JamiiForums
52.9K subscribers
34.3K photos
2.43K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
TAIFA STARS YAELEKEA MISRI KUSHIRIKI AFCON

- Imeenda kuweka kambi maalumu ya maandalizi ya michuano hiyo itakayofanyika nchini humo kuanzia Juni 21

- Kocha wa Stars, Emanuel Amunike amesema amechagua timu yenye vipaji na ana imani nayo

Zaidi, soma https://jamii.app/StarsYaendaMisri
ARUSHA: NYAMA ZISIZOFAA KWA WANANCHI ZAKAMATWA ZIKIUZWA

- Nyama hizo zinazokadiriwa kuwa na kilo zaidi ya 400 zimekamatwa katika operesheni inayoendelea ya kukagua mabucha

- Kati ya mabucha 235 yaliyokaguliwa, 16 yamekutwa yanakiuka sheria

Zaidi, soma https://jamii.app/NyamaMbovuArusha
SHINYANGA: WANANDOA WAUAWA SABABU YA KUGOMBANIA MASHAMBA YA FAMILIA

> Inadaiwa Manyara Ndelema (48) na mkewe Nyamizi Mserengeti (40) walinunua mashamba ya familia yao baada ya kuuziwa na wanafamilia, lakini baada ya ndugu hao kukosa mahali pa kulima, waliibua mgogoro kuyataka mashamba hayo na kusababisha mauaji

Soma - https://jamii.app/MeKeKifoShamba
Rais John Magufuli amemteua Innocent Bashungwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara akichukua nafasi ya Joseph Kakunda ambaye uteuzi wake umetenguliwa

> Edwin Mhede ateuliwa kuwa Kamishna Mkuu TRA; aliyekuwa Kamishna wa TRA, Charles Kichere uteuzi wake umetenguliwa na ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe
WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA AZURU SUDAN KUSULUHISHA

- Waziri Mkuu, Abiy Ahmed yupo Mjini Khartoum, kwa mazungumzo ya usuluhishi baina ya Baraza la Kijeshi na viongozi wa Waandamanaji kufuatia ukandamizaji uliofanywa na Jeshi wiki hii

Zaidi, soma https://jamii.app/WaziriETHPSuluhuSDN
MICHEZO: Rais wa shirikisho la soka barani Afrika, Ahmad Ahmad ameachiliwa huru nchini Ufaransa bila kufunguliwa mashtaka yoyote  baada ya kuhojiwa kama sehemu ya uchunguzi kuhusu ufisadi na ulaghai wa kughushi stakabadhi

#JFMichezo
LIBERIA: WANANCHI WAANDAMANA, MITANDAO YA KIJAMII YAZIMWA

- Wameandamana katika Mji Mkuu, Monrovia jana wakipinga masuala ya rushwa na wanaouita Udikteta uliokithiri

- Pia, WhatsApp, Instagram, Snapchat, Facebook, huduma za Google zilifungwa

Zaidi, soma https://jamii.app/MaandamanoLiberiaMitandao
NJOMBE: WAWILI WAUAWA WAKISADIKIWA KUWA NI MAJAMBAZI

> Jeshi la Polisi limewaua watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni majambazi huku mmoja akifanikiwa kutoroka

> Walijaribu kufanya unyang’anyi wa kutumia silaha katika kituo cha kuuza mafuta kiitwacho Negelo

Soma - https://jamii.app/PolisiWauaMajambazi
TUNDURU, RUVUMA: MWALIMU AFARIKI BAADA YA KUNYWA GONGO

- Ni Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Matemanga, Hekima Gregory maarufu Mvomela(49)

- Inadaiwa alikutwa akiwa anakunywa pombe hiyo ya kienyeji bila ya kula chakula chochote

Zaidi, soma https://jamii.app/MwalimuAfarikiGongo
KAGERA SUGAR NA MWADUI FC ZASALIA LIGI KUU BARA

- Mwadui FC imeitoa Geita Gold FC na Kagera Sugar imeitoa Pamba FC katika mechi za mtoano

- Hivyo basi, Polisi Tanzania na Namungo FC ndio timu pekee zilizopanda zikitokea Ligi daraja la kwanza

Zaidi, soma https://jamii.app/KageraMwaduiLigiKuu
DAR: HALIMA MDEE ALAZWA, AFANYIWA UPASUAJI

- Mbunge huyo wa Kawe jijini Dar kupitia CHADEMA, amelazwa katika hospitali ya Agakhan jijini humo

- Kwa sasa anaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji na kutolewa uvimbe aliokuwa nao tumboni

Zaidi, soma https://jamii.app/HalimaMdeeAlazwa
HUAWEI YAZUIWA KUTUMIA HUDUMA ZA KAMPUNI YA FACEBOOK

> Kampuni ya Facebook imezuia huduma wezeshi(APP) zake kutumika katika simu za Huawei huku zuio hilo likilenga huduma mama ya Facebook na nyingine kutoka kampuni washirika ambazo ni WhatsApp na Instagram

Soma - https://jamii.app/FacebookBansHuawei
SUDAN: VIONGOZI WALIOHUDHURIA MKUTANO WA UPATANISHI WAKAMATWA

> Vikosi vya usalama vimewakamata viongozi watatu wa upinzani baada ya kukutana na Waziri Mkuu wa Ethiopia mjini Khartoum ili kusaidia katika mazungumzo ya amani

> Waliokamatwa ni Mohamed Ismat, Imsail jalab na Mubarak Ardol

Soma - https://jamii.app/OppLeadersArrested
HALI YA MAMA MARIA NYERERE INAENDELEA KUIMARIKA

- Mke wa Baba wa Taifa, aliugua ghafla akiwa Namugongo, Uganda alipokwenda kwenye hija

- Baada ya madaktari Nchini humo kuona afya imeimarika kidogo, waliruhusu asafiri kuja Dar Juni 5, 2019

Soma > https://jamii.app/MariaNyerereAnaendeleaVyema
GAIRO, MOROGORO: WACHIMBA MADINI WAHOFIWA KUFA BAADA YA KUFUKIWA NA KIFUSI

> Wachimbaji wadogo 4 wa dhahabu wanahofiwa kufa baada ya kufukiwa na kifusi cha mchanga kijijini Iyogwe

> Taarifa hii ya awali ni kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Chama cha Wachimbaji madini mkoani humo
PROF. LIPUMBA: CUF HAITARUDI NYUMA JAPOKUWA INAPIGWA VITA NA VYAMA VINGINE VYA SIASA

- Alisema hayo jana kwenye mkutano wa Chama wa kujiandaa na Uchaguzi wa Serikali za mitaa

- Pia, Naibu Katibu Mkuu wa CUF, amewaasa viongozi kuachana na makundi

Soma > https://jamii.app/CUFInapigwaVita
ZANZIBAR: ALIYEWAHI KUWA RPC AJINYONGA HADI KUFA

> Aliyewahi kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, DCP Aziz Juma Mohammed amekutwa amejinyonga nje ya nyumba yake huko Kibweni, Unguja usiku wa kuamkia leo

Zaidi, soma > https://jamii.app/RPCZnZAjinyonga
MOSHI, KILIMANJARO: MWALIMU AHUKUMIWA MIAKA 20 JELA KWA KUMDHALILISHA MTOTO KINGONO

> Ni Mwalimu Fidelis Matemu(60) wa Shule ya Msingi Uru

> Aliyedhalilishwa kingono ni mtoto wa miaka 11, mwanafunzi wa darasa la 6 shule ya msingi Msareni

Soma > https://jamii.app/Jela20UdhalilishajiKingonoMoshi