JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MIILI YA WAFANYAKAZI WATANO WA AZAM MEDIA GROUP YAAGWA

- Miili ya Wafanyakazi hao waliofariki jana inaagwa leo katika ofisi za Azam Media zilizopo Tabata jijini Dar

- Viongozi kadhaa wamehudhuria akiwemo Waziri wa Habari, Harrison Mwakyembe

Zaidi, soma https://jamii.app/WafanyakaziAzamWaagwa
Amesema hayo wakati wa Uzinduzi wa Hifadhi ya Burigi-Chato unaofanyika Wilayani Chato Mkoani Geita ambapo Rais Magufuli ni mgeni rasmi
KATIBU MKUU CCM AMUONYA WAZIRI WA VIWANDA

- Dkt. Bashiru Ally amesema Waziri Innocent Bashungwa atatumbuliwa ikiwa atashindwa kutizima azma ya Serikali ya kufufua viwanda

- Amehoji “Barabara zinajengwa unaziona, SGR unaiona, kwa nini hatuoni viwanda vinafufuliwa?”

Zaidi, soma https://jamii.app/BashiruAmuonyaWaziriViwanda
IRAN: TUTAJIBU HATUA YA UINGEREZA KUKAMATA MELI YETU

- Imesema Uingereza kukamata meli yao ya mafuta iitwayo Grace 1, nje ya eneo la Gibraltar hakutapita bila majibu

- Ilikamatwa Alhamisi ikishutumiwa kuvunja vikwazo kwa kupeleka mafuta Syria

Zaidi, soma https://jamii.app/IranKisasiUK
RAIS MAGUFULI AZINDUA HIFADHI YA BURIGI-CHATO, AMPONGEZA FARU RAJABU

- Amempongeza Faru huyo kwa kuzalisha Watoto 40 na hivyo kuongeza idadi ya Faru

- Aidha, amesema “Nadhani wajina wangu John(baba wa Faru Rajabu) alikuwa hajitumi vizuri”

Zaidi, soma https://jamii.app/MagufuliAmpongezaFaruRajabu
KENYA: MZEE WA MIAKA 60 MBARONI KWA KUMBAKA MTOTO WA MIAKA 9

> Tukio hilo limetokea wakati wakiwa kwenye usafiri maarufu kama ‘Matatu’

> Mtoto alizimia, alipoamka alisimulia kisa hicho

> Mtoto anafanyiwa uchunguzi Kituo cha Afya Kiganjo

Soma https://jamii.app/MzeeMbaroniKwaUnyanyasaji
PSG: NEYMAR ANAWEZA KUONDOKA IWAPO OFA YA KUNUFAISHA PANDE ZOTE ITAPATIKANA

- Mkurugenzi wa Michezo wa Klabu ya Paris St-Germain(#PSG), Leonardo ameongeza kuwa hawajapokea ofa yoyote kwa ajili ya #Neymar ila kulikuwa na mawasiliano madogo sana na Barcelona
MSAIDIZI WA BERNARD MEMBE, ANAYEDAIWA KUTEKWA APATIKANA

- Allan Kiluvya amepatikana baada ya kuachwa na wanaodaiwa kuwa watekaji katika eneo la Njia Panda ya Segerea

- Amesema hapo palikuwa sehemu salama kwani aliweza kupata usafiri na kuwa Watu hao walimuacha hapo baada ya kumuuliza wapi wamuache

Zaidi, soma https://jamii.app/AllanApatikanaNjiaSegerea
XABI ALONSO AJITOSA KWENYE UKOCHA

- Mchezaji huyo wa zamani aliyewika katika vilabu vya Liverpool, Real Madrid na Bayern Munich amekubali kuinoa timu ya Real Sociedad B

- Miaka 20 iliyopita, Alonso alianza kucheza soka la kulipwa katika Klabu hiyo ya Uhispania
WAZIRI KALEMANI: CHATO ITAKUWA MIONGONI MWA MAJIJI MAKUBWA

- Amewataka Wawekezaji wa nje na ndani ya nchi kwenda kuwekeza katika Wilaya hiyo akisema kuna fursa

- Amesema licha ya Hifadhi iliyozinduliwa leo pia kuna madini na Ziwa Victoria

Zaidi, soma https://jamii.app/WilayaChatoJiji
UBALOZI WA NORWAY NCHINI TANZANIA KUTOSHUGHULIKIA MASUALA YA ‘VISA’

- Kuanzia Agosti 01, 2019 maombi ya ‘visa’ za safari au Makazi kwa Watanzania wanaotaka kwenda Norway, yatatumwa na kushughulikiwa katika Ubalozi wa Norway uliopo Nairobi

Zaidi, soma https://jamii.app/NorwegianVisa-Nairobi
NEPAL: AFISA WA ZAMANI WA UN AFUNGWA JELA KWA KUDHALILISHA WATOTO

- Peter John Dalglish(62) amehukumiwa kifungo cha miaka 9 kwa kumdhalilisha mtoto wa kiume wa miaka 12 na kifungo cha miaka 7 kwa kumdhalilisha kingono mtoto wa miaka 14

Zaidi, soma https://jamii.app/Ex-UNOfficialJailed-Nepal
JAJI MUTUNGI: VYAMA VYA UPINZANI HAVIJAWAHI KULALAMIKA KUZUIWA MIKUTANO

- Msajili wa Vyama vya Siasa, amesema ofisi yake haijawahi kupokea malalamiko ya maandishi

- Amesema vyama vinapaswa kutuma maandishi ili ofisi yake ipate pa kuanzia

Zaidi, soma https://jamii.app/MsajiliMalalamikoMikutanoMsajili
TAKUKURU YAMKAMATA ALIYETAKA KUMTAPELI MKUU WA WILAYA YA KISARAWE

- Omari Khamis Chuma(55), anashikiliwa kwa tuhuma za kujifanya Afisa wa Usalama wa Taifa

- Mtuhumiwa alifika katika Ofisi za DC wa Kisarawe, Jokate Mwegelo kwa nia ya kumtapeli

Zaidi, soma https://jamii.app/TAKUKURU-TapeliSuguMbaroni
MAREKANI KUUNDA MUUNGANO WA MATAIFA DHIDI YA VITISHO VYA IRAN

- Ni vitisho dhidi ya shughuli za usafirishaji katika eneo ghuba na mlango bahari wa Hormuz

- Ni kutokana na wasiwasi kuwa Iran ndiyo ilishambulia meli za mafuta katika eneo hilo

Zaidi, soma https://jamii.app/MarekaniMataifa-Iran
BALOZI WA UINGEREZA NCHINI MAREKANI AJIUZULU

- Balozi Kim Darroch amejiuzulu ikiwa ni matokeo ya kuvuja kwa barua pepe zake zinazoukosoa utawala wa Rais wa Marekani, Donald Trump kwa kusema kuwa utawala huo hauna weledi na usiojali diplomasia

Zaidi, soma https://jamii.app/BaloziUK-AjiuzuluUSA
WAZIRI KIGWANGALLA AZUNGUMZIA SANAMU YA NYERERE

- Asema “Hatuyapuuzi maneno ya Watanzania kuhusu ile sanamu, kama kuna mapungufu sisi ndio wenye dhamana ya kuangalia. Wataalamu tunao tutawaita watuelekeze kama kuna mapungufu yatarekebishwa”

Zaidi, soma https://jamii.app/SanamuNyerereMarekebisho
TABORA: AHUKUMIWA KWA KUENDESHA TRENI AKIWA AMELEWA

- Elirehema Macha amehukumiwa kifungo cha miezi 12 au kulipa faini ya Tsh. Milioni 2

- Alikuwa akiendesha treni kutoka Dar kwenda Kigoma na alipita bila kusimama katika Kituo cha Malongwe

Zaidi, soma https://jamii.app/DerevaTreniMleviAhukumiwa
#AFCON2019: #Senegal inakuwa timu ya kwanza kufuzu kucheza hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo baada ya kuifunga #Benin goli 1-0 katika mchezo wa robo fainali

- Senegal sasa inasubiri kucheza nusu fainali na mshindi wa mechi kati ya #Madagascar na #Tunisia
WAZIRI KABUDI: AZORY GWANDA SIO MTU PEKEE ALIYEPOTEA NA KUFA

- Akiwa katika kipindi cha ‘Focus on Africa’ cha BBC, amesema kupotea kwa Azory ni moja ya mambo ya kuumiza sana ambayo Tanzania imepitia kwani katika eneo la Rufiji si Azory pekee aliyepotea na kufa

Zaidi, soma https://jamii.app/AzoryKabudiKupoteaKufa