JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
TANZANIA KUANZA KUUZA TENA BIDHAA ZA MALIASILI MAREKANI

> Miaka mitano iliyopita, Marekani ilizuia bidhaa zinazotokana na shughuli za uwindaji kutoka Tanzania, kutokana na kile ambacho ilidai ni kutokuwa na imani na jinsi Tanzania ilivyokuwa ikiendesha jitihada za uhifadhi wa maliasili na mazingira

Soma - https://jamii.app/MauzoBidhaaMaliasili
WHO: MAAMBUKIZI MAPYA MILIONI 1 YA MAGONJWA YA ZINAA HUTOKEA KILA SIKU

- Magonjwa hayo ni pamoja na kisonono, kaswende na trichomoniasis

- Aidha, Wataalamu wanahofu magonjwa hayo kuwa sugu kiasi cha kutotibiwa na dawa zilizopo sasa

Zaidi, soma https://jamii.app/WHOMaambukiziZinaa
LUGOLA KUANZA KUKAGUA PIKIPIKI KWENYE VITUO VYA POLISI

> Waziri wa Mambo ya Ndani amesema kuanzia Juni 15 ataanza ziara katika vituo mbalimbali vya Polisi kukagua utekelezaji wa agizo lake kuhusu Jeshi hilo kuzishikilia bodaboda zenye makosa ya kofia ngumu au kupakia abiria zaidi ya watatu

Soma - https://jamii.app/LugolaUkaguzibodaboda
IKULU, DAR: RAIS MAGUFULI AKUTANA NA WAFANYABIASHARA

- Anazungumza na Wafanyabiashara wa 5 kutoka wilaya zote nchini pamoja na Wajumbe wa Baraza la Biashara la Taifa

- Lengo ni kufahamu changamoto za Wafanyabiashara na kusikiliza mawazo yao

Zaidi, soma https://jamii.app/MagufuliWafanyabiashara-Ikulu
CHINA NA URUSI ZATIA SAINI KUZUIA MATUMIZI YA FEDHA YA MAREKANI

> Rais Xi Jinping wa China ametangaza habari ya kutiwa saini mapatano ya kufutwa kwa sarafu ya dola ya Marekani katika miamala ya kibiashara ya nchi yake na Urusi na badala yake sarafu za mataifa hayo zitachukua nafasi ya dola katika mabadilishano

Soma - https://jamii.app/RussiaChinaBanDollar
KLABU YA SIMBA YAPANGA KUJITOA MICHUANO YA KAGAME CUP

> Mkurugenzi wa klabu hiyo, Crescentus Magori amedai kutokana na sababu za kubadilika kwa ratiba ya CAF, michuano ya Afcon itakuwa ngumu kwa klabu hiyo kushiriki mashindano ya Kagame Cup kwa kuwa inatarajia kwenda kuweka kambi ya mwezi mmoja nje ya nchi kujiandaa na msimu wa 2019/20

Soma - https://jamii.app/SimbaKujitoaKagameCup
#JFMichezo
MICHEZO: Klabu ya Manchester United imekubaliana na klabu ya Swansea City dau la Paundi Milioni 15(Tsh. 43,970,758,245) kumsajili Mchezaji wake, Daniel James

- Mchezaji huyo mwenye miaka 21, raia wa Wales amekamilisha vipimo vya Afya pale Old Trafford kwa siku ya jana
TAIFA STARS YAELEKEA MISRI KUSHIRIKI AFCON

- Imeenda kuweka kambi maalumu ya maandalizi ya michuano hiyo itakayofanyika nchini humo kuanzia Juni 21

- Kocha wa Stars, Emanuel Amunike amesema amechagua timu yenye vipaji na ana imani nayo

Zaidi, soma https://jamii.app/StarsYaendaMisri
ARUSHA: NYAMA ZISIZOFAA KWA WANANCHI ZAKAMATWA ZIKIUZWA

- Nyama hizo zinazokadiriwa kuwa na kilo zaidi ya 400 zimekamatwa katika operesheni inayoendelea ya kukagua mabucha

- Kati ya mabucha 235 yaliyokaguliwa, 16 yamekutwa yanakiuka sheria

Zaidi, soma https://jamii.app/NyamaMbovuArusha
SHINYANGA: WANANDOA WAUAWA SABABU YA KUGOMBANIA MASHAMBA YA FAMILIA

> Inadaiwa Manyara Ndelema (48) na mkewe Nyamizi Mserengeti (40) walinunua mashamba ya familia yao baada ya kuuziwa na wanafamilia, lakini baada ya ndugu hao kukosa mahali pa kulima, waliibua mgogoro kuyataka mashamba hayo na kusababisha mauaji

Soma - https://jamii.app/MeKeKifoShamba
Rais John Magufuli amemteua Innocent Bashungwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara akichukua nafasi ya Joseph Kakunda ambaye uteuzi wake umetenguliwa

> Edwin Mhede ateuliwa kuwa Kamishna Mkuu TRA; aliyekuwa Kamishna wa TRA, Charles Kichere uteuzi wake umetenguliwa na ameteuliwa kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Njombe
WAZIRI MKUU WA ETHIOPIA AZURU SUDAN KUSULUHISHA

- Waziri Mkuu, Abiy Ahmed yupo Mjini Khartoum, kwa mazungumzo ya usuluhishi baina ya Baraza la Kijeshi na viongozi wa Waandamanaji kufuatia ukandamizaji uliofanywa na Jeshi wiki hii

Zaidi, soma https://jamii.app/WaziriETHPSuluhuSDN
MICHEZO: Rais wa shirikisho la soka barani Afrika, Ahmad Ahmad ameachiliwa huru nchini Ufaransa bila kufunguliwa mashtaka yoyote  baada ya kuhojiwa kama sehemu ya uchunguzi kuhusu ufisadi na ulaghai wa kughushi stakabadhi

#JFMichezo
LIBERIA: WANANCHI WAANDAMANA, MITANDAO YA KIJAMII YAZIMWA

- Wameandamana katika Mji Mkuu, Monrovia jana wakipinga masuala ya rushwa na wanaouita Udikteta uliokithiri

- Pia, WhatsApp, Instagram, Snapchat, Facebook, huduma za Google zilifungwa

Zaidi, soma https://jamii.app/MaandamanoLiberiaMitandao
NJOMBE: WAWILI WAUAWA WAKISADIKIWA KUWA NI MAJAMBAZI

> Jeshi la Polisi limewaua watu wawili wanaosadikiwa kuwa ni majambazi huku mmoja akifanikiwa kutoroka

> Walijaribu kufanya unyang’anyi wa kutumia silaha katika kituo cha kuuza mafuta kiitwacho Negelo

Soma - https://jamii.app/PolisiWauaMajambazi