JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KENYA: MWANAFUNZI AMUUA MWENZAKE KISA MVULANA

- Mwanafunzi wa Kidato cha 4, Juni 21 anadaiwa kumchoma kwa kitu chenye ncha, Mwanafunzi wa darasa la 8 huko Lukose, Kakamega

- Alikuwa akimtuhumu wa darasa la 8 kumchukulia 'Mchumba' wake

Zaidi, soma https://jamii.app/StudentKillsAnother-KE
INDIA: WATU 14 WAFARIKI BAADA YA KUANGUKIWA NA HEMA KUBWA

- Watu wengine 50 wamejeruhiwa katika tukio hilo hapo jana Juni 23 Wilayani Barmer katika jimbo la Rajasthan

- Hema hilo lilianguka kutokana na mvua kubwa na upepo mkali

Zaidi, soma https://jamii.app/TentCollapseKills14-India
POLISI 6 MBARONI KWA KUOMBA RUSHWA KWA MZEE WA MIAKA 95

> Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) Wilaya ya Igunga inawachunguza askari Polisi wa Kituo cha Igunga kwa tuhuma za kuomba rushwa ya Tsh. milioni 8 Ngaka Mataluma ili wasimpeleke kituoni

Soma - https://jamii.app/PolisiMadaiRushwa
KISUTU: MAHAKAMA YAMUONYA WEMA. YAMREJESHEA DHAMANA

- Wema Sepetu(30) ameonywa kutokiuka masharti ya dhamana, vinginevyo Mahakama itamfutia dhamana

- Wema alikuwa rumande siku 7 hadi leo kutokana na kushindwa kufika Mahakamani bila taarifa

Zaidi, soma https://jamii.app/WemaAonywaDhamana
JEAN PIERRE BEMBA AREJEA RASMI DR CONGO

- Amerejea jana akitokea Brussels, Ubelgiji na kulakiwa na umati wa watu baada ya kukaa miezi 10 ugenini

- Inadaiwa amerudi kumsaidia mpinzani Martin Fayulu anayesisitiza kushinda Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2018

Zaidi, soma https://jamii.app/BembaArejeaCongo
TARIME: MWALIMU AMKATA MWANAFUNZI NA PANGA KICHWANI

> Jeshi la Polisi Mkoani Mara linamshikilia Mwalimu Kangoyi Marwa wa shule ya msingi Nyamumbara kwa tuhuma za kumjeruhi mwanafunzi wa darasa la tatu kwa kumkata panga kichwani

> Uongozi wa Halmashauri umemsimamisha kazi mwalimu huyo

Soma - https://jamii.app/MwlAmkataPangaMwf
MBUNGE AOMBA MUONGOZO JUU YA MADAI YA TAIFA STARS KUKATWA POSHO

> Mbunge wa Mbozi, Paschal Haonga(CHADEMA) amedai kuna tetesi kwamba wachezaji hao walitakiwa kupewa posho ya Dola 300 kwa siku lakini Serikali imewapa Dola 70

> Inadaiwa kuna mgomo wa kimyakimya katika timu hiyo na kuna siku wachezaji waligoma kufanya mazoezi

Soma - https://jamii.app/PoshoStarsAFCON
#JFMichezo
UBUNGO: ABIRIA AFARIKI NDANI YA BASI KABLA YA SAFARI KUANZA
-
Mwanaidi Said (83), aliyekuwa anasafiri kutoka Dar Es Salaaam kwenda Tabora, alifariki jana alfajiri na alikuwa akisumbuliwa na saratani

> Alikuwa anakwenda mkoani Tabora baada ya kumaliza matibabu yake hapa Dar

Soma - https://jamii.app/AbiriaAfarikiBasi
SAUDI ARABIA: UWANJA WA NDEGE WASHAMBULIWA, MMOJA AFARIKI

> Waasi wa Houthi wa nchini Yemen wameushambulia uwanja wa ndege wa Abha ulioko Kusini Magharibi mwa Saudi Arabia leo, Juni 24 na kusababisha kifo cha mtu mmoja huku wengine saba wakijeruhiwa

> Hata hivyo, mpaka sasa Serikali haijatoa tamko kuhusiana na shambulio hilo

Soma - https://jamii.app/ShambulioUwanjaNdege
TANZANIA YAPATIWA TSH. BILIONI 60 ZA MSAADA NA CHINA

- Imepatiwa fedha hizo bila masharti yoyote na itaamua matumizi yake katika miradi ya maendeleo

- Baadhi ya maeneo ya kipaumbele ni ujenzi wa mabwawa ya umeme ya Ruhudji na Rumakali

Zaidi, soma https://jamii.app/ChinaTanzania-Bilioni60
NDUGAI: LISHE DUNI IMECHANGIA TAIFA STARS KUFUNGWA

> Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema miongoni mwa sababu iliyochangia timu ya Taifa kupoteza mchezo wa kwanza jana kwenye michuano ya AFCON dhidi ya Senegal ni lishe duni ya wachezaji wetu

> Amesema viongozi wengi wa soka na michezo mingine hapa nchini siyo watu sahihi wa kuongoza

Soma - https://jamii.app/NdugaiMpiraStars
#JFMichezo
AFCON2019: Timu ya Taifa ya Ivory Coast imefanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya timu ya Taifa ya South Afrika katika mchezo wa pili wa Kundi D

- Kwa matokeo hayo Ivory Coast inaongoza katika Kundi D lakini ikiwa na alama 3 sawa na Morocco iliyo nafasi ya pili
BAADHI YA MAMBO YANAYODAIWA KUWEPO KWENYE SAIKOLOJIA YA MAPENZI

> Ni ngumu kubaki na hasira kwa mtu unayempenda kwa dhati kwasababu hasira zinazoishi hadi kufikia siku tatu zinadhibitisha kuwa hakuna mapenzi ya dhati baina ya wapenzi hao

> Mapenzi huwa yanaacha kumbukumbu ambayo ni ngumu kwa mtu mwingine kuifuta, vilevile huacha maumivu ambayo ni ngumu kwa mwingine kuyatibu

Una maoni gani kuhusu madai haya?

Tembelea zaidi - https://jamii.app/SaikolojiaMapenzi
#JFMahusiano
IRAN: SHAMBULIO LA KIMTANDAO LA MAREKANI HALIKUFANIKIWA

- Imesema mashambulio hayo yaliyofanywa dhidi ya mifumo yake ya kufyetulia makombora hayakufanikiwa

- Imesema mwaka 2018 imezuia mashambulizi Milioni 33 kama hayo na kuyaita ni ugaidi

Zaidi, soma https://jamii.app/IranShambulioMtandao-US
AFCON2019: Timu ya Tunisia imetoka sare ya goli 1-1 na timu ya Angola katika mchezo wa kwanza wa Kundi E katika dimba la Suez nchini Misri

- Mchezo unaofuata majira ya saa 5:00 usiku, saa za Afrika Mashariki ni katika ya Mali na Mauritania ambazo zote zipo Kundi E
TRUMP AMUWEKEA KIONGOZI WA DINI WA IRAN VIKWAZO

- Ameiwekea Iran vikwazo vipya vikali ikiwemo Ofisi ya Kiongozi Mkuu wa dini, Ali Khamenei

- Iran imesema Marekani haipendi diplomasia na kuushutumu utawala wa Trump kwa kuwa na kiu ya vita

Zaidi, soma https://jamii.app/VikwazoKiongoziDini-Iran
TABORA: MKUU WA MKOA AMSIMAMISHA KAZI MENEJA WA TRA, IGUNGA

- Aggrey Mwanri amemsimamisha kazi, John Mgeni ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za rushwa zinazomkabili

- Inadaiwa alidai Mfanyabiashara mmoja rushwa ya Tsh. Milioni 2

Zaidi, soma https://jamii.app/MenejaTRAIgunga
UGANDA YAPINGA MAHAKAMA YA EAC KUAMUA KUHUSU UKOMO WA MIAKA YA URAIS

> Serikali ya Uganda imesema Mahakama ya Afrika Mashariki iliyoko Arusha, haina mamlaka ya kusikiliza kesi kuhusu kipengele cha umri wa Rais

> Kesi hiyo ilipelekwa na wanaharakati wakitaka ibatilishe uamuzi wa Mahakama ya Katiba iliyokubaliana na Bunge kuondolewa kwa ukomo wa umri wa mtu kuwania urais mwezi Aprili 2019

Soma - https://jamii.app/UGVsEACCourt
#JFInternational
HARRY MAGUIRE AGOMBANIWA NA MANCHESTER UNITED NA MANCHESTER CITY

- Inadaiwa beki huyo wa Leicester City yupo tayari kujiunga na Man. City na 'kuitosa' Man. Utd

- Inadaiwa United ipo tayari kulipa ada ya Tsh. 234,597,076,000 lakini yeye anataka kujiunga na Man. City
IRINGA: WATUMISHI 2 WA TARURA MKOANI SONGWE WAFARIKI AJALINI

- Wengine 3 wamejeruhi katika ajali hiyo iliyotokea maeneo ya Izazi katika barabara kuu ya Iringa-Dodoma

- Gari lao limegongana na lori lililohama upande baada ya kumshinda dereva

Zaidi, soma https://jamii.app/AjaliTARURASongwe-IRN