JamiiForums
55.8K subscribers
33.1K photos
1.94K videos
30.2K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
ETHIOPIA: PIKIPIKI ZAPIGWA MARUFUKU ADDIS ABABA

> Matumizi ya usafiri huo yamepigwa marufuku na Serikali kutokana na kukithiri kwa matukio ya wizi na makosa ya jinai

> Watakaoruhusiwa kutumia usafiri huo ni watumishi wa misheni na shirika la Posta

Soma > https://jamii.app/Pikipiki-AddisAbaba
DAR: ALIYEKAMATWA KWA KUSAFIRISHA DHAHABU AFIKISHWA MAHAKAMANI

> Mirajdin Tajdin mwenye umri wa miaka 32, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashtaka hayo

> Mtuhumiwa amekiri kutenda kosa hilo

Zaidi, soma => https://jamii.app/KusafirishaDhahabu
ARUSHA: WAFANYABIASHARA WAFUNGA MADUKA, WAANDAMANA KUPINGA UWEPO WA MACHINGA

> Wafanyabiashara wa eneo la Ranger Safari, wamefunga maduka yao na kuandamana wakishinikiza kuondolewa kwa machinga wanaopanga biashara mbele ya maduka yao

Zaidi, soma => https://jamii.app/MadukaYafungwaArusha
MISRI: UTEPE WA MICHUANO YA AFCON KUKATWA LEO

> Fainali hizo ni za 32 tangu michuano hiyo iasisiwe

> Mataifa ya Afrika 24 yanatarajiwa kushiriki ikiwa ni mara ya kwanza kihistoria michuano hiyo kuwa na idadi hiyo ya washiriki

Zaidi, soma => https://jamii.app/AfconMisriLeo
MPANDA, KATAVI: AJINYONGA KWA MADAI KUWA DAWA ZA KUZUIA ASIFE ZIMEISHA NGUVU

> Aliyejinyonga ni Juma Sadi mwenye umri wa miaka 50

> Alimueleza Shemeji yake kuwa alimeza vipande 3 vya dawa aina ya mpigi lakini amevitapika hivyo lazima afe

Zaidi, soma > https://jamii.app/AjinyongaKatavi
PETR CECH AREJEA CHELSEA KAMA MSHAURI WA MASUALA YA KIUFUNDI NA UTENDAJI

- Cech aliyestaafu kucheza soka mwezi Mei mwaka huu, amerejea Stamford Bridge ikiwa ni miaka minne tangu aondoke na kujiunga Arsenal

- Atafanya kazi kwa karibu na timu ya Wanaume na benchi la ufundi
VIPIMO VYA DENGUE KUTOLEWA BURE KWENYE VITUO VYA AFYA VYA UMMA

- Serikali imesema kuwa vipimo hivyo vitatolewa bure wakati huu wa mlipuko

- Aidha, tangu Januari hadi Juni 19 mwaka huu, wagonjwa 4,320 na vifo vinne vimetolewa taarifa

Zaidi, soma https://jamii.app/VipimoDengueBure
RAIS TRUMP ASITISHA KUTAKA KUISHAMBULIA IRAN

- Amesitisha hatua ya kuishambulia Iran muda mfupi baada ya kutoa idhini ya kufanya hivyo kujibu shambulio la Iran lililoidungua na kuiangusha ndege ya Jeshi la Marekani isiyo na rubani

Zaidi, soma https://jamii.app/TrumpAsitishaKuchambuliaIran
WAMILIKI WA VIWANJA ENEO LA PEMBA MNAZI WATAKIWA KULIPA

- Waliopewa viwanja eneo la Pemba Mnazi, Kigamboni wanatakiwa kukamilisha malipo kabla ya Julai 31, 2019

- Watakaoshindwa kulipa, viwanja vyao vitagawiwa kwa waombaji wengine bila taarifa yoyote

Zaidi, soma https://jamii.app/WamilikiViwanjaPembaMnazi
VURUGU ZAIBUKA KATIKA BARABARA YA KAJIADO-NAMANGA, WAFANYABIASHARA WAKIPIGANA

- Usafiri katika barabara hiyo ulisimama baada ya Wafanyabiashara wa Mchanga kufunga barabara

- Vurugu zimetokea kufuatia Wachimba mchanga kutoka Purko kutakiwa kutotumia soko la Ilbisil

Zaidi, soma https://jamii.app/ChaosKajiado-NamangaRoad
ANAYEDAIWA 'KUMTUSI' RAIS MUSEVENI AKUTWA NA KESI YA KUJIBU

- Mwanaharakati na Mtafiti wa Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda, Dkt. Stella Nyanzi anadaiwa kutumia ukurasa wake wa Facebook kuandika maneno machafu kwa Rais na marehemu mamaye

Zaidi, soma https://jamii.app/StellaNyanziKesiKujibu-UG
DAR: RAIA WA NIGERIA AHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 30

- Mahakama ya Mafisadi imemuhukumu Christian Ugbechi baada ya kukutwa na hatia ya kusafirisha kete 56 za #DawaZaKulevya aina ya Heroin Hydrochloride zenye uzito wa gramu 947.57

Zaidi, soma https://jamii.app/MnigeriaMiaka30-TZ
ARUSHA: HOTEL YA KITALII YA SNOWCREST YAFILISIWA

- Ni baada ya kushindwa kujiendesha kutokana na madeni makubwa inayodaiwa yanayofikia Tsh. Bilioni 14

- Kampuni ya udalali ilifika hotelini hapo na kuchukua kila kitu kilichokuwepo ndani

Zaidi, soma https://jamii.app/HoteliSnowcrestYafilisiwa-AR
MAHUSIANO: WAKWE ZANGU WAMEHAMIA NYUMBANI KWANGU, NIMECHOKA VIKAO

> Wazazi wa Mke wangu walikuja Dar kututembelea na ilikuwa wakae kwa muda wa mwezi mmoja lakini cha kushangaza wanakuwa kama wamehamia

> Napata changamoto nyingi ikiwemo Baba Mkwe kutoa amri ndani ya nyumba yangu

Zaidi, soma > https://jamii.app/KeroYaWakwe
NDEGE ZA KIMATAIFA ZAEPUKA ANGA LA IRAN

- Ni baada ya ndege ya Marekani isiyokuwa na rubani kudunguliwa na Iran

- Ndege hizo ni za Mashirika ya Cathay Pacific, Emirates, FlyDubai, British Airways, KLM, Qantas, Singapore Airlines na Lufthansa

Zaidi, soma https://jamii.app/NdegeKimataifaAngaIran
TETESI ZA SOKA: Gazeti la Tuttosport la Italia limedai kuwa Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba amempigia simu Kocha mpya wa Juventus, Maurizio Sarri kumshawishi amsajili

- Aidha, inadaiwa kuwa Manchester United inataka kumpa mkataba wa mnono wa miaka mitano wa thamani ya Paundi 350,000(Tsh. 1,024,788,755) kwa wiki, Kipa wake David De Gea
HAWAII: NDEGE YAANGUKA YAUA WATU WOTE 9 WALIOKUWEMO NDANI

- Imeanguka na kuwaka moto karibu na Uwanja wa ndege wa Dillingham huko Oahu, Honolulu

- Haijaeleweka sababu za ndege hiyo kuanguka na kama ilikuwa inatua au kupaa katika uwanja huo

Zaidi, soma https://jamii.app/HawaiiPlaneKills9
SHINYANGA: MUME MBARONI AKITUHUMIWA KUMUUA ALIYEMFUMANIA NA MKEWE

- Rafael Martine(34) anatuhumiwa kumuua Shija Mahoiga(45) baada ya kumfumania akiwa amelala na mkewe

- Anatuhumumiwa kumshambulia marehemu kwa kipande cha chuma

Zaidi, soma https://jamii.app/AmuuaAliyemfumania-SHY
BUKOMBE, GEITA: AFISA MTENDAJI AFARIKI KWA KUSHAMBULIWA NA WASIOJULIKANA

- Ni Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Ibambilo, Kata ya Bulega, Juma Maziku

- Amefariki baada ya kuokotwa kwenye barabara iendayo Mnekesi, Chato akiwa na majeraha mwilini

Zaidi, soma https://jamii.app/AfisaMtendajiAuawa-GIT
IRAN YAMPUUZA TRUMP, YASEMA ITAJIBU MAPIGO

- Imeyapuuza madai ya Trump kuwa alisitisha shambulizi dhidi yake kwa hofu ya kusababisha idadi kubwa ya vifo

- Pia, haitovumilia uvamizi katika eneo lake na hivyo kukabiliana na hatari yoyote

Zaidi, soma https://jamii.app/IranYampuuzaTrump