JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
AFCON2019: Madagascar imeibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi Burundi katika mchezo wa Kundi B

- Madagascar inafikisha alama 4 huku Kundi hilo likiongozwa na Nigeria yenye alama 6, Guinea ina alama 1 na Burundi ina alama 0 ambapo timu zote zimecheza michezo miwili
AFCON2019: Michezo inayofuata ni ya Kundi C ambapo Senegal inakutana na Algeria majira ya saa mbili kamili usiku huu

- Katika Kundi hilo hilo Kenya ‘HarambeeStars’ inakutana na Tanzania ‘TaifaStars’ majira ya saa tano kamili usiku
NIGERIA: FEDHA ZILIZOKUWA ZIMEFICHWA NA RAIS MSTAAFU ZATAIFISHWA

> Fedha hizo ni zaidi ya Dola milioni 267 (zaidi ya Tsh bilioni 600) ambazo zilifichwa na Rais San Abacha katika benki iliyopo kisiwa cha Jersey

> Zilipatikana kwa njia za rushwa wakati wa utawala wake kati ya mwaka 1993 hadi kifo chake mwaka 1998

Soma - https://jamii.app/TaifishoFedhaRais
URUSI: WAWILI WAFARIKI, SABA WAJERUHIWA KATIKA AJALI YA NDEGE

- Ni baada ya ndege kutua kwa dharura katika uwanja wa ndege katika eneo la Buryatia huko Siberia na kuwaka moto

- Waliofariki katika ndege hiyo iliyokuwa imebeba watu 48 ni rubani na fundi

Zaidi, soma https://jamii.app/TwoKilledPlaneAcc-Urusi
KOREA KASKAZINI YAITAKA KOREA KUSINI KUSITISHA MAZUNGUMZO NA MAREKANI

> Korea Kaskazini imeitaka Korea Kusini kusitisha juhudi zake za upatanishi katika mazungumzo yake na Marekani

> Rais Donald Trump atakutana tena na kiongozi wa Korea Kusini, Moon Jae In mjini Seoul Jumapili baada ya mkutano wa kilele wa G20 huko Osaka Japan

Soma - https://jamii.app/NorthKoreaVsUs
AFCON2019: Mchezo kati ya timu za Taifa za Tanzania ‘Taifa Stars’ na Kenya ‘Harambee Stars’ umeenda mapumziko huku Tanzania ikiwa inaongoza kwa goli 2-1

Magoli ya Tanzania yamefungwa na Simon Msuva katika dakika ya 6 na Mbwana Samatta katika dakika ya 40 huku goli la Kenya likifungwa na Michael Olunga katika dakika ya 39
AFCON2019: Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imepoteza mchezo wake wa pili katika hatua ya makundi baada ya kukubali kufungwa goli 3-2 na timu ya Taifa ya Kenya ‘Harambee Stars’
-
Kwa matokeo yao, Algeria inaongoza Kundi C ikiwa na alama 6 huku Kenya na Senegal wakiwa wanafuata wakiwa na alama 3 kila moja, Tanzania inashika nafasi ya mwisho ikiwa na alama 0
Bunge la Tanzania jana lilipitisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (No.3) wa 2019

> Muswada unagusa Sheria za Takwimu, Makampuni, Asasi za Kiraia, Vikundi vya Kijamii, Uwakala wa Usafirishaji Majini, Filamu na Michezo ya Kuigiza

Zaidi, soma - https://jamii.app/PitishoSheriaAZAKI
#UhuruWetu
KAKA AMUUA MDOGO WAKE KWA MADAI YA KUPENDWA SANA NA BABA YAO

> Hassan Chacha(7) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la kwanza katika Kijiji cha Getenga Wilayani Tarime ameuawa kwa kushambuliwa na kaka yake Mniko Chacha (20) kwa kumning'iniza juu na kumtupa chini mara 2

> Mtuhumiwa alitoroka baada ya kutenda tukio hilo na juhudi za kumtafuta zinaendelea

Soma - https://jamii.app/KakaAuaMdogo
ACACIA YAKATAA KUUZA HISA ZAKE KWA BARRICK, YADAI $979M HAIAKISI THAMANI YAKE HALISI

> Barrick inayomiliki 63.9% ya Acacia ilipendekeza kuinunua Acacia kwa mfumo wa hisa, ambapo hisa 1 ya Acacia itabadilishwa kwa hisa 0.153 ya Barrick

Soma - https://jamii.app/AcaciaVsBarrick

#JFLeo
WALIOFANYA UDANGANYIFU KUPATA NAFASI ZA KAZI JKT KUSHTAKIWA

> Jeshi la Wananchi (JWTZ) limetangaza kuwachukulia hatua viongozi wa ndani na nje ya Jeshi hilo na vijana waliohusika katika vitendo vya udanganyifu katika uandikishaji wa majina ya kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT)

> Udanganyifu ulihusisha ukiukaji wa taratibu na kughushi nyaraka na vyeti vilivyotumika katika uandikishaji

Soma - https://jamii.app/UdanganyifuNafasiJKT
JAGUAR ANYIMWA DHAMANA, KUSHIKILIWA KWA SIKU 3 ZAIDI

- Mahakama imeruhusu Polisi kuendelea kumshikilia kwa siku 3 za kazi ili imalize uchunguzi

- Atakuwa katika Kituo cha Kileleshwa kuanzia leo hadi Jumanne(bila kuhesabu Jumamosi na Jumapili)

Zaidi, soma https://jamii.app/JaguarRumandeSiku3
AC MILAN YAFUNGIWA KUSHIRIKI MICHUANO YA ULAYA

- Itatumikia kifungo cha mwaka mmoja kutokushiriki michuano ya Ulaya inayoandaliwa na UEFA hivyo itakosa Ligi ya Europa ya msimu ujao

- Ni baada ya kuvunja sheria ya soka ya Financial Fair Play

Zaidi, soma https://jamii.app/ACMilanBannedEuropeanComptn
AFGHANISTAN: POLISI 8 WAFARIKI KWENYE SHAMBULIO LA BOMU

> Askari polisi nane wamethibitika kufariki na wengine 66 wamejeruhiwa ktk shambulio la kujitoa muhanga katika lango la kukagua usalama kwenye mkoa wa Daikundi

> Kundi la Taliban limedai kuhusika na mlipuko huo

Soma - https://jamii.app/Bomb8DeadAfgh
WIZARA YA FEDHA YAKANUSHA KUTOA MIKOPO

- Imekanusha taarifa kuwa inatoa mikopo ya kilimo na biashara bila riba

- Taarifa iliyokanushwa inadai kuwa Wizara pamoja na Taasisi ya Global Entrepreneurship na Benki ya Dunia zimeungana kutoa mikopo

Zaidi, soma https://jamii.app/MikopoWizaraFedhaHakuna
LISSU AVULIWA UBUNGE, JIMBO LIPO WAZI

- Spika Ndugai amekitangaza kiti cha ubunge cha jimbo la Singida Mashariki lililokuwa linashikiliwa na Tundu Lissu(CHADEMA) kuwa wazi

- Amesema ameshamwandikia Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi juu ya uamuzi huo

Zaidi, soma https://jamii.app/LissuAvuliwaUbunge
MBEYA: SHEHENA YA VIUATILIFU YAKAMATWA IKIWA NA NEMBO BANDIA

> Viuatilifu hivyo vina thamani ya zaidi ya Tsh. milioni 600 na ni mali ya Mfanyabiashara Yona Kalinga

> Malalamiko yalitolewa na Kampuni ya Rista life Sayansi Tanzania Limited kuwa kuna mfanyabiashara anavunja sheria ya alama za bidhaa

Soma - https://jamii.app/ViuatilifuBandiaMBY
#JFLeo
KAMPUNI YA APPLE YAPOTEZA DOLA BILIONI 9 NDANI YA SAA MOJA

> Imepoteza fedha hizo ambazo ni sawa na Trilioni Tsh. 21 katika soko la hisa, saa moja baada ya Jony Ive aliyehusika katika ubunifu wa takribani bidhaa zote za Apple, kutangaza kuondoka ndani ya kampuni hiyo

> Jony alijiunga na Apple mwaka 1992 na ametangaza kufungua kampuni yake ya ubunifu

Soma - https://jamii.app/IveLeavesApple
#JFTeknolojia
WATANZANIA 9 WAULIWA MPAKANI MWA TANZANIA NA MSUMBIJI

> Raia 9 wa Tanzania pamoja na wawili wa Msumbiji wameuliwa na watu wasiojulikana huku watanzania wengine 6 wakijeruhiwa vibaya katika kijiji cha Mtole kilichopo upande wa Msumbiji mpakani mwa Tanzania na Msumbiji

> IGP Siro amesema msako unaanza mara moja kwa kushirikiana na Serikali ya Msumbiji ili kuwakamata waliohusika na mauaji hayo

Soma - https://jamii.app/TznsDeadBoader
TUNDU LISSU KWENDA MAHAKAMANI KUPINGA KUVULIWA UBUNGE

> Mbunge huyo wa Singida Mashariki (CHADEMA), amesema atakwenda Mahakamani kupinga uamuzi wa Spika wa Bunge kumvua uongozi kwa madai kuwa amepoteza sifa ya kuendelea kuwa Mbunge

> Amesisitiza kuwa bado anapata matibabu nje ya nchi lakini Septemba 7, 2019 atarudi nchini

Soma - https://jamii.app/LissuKesiUbunge