JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
WABUNGE 83 KUSAFIRI HADI MISRI KWENDA KUISHANGILIA TAIFA STARS

> Idadi hiyo ya Wabunge itakwenda nchini Misri kuiunga mkono timu ya Taifa katika mashindano ya AFCON 2019.

> Msafara huo utaongozwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai

Zaidi, soma => https://jamii.app/WabungeMisri
TUME YA SHERIA YAPENDEKEZA UWEPO WA SHERIA MOJA YA UFILISI

> Tume ya Kurekebisha Sheria imependekeza kutungwa kwa sheria moja baada ya kubaini baadhi ya zilizopo kupitwa na wakati na baadhi zinatoa adhabu au faini ndogo kwa wale wanaokiuka taratibu za ufilisi kama vile Tsh. 200 au Tsh. 1,000

Soma - https://jamii.app/UtafitiSheriaUfilisi
SUDAN KUSINI KUFUNGA BAADHI YA BALOZI ZAKE ILI KUBANA MATUMIZI

> Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje amesema kwamba Sudan Kusini imechukua hatua ya kuzifunga balozi zake katika nchi za Ufaransa, Norway, Ghana, Kuwait na Italia kutokana na kuzorota kwa uchumi na ukosefu wa utulivu wa kisiasa

Soma - https://jamii.app/FinancialCrisisSudan
#JFInternational
KYELA, MBEYA: POLISI ALIYEMPA UJAUZITO MWANAFUNZI ATOWEKA

> Konstebo Mlanda ametoroka baada ya kutuhumiwa kumbaka na kumpa ujauzito Mwanafunzi wa kidato cha kwanza mwenye miaka 14

> Mwanafunzi adai alibakwa kwa shinikizo la Mama yake mlezi

Soma > https://jamii.app/AskariAbakaKyela
MOROGORO: POLISI WAWAZUIA CHADEMA KUFANYA MKUTANO
-
Mkutano wa hadhara wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo uliokuwa ufanyike tarehe Juni 16, 2019 umefutwa na Jeshi la Polisi kwa sababu za kiusalama
-
Hata hivyo, inadaiwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wao wamepata kibali cha kufanya mkutano wao leo Mkoani humo
WATATU MBARONI KWA KUHUSIKA NA MAUAJI YA KATIBU WA CHADEMA

> Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linawashikilia watu 3 kwa tuhuma za kumuua Katibu mwenezi wa CHADEMA Wilaya ya Malinyi, Lucas Lihambalimu (42)

> Uchunguzi uliofanywa umebaini chanzo cha mauaji kuwa ni mgogoro wa mashamba

Soma - https://jamii.app/3MbaroniMauajiCDM
YEMEN: WATOTO WACHANGA 6 HUFARIKI KILA BAADA YA SAA MBILI

> Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto limesema tangu kuongezeka kwa mapigano, vifo wakati wa kujifunga vimeongezeka kutoka vifo 5 kwa siku mwaka 2013 na kufikia 12 kwa siku mwaka 2018

Soma - https://jamii.app/VifoVichangaWajawazito
HONG KONG: MUSWADA WA SHERIA WASITISHWA KUFUATIA MAANDAMANO

> Serikali inayoongoza Jimbo hilo imetangaza kusitisha muswada uliolenga kuruhusu watuhumiwa wa makosa mbalimbali kushtakiwa China

> Hong Kong ni Jimbo la China lenye mamlaka yake

Soma => https://jamii.app/MuswadaHongKong
KYELA, MBEYA: WATU ZAIDI YA 10 WAJERUHIWA KATIKA AJALI YA GARI

> Wamejeruhiwa katika ajali inayoelezwa kuwa imesababishwa na mwendokasi wa basi aina ya Coaster walilokuwa wakisafiria

> Ajali imetokea katika Kijiji cha Ikomelo mchana wa leo

Soma > https://jamii.app/AjaliKyela
HAPPY FATHER’S DAY: Leo ni Siku ya kusherekea, kuenzi na kutambua nafasi ya Baba kwenye maisha ya mtoto
-
Menejimenti na Wafanyakazi wa JamiiForums wanawatakia kina Baba wote Upendo na Amani kwenye siku hii muhimu
MOGADISHU: WATU 11 WAMEFARIKI NA 25 KUJERUHIWA KWENYE MILIPUKO

- Ni milipuko ya kujitoa muhanga iliyohusisha magari kwenye eneo la ukaguzi la Kasri ya Rais na eneo la ukaguzi la Uwanja wa Ndege

- Al-Shabab wamekiri kuhusika na milipuko hiyo

Soma https://jamii.app/MilipukoMogadishu
KOCHA WA CHELSEA, MAURIZIO SARRI AJIUNGA JUVENTUS

- Kocha huyo amejiunga na Juventus kwa kandarasi ya miaka 3 baada ya kukaa Chelsea kwa msimu mmoja

- Akiwa Chelsea, alifanikiwa kuchukua Kombe la Europa likiwa ndio taji lake kubwa katika maisha yake ya Ukocha
ISRAEL: MKE WA WAZIRI MKUU AHUKUMIWA KWA MATUMIZI MABAYA YA FEDHA ZA SERIKALI

- Sara Netanyahu amehukumiwa kulipa faini ya $15,000(Tsh. 34,582,500) baada ya kukutwa na hatia ya kutumia vibaya fedha za Serikali katika manunuzi ya chakula

Zaidi, soma https://jamii.app/SaraNetanyahuConvicted
INDIA YAONGEZA USHURU KWA BIDHAA ZA MAREKANI

- Imesema imeamua kuongeza ushuru kwa bidhaa 28 zinazoagizwa kutoka Marekani kuanzia jana

- Ni kutokana na Marekani kuongeza ushuru wa bidhaa za chuma na aluminium zinazoingizwa nchini humo

Zaidi, soma https://jamii.app/IndiaMarekaniUshuru
MTU MWENYE DALILI KAMA ZA EBOLA AONEKANA KENYA, MAMLAKA ZA AFYA ZACHUKUA TAHADHARI

- Dalili zimeonekana kwa Mwanamke mmoja aliyetoka Mabala, mpakani mwa Kenya na Uganda

- Amelazwa katika hospitali ya rufaa ya Kaunti ya Kericho tangu jana

Zaidi, soma https://jamii.app/SuspectedEbolaCase-KE
DR CONGO MASHARIKI: ENEO LENYE UTAJIRI WA MITI INAYOZALISHA DAWA AINA YA QUININE

> Jimbo la Kivu(Kusini na Kaskazini) linahifadhi kubwa ya miti aina ya Cinchona inayotumika kutengeneza dawa hizo

> Hata hivyo DRC ni Taifa la pili Duniani kwa vifo vya Malaria

Soma > https://jamii.app/QuinineDRC
MTAMBO WA MAJI WA RUVU JUU KUZIMWA

- Uzalishaji wa maji katika mtambo wa Ruvu Juu umesimamishwa kwa muda ili kuruhusu mafundi wa TANESCO na DAWASA kufanya maboresho

- Baadhi ya maeneo ya Jiji la Dar na maeneo ya Mlandizi na Kibaha yatakosa maji

Zaidi, soma https://jamii.app/RuvuJuuKuzimwa-DAWASA
INDIA: MFANYAMAZINGAOMBWE APOTEA MTONI AKIJARIBU KUONESHA UJUZI

- Chanchal Lahiri aliyefungwa kwa minyororo na makufuli na kisha kutumbukizwa mtoni anaofiwa kufa hapo jana

- Alitakiwa kuibuka akiwa amejifungua minyororo hiyo lakini hakuibuka na hadi jana jioni alitafutwa bila mafanikio

Zaidi, soma https://jamii.app/MfanyamazingaombweAhofiwaKufa-IND
WEMA SEPETU KWENDA MAHABUSU KWA SIKU 7

- Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu imeamuru msanii huyo kukaa mahabusu akisubiri uamuzi wa dhamana baada ya kukiuka masharti

- Mara ya mwisho shauri hilo kusikilizwa, Mahakama iliamuru Wema akamatwe

Zaidi, soma https://jamii.app/WemaSepetuMahabusuSiku7