JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
WATATU MBARONI KWA KUHUSIKA NA MAUAJI YA KATIBU WA CHADEMA

> Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linawashikilia watu 3 kwa tuhuma za kumuua Katibu mwenezi wa CHADEMA Wilaya ya Malinyi, Lucas Lihambalimu (42)

> Uchunguzi uliofanywa umebaini chanzo cha mauaji kuwa ni mgogoro wa mashamba

Soma - https://jamii.app/3MbaroniMauajiCDM
YEMEN: WATOTO WACHANGA 6 HUFARIKI KILA BAADA YA SAA MBILI

> Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto limesema tangu kuongezeka kwa mapigano, vifo wakati wa kujifunga vimeongezeka kutoka vifo 5 kwa siku mwaka 2013 na kufikia 12 kwa siku mwaka 2018

Soma - https://jamii.app/VifoVichangaWajawazito
HONG KONG: MUSWADA WA SHERIA WASITISHWA KUFUATIA MAANDAMANO

> Serikali inayoongoza Jimbo hilo imetangaza kusitisha muswada uliolenga kuruhusu watuhumiwa wa makosa mbalimbali kushtakiwa China

> Hong Kong ni Jimbo la China lenye mamlaka yake

Soma => https://jamii.app/MuswadaHongKong
KYELA, MBEYA: WATU ZAIDI YA 10 WAJERUHIWA KATIKA AJALI YA GARI

> Wamejeruhiwa katika ajali inayoelezwa kuwa imesababishwa na mwendokasi wa basi aina ya Coaster walilokuwa wakisafiria

> Ajali imetokea katika Kijiji cha Ikomelo mchana wa leo

Soma > https://jamii.app/AjaliKyela
HAPPY FATHER’S DAY: Leo ni Siku ya kusherekea, kuenzi na kutambua nafasi ya Baba kwenye maisha ya mtoto
-
Menejimenti na Wafanyakazi wa JamiiForums wanawatakia kina Baba wote Upendo na Amani kwenye siku hii muhimu
MOGADISHU: WATU 11 WAMEFARIKI NA 25 KUJERUHIWA KWENYE MILIPUKO

- Ni milipuko ya kujitoa muhanga iliyohusisha magari kwenye eneo la ukaguzi la Kasri ya Rais na eneo la ukaguzi la Uwanja wa Ndege

- Al-Shabab wamekiri kuhusika na milipuko hiyo

Soma https://jamii.app/MilipukoMogadishu
KOCHA WA CHELSEA, MAURIZIO SARRI AJIUNGA JUVENTUS

- Kocha huyo amejiunga na Juventus kwa kandarasi ya miaka 3 baada ya kukaa Chelsea kwa msimu mmoja

- Akiwa Chelsea, alifanikiwa kuchukua Kombe la Europa likiwa ndio taji lake kubwa katika maisha yake ya Ukocha
ISRAEL: MKE WA WAZIRI MKUU AHUKUMIWA KWA MATUMIZI MABAYA YA FEDHA ZA SERIKALI

- Sara Netanyahu amehukumiwa kulipa faini ya $15,000(Tsh. 34,582,500) baada ya kukutwa na hatia ya kutumia vibaya fedha za Serikali katika manunuzi ya chakula

Zaidi, soma https://jamii.app/SaraNetanyahuConvicted
INDIA YAONGEZA USHURU KWA BIDHAA ZA MAREKANI

- Imesema imeamua kuongeza ushuru kwa bidhaa 28 zinazoagizwa kutoka Marekani kuanzia jana

- Ni kutokana na Marekani kuongeza ushuru wa bidhaa za chuma na aluminium zinazoingizwa nchini humo

Zaidi, soma https://jamii.app/IndiaMarekaniUshuru
MTU MWENYE DALILI KAMA ZA EBOLA AONEKANA KENYA, MAMLAKA ZA AFYA ZACHUKUA TAHADHARI

- Dalili zimeonekana kwa Mwanamke mmoja aliyetoka Mabala, mpakani mwa Kenya na Uganda

- Amelazwa katika hospitali ya rufaa ya Kaunti ya Kericho tangu jana

Zaidi, soma https://jamii.app/SuspectedEbolaCase-KE
DR CONGO MASHARIKI: ENEO LENYE UTAJIRI WA MITI INAYOZALISHA DAWA AINA YA QUININE

> Jimbo la Kivu(Kusini na Kaskazini) linahifadhi kubwa ya miti aina ya Cinchona inayotumika kutengeneza dawa hizo

> Hata hivyo DRC ni Taifa la pili Duniani kwa vifo vya Malaria

Soma > https://jamii.app/QuinineDRC
MTAMBO WA MAJI WA RUVU JUU KUZIMWA

- Uzalishaji wa maji katika mtambo wa Ruvu Juu umesimamishwa kwa muda ili kuruhusu mafundi wa TANESCO na DAWASA kufanya maboresho

- Baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar na maeneo ya Mlandizi na Kibaha yatakosa maji

Zaidi, soma https://jamii.app/RuvuJuuKuzimwa-DAWASA
INDIA: MFANYAMAZINGAOMBWE APOTEA MTONI AKIJARIBU KUONESHA UJUZI

- Chanchal Lahiri aliyefungwa kwa minyororo na makufuli na kisha kutumbukizwa mtoni anaofiwa kufa hapo jana

- Alitakiwa kuibuka akiwa amejifungua minyororo hiyo lakini hakuibuka na hadi jana jioni alitafutwa bila mafanikio

Zaidi, soma https://jamii.app/MfanyamazingaombweAhofiwaKufa-IND
WEMA SEPETU KWENDA MAHABUSU KWA SIKU 7

- Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu imeamuru msanii huyo kukaa mahabusu akisubiri uamuzi wa dhamana baada ya kukiuka masharti

- Mara ya mwisho shauri hilo kusikilizwa, Mahakama iliamuru Wema akamatwe

Zaidi, soma https://jamii.app/WemaSepetuMahabusuSiku7
HUAWEI KUPATA HASARA YA DOLA BILIONI 30 KWA MIAKA 2 IJAYO

> CEO wa Huawei, Ren Zhengfei amesema kampuni hiyo anailaumu Marekani kwa kupinga biashara yake

> Amesema mauzo ya nje ya bidhaa za kampuni hiyo yameshuka kwa asilimia 40 kwa mwaka huu

Soma > https://jamii.app/HuaweiLoss
MWANAFUNZI CHUO KIKUU KIU AFARIKI BAADA YA KUSHAMBULIWA NA VIBAKA

> Aliyefariki ni Anifa Mgaya mwanafunzi wa Stashahada ya Maabara katika Chuo Kukuu cha Kampala tawi la Tanzania

> Alivamiwa na vibaka waliomjeruhi kwa kisu

Zaidi, soma https://jamii.app/RIPAnifaMgaya
NIGERIA: WATU 30 WAMEFARIKI KATIKA MASHAMBULIO MATATU YA BOMU

- Watu wengine 40 wamejeruhiwa katika milipuko hiyo iliyotokea nje ya ukumbi huko Konduga, Borno

- Katika ukumbi huo Mashabiki wa mpira walikuwa wakifuatilia mechi kupitia runinga

Zaidi, soma https://jamii.app/30WauawaNigeriabomu
KIRINYAGA, KENYA: AMCHOMA MKEWE KWA KUPIKA WALI BADALA YA KANDE

> Peter Ngugi(32) anashikiliwa na kwa kumjeruhi mkewe kwa kumwagia moto

> Alimuagiza Mkewe apike 'Githeri' (Kande) lakini Mkewe alipika wali

Zaidi, soma => https://jamii.app/AmchomaMkeweKE
TAASISI ZA KIDINI NA JUMUIYA ZA KIJAMII KUFUTIWA USAJILI ZISIPO HAKIKIWA

-Serikali inafanya uhakiki wa Jumuiya na Taasisi hizo nchi nzima ambapo awamu ya 2 itafanyika Dodoma, Morogoro, Singida na Manyara kuanzia Juni 23 hadi Julai 2 mwaka huu

Zaidi, soma https://jamii.app/TaasisiZisizohakikiwaKufutwa
RIPOTI: KIWANGO CHA SILAHA ZA NYUKLIA CHAPUNGUA DUNIANI

- Kituo cha Kimataifa cha Utafiti wa Amani kimesema kiwango kimepungua kwa silaha 800 katika nchi 9 katika kipindi cha mwaka mmoja ila Mataifa yanatengeneza silaha za kisasa zaidi

Zaidi, soma https://jamii.app/SilahaNyukliaZapungua