JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
RAIS MAGUFULI KUONGOZA KONGAMANO LA KOROSHO, MTWARA

- Anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kongamano hilo litakalofanyikia Julai 12 na 13 mwaka huu

- Lengo la kongamano ni kuwavutia Wawekezaji waanzishe miradi na viwanda vya kusindika korosho

Zaidi, soma https://jamii.app/MagufuliKongamanoKorosho
JESHI LA POLISI: TAARIFA ZA TISHIO LA SHAMBULIO DAR, TUNAZIFANYIA KAZI

> Jeshi la Polisi limesema kuwa taarifa hizo wanazo na wanaendelea kuzifanyia kazi

> Mussa Taibu, RPC Kinondoni amewataka Wananchi kutoa taarifa za viashiria vya hatari

Zaidi, soma => https://jamii.app/PolisiOnyoShambulioDar
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
MAKONDA: DAR NI SHWARI, WANANCHI MSIWE NA HOFU

- Baada ya Tahadhari ya Usalama katika Jiji la Dar iliyotolewa na Ubalozini wa Marekani, RC wa Dar, Paul Makonda amewahakikishia Wananchi kuwa hali ni shwari

- Aidha, ameomba watoa taarifa kuzigatia sheria, Kanuni na Katiba ya nchi kwani kuna vyombo maalumu vilivyopewa mamlaka ya kutangaza hali ya hatari
KENYA: MTANZANIA AKUTWA NA HATIA KATIKA MAKOSA YA UGAIDI

- Rashid Mberesero mwenyeji wa Kilimanjaro na Wakenya wawili wamekutwa na hatia ya kutekeleza shambulio la kigaidi mwaka 2015 katika Chuo Kikuu cha Garissa, Kenya na kuua Wanafunzi 148

Zaidi, soma https://jamii.app/MtanzaniaHatianiUgaidi-KE
MWANZA: AJITEKETEZA KWA MOTO BAADA YA KUMUUA MPENZI WAKE

> Fungi Mayala adaiwa kujichoma kwa moto baada ya kumuua mpenzi wake kwa kumkata kwa panga

> Inaelezwa kuwa alikuwa katika ugomvi na mpenzi wake ambaye alimshitaki na kesi iko Mahakamani

Soma > https://jamii.app/AjichomaMotoMwanza
KENYA: WAPENZI WA JINSIA MOJA WALIOTOROKA KAMBI YA WAKIMBIZI KAKUMA WARUDISHWA

> Walitoroka katika kambi hiyo ya Kakuma kwa madai kuwa walikuwa walengwa wa matukio ya ubaguzi dhidi yao, wamekamatwa Nairobi na wamerudishwa katika kambi hiyo

Soma => https://jamii.app/LGBTQKakuma
MICHEZO: MSHAMBULIAJI WA KLABU YA MBEYA CITY ASAJILIWA NA TP MAZEMBE

> Eliud Ambokile mchezaji wa nafasi ya ushambuliaji amesajiliwa na TP Mazembe ya DRC kwa dau la shilingi milioni 50

> Aliifungia Mbeya City magoli 10 katika mzunguko wa kwanza wa ligi

Soma > https://jamii.app/AmbokileTPMazembe
SERIKALI YASHAURIWA KUFUTA TOZO YA MAITI

- Mbunge wa Kahama, Jumanne Kishimba ameishauri Serikali kufuta tozo hiyo kwenye chumba cha kuhifadhia maiti hospitalini(Mortuary)

- Amesema kutokana tozo hizo, ndugu wengi hukwepa kuchukua maiti

Zaidi, soma https://jamii.app/TozoMaitiIfutwe
KENYA: ALIYEKUWA MGOMBEA URAIS KENYA AKAMATWA AKISAFIRISHA BANGI

- Jaffer Isaak Sora aliyekuwa anagombea Urais Kenya mwaka 2017, alikuwa akisafirisha Kilo 445 za bangi kwenye gari lake

- Polisi wanasema bangi hizo zinadhaniwa zimetoka Ethiopia

Zaidi, soma https://jamii.app/JafferSoraArrested-KE
KAIMU BALOZI WA MAREKANI AITWA WIZARA YA MAMBO YA NJE

> Wito huu umetokana na taarifa ya tahadhari ya kiusalama iliyotolewa na Ubalozi huo ikieleza juu ya uwepo wa dalili za kutokea kwa shambulio katika mitaa ya Msasani Jijini, Dar

Zaidi, soma => https://jamii.app/USAvsTZ-UsalamaTZ
UGANDA: MZEE WA MIAKA 70 AKAMATWA KWA KULIPIGA MAWE GARI LA RAIS MUSEVENI

> Mzee Omar Risasi Amabua anatuhumiwa kwa kulipiga mawe gari la Rais Museveni likiwa kwenye msafara mwishoni mwaka jana

> Atashtakiwa kwa makosa ya uhaini

Zaidi, soma => https://jamii.app/Mzee70ApigaGariMuseveni
INDIA: JOTO LAZIDI KUONGEZEKA, WATU 92 WAFARIKI

- Vifo vingi vimetokea katika Jimbo la Bahir hasa katika maeneo ya Aurangabad, Gaya na Nawada, ambapo joto limefikia jotoridi 45

- Aidha, Watu 562 wamelazwa na kuongeza hofu ya vifo kuongezeka

Zaidi, soma https://jamii.app/IndianHeatwaveKills92
TAHADHARI: UBALOZI WA MAREKANI UGANDA WATOA ONYO LA SHAMBULIO

- Umesema kuna uvumi wa shambulio katika maeneo yanayopendwa kutembelewa na raia wa kigeni Afrika Mashariki ikiwemo Uganda

- Japo umesema hauna ushahidi wa kutosha, umewaonya Wakazi kuchukua tahadhari

Zaidi, soma https://jamii.app/TahadhariShambulioUganda
ETHIOPIA: PIKIPIKI ZAPIGWA MARUFUKU ADDIS ABABA

> Matumizi ya usafiri huo yamepigwa marufuku na Serikali kutokana na kukithiri kwa matukio ya wizi na makosa ya jinai

> Watakaoruhusiwa kutumia usafiri huo ni watumishi wa misheni na shirika la Posta

Soma > https://jamii.app/Pikipiki-AddisAbaba
DAR: ALIYEKAMATWA KWA KUSAFIRISHA DHAHABU AFIKISHWA MAHAKAMANI

> Mirajdin Tajdin mwenye umri wa miaka 32, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, akikabiliwa na mashtaka hayo

> Mtuhumiwa amekiri kutenda kosa hilo

Zaidi, soma => https://jamii.app/KusafirishaDhahabu
ARUSHA: WAFANYABIASHARA WAFUNGA MADUKA, WAANDAMANA KUPINGA UWEPO WA MACHINGA

> Wafanyabiashara wa eneo la Ranger Safari, wamefunga maduka yao na kuandamana wakishinikiza kuondolewa kwa machinga wanaopanga biashara mbele ya maduka yao

Zaidi, soma => https://jamii.app/MadukaYafungwaArusha
MISRI: UTEPE WA MICHUANO YA AFCON KUKATWA LEO

> Fainali hizo ni za 32 tangu michuano hiyo iasisiwe

> Mataifa ya Afrika 24 yanatarajiwa kushiriki ikiwa ni mara ya kwanza kihistoria michuano hiyo kuwa na idadi hiyo ya washiriki

Zaidi, soma => https://jamii.app/AfconMisriLeo
MPANDA, KATAVI: AJINYONGA KWA MADAI KUWA DAWA ZA KUZUIA ASIFE ZIMEISHA NGUVU

> Aliyejinyonga ni Juma Sadi mwenye umri wa miaka 50

> Alimueleza Shemeji yake kuwa alimeza vipande 3 vya dawa aina ya mpigi lakini amevitapika hivyo lazima afe

Zaidi, soma > https://jamii.app/AjinyongaKatavi
PETR CECH AREJEA CHELSEA KAMA MSHAURI WA MASUALA YA KIUFUNDI NA UTENDAJI

- Cech aliyestaafu kucheza soka mwezi Mei mwaka huu, amerejea Stamford Bridge ikiwa ni miaka minne tangu aondoke na kujiunga Arsenal

- Atafanya kazi kwa karibu na timu ya Wanaume na benchi la ufundi
VIPIMO VYA DENGUE KUTOLEWA BURE KWENYE VITUO VYA AFYA VYA UMMA

- Serikali imesema kuwa vipimo hivyo vitatolewa bure wakati huu wa mlipuko

- Aidha, tangu Januari hadi Juni 19 mwaka huu, wagonjwa 4,320 na vifo vinne vimetolewa taarifa

Zaidi, soma https://jamii.app/VipimoDengueBure