMBANI KWAO

Daudi Bundala amemuua Suzana Bundala (21) kwa kumpiga na kitu kizito kichwani baada ya kumkuta amelala na mpenzi wake nyumbani kwao

> Mtuhumiwa baada ya kutekeleza mauaji hayo alikimbia na juhudi za kumtafuta na kumkamata zinaendelea

Soma - https://jamii.app/KakaAuaDadaMpnz
GEITA: RAIS MAGUFULI KUZINDUA NYUMBA ZAIDI YA 114 ZA POLISI

> Tukio litafanyika leo ktk nyumba za makazi zilizopo eneo la Magugu mkoani humo

> Rais Magufuli atazindua zaidi ya nyumba 114 zilizokwishakamilika huku matarajio ya mradi huo ni kuwa na nyumba takribani 400 kwa nchi nzima

Soma - https://jamii.app/UzinduziNyumbaPolisi
BEI YA PAMBA NYUZI SOKO LA DUNIA YAPOROMOKA, WANUNUZI WAOGOPA HASARA

> Bei ya pamba nyuzi katika soko la dunia kwa sasa ni dola 0.63 ambayo ni Tsh. 1,449 hivyo endapo watanunua pamba mbegu kwa Tsh. 1,200 watapata hasara

> Wanunuzi wameomba bei ya mkulima ishuke sokoni au Serikali iwape kinga (guarantee) ya kuwafidia hasara itakayopatikana

Soma - https://jamii.app/KushukaBeiPamba
SERIKALI: TUNAENDELEA KUTAFUTA MASOKO YA TUMBAKU

- Imesema inaendelea kutafuta masoko ili kuwawezesha Wakulima kuzalisha kwa wingi na kuinua kipato

- Imebainisha kuwa imeshafanya mazungumzo na nchi mbalimbali zikiwemo Vietnam na Misri

Zaidi, soma https://jamii.app/SokoTumbakuLatafutwa
KENYA: POLISI AJIUA AKIDAIWA ALIKUWA NA UGOMVI NA MKEWE

- Polisi wa Kituo cha Kizurini huko Kaloleni, Kaunti ya Kilifi, Kelvin Kipkemoi amejiua jana kwa kujipiga risasi

- Amejiua majira ya saa 11 alfajiri baada ya kutoka lindoni

Zaidi, soma https://jamii.app/PolisiAjiuaKilifi
MAREKANI YAZINDUA KAMPENI YA UKAGUZI WA WAHAMIAJI HOLELA

> Idara ya forodha na uhamiaji ya Marekani imezindua ukaguzi wa kushtukiza unaowalenga wahamiaji 2,000 wasio na vibali nchini humo

> Operesheni hiyo itakayofanyika katika miji mikubwa ikiwemo Los Angeles, New York, Chicago na Houston

Soma - https://jamii.app/USMigrantsInspection