JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
VIONGOZI 3 WATUHUMIWA KUTAFUNA FEDHA ZA MAUZO YA DHAHABU

> M/kiti, Katibu na Meneja wa kikundi cha wachimbaji dhahabu cha Winima Group kilichopo katika mgodi wa Kitunda Wilayani Sikonge wako hatiani kukamatwa kwa tuhuma za kutafuna Tsh milioni 342 za mauzo ya kilo 1.549 za dhahabu

> Walikwenda kufanya mauzo ya dhahabu ikiwa ni mali ya wanakikundi lakini hawakukabidhi fedha za mauzo

Soma - https://jamii.app/HujumaMauzoDhahabu
KISUTU, DAR: WEMA SEPETU AACHIWA NA KUKAMATWA TENA

> Msanii huyo wa filamu amezua kizaazaa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu alipokuwa akigoma kukamatwa tena na Askari wa Jeshi la Polisi

> Wema aliachiwa huru baada ya shahidi wa Jamhuri kutofika Mahakamani

Soma > https://jamii.app/WemaAkamtwaTena
KAMPUNI YA ACACIA YATAKA MAZUNGUMZO NA SERIKALI YA TANZANIA

> Acacia inatafuta suluhu ya mgogoro wa kodi uliopo baina yake na Tanzania

> Tanzania ilizuia shehena ya Makinikia hadi hapo Acacia itakapolipa deni la kodi la kiasi cha TSh. Trilioni 436

Soma > https://jamii.app/Acacia-Tanzania
NIGERIA: MWANAUME AFARIKI BAADA YA KUFANYA MAPENZI KWA MIZUNGUKO 7

> Mwanaume huyo aliyefahamika kwa jina moja tu la Davy amefariki wakati akiwa kwenye mashindano ya kufanya mapenzi na Mwanamke aitwaye Loveth

> Inaelezwa kuwa Davy aliimudu vyema mizunguko ya awali kabla ya kuzidiwa na kufariki akiwa kwenye mzunguko wa 7

Kusoma kisa hiki, fungus => https://jamii.app/AfarikiAkifanyaMapenzi
MUME AWACHOMA MOTO KWA PETROLI MAMA NA MTOTO

> Mkazi wa kijiji cha Mlazo, Wilaya ya Chamwino, Mkami Mbarahi(19) na mwanaye wenye umri wa miezi mitatu wamelazwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma baada ya kujeruhiwa kwa moto na mumewe, kwenye maeneo mbalimbali ya mwili

> Tukio hilo lilitokea Juni 28 baada ya mume kumkuta mkewe akipika kwa kutumia kuni

Soma - https://jamii.app/MeAchomaKeMtoto
TANZIA: MAMA MKUU WA SHIRIKA LA KIFUNGILO PAMOJA NA DEREVA WAFARIKI KATIKA AJALI

> Waliofariki ni Sister Octavia pamoja na dereva wake Aminiel

> Ajali hiyo imetokea katika maeneo ya Wilaya ya Same, Kilimanjaro

Zaidi, soma => https://jamii.app/TanziaSisterKifungilo
FARU MWEUSI AFARIKI WAKATI AKISAFIRISHWA KUTOKA UINGEREZA KUJA TANZANIA

> Faru huyo alikuwa akisafirishwa kwa ushirikiano wa Grumeti na Serikali ya Tanzania kama sehemu ya mkakati wa kuongeza idadi ya Faru Weusi kwenye Hifadhi ya Serengeti

Soma > https://jamii.app/FaruUKTanzaia
HISTORIA: FAHAMU KUHUSU ASILI YA KABILA LA WAKURYA

> Wakurya ni kabila la watu wanaoishi katika Wilaya ya Rorya, Tarime na Serengeti Kaskazini mwa Tanzania, na katika Wilaya za Magharibi na Mashariki mwa Mkoa wa Nyanza katika sehemu ya Kenya

> Shuguli zao kubwa ni Kilimo na Ufugaji, huku Wakurya wa Kenya wakiegemea sana kwenye kilimo na Tanzania wakiegemea sana kwenye ufugaji

> Wakurya hawapendi kutawaliwa wala kuonewa hivyo walikuwa na saiga lika ya vijana kwa ajili ya ulinzi na usalama hivyo utumwa haukuwaathiri sana

Fahamu zaidi - https://jamii.app/HistoriaKabilaWakurya
#JFHistoria
CHATO: RAIS MAGUFULI KUZINDUA HIFADHI YA BURIGI JULAI 9, 2019

> Hifadhi ya Taifa ya Burigi iliyopo Chato, Geita itazindulia siku ya Jumanne baada ya kupandishwa hadhi hivi karibuni

> Hifadhi hii ilikuwa ikijulikana kama Pori la Akiba la Burigi.

Soma > https://jamii.app/HifadhiBurigi
MALI ZA MBOWE KUPIGWA MNADA, ADAIWA KUTOLIPA KODI

> Mali hizo ni zile zilizokuwa kwenye ukumbi wa disko wa Club Bilicanas uliokuwa unamilikiwa na Mbowe Limited

> Kampuni hiyo inadaiwa kodi ya shilingi bilioni 1.1. Mnada utafanyika Jumamosi wiki hii

Soma > https://jamii.app/MaliMbowe-Mnada
TUNISIA: TAKRIBANI WAKIMBIZI 82 WANAHOFIWA KUFARIKI BAADA YA BOTI WALIYOKUWA WAKISAFIRIA KUZAMA

> Boti hiyo imezama katika Pwani ya Tunisia na ilikuwa ikisafirisha Wakimbizi 86

> Manusura wanne wameeleza kuwa Boti hiyo ilizama katika eneo la Zarzis

Soma > https://jamii.app/WakimbiziWazama
WATANZANIA WAPEWA SIKU 3 KUONDOKA KWENYE KIJIJI MPAKANI MWA MSUMBIJI

> Serikali ya Tanzania na Msumbiji zimekubaliana kutoa siku tatu kwa wakazi wa kijiji cha Kitaya Wilaya ya Mtwara kuhamisha mali zao zilizopo katika kijiji cha Mtole nchini Msumbiji baada ya kutokea kwa mauaji ya Watanzania 10 waliopigwa risasi na watu wasiojulikana

Soma - https://jamii.app/UhamishoWatzMsumbiji
#JFLeo
MWALIMU ANUSURIKA KIFO AKITAKA KUJIUA KUTOKANA NA UGUMU WA MAISHA

> Mwalimu wa Shule ya Msingi Rung'abure Wilaya ya Serengeti mkoani Mara, Godfrey Tarimo (35) amenusurika kifo baada ya kujikata shingoni kwa chupa, huku ikidaiwa ni kwasababu ya ugumu wa maisha

> Hajapata athari yoyote katika mfumo wake wa upumuaji

Soma - https://jamii.app/KujiuaUgumuMaisha
DODOMA: WATATU WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUBAKA NA KULAWITI

> Jeshi la Polisi linawashikilia watu hao kwa makosa ya ulawiti na ubakaji wa watoto na wazee katika matukio tofauti

> Kati yao, yupo kijana(28) aliyemlawiti mama yake mzazi mwenye umri wa miaka 56

Soma - https://jamii.app/KijanaAlawitiMama
CHINA NA UINGEREZA ZAZOZANA KUHUSU MASUALA YA HONG KONG

> Uingereza imeahidi kuendelea kuishinikiza China kuhusu njia za nguvu inazotumia dhidi ya waandamanaji mjini Hong Kong

> Naye Balozi wa China nchini Uingereza, Liu Xiaoming ameitaka Uingereza kukoma kuingilia masuala ya ndani ya Hong Kong

Soma - https://jamii.app/ChinaHongKongUK
POLISI: TUNACHUNGUZA KUTEKWA KWA RAPHAEL NA KUKUTWA JIRANI NA NYUMBA YA SHANGAZI YAKE

> Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Interpol nchini Kenya, linaendelea kufanya uchunguzi ili kubaini ni namna gani, Raphael Ongangi alitekwa na kufikishwa Mombasa

> Inadaiwa miaka 2 iliyopita, alishawahi kutoa taarifa ‘za uzushi’ kwamba anataka kutekwa

Soma https://jamii.app/UchunguziKutekwaRaphael

#JFLeo
POLISI WAMUACHIA WEMA SEPETU BAADA YA KUMKAMATA JANA

> Msanii huyo wa filamu nchini, amenusurika kulala Mahabusu jana baada ya Kituo Kikuu cha Polisi kumuachia huru kwa dhamana hadi hapo watakapomuhitaji

> Wema alikamatwa tena jana na Polisi baada ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kumwachia huru kutokana na Hakimu kuzikubali hoja za upande wa utetezi
NEC YATANGAZA UCHAGUZI JIMBO LA LISSU KUFANYIKA JULAI 31, 2019

> NEC imetangaza uchaguzi mdogo katika Jimbo la Singida Mashariki lililokuwa chini ya Tundu Lissu

> Lissu alifutiwa Ubunge kwa kutohudhuria vikao vya Bunge kwa muda mrefu bila taarifa rasmi

Soma > https://jamii.app/UchaguziSingidaEast
FAHAMU MAMBO MACHACHE KUHUSU MNYAMA TWIGA

> Twiga huwa na urefu wa kati ya mita 4.8 na 5.5, Uzito wake ni kati ya kilo 700 na 1500 na hubeba mimba kwa siku 400 hadi 460, ambazo ni sawa na miezi 14 hadi 15

> Shingo yake ndio sehemu inayomsisimua kimahaba, wanapokutana dume na jike hufanya mchezo wa kuzungusha kwa kuzifunga shingo zao

> Twiga jike ni mwaminifu kwa dume lake na hutafuta dume jingine endapo dume wake atakufa na kama atakosa anaweza kufa kwa upweke

Soma zaidi - https://jamii.app/SifaTwiga
SUDAN: JESHI NA WANANCHI WAKUBALIANA KUUNDA SERIKALI YA MPITO

> Viongozi wa Jeshi na Muungano wa upinzani wamekubaliana na kuundwa kwa Serikali ya mpito itakayoongozwa kitaalamu pamoja na kuchunguza machafuko ya hivi karibuni yaliyosababisha watu wengi kuuawa

> Mazungumzo kati ya pande hizo mbili yaliongozwa na Waziri Mkuu wa Ethiopia na wajumbe wa Umoja wa Afrika

Soma - https://jamii.app/PitishoSerikaliMpito