JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MKE WA MTAWALA WA DUBAI AKIMBILIA UINGEREZA NA KUOMBA HIFADHI YA UKIMBIZI

> Haya bint Hussein ambaye ni Mtoto wa aliyekuwa Mfalme wa Jordan, ametoroka nchini humo pamoja na Watoto wake wawili na kukimbilia nchini Uingereza akimtuhumu mumewe kumnyanyasa

Zaidi, soma => https://jamii.app/PrincessHaya-UK
KENYA: MWANAHABARI ZA MTANDAONI ALIYETUHUMIWA KUSHIRIKIANA NA AL-SHABAAB AACHIWA KWA DHAMANA

> Robert Alai Onyango alishtakiwa kwa makosa mawili likiwemo la kuvujisha siri kwa nia ya kuwasaidia Wanamgambo wa Al-Shabaab na kuvuruga uchunguzi wa Polisi

Soma > https://jamii.app/AlaiAachiwaDhamana
URUSI: MVUA YASABABISHA MAFURIKO NA KUUA WATU 12

> Mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika jimbo la Irkutsk imesababisha vifo vya watu 12 huku wengine 9 wakiwa hawajulikana walipo baada ya makazi yao kukumbwa na maji

> Nyumba zaidi ya 3000 zimeathirika na mafuriko hayo

Soma - https://jamii.app/MvuaMaafaVifo
MATUMIZI YA ASALI KWENYE UREMBO WA NGOZI NA NYWELE

> Chukua asali mbichi kijiko 1 cha chakula na baking soda kijiko 1 na changanya mchanganyiko uwe mlaini kisha paka usoni huku ukisugua taratibu kwa kufanya kama viduara. Epuka kufikisha machoni halafu osha uso wako

> Asali inatibu nywele kavu zilizopauka, na kulainisha ngozi kavu ya kichwa na kutibu muwasho kichwani

> Changanya kijiko kikubwa cha asali na maji ya uvuguvugu kisha paka kichwani. Acha kwa muda wa saa 1 iwe kama 'conditioner ' kisha safisha nywele zako

Soma - https://jamii.app/AsaliNgoziNywele
KISUMU, KENYA: NAIBU MKUU WA SHULE ASHIKILIWA KWA TUHUMA ZA KUMNAJISI MWANAFUNZI

> Mwalimu Dan Odhiambo Osok wa Shule ya Msingi Arombo ataendelea kukaa rumande hadi Julai 8 atakapopelekwa tena Mahakamani kwa tuhuma za kumnajisi Mwanafunzi wa Kike

Zaidi, soma => https://jamii.app/MwalimuAnajisi-Kisumu
MSICHANA WA KAZI ALIYEIBA MTOTO WA MWAKA 1 AKAMATWA

> Christina Claudia (23) anashikiliwa na Polisi mkoani Morogoro kwa tuhuma za kuiba mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja Wilayani Kilosa na kukimbia naye Mkoani Tabora

> Alidanganya anaenda naye kufua nguo bombani ndipo alipopata upenyo na kutoroka

Soma - https://jamii.app/MbaroniWiziMtoto
KESI YA JAMIIFORUMS: JAMHURI YAKOSA SHAHIDI, HAKIMU ASITA KUFUTA KESI

> Kesi iliyoahirishwa ni namba 458 inayowatuhumu Wakurugenzi wa JamiiForums kwa kuendesha mtandao huo bila kutumia Kikoa cha do.TZ pamoja na kuzuia upelelezi wa Polisi

Soma > https://jamii.app/KesiJF-Jamhuri
MICHEZO: Taarifa kutoka klabu ya mpira Simba imesema Ibrahim Ajibu amesaini kandarasi ya miaka miwili kuitumikia timu ya Simba akitokea timu ya Yanga ambako alimaliza mkataba Juni 30

> Kwenye msimu wa 2018/2019 alitoa jumla ya pasi za mabao 17 na kufunga mabao sita

#JFMichezo
KENYA: ALIYEKUWA AFISA WA IKULU AKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUTAKA KUMUUA MAKAMU WA RAIS

> Dennis Itumbi, aliyekuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Kidijitali Ikulu anashikiliwa akihojiwa kuhusu njama za kumuua William Ruto

> Wapo Mawaziri wanaotuhumiwa kuhusika

Soma > https://jamii.app/ItumbiVsRuto
LIBYA: KAMBI YA WAHAMIAJI YASHAMBULIWA, ZAIDI YA 40 WAFARIKI

> Wahamiaji zaidi ya 40 wameuawa katika shambulio la angani dhidi ya kambi yao katika moja ya vitongoji vya mji wa Tripoli na watu wengine 70 wamejeruhiwa katika shambulio hilo

> Inaripotiwa idadi ya waliofariki inaweza kuongezeka kutokana watu wengi kufunikwa na kifusi

Soma - https://jamii.app/MigrantsCampAttack
#JFLeo
MARA: MWAMUZI AFARIKI UWANJANI MECHI IKIENDELEA

> Gugumiya Werema(30) amepoteza maisha ghafla wakati akichezesha mpira kati ya Nyakitono FC na Nyanungu FC Wilaya ya Serengeti

> Tukio hilo lilitokea jana muda mfupi baada ya mwamuzi huyo kupokea simu na ghafla kuishiwa nguvu na kuanguka

#JFMichezo
MITANDAO YA WHATSAPP, INSTAGRAM NA FACEBOOK YASUMBUA BAADHI YA MAENEO

> Watumiaji wa mitandao hiyo duniani wametoa malalamiko hasa kupitia mtandao wa Twitter kuhusu kupata shida katika kutuma ujumbe wa maandishi, kutuma na kupokea picha

> Hali inaonekana kuwa mbaya zaidi katika maeneo ya Ulaya, Brazil na Kaskazini mwa Marekani

Soma - https://jamii.app/WhatsupFBIGDown
#JFLeo
NIGERIA: LORI LA MAFUTA LALIPUKA, WATU 35 WAPOTEZA MAISHA

> Watu 35 wamefariki na wengine 101 kujeruhiwa baada ya lori ya mafuta ya Petroli kulipuka katika kijiji cha Ahumbe

> Janga hilo lilitokea jana baada ya lori hilo kupoteza uelekeo na kuanguka na kisha kugongwa na basi aina ya Toyota na kusababisha milipuko 2

Soma - https://jamii.app/AjaliMlipukoLori
RAIS KENYATTA KUFANYA ZIARA YA SIKU 2 NCHINI, ATAWASILI CHATO IJUMAA HII

> Rais wa Kenya anatarajiwa kufanya ziara binafsi nchini kwa mwaliko wa Rais Magufuli

> Atawasili katika Uwanja wa Ndege wa Chato Mkoani Geita Ijumaa wiki hii

Zaidi, soma => https://jamii.app/KenyattaChato
UNASHAURIWA KUZINGATIA HAYA KATIKA KUCHAJI SIMU ILI KUTUNZA UBORA WA BETRI

> Usiache simu yako iishe chaji hadi 0% ndipo uichaji. Weka utaratibu wa kuchaji simu yako ikiwa kati ya asilimia 5 – 50%

> Kuacha simu yako kwenye umeme muda mrefu hasa pale ambapo imeshajaa huharibu ubora wa betri la simu yako hasa kuacha simu ikichaji usiku kucha

> Kama umenunua simu kwa bei ya juu, ni bora pia uhakikishe unatumia chaja zenye kiwango cha juu cha ubora

Soma - https://jamii.app/ChajiSimuBetri
#JFTeknolojia
KENYA: MTANZANIA AHUKUMIWA JELA MAISHA KWA KUHUSIKA NA UGAIDI

> Mahakama ya Kenya imemhukumu Rashid Mberesero na wenzake 2 baada ya kuwakuta na hatia ya kutekeleza shambulio la kigaidi mwaka 2015 katika Chuo Kikuu cha Garissa, Kenya na kusababisha vifo vya wanafunzi 148

> Walitekeleza shambulio hilo wakishirikiana na kundi la Al Shabaab

Soma - https://jamii.app/MtzJelaUgaidiGarisa
BEIJING, CHINA: UWANJA MKUBWA ZAIDI WA NDEGE KUFUNGULIWA

> Uwanja huo wenye mita za mraba milioni 1.4 unatarajiwa kuwa na uwezo wa kuhudumia wasafiri milioni 45 kwa mwaka ifikapo mwaka 2021 na kuhudumia watu milioni 75 ifikapo 2025

Zaidi, soma > https://jamii.app/BeijingDaxing
UN: SHAMBULIO LA WAHAMIAJI LIBYA LAWEZA KUWA NI UHALIFU WA KIVITA

> Afisa wa Umoja wa Mataifa amesema, shambulio lililofanywa dhidi ya kituo cha wahamiaji na kuua zaidi ya watu 44 linaweza kuwa ni uhalifu wa kivita

> Wengi wa waliouawa wanaaminiwa kuwa ni watu wa asili ya Kiafrika kutoka eneo la jangwa la Sahara ambao wamekuwa wakijaribu kuingia Ulaya kupitia Libya

Soma - https://jamii.app/UhalifuKivitaLibya
#JFLeo
TAKWIMU KIWANGO CHA UMASIKINI: MKOA WA RUKWA WAONGOZA

> Ofisi ya Taifa ya Takwimu imesema mikoa inayoongoza kwa wananchi wake kuwa masikini Tanzania bara kwa mwaka 2017/2018 ni mkoa wa Rukwa kwa 45%, Simiyu 39.2%, Geita 37.5%, Lindi 36% na Kigoma 34.5%

> Umasikini wa mahitaji ya msingi umepungua kutoka 28.2% mwaka 2011/12 hadi 26.4% mwaka 2017/18

Soma - https://jamii.app/HaliUmasikiniTz
#JFLeo
ENGLAND: FRANK LAMPARD KOCHA MPYA WA CHELSEA FC

> Frank Lampard ambaye ni miongoni mwa Wachezaji waliowahi kuichezea Klabu hiyo kwa mafanikio makubwa ametangazwa rasmi kuwa kocha mpya baada ya tetesi za muda mrefu

Zaidi, soma => https://jamii.app/Lampard-ChelseaFC

#JFLeo #JFSports