JamiiForums
โœ”
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MAXENCE MELO KUHOJIWA KWA DCI JUU YA MADAI YA MUSIBA KUTAKA KUULIWA

- Ni kuhusiana na tuhuma za kupanga njama za kumuua Cyprian Musiba zilizoandikwa na magazeti ya Tanzanite na Fahari Yetu

- Magazeti hayo yamedai amepanga njama hizo kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, TCRA, Balozi Emmanuel Nchimbi na Benard Membe

Zaidi, soma https://jamii.app/MaxMeloDCIMusiba
NAHODHA WA ARSENAL AGOMA KUSAFIRI NA TIMU

- Laurent Koscielny amegoma kwenda Marekani na timu hiyo kwenye maandalizi ya msimu mpya wa Soka wa mwaka 2019/20

- Anadaiwa analazimisha kuondoka klabuni hapo na tayari ana ofa kubwa kutoka vilabu vya Bordeaux, Lyon na Rennes
WAZIRI KABUDI AKANUSHA KUTHIBITISHA KIFO CHA AZORY GWANDA

- Amesema amepokea kwa masikitiko taarifa potofu zinazochapishwa kimakosa kuwa amethibitisha kifo cha Azory

- Amesema "Mpaka sasa hakuna uthibitisho kuwa Azory yuko hai au amefariki.โ€

Zaidi, soma https://jamii.app/KabudiAkanaKuthibitishaKifoAzory
ALGERIA: MBUNGE WA UPINZANI ACHAGULIWA KUWA SPIKA

> Aliyechaguliwa kuwa Spika ni Slimane Chenine kiongozi wa muungano wa vyama vitatu vidogo vya Kiislamu katika Bunge

> Hii ni Mara ya kwanza katika siasa za Algeria

Zaidi, soma => https://jamii.app/ChenineSpikaAlgeria
MBUNGE FRANK MWAKAJOKA (CHADEMA) MBARONI

- Mbunge huyo wa Tunduma amekamatwa na Polisi leo ikielezwa atafikishwa Mahakamani kujibu tuhuma za kumpiga Mtu mwaka 2018

- Inadaiwa amekamatwa kwa madai ya kumpiga Afisa Mtendaji, Deus Mwampashe

Zaidi, soma https://jamii.app/MwakajokaMbaroniTuhuma2018
AFCON2019: Timu ya Taifa ya Ivory Coast imetoshana nguvu na timu ya Taifa ya Algeria katika dakika 90 za mchezo wa robo fainali kwa kufungana goli 1-1

- Timu hizo zinaenda katika dakika 30 za nyongeza na zikitoka suluhu mshindi atatafutwa kwa mikwaju ya penati
DAR: WATU 7 WATUHUMIWA WA UJAMBAZI WAKAMATWA

- Walivunja maduka matatu na kuiba bidhaa mbalimbali, fedha na bajaji mbili huko Ukonga

- Polisi imesema Watuhumiwa hao walikuwa wakitumia gari aina ya Toyota Harrier nyeusi yenye namba T 666 DJG

Zaidi, soma https://jamii.app/Majambazi7Mbaroni-DarJul2019
AFCON2019: Algeria imefuzu kucheza nusu fainali baada ya kuiondosha Ivory Coast kwa penati 4-3

- Mchezo huo umeamuliwa kwa penati baada ya timu hizo kutoka sare ya goli 1-1 ndani ya dakika 120

- Algeria itakutana na Nigeria Julai 14, 2019 katika nusu fainali
TFF IMEMCHAGUA KOCHA WA AZAM KUKAIMU UKOCHA WA TAIFA STARS

- Ndayiragije Etienne anakaimu ukocha na ataiongoza Stars kufuzu CHAN

- Kocha wa Coastal Union, Juma Mgunda na Kocha Msaidizi wa Polisi Tanzania, Suleiman Matola wapo benchi la ufundi

Zaidi, soma https://jamii.app/NdiyaragijeKaimuStars
AFCON2019: Timu ya Taifa ya Tunisia ๐Ÿ‡น๐Ÿ‡ณ imefanikiwa kufuzu kucheza hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo baada ya kuifunga timu ya Taifa ya Madagascar ๐Ÿ‡ฒ๐Ÿ‡ฌ goli 3-0

- Tunisia itapambana na timu ya Taifa ya Senegal ๐Ÿ‡ธ๐Ÿ‡ณ katika mchezo wa nusu fainali mnamo Julai 14, 2019
MAREKANI: R. KELLY AKAMATWA TENA KWA TUHUMA ZA UNYANYASAJI WA KINGONO

> Akamatwa na Idara ya Polisi ya New York kwa tuhuma za kuwasafirisha Wanawake kwa ajili ya kuwatumikisha kingono

> Ametiwa nguvuni wakati akiwa katika Jimbo la Chicago

Soma > https://jamii.app/RKellyArrested
KENYA: AUA WATOTO WAKE NA KUWATUPA CHOONI

- Polisi katika Kaunti ya Nandi inamtafuta Mwanamke, Floxy Cheptoo(32) anayedaiwa kumuua Mtoto wake wa Kike(7) na wa Kiume(11)

- Miili iligundulika baada ya Mwanakijiji kubaini alama za damu chooni

Zaidi, soma https://jamii.app/AuaWatotoChooni-KE
RAIS WA UGANDA KUFANYA ZIARA BINAFSI, NCHINI

- Rais Yoweri Museveni Kesho, Julai 13, 2019 atafanya ziara binafsi ya siku moja kwa kumtembelea Rais Magufuli

- Atamtembelea Rais Magufuli Kijijini kwake, Mlimani katika Wilaya ya Chato, Mkoani Geita

Zaidi, soma https://jamii.app/MuseveniZiaraBinafsi-TZ
UINGEREZA YADAI IRAN ILITAKA KUIZUIA MELI YAKE YA MAFUTA. IRAN YAKANUSHA

- Imedai tukio limetokea katika mlango bahari wa Hormuz, ila meli yake ya Kivita iliinda meli ya mafuta

- Iran imesema haikuwa na makabiliano na meli yoyote ya kigeni

Zaidi, soma https://jamii.app/Iran-UK-Hormuz
MENEJA MAABARA TUME YA MADINI AKAMATWA KWA WIZI WA DHAHABU

> Donald Njonjo anatuhumiwa kuiba kilo 6.244 za dhahabu yenye thamani ya zaidi ya Tsh. milioni 507

> Dhahabu hiyo ilikuwa imehifadhiwa katika Ofisi za Wakala wa Madini Masaki, Dar

Soma > https://jamii.app/DhahabuYaibwa
MAREKANI: AISHI NA MAITI YA MAMAYE NDANI KWA MIAKA MITATU

- Mwanamke mmoja(47) huko Texas, amekamatwa baada ya maiti ya mamaye iliyooza kugunduliwa nyumbani

- Polisi inaamini Mwanamke huyo(71) alifariki kutokana na kuanguka mnamo mwaka 2016

Zaidi, soma https://jamii.app/MaitiMamaChumbani-USA
PETER CROUCH ASTAAFU KUCHEZA SOKA

- Mchezaji huyo wa zamani wa timu ya Taifa ya England mwenye miaka 38 amechukua uamuzi huo akiwa amecheza soka la kulipwa kwa miaka 21

- Amevitumikia vilabu 11 vikiwemo Portsmouth, Tottenham, Aston Villa, Liverpool, Stoke na Burnley
KENYA: WANAWAKE 11 WAKAMATWA WAKIREKODI VIDEO ZA NGONO

- Wamekamatwa kwenye nyumba moja iliyopo Nyali, Mombasa na wanatarajiwa kufikishwa Mahakamani leo

- โ€˜Midoli ya kufanyia ngonoโ€™ imekutwa katika nyumba hiyo walimokuwa wakirekodi video

Zaidi, soma https://jamii.app/WaigizaNgonoMbaroni-KE