JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MAREKANI: Watu 10 wamepoteza maisha katika jimbo la Texas baada ya kutokea kwa ajali ya ndege katika eneo la Addison kwenye kiwanja cha ndege
-
Pindi ikiruka, ndege hiyo ilipoteza muelekeo na hatimaye kujibamiza na kuwaka moto na mpaka sasa mamlaka hazijatoa sababu ya ajali hiyo
-
Kati ya waliofariki, watu 4 ni ndugu wa familia moja
Je, unaifahamu Dawa ya usingizi inayotumiwa na wezi kuwapulizia watu kabla ya kuiba?

> Kwa muda mrefu kumekithiri vitendo vya uhalifu unaohusisha wezi kuingia kwenye nyumba za watu nyakati za usiku na kuwapulizia dawa ya usingizi na kisha kuchukua chochote wanachokitaka ndani ya nyumba

> Baadhi ya watu wamekuwa wakihusisha aina hiyo ya uhalifu na ushirikina lakini ukweli ni kwamba ipo dawa mojawapo ya usingizi ambayo hutumiwa na wezi wengi kutekeleza uhalifu huo. Dawa hiyo kitaalamu inaitwa CHLOROFORM

Soma uchambuzi wa kina kuhusu dawa hii hatari => https://jamii.app/ElimuChroloformJF
INDIA: WATU 16 WAMEKAMATWA KWA KUMCHAPA AFISA MISITU

> Wanaume 16 wamekamatwa baada ya umati wa watu kumpiga vibaya kwa fito Afisa mwanamke wa misitu wakati maafisa wa Polisi wakitazama katika jimbo la Kusini, Telangana

> Umati huo ulikuwa ukilalamika kuhusu kampeni ya upandaji wa miti iliyoidhinishwa Jumapili

Soma https://jamii.app/KipigoAfisaMisitu
#JFLeo
INDIA: WATU 13 WAFARIKI BAADA YA UKUTA WA MPAKA KUANGUKA

> Takribani watu 13 wamefariki na wengine 4 kujeruhiwa baada ya ukuta wa mpaka kuporomoka mjini Mumbai asubuhi ya leo kutokana na mvua kubwa kunyesha siku chache zilizopita

> Ukuta mwingine uliporomoka Jumamosi na watu wasiopungua 15 walifariki huko Kondhwa mjini Pune

Soma - https://jamii.app/VifoAngukoUkuta
HALMASHAURI KUU YA CCM YAMVUA UJUMBE WA KAMATI KUU 'KEISHA'

> Khadija Shabani Taya maarufu ‘Keisha’ ameondolewa ndani ya Kamati Kuu ya chama hicho baada ya kuitumikia kwa siku 396

> Taarifa zisizo rasmi zinadai Keisha anatuhumiwa kuvujisha siri za CCM

Soma > https://jamii.app/KeishaAtenguliwaCCM
UINGEREZA: MWILI WA MZAMIAJI WAANGUKA NDEGE IKIWA ANGANI

> Mwili wa mwanaume anayedhaniwa kuzamia kisiri kwenye ndege ya Kenya Airways umeanguka katika bustani ya Clapham wakati ndege hiyo ikielekea kutua katika Uwanja wa ndege wa Heathrow jijini London juzi, Juni 30

> Mwili huo utafanyiwa uchunguzi kubaini kilichosababisha kifo

Soma - https://jamii.app/KifoMzamiajiNdege
MFANYABIASHARA RAPHAEL ONGANGI APATIKANA MOMBASA NCHINI KENYA

> Aliripotiwa kutekwa na watu wasiojulikana wiki iliyopita Jijini Dar na amepatikana leo akiwa hai

> Raphael ni Mfanyabiashara mwenye asili ya Kenya, aliyesoma na kuamua kuishi nchini

Soma > https://jamii.app/OngangiApatikanaMombasa
WANAOTAFSIRI FILAMU KUPIGWA FAINI YA TSH MILIONI 20 MPAKA 30

> Chama Cha Hakimiliki Tanzania kimesema watu wote wanaorudufu na kuuza kazi ambazo sio zao ziwe za Tanzania au nje ya nchi na za kutafsiri ni maharamia

> Adhabu hiyo inaweza kuongezeka mara 3 endapo mzigo uliokutwa eneo la biashara una thamani zaidi ya faini iliyowekwa

Soma - https://jamii.app/HaramuTafsiriFilamu
MICHEZO: LEICESTER CITY YAKATAA KUMUUZA HARRY MAGUIRE KWA MAN UTD

> Klabu hiyo imekataa kumuuza beki huyo kwenda Manchester United dau la Paundi Milioni 70

> Taarifa zinaeleza kuwa mmiliki wa Klabu hiyo Aiyawatt Shrivaddhanaprabha hana mpango wa kumuuza mchezaji huyo

Soma > https://jamii.app/MaguireHauzwi
MUSIBA APEWA SIKU 7 KUWASILISHA MAJIBU KUHUSU MADAI YA MEMBE

> Mahakama Kuu Kanda ya Dar, imempa siku 7 mmiliki na wachapishaji wa gazeti la Tanzanite wawe wamewasilisha majibu dhidi ya madai ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe anayetaka kulipwa Tsh bilioni 10 kwa kuchafuliwa

Soma - https://jamii.app/MembeKesiMusiba
RAIS KENYATTA AKERWA NA KAULI YA 'JAGUAR', AMTUMIA UJUMBE RAIS MAGUFULI

> Serikali yake imekerwa na matamshi ya Mbunge jimbo la Starehe, Charles Njagua 'Jaguar'

> Ujumbe huo umepokelewa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa niaba ya Rais

Soma => https://jamii.app/UjumbeKenyatta-Magufuli
MKE WA MTAWALA WA DUBAI AKIMBILIA UINGEREZA NA KUOMBA HIFADHI YA UKIMBIZI

> Haya bint Hussein ambaye ni Mtoto wa aliyekuwa Mfalme wa Jordan, ametoroka nchini humo pamoja na Watoto wake wawili na kukimbilia nchini Uingereza akimtuhumu mumewe kumnyanyasa

Zaidi, soma => https://jamii.app/PrincessHaya-UK
KENYA: MWANAHABARI ZA MTANDAONI ALIYETUHUMIWA KUSHIRIKIANA NA AL-SHABAAB AACHIWA KWA DHAMANA

> Robert Alai Onyango alishtakiwa kwa makosa mawili likiwemo la kuvujisha siri kwa nia ya kuwasaidia Wanamgambo wa Al-Shabaab na kuvuruga uchunguzi wa Polisi

Soma > https://jamii.app/AlaiAachiwaDhamana
URUSI: MVUA YASABABISHA MAFURIKO NA KUUA WATU 12

> Mvua kubwa inayoendelea kunyesha katika jimbo la Irkutsk imesababisha vifo vya watu 12 huku wengine 9 wakiwa hawajulikana walipo baada ya makazi yao kukumbwa na maji

> Nyumba zaidi ya 3000 zimeathirika na mafuriko hayo

Soma - https://jamii.app/MvuaMaafaVifo
MATUMIZI YA ASALI KWENYE UREMBO WA NGOZI NA NYWELE

> Chukua asali mbichi kijiko 1 cha chakula na baking soda kijiko 1 na changanya mchanganyiko uwe mlaini kisha paka usoni huku ukisugua taratibu kwa kufanya kama viduara. Epuka kufikisha machoni halafu osha uso wako

> Asali inatibu nywele kavu zilizopauka, na kulainisha ngozi kavu ya kichwa na kutibu muwasho kichwani

> Changanya kijiko kikubwa cha asali na maji ya uvuguvugu kisha paka kichwani. Acha kwa muda wa saa 1 iwe kama 'conditioner ' kisha safisha nywele zako

Soma - https://jamii.app/AsaliNgoziNywele
KISUMU, KENYA: NAIBU MKUU WA SHULE ASHIKILIWA KWA TUHUMA ZA KUMNAJISI MWANAFUNZI

> Mwalimu Dan Odhiambo Osok wa Shule ya Msingi Arombo ataendelea kukaa rumande hadi Julai 8 atakapopelekwa tena Mahakamani kwa tuhuma za kumnajisi Mwanafunzi wa Kike

Zaidi, soma => https://jamii.app/MwalimuAnajisi-Kisumu
MSICHANA WA KAZI ALIYEIBA MTOTO WA MWAKA 1 AKAMATWA

> Christina Claudia (23) anashikiliwa na Polisi mkoani Morogoro kwa tuhuma za kuiba mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja Wilayani Kilosa na kukimbia naye Mkoani Tabora

> Alidanganya anaenda naye kufua nguo bombani ndipo alipopata upenyo na kutoroka

Soma - https://jamii.app/MbaroniWiziMtoto
KESI YA JAMIIFORUMS: JAMHURI YAKOSA SHAHIDI, HAKIMU ASITA KUFUTA KESI

> Kesi iliyoahirishwa ni namba 458 inayowatuhumu Wakurugenzi wa JamiiForums kwa kuendesha mtandao huo bila kutumia Kikoa cha do.TZ pamoja na kuzuia upelelezi wa Polisi

Soma > https://jamii.app/KesiJF-Jamhuri
MICHEZO: Taarifa kutoka klabu ya mpira Simba imesema Ibrahim Ajibu amesaini kandarasi ya miaka miwili kuitumikia timu ya Simba akitokea timu ya Yanga ambako alimaliza mkataba Juni 30

> Kwenye msimu wa 2018/2019 alitoa jumla ya pasi za mabao 17 na kufunga mabao sita

#JFMichezo
KENYA: ALIYEKUWA AFISA WA IKULU AKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUTAKA KUMUUA MAKAMU WA RAIS

> Dennis Itumbi, aliyekuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Kidijitali Ikulu anashikiliwa akihojiwa kuhusu njama za kumuua William Ruto

> Wapo Mawaziri wanaotuhumiwa kuhusika

Soma > https://jamii.app/ItumbiVsRuto