JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
TUNDURU, RUVUMA: MWALIMU AFARIKI BAADA YA KUNYWA GONGO

- Ni Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Matemanga, Hekima Gregory maarufu Mvomela(49)

- Inadaiwa alikutwa akiwa anakunywa pombe hiyo ya kienyeji bila ya kula chakula chochote

Zaidi, soma https://jamii.app/MwalimuAfarikiGongo
KAGERA SUGAR NA MWADUI FC ZASALIA LIGI KUU BARA

- Mwadui FC imeitoa Geita Gold FC na Kagera Sugar imeitoa Pamba FC katika mechi za mtoano

- Hivyo basi, Polisi Tanzania na Namungo FC ndio timu pekee zilizopanda zikitokea Ligi daraja la kwanza

Zaidi, soma https://jamii.app/KageraMwaduiLigiKuu
DAR: HALIMA MDEE ALAZWA, AFANYIWA UPASUAJI

- Mbunge huyo wa Kawe jijini Dar kupitia CHADEMA, amelazwa katika hospitali ya Agakhan jijini humo

- Kwa sasa anaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji na kutolewa uvimbe aliokuwa nao tumboni

Zaidi, soma https://jamii.app/HalimaMdeeAlazwa
HUAWEI YAZUIWA KUTUMIA HUDUMA ZA KAMPUNI YA FACEBOOK

> Kampuni ya Facebook imezuia huduma wezeshi(APP) zake kutumika katika simu za Huawei huku zuio hilo likilenga huduma mama ya Facebook na nyingine kutoka kampuni washirika ambazo ni WhatsApp na Instagram

Soma - https://jamii.app/FacebookBansHuawei
SUDAN: VIONGOZI WALIOHUDHURIA MKUTANO WA UPATANISHI WAKAMATWA

> Vikosi vya usalama vimewakamata viongozi watatu wa upinzani baada ya kukutana na Waziri Mkuu wa Ethiopia mjini Khartoum ili kusaidia katika mazungumzo ya amani

> Waliokamatwa ni Mohamed Ismat, Imsail jalab na Mubarak Ardol

Soma - https://jamii.app/OppLeadersArrested
HALI YA MAMA MARIA NYERERE INAENDELEA KUIMARIKA

- Mke wa Baba wa Taifa, aliugua ghafla akiwa Namugongo, Uganda alipokwenda kwenye hija

- Baada ya madaktari Nchini humo kuona afya imeimarika kidogo, waliruhusu asafiri kuja Dar Juni 5, 2019

Soma > https://jamii.app/MariaNyerereAnaendeleaVyema
GAIRO, MOROGORO: WACHIMBA MADINI WAHOFIWA KUFA BAADA YA KUFUKIWA NA KIFUSI

> Wachimbaji wadogo 4 wa dhahabu wanahofiwa kufa baada ya kufukiwa na kifusi cha mchanga kijijini Iyogwe

> Taarifa hii ya awali ni kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji madini mkoani humo
PROF. LIPUMBA: CUF HAITARUDI NYUMA JAPOKUWA INAPIGWA VITA NA VYAMA VINGINE VYA SIASA

- Alisema hayo jana kwenye mkutano wa Chama wa kujiandaa na Uchaguzi wa Serikali za mitaa

- Pia, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, amewaasa viongozi kuachana na makundi

Soma > https://jamii.app/CUFInapigwaVita
ZANZIBAR: ALIYEWAHI KUWA RPC AJINYONGA HADI KUFA

> Aliyewahi kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, DCP Aziz Juma Mohammed amekutwa amejinyonga nje ya nyumba yake huko Kibweni, Unguja usiku wa kuamkia leo

Zaidi, soma > https://jamii.app/RPCZnZAjinyonga
MOSHI, KILIMANJARO: MWALIMU AHUKUMIWA MIAKA 20 JELA KWA KUMDHALILISHA MTOTO KINGONO

> Ni Mwalimu Fidelis Matemu(60) wa Shule ya Msingi Uru

> Aliyedhalilishwa kingono ni mtoto wa miaka 11, mwanafunzi wa darasa la 6 shule ya msingi Msareni

Soma > https://jamii.app/Jela20UdhalilishajiKingonoMoshi
YANGA YAIFUATA SIMBA KUJITOA MICHUANO YA KOMBE LA KAGAME

> Sababu waliyoitoa ni kushindwa kuunda kikosi imara kwa muda huu kwa sababu ya wachezaji wengi kumaliza mikataba na wanaoendelea kuwasajili kutomaliza taratibu za mwisho kwenye vilabu vyao

> Michuano hiyo imepangwa kufanyika Julai 7-21, 2019 huko Kigali, Rwanda

Soma > https://jamii.app/YangaYajitoaKagame2019
MAJI YAKATIKA KWA SIKU NNE SEHEMU MBALIMBALI ZA JIJI LA DAR

> Maeneo yanayolalamikiwa kukosa maji ni Kimara, Kibamba, Changanyikeni, Ubungo Riverside, Mbezi Mwisho, Mbezi kwa Msuguli

> Aidha, Majimbo ya Kibamba na Ubungo yametajwa kuathirika zaidi

Soma > https://jamii.app/MajiKibamba
VIONGOZI WAPYA KUAPISHWA LEO, SERIKALI KUPOKEA GAWIO KUTOKA AIRTEL

> Rais Magufuli leo Juni 10, atawaapisha Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa, Kamishna Mkuu wa TRA, Dkt. Edwin Mhede na Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe, Charles Kichere

> Pia atashuhudia tukio la makabidhiano ya kiasi cha Tsh bilioni 5.27 kutoka Airtel kwenda Serikalini

Soma - https://jamii.app/UapishoGawioAirtel
KENYA: MAAFISA WA POLISI WAKAA CHONJO DHIDI YA TUKIO LA UGAIDI

> Tetesi za mipango ya shambulio zimepatikana baada ya kukamatwa kwa watuhumiwa 4 wa ugaidi

> Wanausalama wameripoti kukutwa kwa vifaa vya milipuko ktk barabara ya Narok-Bomet

Soma > https://jamii.app/TetesiUgaidiKenya
IRAN YAZINDUA MFUMO WA KISASA WA MAKOMBORA

> Mfumo huo uliopewa jina la Khordad 15, unaweza kulenga shabaha 6 kwa adui kwa wakati mmoja na una uwezo wa kugundua ndege za kivita na droni kutoka umbali wa kilomita 150 na kuzifuatilia katika umbali wa kilomita 120

Soma - https://jamii.app/Khordad15Launch
CHAMA CHA ACT WAZALENDO CHAIMARISHA SAFU YAKE YA UONGOZI

> Maalim Seif Sharif ameteuliwa kuwa Mshauri Mkuu wa chama hicho

> Kamati Kuu imefanya uteuzi wa safu ya viongozi mbalimbali wa kitaifa yenye mseto wa wanachama waliohamia kutoka CUF

Soma > https://jamii.app/UongoziACT
WAENDESHA BAJAJI NA BODABODA WATAWANYWA KWA MABOMU

> Jeshi la Polisi Dar limetumia mabomu ya Machozi kuwatawanya Waendesha bodaboda na bajaji ktk eneo la Posta mpya karibu na jengo la Benjamin Mkapa baada ya uongozi kuwataka kuondoka kwa madai kuwa hawaruhusiwi kufanya biashara eneo hilo

Soma - https://jamii.app/BajajiBodabodaMabomu
AFYA: YAJUE MAGONJWA YA FANGASI YA NGOZI NA TIBA ZAKE

> Fangasi ni ugonjwa unaoathiri sana ngozi, kucha na nywele. Mara nyingine huathiri mdomo na sehemu za siri

> Kuna fangasi za kichwa, mwili, kucha na miguu ambazo huambukizwa kwa njia ya kugusana au kushirikiana nguo za ndani na taulo

Kwa elimu zaidi pamoja na tiba, fungua => https://jamii.app/UgonjwaFangasi