JamiiForums
52.9K subscribers
34.3K photos
2.42K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MARA: BOMU LAGUNDULIKA MIONGONI MWA VYUMA CHAKAVU

- Ni katika gari la Mfanyabiashara aliyekuwa akisafirisha vyuma hivyo kutoka Serengeti kwenda Mwanza

- Amesema wakati anapakia mzigo aliona chuma kisicho cha kawaida na kutoa taarifa Polisi

Zaidi, soma https://jamii.app/BomuLagundulika-Mara
DAR: AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA KUMBAKA MTOTO WAKE WA MIAKA 13

> Said Rashid(36), anatuhumiwa kutenda kosa hilo mnamo mwaka 2016 na Aprili 2019 huko nyumbani kwake eneo la Mbezi Juu

> Aamekana kosa hilo na kurudishwa rumande

Soma > https://jamii.app/BabaKizimbaniUbakaji
IRINGA: WAANDISHI WA HABARI WAMTAKA RC ALLY HAPI AWAOMBE RADHI

- Wamempa siku 7 kufanya hivyo baada ya kuwataka kuwa na vitambulisho vya Wafanyabiashara wadogo

- Wamesema kuwachukulia kama vibarua wasio rasmi kunadhalilisha taaluma ya habari

Zaidi, soma https://jamii.app/WanaHabariVsHapi-IRN
SHERIA: MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOJITETEA MAHAKAMANI

> Watu wengi hupata shida ya kutoa maelezo au kujitetea pindi waitwapo Mahakamani

> Wapo waliokutwa na makosa au kushindwa kesi na kupoteza haki zao kwa makosa waliyofanya wakati wa kujitetea

Kwa elimu, soma => https://jamii.app/KujielezaMahakama
ALIYEKUWA MKUU WA UPELELEZI KINONDONI AKATA RUFAA KUEPUKA KUNYONGWA

> Christopher Bageni, alihukumiwa kunyongwa kwa kuwaua Wafanyabiashara wa madini kutoka Mahenge, Morogoro

> Kesi hiyo pia ilikuwa ikimhusu aliyekuwa RCO wa Dar, Abdallah Zombe

Soma > https://jamii.app/RufaaKunyongwa
BODI YA LIGI YAIPA KAGERA SUGAR NAFASI YA KUJITETEA ISISHUKE DARAJA

> Kiongizi wa bodi Boniface Wambura amesema kuna makosa ya takwimu hivyo wameirudisha Kagera Sugar

> Kagera Sugar sasa itacheza michezo 2 ili kutafuta nafasi ya kushiriki Ligi Kuu

Soma > https://jamii.app/KageraSugarPlayoff

#JFSports
ARUSHA: JAMBAZI SUGU NA KADA MAARUFU WA CCM AKAMATWA

- Polisi inamshikilia Jumanne Mjuzi, mkazi wa Ngarenaro kwa kosa la kuvunja na kuiba vitu mbalimbali

- Ni kada aliyelishiriki kwenye chaguzi mbalimbali kama kiongozi wa kikosi cha ulinzi

Zaidi, soma https://jamii.app/JambaziKadaCCMAkamatwa
DR CONGO: MATEKA 22 WAACHIWA HURU

- Kundi la Dola ya Kiislamu liliwateka wiki iliyopita katika Mji wa Samboko-Tchani Tchani

- Kiongozi mmoja katika Mji wa Beni amedai Watekaji walikuwa wakizungumza Kiswahili vizuri kama wanatoka Afrika Mashariki(Tanzania)

Zaidi, soma https://jamii.app/Mateka22Waachiwa-DRC
DAR: KIPINDUPINDU CHAUA MTU 1, 32 WALAZWA

- Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema hayo wakati akiangali hali ya Kipindupindu na Dengue jijini humo

- Aidha, ametaka wanaotiririsha maji machafu walipe faini ya Tsh. 200,000 badala ya Tsh. 30,000

Zaidi, soma https://jamii.app/KipindupinduChaua-Dar
WAZIRI KALEMANI: TANESCO INADAIWA BILIONI 957, ITAMALIZA KULIPA 2026

> Waziri huyo wa Nishati amesema shirika hilo 2017 lilipata hasara ya TSh. bilioni 349

> 2018 TANESCO ilipata hasara ya Tsh. bilioni 122 huku 2019 ikipata faida ya Tsh. bilioni 9

Soma > https://jamii.app/DeniTanesco
RAIS MAGUFULI AUOMBA UMOJA WA ULAYA NA MAREKANI KUIONDOLEA VIKWAZO ZIMBABWE

> Rais Magufuli amesisitiza kwamba Zimbabwe ipo kwenye njia sahihi ya kuufufua uchumi wake chini ya Serikali ya Rais Emmerson Mnangagwa

Zaidi, soma => https://jamii.app/MagufuliVikwazoZimb
WAZIRI MBARAWA: MIRADI 88 IMEJENGWA CHINI YA KIWANGO

- Waziri huyo wa Maji, amekiri kuwepo kwa miradi hiyo ya maji iliyojengwa kati ya mwaka 2010 na 2015

- Amesema Serikali imekuwa ikikarabati vyanzo vya maji na pia imetenga Tsh. Milioni 135

Zaidi, soma https://jamii.app/Miradi88MajiChiniKiwango
CHELSEA YANYAKUA KOMBE LA EUROPA LIGI

- Imechukua ubingwa huo baada ya kuifunga Arsenal goli 4-1 katika fainali iliyofanyika Baku, Azerbaijan

- Magoli ya Chelsea yamefungwa na Giroud(49’), Pedro(60’) na Hazard(65’ na 72’) huku goli la Arsenal likifungwa na Iwobi(69’)
TABORA: ADAIWA KUMUUA MUMEWE KISA WIVU WA MAPENZI

- Sada Abdallah anatuhumiwa kumuua mumewe kwa kumpiga na kisha kumsukuma na kusababisha aangukie kisogo

- Alikuwa akimtuhumu mumewe huyo kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Mwanamke mwingine

Zaidi, soma https://jamii.app/AmuuaMumeweMapenzi-TBR
JE, WAIJUA HISTORIA YA NENO KILIMANJARO?

> Asili ya neno hili ni makosa ya kisarufi yaliyofanywa na wageni kutoka Ulaya

> Wazawa waliuita Kilimakyaro (Kilimakirefu) lakini makosa ya kimatamshi ya Wageni yalipelekea kuzaliwa neno Kilimanjaro

Soma > https://jamii.app/HistiriaKilimanjaro

#JFHistoria
SERIKALI: NGUVU YA SOKO CHANZO KUTOSHUKA BEI YA TAULO ZA KIKE

- Imesema bei haijashuka licha ya kuondoa Kodi ya Ongezeko la Thamani katika taulo hizo

- Imeeleza bei inatokana na sababu mbalimbali zikiwemo gharama za malighafi na uwekezaji

Zaidi, soma https://jamii.app/BeiTauloKikeKutoshuka
BAKWATA: BARAZA LA EID EL FITR KUFANYIKA TANGA

> Taarifa rasmi ya BAKWATA imeeleza kuwa sikukuu hiyo itafanyika Juni 5/6 kulingana na mwandamo wa mwenzi

> Baraza la Eid litafanyika mkoani Tanga na Waziri Mkuu, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi

Soma > https://jamii.app/EidalFitrTz
RUKWA: MWALIMU MBARONI KWA KUMPIGA MWANAFUNZI HADI KUMSABABISHIA UPOFU

- Mwalimu Peter Silamba wa Sekondari ya Kate, Wilayani Nkasi anatuhumiwa kumpiga machoni kwa fimbo, Nicholaus Kwimba(17) wa kidato cha 3 wakati akimuadhibu kwa uchelewaji

Zaidi, soma https://jamii.app/MwalimuUpofuMwanafunzi-RKW
ARUSHA: WATAKAO KAMATWA NA MIFUKO YA PLASTIKI KUFUNGIWA UWANJA WA SHEIKH AMRI ABEID

> Jeshi la Polisi limesema litalazimika kufanya hivyo endapo mahabusu zitakuwa zimejaa

> Watuhumiwa watahifadhiwa uwanjani hapo hadi watakapofikishwa Mahakamani

Soma > https://jamii.app/MifukoPlastikiArusha
ISRAEL: WAZIRI MKUU ASHINDWA KUUNDA SERIKALI. BUNGE KUVUNJWA

- Israel itafanya uchaguzi mpya Septemba 2019 baada ya Wabunge kupitisha hoja ya kulivunja Bunge kufuatia Waziri Mkuu, Benjamin Netanyahu kushindwa kuunda Serikali ya muungano

Zaidi, soma https://jamii.app/UchaguziMpyaIsrael