JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
WIZARA YA FEDHA YAKANUSHA KUTOA MIKOPO

- Imekanusha taarifa kuwa inatoa mikopo ya kilimo na biashara bila riba

- Taarifa iliyokanushwa inadai kuwa Wizara pamoja na Taasisi ya Global Entrepreneurship na Benki ya Dunia zimeungana kutoa mikopo

Zaidi, soma https://jamii.app/MikopoWizaraFedhaHakuna
LISSU AVULIWA UBUNGE, JIMBO LIPO WAZI

- Spika Ndugai amekitangaza kiti cha ubunge cha jimbo la Singida Mashariki lililokuwa linashikiliwa na Tundu Lissu(CHADEMA) kuwa wazi

- Amesema ameshamwandikia Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi juu ya uamuzi huo

Zaidi, soma https://jamii.app/LissuAvuliwaUbunge
MBEYA: SHEHENA YA VIUATILIFU YAKAMATWA IKIWA NA NEMBO BANDIA

> Viuatilifu hivyo vina thamani ya zaidi ya Tsh. milioni 600 na ni mali ya Mfanyabiashara Yona Kalinga

> Malalamiko yalitolewa na Kampuni ya Rista life Sayansi Tanzania Limited kuwa kuna mfanyabiashara anavunja sheria ya alama za bidhaa

Soma - https://jamii.app/ViuatilifuBandiaMBY
#JFLeo
KAMPUNI YA APPLE YAPOTEZA DOLA BILIONI 9 NDANI YA SAA MOJA

> Imepoteza fedha hizo ambazo ni sawa na Trilioni Tsh. 21 katika soko la hisa, saa moja baada ya Jony Ive aliyehusika katika ubunifu wa takribani bidhaa zote za Apple, kutangaza kuondoka ndani ya kampuni hiyo

> Jony alijiunga na Apple mwaka 1992 na ametangaza kufungua kampuni yake ya ubunifu

Soma - https://jamii.app/IveLeavesApple
#JFTeknolojia
WATANZANIA 9 WAULIWA MPAKANI MWA TANZANIA NA MSUMBIJI

> Raia 9 wa Tanzania pamoja na wawili wa Msumbiji wameuliwa na watu wasiojulikana huku watanzania wengine 6 wakijeruhiwa vibaya katika kijiji cha Mtole kilichopo upande wa Msumbiji mpakani mwa Tanzania na Msumbiji

> IGP Siro amesema msako unaanza mara moja kwa kushirikiana na Serikali ya Msumbiji ili kuwakamata waliohusika na mauaji hayo

Soma - https://jamii.app/TznsDeadBoader
TUNDU LISSU KWENDA MAHAKAMANI KUPINGA KUVULIWA UBUNGE

> Mbunge huyo wa Singida Mashariki (CHADEMA), amesema atakwenda Mahakamani kupinga uamuzi wa Spika wa Bunge kumvua uongozi kwa madai kuwa amepoteza sifa ya kuendelea kuwa Mbunge

> Amesisitiza kuwa bado anapata matibabu nje ya nchi lakini Septemba 7, 2019 atarudi nchini

Soma - https://jamii.app/LissuKesiUbunge
MEXICO: POLISI WANENE HATARINI KUFUKUZWA KAZI WASIPOPUNGUA

> Maafisa wa Polisi wanaotaka kujiunga na kikosi kipya cha ulinzi wa Taifa nchini Mexico wamepewa hadi miezi 6 kupunguza uzito la sivyo wafutwe kazi

> Agizo hilo limetolewa katika maandalizi ya kukabiliana na wahamiaji haramu na tayari maafisa 625 tayari wamefeli vigezo vya kiafya vya kujiunga na kikosi hicho

Soma - https://jamii.app/FatPoliceTrouble
DRC: WATU 43 WAMEPOTEZA MAISHA KWENYE MAPOROMOKO YA UDONGO

> Watu 43 wamefariki na wengine kadhaa wajeruhiwa katika maporomoko ya ardhi yaliyotokea kwenye mgodi wa shaba huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

> Mgodi huo unamilikiwa na shirika la Uingereza la Kamoto Copper Company
MAGARI YA MIZIGO YAGONGANA RUVU, YAPELEKEA FOLENI KUBWA

> Malori mawili yaliyogongana uso kwa uso katika eneo la Ruvu na kuwaka moto saa 7 usiku wa kuamkia leo yamepelekea foleni kubwa sana katika barabara ya Morogoro

Soma https://jamii.app/AjaliMaloriRuvu
TRUMP AKUTANA NA KIM JONG-UN “DEMILITARIZED ZONE”

> Donald Trump awa Rais wa kwanza wa Marekani kukanyaga ardhi ya Korea Kaskazini akiwa madarakani

> Licha ya mkutano huo, Trump amesema vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini viko pale pale

Zaidi, soma jamii.app/TrumpKimMeetDMZ
CHADEMA: LISSU KAVULIWA UBUNGE ILI ASIGOMBEE URAIS 2020

Wadai kumvua Lissu Ubunge kunamfanya asiruhusiwe kugombea ndani ya miaka mitano, na hawezi kugombea Urais wa Tanzania 2020 kama hana sifa za kugombea Ubunge kwa mujibu wa ibara ya 39(1)(d) ya Katiba

Zaidi, soma => https://jamii.app/CDMLissuUrais2020
SUDAN: WATU 7 WAMEUAWA WAKATI WA MAANDAMANO

> Wananchi wanaendelea kushinikiza Baraza la Kijeshi la Mpito linalotawala nchi hiyo, kurudisha madaraka kwa raia

> Maandamano hayo yanafanyika ikiwa ni wiki kadhaa tangu Jeshi livamie kambi ya Waandamanaji

Soma https://jamii.app/Wasudan7wauawa
KENYA: MTENDAJI MKUU WA KAMPUNI YA SAFARICOM AFARIKI DUNIA

> Robert Collymore(61) maarufu ‘Bob’ amefariki dunia asubuhi ya leo akiwa nyumbani kwake Jijini Nairobi baada ya kuugua saratani ya damu kwa muda mrefu

> Bob alipanga kustaafu Agosti, 2020

Soma => https://jamii.app/RIPCollymore
AUSTRALIA: MAFUA YASABABISHA VIFO 228

> Takribani watu 228 wameripotiwa kufariki huku wengine 100,000 wakiugua ugonjwa huo

> Virusi vya ugonjwa huo vinaendelea kusambaa licha ya chanjo kutolewa kwa zaidi ya watu milioni 11 kutokana na msimu wa baridi

Soma - https://jamii.app/DeathFluSeason
BURUNDI YAADHIMISHA MIAKA 57 TANGU KUPATA UHURU

> Wananchi wa Burundi leo wanaadhimisha kumbukizi ya miaka 57 tangu Taifa hilo lilipojipatia uhuru wake kutoka kwa wakoloni wa Ubelgiji Julai 1, 1962

> Miaka 57 inatimia huku Wanasiasa wengi wa upinzani wako ukimbizini na watu zaidi ya 300,000 wamekimbilia nchi jirani

Soma https://jamii.app/BRN57Independence
KILIMANJARO: MFUNGWA AJIUA KWA KUJIKATA NA WEMBE GEREZANI

> Agustino Moshi (70) aliyekuwa akitumikia kifungo cha miaka 30 jela kwa ubakaji, amejiua kwa kujikata mara tatu kwenye mshipa wa fahamu shingoni akiwa kwenye Gereza la Karanga

> Ni baada ya kuzozana na Askari kuhusu kufanya kazi za shambani

Soma - https://jamii.app/MfungwaAjiuaKLM
ZITTO KABWE: WATEKAJI MWACHIENI ONGANGI HANA TAARIFA MNAZOHITAJI

> Zitto amehusisha tukio la kudukuliwa kwa mitandao yake ya Kijamii na kutekwa kwa msaidizi wake, Raphel Ongangi

> Amewasihi watekaji hao wamuache Raphael mahali popote kisha wao watakwenda kumchukua

Soma => https://jamii.app/ZittoKutekwaOgangi
MICHEZO: Kocha wa Taifa Stars, Emmanuel Amunike ameihakikishia Tanzania ushindi leo dhidi ya Algeria baada ya kukosa nafasi ya kusonga mbele kutokana na kufanya vibaya katika mechi 2

> Mechi hiyo itachezwa saa 4 usiku kwenye Uwanja wa Al Salaam

#JFMichezo #AFCON2019
SIMIYU: PAMBA YAKWAMA KWENYE MAGHALA, WAKULIMA WAZUIA MAGARI

> Wameyazuia magari hayo baada ya kutolipwa fedha zao tangu msimu wa mauzo ufunguliwe

> Wakulima wamekuwa wakishinda na kulala kwenye maghala wakishinikiza walipwe madai yao

Zaidi, soma => https://jamii.app/WakulimaPamba