JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
RAIS TRUMP ASITISHA KUTAKA KUISHAMBULIA IRAN

- Amesitisha hatua ya kuishambulia Iran muda mfupi baada ya kutoa idhini ya kufanya hivyo kujibu shambulio la Iran lililoidungua na kuiangusha ndege ya Jeshi la Marekani isiyo na rubani

Zaidi, soma https://jamii.app/TrumpAsitishaKuchambuliaIran
WAMILIKI WA VIWANJA ENEO LA PEMBA MNAZI WATAKIWA KULIPA

- Waliopewa viwanja eneo la Pemba Mnazi, Kigamboni wanatakiwa kukamilisha malipo kabla ya Julai 31, 2019

- Watakaoshindwa kulipa, viwanja vyao vitagawiwa kwa waombaji wengine bila taarifa yoyote

Zaidi, soma https://jamii.app/WamilikiViwanjaPembaMnazi
VURUGU ZAIBUKA KATIKA BARABARA YA KAJIADO-NAMANGA, WAFANYABIASHARA WAKIPIGANA

- Usafiri katika barabara hiyo ulisimama baada ya Wafanyabiashara wa Mchanga kufunga barabara

- Vurugu zimetokea kufuatia Wachimba mchanga kutoka Purko kutakiwa kutotumia soko la Ilbisil

Zaidi, soma https://jamii.app/ChaosKajiado-NamangaRoad
ANAYEDAIWA 'KUMTUSI' RAIS MUSEVENI AKUTWA NA KESI YA KUJIBU

- Mwanaharakati na Mtafiti wa Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda, Dkt. Stella Nyanzi anadaiwa kutumia ukurasa wake wa Facebook kuandika maneno machafu kwa Rais na marehemu mamaye

Zaidi, soma https://jamii.app/StellaNyanziKesiKujibu-UG
DAR: RAIA WA NIGERIA AHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 30

- Mahakama ya Mafisadi imemuhukumu Christian Ugbechi baada ya kukutwa na hatia ya kusafirisha kete 56 za #DawaZaKulevya aina ya Heroin Hydrochloride zenye uzito wa gramu 947.57

Zaidi, soma https://jamii.app/MnigeriaMiaka30-TZ
ARUSHA: HOTEL YA KITALII YA SNOWCREST YAFILISIWA

- Ni baada ya kushindwa kujiendesha kutokana na madeni makubwa inayodaiwa yanayofikia Tsh. Bilioni 14

- Kampuni ya udalali ilifika hotelini hapo na kuchukua kila kitu kilichokuwepo ndani

Zaidi, soma https://jamii.app/HoteliSnowcrestYafilisiwa-AR
MAHUSIANO: WAKWE ZANGU WAMEHAMIA NYUMBANI KWANGU, NIMECHOKA VIKAO

> Wazazi wa Mke wangu walikuja Dar kututembelea na ilikuwa wakae kwa muda wa mwezi mmoja lakini cha kushangaza wanakuwa kama wamehamia

> Napata changamoto nyingi ikiwemo Baba Mkwe kutoa amri ndani ya nyumba yangu

Zaidi, soma > https://jamii.app/KeroYaWakwe
NDEGE ZA KIMATAIFA ZAEPUKA ANGA LA IRAN

- Ni baada ya ndege ya Marekani isiyokuwa na rubani kudunguliwa na Iran

- Ndege hizo ni za Mashirika ya Cathay Pacific, Emirates, FlyDubai, British Airways, KLM, Qantas, Singapore Airlines na Lufthansa

Zaidi, soma https://jamii.app/NdegeKimataifaAngaIran
TETESI ZA SOKA: Gazeti la Tuttosport la Italia limedai kuwa Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba amempigia simu Kocha mpya wa Juventus, Maurizio Sarri kumshawishi amsajili

- Aidha, inadaiwa kuwa Manchester United inataka kumpa mkataba wa mnono wa miaka mitano wa thamani ya Paundi 350,000(Tsh. 1,024,788,755) kwa wiki, Kipa wake David De Gea
HAWAII: NDEGE YAANGUKA YAUA WATU WOTE 9 WALIOKUWEMO NDANI

- Imeanguka na kuwaka moto karibu na Uwanja wa ndege wa Dillingham huko Oahu, Honolulu

- Haijaeleweka sababu za ndege hiyo kuanguka na kama ilikuwa inatua au kupaa katika uwanja huo

Zaidi, soma https://jamii.app/HawaiiPlaneKills9
SHINYANGA: MUME MBARONI AKITUHUMIWA KUMUUA ALIYEMFUMANIA NA MKEWE

- Rafael Martine(34) anatuhumiwa kumuua Shija Mahoiga(45) baada ya kumfumania akiwa amelala na mkewe

- Anatuhumumiwa kumshambulia marehemu kwa kipande cha chuma

Zaidi, soma https://jamii.app/AmuuaAliyemfumania-SHY
BUKOMBE, GEITA: AFISA MTENDAJI AFARIKI KWA KUSHAMBULIWA NA WASIOJULIKANA

- Ni Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Ibambilo, Kata ya Bulega, Juma Maziku

- Amefariki baada ya kuokotwa kwenye barabara iendayo Mnekesi, Chato akiwa na majeraha mwilini

Zaidi, soma https://jamii.app/AfisaMtendajiAuawa-GIT
IRAN YAMPUUZA TRUMP, YASEMA ITAJIBU MAPIGO

- Imeyapuuza madai ya Trump kuwa alisitisha shambulizi dhidi yake kwa hofu ya kusababisha idadi kubwa ya vifo

- Pia, haitovumilia uvamizi katika eneo lake na hivyo kukabiliana na hatari yoyote

Zaidi, soma https://jamii.app/IranYampuuzaTrump
AFCON-2019: Timu ya Taifa ya Nigeria imefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Burundi katika mchezo wa kwanza wa kundi B

- Nigeria sasa inaongoza kundi huku ikisubiri matokeo ya mchezo baina ya Guinea na Madagascar utakaoanza saa 5:00 usiku huu
ETHIOPIA: MKUU WA MAJESHI APIGWA RISASI KATIKA JARIBIO LA MAPINDUZI

- Waziri Mkuu wa nchi hiyo ameongea hayo huku akikemea jaribio hilo la Mapinduzi lililotokea huko Amhara

- Hali ya Mkuu wa Majeshi kwa sasa bado haifahamiki

Soma https://jamii.app/EthiopiaCoupAttempt
GEITA: MAMA ADAIWA KUMCHINJA MTOTO WAKE NA KUMPIKA

- Ni Happiness Shadrack(36) mwenye tatizo la akili, amemchinja mtoto wake wa mwaka mmoja

- Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Kamishna Msaidizi Dismas Kisusi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo

Soma https://jamii.app/MamaAmchinjaMtoto
GEITA: WANAFUNZI 6 WA MIAKA 13-16 WAKUTWA WAKIISHI KINYUMBA

- Ni Wanafunzi wa kike wa darasa la 7 wa Shule ya msingi Nyamalele wenye miaka 13 na wa kiume wenye miaka 16 wa Shule ya Sekondari Nkome

- Watoto wa kike walitoroka nyumbani kwao na kwenda kuishi na watoto hao wa kiume

Zaidi, soma https://jamii.app/WatotoWaishiKinyumba
ETHIOPIA: MKUU WA MAJESHI AFARIKI KWA KUPIGWA RISASI KWENYE JARIBIO LA MAPINDUZI

- Seare Mekonnen amefariki dunia baada ya kupigwa risasi na mlinzi huko Addis Ababa

- Rais wa Mkoa wa Amhara na Mshauri Mkuu pia wamefariki kwenye tukio hilo

Soma https://jamii.app/EthiopiaCoupAttempt
AFCON2019: Morocco imefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Namibia katika mchezo wa Kundi D na kufanikiwa kuongoza kundi hilo

- Timu nyingine katika kundi hilo za Ivory Coast na South Africa zinashuka dimbani kuchuana kesho saa 11:30 jioni
AFCON2019: Mtanange unaofuta saa mbili usiku na kusubiriwa kwa hamu na Watanzania ni kati ya timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ na Senegal

- Ni mchezo wa kwanza wa kundi C huku mchezo wa 2 katika kundi hilo kati ya Algeria na Kenya ukipigwa saa 5:00 usiku huu