JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
AFCON-2019: Timu ya Taifa ya Nigeria imefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Burundi katika mchezo wa kwanza wa kundi B

- Nigeria sasa inaongoza kundi huku ikisubiri matokeo ya mchezo baina ya Guinea na Madagascar utakaoanza saa 5:00 usiku huu
ETHIOPIA: MKUU WA MAJESHI APIGWA RISASI KATIKA JARIBIO LA MAPINDUZI

- Waziri Mkuu wa nchi hiyo ameongea hayo huku akikemea jaribio hilo la Mapinduzi lililotokea huko Amhara

- Hali ya Mkuu wa Majeshi kwa sasa bado haifahamiki

Soma https://jamii.app/EthiopiaCoupAttempt
GEITA: MAMA ADAIWA KUMCHINJA MTOTO WAKE NA KUMPIKA

- Ni Happiness Shadrack(36) mwenye tatizo la akili, amemchinja mtoto wake wa mwaka mmoja

- Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Kamishna Msaidizi Dismas Kisusi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo

Soma https://jamii.app/MamaAmchinjaMtoto
GEITA: WANAFUNZI 6 WA MIAKA 13-16 WAKUTWA WAKIISHI KINYUMBA

- Ni Wanafunzi wa kike wa darasa la 7 wa Shule ya msingi Nyamalele wenye miaka 13 na wa kiume wenye miaka 16 wa Shule ya Sekondari Nkome

- Watoto wa kike walitoroka nyumbani kwao na kwenda kuishi na watoto hao wa kiume

Zaidi, soma https://jamii.app/WatotoWaishiKinyumba
ETHIOPIA: MKUU WA MAJESHI AFARIKI KWA KUPIGWA RISASI KWENYE JARIBIO LA MAPINDUZI

- Seare Mekonnen amefariki dunia baada ya kupigwa risasi na mlinzi huko Addis Ababa

- Rais wa Mkoa wa Amhara na Mshauri Mkuu pia wamefariki kwenye tukio hilo

Soma https://jamii.app/EthiopiaCoupAttempt
AFCON2019: Morocco imefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Namibia katika mchezo wa Kundi D na kufanikiwa kuongoza kundi hilo

- Timu nyingine katika kundi hilo za Ivory Coast na South Africa zinashuka dimbani kuchuana kesho saa 11:30 jioni
AFCON2019: Mtanange unaofuta saa mbili usiku na kusubiriwa kwa hamu na Watanzania ni kati ya timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ na Senegal

- Ni mchezo wa kwanza wa kundi C huku mchezo wa 2 katika kundi hilo kati ya Algeria na Kenya ukipigwa saa 5:00 usiku huu
KENYA: MWANAFUNZI AMUUA MWENZAKE KISA MVULANA

- Mwanafunzi wa Kidato cha 4, Juni 21 anadaiwa kumchoma kwa kitu chenye ncha, Mwanafunzi wa darasa la 8 huko Lukose, Kakamega

- Alikuwa akimtuhumu wa darasa la 8 kumchukulia 'Mchumba' wake

Zaidi, soma https://jamii.app/StudentKillsAnother-KE
INDIA: WATU 14 WAFARIKI BAADA YA KUANGUKIWA NA HEMA KUBWA

- Watu wengine 50 wamejeruhiwa katika tukio hilo hapo jana Juni 23 Wilayani Barmer katika jimbo la Rajasthan

- Hema hilo lilianguka kutokana na mvua kubwa na upepo mkali

Zaidi, soma https://jamii.app/TentCollapseKills14-India
POLISI 6 MBARONI KWA KUOMBA RUSHWA KWA MZEE WA MIAKA 95

> Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) Wilaya ya Igunga inawachunguza askari Polisi wa Kituo cha Igunga kwa tuhuma za kuomba rushwa ya Tsh. milioni 8 Ngaka Mataluma ili wasimpeleke kituoni

Soma - https://jamii.app/PolisiMadaiRushwa
KISUTU: MAHAKAMA YAMUONYA WEMA. YAMREJESHEA DHAMANA

- Wema Sepetu(30) ameonywa kutokiuka masharti ya dhamana, vinginevyo Mahakama itamfutia dhamana

- Wema alikuwa rumande siku 7 hadi leo kutokana na kushindwa kufika Mahakamani bila taarifa

Zaidi, soma https://jamii.app/WemaAonywaDhamana
JEAN PIERRE BEMBA AREJEA RASMI DR CONGO

- Amerejea jana akitokea Brussels, Ubelgiji na kulakiwa na umati wa watu baada ya kukaa miezi 10 ugenini

- Inadaiwa amerudi kumsaidia mpinzani Martin Fayulu anayesisitiza kushinda Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2018

Zaidi, soma https://jamii.app/BembaArejeaCongo
TARIME: MWALIMU AMKATA MWANAFUNZI NA PANGA KICHWANI

> Jeshi la Polisi Mkoani Mara linamshikilia Mwalimu Kangoyi Marwa wa shule ya msingi Nyamumbara kwa tuhuma za kumjeruhi mwanafunzi wa darasa la tatu kwa kumkata panga kichwani

> Uongozi wa Halmashauri umemsimamisha kazi mwalimu huyo

Soma - https://jamii.app/MwlAmkataPangaMwf
MBUNGE AOMBA MUONGOZO JUU YA MADAI YA TAIFA STARS KUKATWA POSHO

> Mbunge wa Mbozi, Paschal Haonga(CHADEMA) amedai kuna tetesi kwamba wachezaji hao walitakiwa kupewa posho ya Dola 300 kwa siku lakini Serikali imewapa Dola 70

> Inadaiwa kuna mgomo wa kimyakimya katika timu hiyo na kuna siku wachezaji waligoma kufanya mazoezi

Soma - https://jamii.app/PoshoStarsAFCON
#JFMichezo
UBUNGO: ABIRIA AFARIKI NDANI YA BASI KABLA YA SAFARI KUANZA
-
Mwanaidi Said (83), aliyekuwa anasafiri kutoka Dar Es Salaaam kwenda Tabora, alifariki jana alfajiri na alikuwa akisumbuliwa na saratani

> Alikuwa anakwenda mkoani Tabora baada ya kumaliza matibabu yake hapa Dar

Soma - https://jamii.app/AbiriaAfarikiBasi
SAUDI ARABIA: UWANJA WA NDEGE WASHAMBULIWA, MMOJA AFARIKI

> Waasi wa Houthi wa nchini Yemen wameushambulia uwanja wa ndege wa Abha ulioko Kusini Magharibi mwa Saudi Arabia leo, Juni 24 na kusababisha kifo cha mtu mmoja huku wengine saba wakijeruhiwa

> Hata hivyo, mpaka sasa Serikali haijatoa tamko kuhusiana na shambulio hilo

Soma - https://jamii.app/ShambulioUwanjaNdege
TANZANIA YAPATIWA TSH. BILIONI 60 ZA MSAADA NA CHINA

- Imepatiwa fedha hizo bila masharti yoyote na itaamua matumizi yake katika miradi ya maendeleo

- Baadhi ya maeneo ya kipaumbele ni ujenzi wa mabwawa ya umeme ya Ruhudji na Rumakali

Zaidi, soma https://jamii.app/ChinaTanzania-Bilioni60
NDUGAI: LISHE DUNI IMECHANGIA TAIFA STARS KUFUNGWA

> Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema miongoni mwa sababu iliyochangia timu ya Taifa kupoteza mchezo wa kwanza jana kwenye michuano ya AFCON dhidi ya Senegal ni lishe duni ya wachezaji wetu

> Amesema viongozi wengi wa soka na michezo mingine hapa nchini siyo watu sahihi wa kuongoza

Soma - https://jamii.app/NdugaiMpiraStars
#JFMichezo
AFCON2019: Timu ya Taifa ya Ivory Coast imefanikiwa kupata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya timu ya Taifa ya South Afrika katika mchezo wa pili wa Kundi D

- Kwa matokeo hayo Ivory Coast inaongoza katika Kundi D lakini ikiwa na alama 3 sawa na Morocco iliyo nafasi ya pili
BAADHI YA MAMBO YANAYODAIWA KUWEPO KWENYE SAIKOLOJIA YA MAPENZI

> Ni ngumu kubaki na hasira kwa mtu unayempenda kwa dhati kwasababu hasira zinazoishi hadi kufikia siku tatu zinadhibitisha kuwa hakuna mapenzi ya dhati baina ya wapenzi hao

> Mapenzi huwa yanaacha kumbukumbu ambayo ni ngumu kwa mtu mwingine kuifuta, vilevile huacha maumivu ambayo ni ngumu kwa mwingine kuyatibu

Una maoni gani kuhusu madai haya?

Tembelea zaidi - https://jamii.app/SaikolojiaMapenzi
#JFMahusiano