JamiiForums
52.9K subscribers
34.3K photos
2.43K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
AMCHOMA MTOTO MOTO NA KUMKATA NA WEMBE AKIDAI KAKOMBA MBOGA

- Magreth Digugulo mkazi wa Mjini Geita anadaiwa kumchoma moto na kumkatakata kwa wembe mjukuu wake kwenye mkono wa kulia kwa madai ya kujipakulia na kukomba mboga aina ya kisamvu

Soma https://jamii.app/AmchomaMotoMjukuu-GIT
DHAHABU NA FEDHA ZILIZOTAIFISHWA ZAKABIDHIWA KWA SERIKALI

> DPP Biswalo Mganga amekabidhi kilo 325 za dhahabu na shilingi milioni 305

> Utaifishwaji huo ulifanywa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza baada ya Washtakiwa kukiri makosa

Zaidi, soma => https://jamii.app/DhahabuDPPGvt

#JFLeo
ALIYEWAHI KUWA MLINZI WA RAIS PAUL KAGAME AUAWA AFRIKA KUSINI

> Camir Nkurunziza hivi karibuni aliibuka kuwa mkosoaji wa Rais Paul Kagame ameuawa kwa kupigwa risasi akiwa Afrika Kusini

> Alianzisha kampeni ya kupinga Rais Kagame kuongezewa muhula wa 3

Soma > https://jamii.app/MauajiNkuruziza

#JFLeo
NKASI, RUKWA: MJAMZITO ADAIWA KUJIPASUA NA KUMTOA MTOTO

- Joyce Kalinda anadaiwa kujipasua tumbo kwa kitu chenye ncha kali na kumtoa mtoto

- Awali alienda hospitali ila baada ya kuambiwa subiri kidogo alitoweka na kurudishwa akiwa amejipasua

Zaidi, soma https://jamii.app/AjipasuaKutoaMtoto
MWILI WA ETIENNE TSHISEKEDI WAWASILI DR CONGO

- Mwili wa kiongozi huyo wa zamani wa upinzani umewasili kutoka Ubelgiji alikofarikia miaka 2 iliyopita

- Mwili ulibaki huko kutokana na wasiwasi wa kisiasa wakati wa utawala wa Rais Joseph Kabila

Zaidi, soma https://jamii.app/TshisekediKuzikwaCongo
WAZIRI KABUDI: HATUWEZI KUPIGA MAGOTI KUOMBA MISAADA

- Waziri huyo wa Mambo ya Nje, amesema Tanzania haikupiga magoti kipindi cha utawala wa awamu ya 2 ilipokuwa na hali ngumu, hivyo haiwezi kufanya hivyo wakati huu ikiwa na hali nzuri zaidi

Zaidi, soma https://jamii.app/TZHaitapigaMagotiMisaada
KOREA KASKAZINI YADAIWA KUMUUA MJUMBE WAKE WA MKUTANO WA HANOI

- Vyombo vya habari vya Korea Kusini vimeripoti kuwa Korea Kaskazini imemuua mjumbe wake maalumu, Kim Hyok Chol kufuatia kushindwa kwa mkutano wa pili kati ya Kim Jong Un na Rais Donald Trump

Zaidi, soma https://jamii.app/MjumbeHanoiAuawa-NK
SUDAN: KAMBI YA WAANDAMANAJI YADAIWA KUWA HATARI. AL JAZEERA YATAKIWA KUFUNGA OFISI

- Kiongozi wa Kijeshi amesema Kambi hiyo iliyopo Khartoum imekuwa tishio kwa usalama wa nchi

- Pia, bila kutoa sababu ameagiza ofisi ya Al Jazeera kufungwa

Zaidi, soma https://jamii.app/AljazeeraSudanKufungwa
BURUNDI YATISHIA KUSITISHA USHIRIKIANO NA MJUMBE WA UN NCHINI HUMO

- Imeeleza kutoridhishwa na namna Mjumbe huyo wa Umoja wa Mataifa (United Nations -UN), Michel Kafando ambavyo amekuwa akiingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo

Zaidi, soma https://jamii.app/MjumbeUNvsBurundi
SERIKALI: TAMKO LA ALLY HAPI KUHUSU VITAMBULISHO SI LA SERIKALI

- Ni la makundi yanayotakiwa kupewa vitambulisho vya Wafanyabiashara wadogo alilotoa RC huyo wa Iringa

- Imetoa wito kwa Wakuu wote wa Mikoa kuzingatia maelekezo ya Serikali

Zaidi, soma https://jamii.app/SerikalivsHapi-Vitambulisho
R. KELLY AKABILIWA NA MASHTAKA MAPYA 11 YA UNYANYASAJI WA KINGONO

- Anadaiwa kufanya vitendo hivyo dhidi ya Watoto wa umri kati ya miaka 13 na 16

- Ikithibitika atakabiliwa na adhabu kali kuliko anazoweza kupata kutokana na mashtaka 10 ya awali

Zaidi, soma https://jamii.app/RKellyMashtakaMapya11
TEKNOLOJIA: BLACKBERRY MESSENGER YAFUNGWA RASMI

> BBM ilioanzishwa 2005 kabla ya mitandao ya WhatsApp, Facebook, Instagram na mingineyo kuundwa

> Aidha, Kampuni ya Emtek imeunda mfumo mbadala na kuupa jina la BBMe ambao utakuwa bora zaidi

Soma https://jamii.app/EndOfBBM
KENYA: WAKAZI WENGI WA NAIROBI HUTEMBEA KWA MIGUU KWENDA KAZINI

> Takwimu zinaonesha kuwa kwa kila Wakenya 10 basi 5 kati yao hutembea kwa miguu wanapokwenda kazini

> Usafiri mbovu na gharama kuwa kubwa vyatajwa kuwa sababu

Zaidi, soma => https://jamii.app/WafanyakaziNairobi
WALIOMALIZA KIDATO CHA 4 2018 WAPANGIWA SHULE NA VYUO VYA UFUNDI

- Waliopangiwa ni Wanafunzi 108,644 sawa na asilimia 98.31 kati ya wote wenye sifa

- Waliochaguliwa kujiunga na kidato cha 5 pekee ni 69,356 sawa na asilimia 62.76 ya wenye sifa

Zaidi, soma https://jamii.app/Kidato4WapangiwaShule
WATU 13 WAMEUAWA KATIKA SHAMBULIO LA RISASI

- Wengine 4 wamejeruhiwa akiwemo Afisa wa Polisi hapo jana huko Virginia Beach, Marekani

- Mfanyakazi wa Idara ya nishati na maji aliwafyatulia risasi wafanyakazi wenzake kabla ya kuuawa na Polisi

Zaidi, soma https://jamii.app/ShambulioRisasiVirginia
MCHEZAJI WA ZAMANI WA ARSENAL NA REAL MADRID, JOSE ANTONIO REYES, AFARIKI

- Amefariki pamoja na binamu zake wawili leo asubuhi katika ajali ya gari iliyotokea Utrera nje kidogo ya Seville nchini Uhispania

- Ameacha mke na watoto watatu, Wasichana wawili na Mvulana mmoja

#JFLeo
CHINA YATANGAZA NYONGEZA YA USHURU KWA BIDHAA ZA MAREKANI

- Imefanya hivyo huku ikijitayarisha kutoa orodha ya kampuni mbaya za kigeni

- Inadaiwa inataka kuiadhibu Marekani na kampuni za kigeni zinazoacha kufanya kazi na kampuni ya Huawei

Zaidi, soma https://jamii.app/ChinaTariffsUSA
LIVERPOOL YATAWAZWA KUWA MABINGWA WAPYA ULAYA

- Imefanikiwa kuwa bingwa wa michuano ya Klabu Bingwa Ulaya baada ya kuifunga Tottenham goli 2-0 katika mchezo wa fainali

- Liverpool sasa inakuwa imechukua kombe hilo mara 6 huku kwa Tottenham hii ilikuwa fainali ya kwanza