JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MEXICO: POLISI WANENE HATARINI KUFUKUZWA KAZI WASIPOPUNGUA

> Maafisa wa Polisi wanaotaka kujiunga na kikosi kipya cha ulinzi wa Taifa nchini Mexico wamepewa hadi miezi 6 kupunguza uzito la sivyo wafutwe kazi

> Agizo hilo limetolewa katika maandalizi ya kukabiliana na wahamiaji haramu na tayari maafisa 625 tayari wamefeli vigezo vya kiafya vya kujiunga na kikosi hicho

Soma - https://jamii.app/FatPoliceTrouble
DRC: WATU 43 WAMEPOTEZA MAISHA KWENYE MAPOROMOKO YA UDONGO

> Watu 43 wamefariki na wengine kadhaa wajeruhiwa katika maporomoko ya ardhi yaliyotokea kwenye mgodi wa shaba huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

> Mgodi huo unamilikiwa na shirika la Uingereza la Kamoto Copper Company
MAGARI YA MIZIGO YAGONGANA RUVU, YAPELEKEA FOLENI KUBWA

> Malori mawili yaliyogongana uso kwa uso katika eneo la Ruvu na kuwaka moto saa 7 usiku wa kuamkia leo yamepelekea foleni kubwa sana katika barabara ya Morogoro

Soma https://jamii.app/AjaliMaloriRuvu
TRUMP AKUTANA NA KIM JONG-UN “DEMILITARIZED ZONE”

> Donald Trump awa Rais wa kwanza wa Marekani kukanyaga ardhi ya Korea Kaskazini akiwa madarakani

> Licha ya mkutano huo, Trump amesema vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini viko pale pale

Zaidi, soma jamii.app/TrumpKimMeetDMZ
CHADEMA: LISSU KAVULIWA UBUNGE ILI ASIGOMBEE URAIS 2020

Wadai kumvua Lissu Ubunge kunamfanya asiruhusiwe kugombea ndani ya miaka mitano, na hawezi kugombea Urais wa Tanzania 2020 kama hana sifa za kugombea Ubunge kwa mujibu wa ibara ya 39(1)(d) ya Katiba

Zaidi, soma => https://jamii.app/CDMLissuUrais2020
SUDAN: WATU 7 WAMEUAWA WAKATI WA MAANDAMANO

> Wananchi wanaendelea kushinikiza Baraza la Kijeshi la Mpito linalotawala nchi hiyo, kurudisha madaraka kwa raia

> Maandamano hayo yanafanyika ikiwa ni wiki kadhaa tangu Jeshi livamie kambi ya Waandamanaji

Soma https://jamii.app/Wasudan7wauawa
KENYA: MTENDAJI MKUU WA KAMPUNI YA SAFARICOM AFARIKI DUNIA

> Robert Collymore(61) maarufu ‘Bob’ amefariki dunia asubuhi ya leo akiwa nyumbani kwake Jijini Nairobi baada ya kuugua saratani ya damu kwa muda mrefu

> Bob alipanga kustaafu Agosti, 2020

Soma => https://jamii.app/RIPCollymore
AUSTRALIA: MAFUA YASABABISHA VIFO 228

> Takribani watu 228 wameripotiwa kufariki huku wengine 100,000 wakiugua ugonjwa huo

> Virusi vya ugonjwa huo vinaendelea kusambaa licha ya chanjo kutolewa kwa zaidi ya watu milioni 11 kutokana na msimu wa baridi

Soma - https://jamii.app/DeathFluSeason
BURUNDI YAADHIMISHA MIAKA 57 TANGU KUPATA UHURU

> Wananchi wa Burundi leo wanaadhimisha kumbukizi ya miaka 57 tangu Taifa hilo lilipojipatia uhuru wake kutoka kwa wakoloni wa Ubelgiji Julai 1, 1962

> Miaka 57 inatimia huku Wanasiasa wengi wa upinzani wako ukimbizini na watu zaidi ya 300,000 wamekimbilia nchi jirani

Soma https://jamii.app/BRN57Independence
KILIMANJARO: MFUNGWA AJIUA KWA KUJIKATA NA WEMBE GEREZANI

> Agustino Moshi (70) aliyekuwa akitumikia kifungo cha miaka 30 jela kwa ubakaji, amejiua kwa kujikata mara tatu kwenye mshipa wa fahamu shingoni akiwa kwenye Gereza la Karanga

> Ni baada ya kuzozana na Askari kuhusu kufanya kazi za shambani

Soma - https://jamii.app/MfungwaAjiuaKLM
ZITTO KABWE: WATEKAJI MWACHIENI ONGANGI HANA TAARIFA MNAZOHITAJI

> Zitto amehusisha tukio la kudukuliwa kwa mitandao yake ya Kijamii na kutekwa kwa msaidizi wake, Raphel Ongangi

> Amewasihi watekaji hao wamuache Raphael mahali popote kisha wao watakwenda kumchukua

Soma => https://jamii.app/ZittoKutekwaOgangi
MICHEZO: Kocha wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike ameihakikishia Tanzania ushindi leo dhidi ya Algeria baada ya kukosa nafasi ya kusonga mbele kutokana na kufanya vibaya katika mechi 2

> Mechi hiyo itachezwa saa 4 usiku kwenye Uwanja wa Al Salaam

#JFMichezo #AFCON2019
SIMIYU: PAMBA YAKWAMA KWENYE MAGHALA, WAKULIMA WAZUIA MAGARI

> Wameyazuia magari hayo baada ya kutolipwa fedha zao tangu msimu wa mauzo ufunguliwe

> Wakulima wamekuwa wakishinda na kulala kwenye maghala wakishinikiza walipwe madai yao

Zaidi, soma => https://jamii.app/WakulimaPamba
TANGA: KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE AGOMA KUZINDUA MRADI WA DARAJA

> Mkongea Ally amegoma kuzindua mradi wa Daraja la Mfuto lililopo eneo la Bwawani, Wilayani Handeni, kutokana na ujenzi wake kutozingatia ushauri wa kitaalamu

> Ametoa wiki mbili kwa Mhandisi wa Wilaya kuhakikisha anafanya upya vipimo vya mradi ili kujiridhisha na ubora malighafi zilizotumika

Soma - https://jamii.app/MgomoMradiMwenge
JAPAN YAWEKA VIKWAZO UUZAJI WA VIFAA VYAKE VYA TEKNOLOJIA, KOREA KUSINI

> Wizara ya Uchumi, Biashara na Viwanda ya Japan imesema kuanzia Julai 04, 2019 kampuni za Japan zitahitajika kuomba kibali cha binafsi ili kuuza vifaa vya kiteknolojia vikiwemo vya kutengenezea simu za mkononi

> Uamuzi huo umeifanya Korea Kusini kuwasilisha waraka wa malalamiko kwa Shirika la Kibiashara Duniani

Soma - https://jamii.app/JapanDeniesTechSK
#JFLeo
CHALINZE, PWANI: WATU WAWILI WAUAWA KATIKA MATUKIO TOFAUTI

> Damian Kimiti(70) ameuawa kwa kupigwa shoka na kuporwa simu 3 aina ya tecno, solar paneli, shuka na baiskeli

> Ngurai Waziri(33) mfugaji huko Msolwa kijiji cha Lukenge ameuawa kwa kukatwa kwa visu akidaiwa kuwa mwizi wa mifugo

Soma https://jamii.app/Mauaji2Chalinze
#JFLeo
MAHUSIANO: Kuishi na Wanaume walevi wa Pombe, Sigara au Bangi kunadaiwa kuwa kero kwa Wanawake wengi hasa ambao wameolewa

- Nini kinachoweza kusaidia Wanaume hao kuacha ulevi huo?

Kutana na mjadala wa wahanga wa tatizo hilo hapa => https://jamii.app/WanaumeUlevi
SRI LANKA YAKATAA WITO WA UN KUTAKA ISITEKELEZE ADHABU YA KIFO
-
Rais Maithiripala Sirisena amekataa wito wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres wa kuangazia upya shinikizo lake la kurejesha upya adhabu ya kifo nchini humo baada ya miaka 43
-
Rais Sirisena amesema, amemueleza Katibu Mkuu huyo katika mazungumzo yao kupitia simu kwamba anataka kuinusuru nchi yake na tatizo la #DawaZaKulevya
RAIS MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA KYELA

> Uteuzi wa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Bi. Lucy Mganga umetenguliwa kwa utendaji usioridhisha

> Mkurugenzi mpya wa Halmashauri hiyo atateuliwa hapo baadaye

Zaidi, soma => https://jamii.app/UtenguziDEDKyela