JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MAHUSIANO: WAKWE ZANGU WAMEHAMIA NYUMBANI KWANGU, NIMECHOKA VIKAO

> Wazazi wa Mke wangu walikuja Dar kututembelea na ilikuwa wakae kwa muda wa mwezi mmoja lakini cha kushangaza wanakuwa kama wamehamia

> Napata changamoto nyingi ikiwemo Baba Mkwe kutoa amri ndani ya nyumba yangu

Zaidi, soma > https://jamii.app/KeroYaWakwe
NDEGE ZA KIMATAIFA ZAEPUKA ANGA LA IRAN

- Ni baada ya ndege ya Marekani isiyokuwa na rubani kudunguliwa na Iran

- Ndege hizo ni za Mashirika ya Cathay Pacific, Emirates, FlyDubai, British Airways, KLM, Qantas, Singapore Airlines na Lufthansa

Zaidi, soma https://jamii.app/NdegeKimataifaAngaIran
TETESI ZA SOKA: Gazeti la Tuttosport la Italia limedai kuwa Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba amempigia simu Kocha mpya wa Juventus, Maurizio Sarri kumshawishi amsajili

- Aidha, inadaiwa kuwa Manchester United inataka kumpa mkataba wa mnono wa miaka mitano wa thamani ya Paundi 350,000(Tsh. 1,024,788,755) kwa wiki, Kipa wake David De Gea
HAWAII: NDEGE YAANGUKA YAUA WATU WOTE 9 WALIOKUWEMO NDANI

- Imeanguka na kuwaka moto karibu na Uwanja wa ndege wa Dillingham huko Oahu, Honolulu

- Haijaeleweka sababu za ndege hiyo kuanguka na kama ilikuwa inatua au kupaa katika uwanja huo

Zaidi, soma https://jamii.app/HawaiiPlaneKills9
SHINYANGA: MUME MBARONI AKITUHUMIWA KUMUUA ALIYEMFUMANIA NA MKEWE

- Rafael Martine(34) anatuhumiwa kumuua Shija Mahoiga(45) baada ya kumfumania akiwa amelala na mkewe

- Anatuhumumiwa kumshambulia marehemu kwa kipande cha chuma

Zaidi, soma https://jamii.app/AmuuaAliyemfumania-SHY
BUKOMBE, GEITA: AFISA MTENDAJI AFARIKI KWA KUSHAMBULIWA NA WASIOJULIKANA

- Ni Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Ibambilo, Kata ya Bulega, Juma Maziku

- Amefariki baada ya kuokotwa kwenye barabara iendayo Mnekesi, Chato akiwa na majeraha mwilini

Zaidi, soma https://jamii.app/AfisaMtendajiAuawa-GIT
IRAN YAMPUUZA TRUMP, YASEMA ITAJIBU MAPIGO

- Imeyapuuza madai ya Trump kuwa alisitisha shambulizi dhidi yake kwa hofu ya kusababisha idadi kubwa ya vifo

- Pia, haitovumilia uvamizi katika eneo lake na hivyo kukabiliana na hatari yoyote

Zaidi, soma https://jamii.app/IranYampuuzaTrump
AFCON-2019: Timu ya Taifa ya Nigeria imefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Burundi katika mchezo wa kwanza wa kundi B

- Nigeria sasa inaongoza kundi huku ikisubiri matokeo ya mchezo baina ya Guinea na Madagascar utakaoanza saa 5:00 usiku huu
ETHIOPIA: MKUU WA MAJESHI APIGWA RISASI KATIKA JARIBIO LA MAPINDUZI

- Waziri Mkuu wa nchi hiyo ameongea hayo huku akikemea jaribio hilo la Mapinduzi lililotokea huko Amhara

- Hali ya Mkuu wa Majeshi kwa sasa bado haifahamiki

Soma https://jamii.app/EthiopiaCoupAttempt
GEITA: MAMA ADAIWA KUMCHINJA MTOTO WAKE NA KUMPIKA

- Ni Happiness Shadrack(36) mwenye tatizo la akili, amemchinja mtoto wake wa mwaka mmoja

- Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Kamishna Msaidizi Dismas Kisusi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo

Soma https://jamii.app/MamaAmchinjaMtoto
GEITA: WANAFUNZI 6 WA MIAKA 13-16 WAKUTWA WAKIISHI KINYUMBA

- Ni Wanafunzi wa kike wa darasa la 7 wa Shule ya msingi Nyamalele wenye miaka 13 na wa kiume wenye miaka 16 wa Shule ya Sekondari Nkome

- Watoto wa kike walitoroka nyumbani kwao na kwenda kuishi na watoto hao wa kiume

Zaidi, soma https://jamii.app/WatotoWaishiKinyumba
ETHIOPIA: MKUU WA MAJESHI AFARIKI KWA KUPIGWA RISASI KWENYE JARIBIO LA MAPINDUZI

- Seare Mekonnen amefariki dunia baada ya kupigwa risasi na mlinzi huko Addis Ababa

- Rais wa Mkoa wa Amhara na Mshauri Mkuu pia wamefariki kwenye tukio hilo

Soma https://jamii.app/EthiopiaCoupAttempt
AFCON2019: Morocco imefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Namibia katika mchezo wa Kundi D na kufanikiwa kuongoza kundi hilo

- Timu nyingine katika kundi hilo za Ivory Coast na South Africa zinashuka dimbani kuchuana kesho saa 11:30 jioni
AFCON2019: Mtanange unaofuta saa mbili usiku na kusubiriwa kwa hamu na Watanzania ni kati ya timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ na Senegal

- Ni mchezo wa kwanza wa kundi C huku mchezo wa 2 katika kundi hilo kati ya Algeria na Kenya ukipigwa saa 5:00 usiku huu
KENYA: MWANAFUNZI AMUUA MWENZAKE KISA MVULANA

- Mwanafunzi wa Kidato cha 4, Juni 21 anadaiwa kumchoma kwa kitu chenye ncha, Mwanafunzi wa darasa la 8 huko Lukose, Kakamega

- Alikuwa akimtuhumu wa darasa la 8 kumchukulia 'Mchumba' wake

Zaidi, soma https://jamii.app/StudentKillsAnother-KE
INDIA: WATU 14 WAFARIKI BAADA YA KUANGUKIWA NA HEMA KUBWA

- Watu wengine 50 wamejeruhiwa katika tukio hilo hapo jana Juni 23 Wilayani Barmer katika jimbo la Rajasthan

- Hema hilo lilianguka kutokana na mvua kubwa na upepo mkali

Zaidi, soma https://jamii.app/TentCollapseKills14-India
POLISI 6 MBARONI KWA KUOMBA RUSHWA KWA MZEE WA MIAKA 95

> Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) Wilaya ya Igunga inawachunguza askari Polisi wa Kituo cha Igunga kwa tuhuma za kuomba rushwa ya Tsh. milioni 8 Ngaka Mataluma ili wasimpeleke kituoni

Soma - https://jamii.app/PolisiMadaiRushwa
KISUTU: MAHAKAMA YAMUONYA WEMA. YAMREJESHEA DHAMANA

- Wema Sepetu(30) ameonywa kutokiuka masharti ya dhamana, vinginevyo Mahakama itamfutia dhamana

- Wema alikuwa rumande siku 7 hadi leo kutokana na kushindwa kufika Mahakamani bila taarifa

Zaidi, soma https://jamii.app/WemaAonywaDhamana
JEAN PIERRE BEMBA AREJEA RASMI DR CONGO

- Amerejea jana akitokea Brussels, Ubelgiji na kulakiwa na umati wa watu baada ya kukaa miezi 10 ugenini

- Inadaiwa amerudi kumsaidia mpinzani Martin Fayulu anayesisitiza kushinda Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2018

Zaidi, soma https://jamii.app/BembaArejeaCongo
TARIME: MWALIMU AMKATA MWANAFUNZI NA PANGA KICHWANI

> Jeshi la Polisi Mkoani Mara linamshikilia Mwalimu Kangoyi Marwa wa shule ya msingi Nyamumbara kwa tuhuma za kumjeruhi mwanafunzi wa darasa la tatu kwa kumkata panga kichwani

> Uongozi wa Halmashauri umemsimamisha kazi mwalimu huyo

Soma - https://jamii.app/MwlAmkataPangaMwf