JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
AMUUA MWENZAKE AKIMTUHUMU KUIBA PANGA MWAKA 2018

> Jeshi la Polisi Wilaya ya Lindi linamshikilia Aisha Mshamu (65) kwa tuhuma za kumuua Zainabu Mikumbi (80) kwa kumpiga na jembe kichwani na shingoni akimtuhumu kwa wizi wa panga lililopotea 2018

Soma - https://jamii.app/MauajiWiziPanga
MISENYI, KAGERA: WALIOMTEKA MWANAFUNZI WA DARASA LA PILI WAHUKUMIWA MIAKA 5 JELA

> Waliohukumiwa ni Khalifa Ahmed(19) na Jonas Deogratias(19). Walimteka Levis Respicius Mei 13, 2019

> Walitaka kumtumia Mtoto huyo kumshinikiza Baba yake awape Milioni 15

Soma > https://jamii.app/WafungwaMisenyi
MOROGORO: WAFANYAKAZI WA MRADI WA SGR NA ASKARI WA JWTZ WAFARIKI KATIKA AJALI

> Waliofariki ni Wafanyakazi wa Yapi Merkezi Modriki Mwaisyupa(41), na Inocent Maiko(37), Askari wa JWTZ ambaye jina halijafahamika na Zainabu Shija (32) aliyekuwa ameomba lifti

Soma > https://jamii.app/AjaliUbena
UKAGUZI WA BIDHAA: MAKONTENA 142 YALIKUTWA NA BIDHAA BANDIA

> Tume ya Ushindani imefanya ukaguzi wa makontena 3,312 katika kipindi cha mwaka wa fedha uliopita 2017/2018 na kubaini makontena 142 yalikuwa na bidhaa bandia

> Ukaguzi huo ulifanywa katika mikoa mbalimbali ikiwemo Dodoma, Morogoro, Mwanza, Arusha, Mbeya na mipaka yote ya nchi

Soma - https://jamii.app/MakontenaBidhaaBandia
UKRAINE: KUFUATIA KUTUNGWA KWA SHERIA YA KUZUIA MATUSI: WAZIRI ASEMA MATUSI NI MAZURI KWA AFYA

> Naibu Waziri wa Afya, Ulana Suprun amesema matusi ni mazuri kwa afya ya Mwanadamu

> Amefafanua kuwa matusi ni mawasiliano mazuri ya kihisia baina ya Watu

Soma > https://jamii.app/MatusiUkraine
FAMILIA 7 ZAKOSA MAHALI PA KUISHI BAADA YA NYUMBA ZAO KUBOMOLEWA

> Familia 7 katika Mtaa wa Olasiti Kati jijini Arusha, hazina mahali pa kuishi kufuatia nyumba zao kubomolewa kwa amri ya Mahakama kutokana na mgogoro wa Ardhi uliokuwa ukiendelea baina yao na Mkazi wa Kiteto, Mwanamkasi Ramadhani

> Baadhi yao wamedai zoezi hilo limetekelezwa bila kufuata utaratibu na hawakupewa muda wa kujiandaa

Soma - https://jamii.app/FamiliMakaziBomoa
Mchezo wa michuano ya #AFCON2019 wa hatua ya 16 bora kati ya #Morocco dhidi ya #Benin umemalizika kwa timu hizo kutoka sare ya goli 1 kwa 1

> Mchezo huo unalazimika kwenda dakika 30 za nyongeza ili kumpata mshindi.

#JFSports
Timu ya taifa ya #Benin imefanikiwa kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya #AFCON2019 baada ya kuifunga timu ya taifa ya #Morocco kwa changamoto ya mikwaju ya penati

> #Benin imeshinda kwa kupata penati 4 dhidi ya penati 1 ya #Morocco

#JFSPorts
Mchezo wa michuano ya #AFCON2019 wa hatua ya 16 bora kati ya #Uganda dhidi ya #Senegal umeenda mapumziko kwa #Uganda kufungwa goli 1 kwa 0

> Goli la #Senegal limefungwa na mshambuliaji wa Liverpool FC, Sadio Mane dakika ya 15

#JFSports
Timu ya Taifa ya #Uganda 'The Cranes' imeondoshwa katika michuano ya #AFCON2019 baada ya kukubali kipigo cha goli 1 kwa 0 kutoka kwa timu ya Taifa ya #Senegal

> #Uganda ndio timu pekee kutoka Afrika Mashariki iliyokuwa imesalia katika michuano hiyo

#JFSports
NEMC: KELELE ZA VIWANDA, NGOMA, MUZIKI, IBADA KUANZA KULIPIWA. WATAKAOKIUKA KUTOZWA FAINI

> NEMC imesema kwa Mtu atakayetaka kufanya shughuli hizo atapaswa kulipa milioni 10

> Watakaokiuka watatozwa faini isiyozidi milioni 50 ama kifungo jela

Soma > https://jamii.app/NEMCVsKelele
Mchezo wa hatua ya 16 bora kati ya #Cameroon na #Nigeria umeenda mapumziko kwa #Cameroon kuongoza kwa magoli 2 kwa 1

> Je, #Nigeria wataweza kujitutumua na kurudisha goli hilo kipindi cha pili?

#AFCON2019 #JFLeo
RAIA WA KIGENI MBARONI KWA KUSAFIRISHA DHAHABU BILA KIBALI

> Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia raia wawili wa Uingereza na mmoja wa Ireland kwa kosa la kusafirisha dhahabu gramu 1,044.95 bila kuwa na kibali kutoka Wilaya ya Chunya kuelekea Jijini Dar es salaam

Soma - https://jamii.app/UsafiriDhahabuWageni