JamiiForums
53K subscribers
34.3K photos
2.42K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
AFYA: FANYA YAFUATAYO KUJITIBU KUTOKWA NA DAMU KWENYE FIZI

> Tumia mswaki laini, badili mswaki kila baada ya miezi mitatu, usichokonoe meno mara kwa mara na epuka uvutaji wa sigara na tumbaku

> Kula mboga za majani, matunda na vyakula vyenye vitamini C na K kwa wingi

Kwa elimu zaidi, soma => https://jamii.app/DamuFizi
MOROGORO: AJIUA BAADA YA KUMUUA MKEWE, MAMA MKWE NA JIRANI

- Inadaiwa mume alimtuhumu mkewe kuwa na mwanaume mwingine huku akituhumu hao wengine kufahamu

- Alitumia panga kumuua Mama mkwe, wengine aliwanywesha sumu na yeye kujiua kwa sumu

Zaidi, soma https://jamii.app/MumeAjiuaAua3-Dumila
BRAZIL: IDADI YA WAFUNGWA WALIOFARIKI GEREZANI YAFIKIA 57

> Wafungwa 15 walifariki siku ya Jumapili na wengine 42 siku ya Jumatatu, vifo hivi vimechochewa na ukosefu wa hewa kutokana na msongamano

> Mamlaka zaanza kufanya uchunguzi

Zaidi, soma => https://jamii.app/VifoGerezaniBrazil
IRINGA: RC ALLY HAPI, ASITISHA LIKIZO ZA MA-DC NA WAKURUGENZI

- Amewataka pia kutosafiri nje ya Mkoa baada ya kufanya vibaya katika ugawaji wa vitambulisho vya Wafanyabiashara wadogo

- Ametoa wiki 3 Wafanyabiashara wote wapatiwe vitambulisho

Zaidi, soma https://jamii.app/RCIringaLikizoDC
AFARIKI NDANI YA NDEGE KUTOKANA NA KUJAZA COCAINE TUMBONI

- Raia wa Japan, Udo N amefariki akiwa anasafiri kwenye ndege iliyokuwa inatoka Mjini Mexico kuelekea Japan, baada ya kumeza paketi 246 za #DawaZaKulevya aina ya Cocaine

Zaidi, soma https://jamii.app/Paketi246CocaineZamuua-MXC
MICHEZO: Mchezaji wa Aston Villa iliyopanda daraja baada ya kuifunga Derby goli 2-1, Jack Grealish aeleza sababu za kuvaa viatu vilivyochakaa kwenye mchezo huo

- Amesema "Baada ya kupata majeraha kwa muda na kurejea uwanjani nilivitumia vikiwa vipya kabisa, wakati huo nilipata kufunga magoli kadhaa na kutoa pasi kadhaa za magoli."

Zaidi, soma https://jamii.app/GrealishViatuChakavu
LAZARO NYALANDU NA WENZAKE WAACHIWA KWA DHAMANA

- Wenzake wamedhaminiwa na Wadhamini 2 huku yeye akidhaminiwa na Wadhamini 3, kila mmoja akiweka bondi ya Tsh. Milioni 5

- Aidha, wote wanatakiwa kuripoti Kituo cha Polisi kilichopo Singida Mjini kesho saa 3 asubuhi

Zaidi, soma https://jamii.app/NyalanduAachiwaDhamana-SGD
DAR: DEREVA TAKSI KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA KUMTEKA MO DEWJI

> Mousa Twaleb(46), amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kusomewa mashtaka 3 likiwemo la kumteka Mfanyabiashara Mohammed Dewji

Zaidi, soma => https://jamii.app/DerevaTaxiUtekajiMo
SERIKALI: AJIRA MPYA ZA SERIKALI HAZITAZINGATIA UZOEFU

- Ajira mpya hazitazingatia uzoefu kwa Waajiriwa ikiwa ni utekelezaji wa sera ya Utumishi ya mwaka 2004

- Pia, imeanza kuwaunganisha Wahitimu wa vyuo na taasisi mbalimbali kupata uzoefu

Zaidi, soma https://jamii.app/AjiraSerikaliUzoefu
TEKNOLOJIA: JE WAJUA MAANA YA 'MEGAPIXEL'?

> Megapixel ni mkusanyiko wa pixel (viboksi vidogo) milioni moja ambavyo hutumika kujenga picha inayochukuliwa na Kamera husika

> Mfano: Kamera yenye Megapixel 14 itakuwa na viboksi vidogo vidogo milioni 14

Soma > https://jamii.app/MegaPixel
TP MAZEMBE YASITISHA NIA YA KUTAKA KUMSAJILI IBRAHIM AJIBU

- TP Mazembe inadaiwa kushindwa kufikia makubaliano binafsi na mshambuliaji huyo wa Yanga

- Ugumu unakuwepo kutokana na taarifa kwamba Ajibu alishaingia makubaliano ya awali na Simba

Zaidi, soma https://jamii.app/AjibuMazembeYashindikana
MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA BUTIAMA ATENGULIWA

- Rais Magufuli ametegua uteuzi wa Alphonce Magori kutokana na utendaji wake usioridhisha na nafasi yake itajazwa baadaye

- Akitoa taarifa hiyo, Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo amewataka Wakurugenzi kufikia malengo ya Serikali

Zaidi, soma https://jamii.app/MkurugenziButiamaAtenguliwa
WATUMISHI WATANO WA TUME YA UMWAGILIAJI WASIMAMISHWA KAZI

- Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga amewasimamisha ili kupisha uchunguzi dhidi yao

- Ni kufuatia uchunguzi wa awali uliofanywa na ofisi ya Waziri Mkuu kubaini udhaifu wa kiutendaji

Zaidi, soma https://jamii.app/WatumishiWasimamaKaziUmwagiliaji
SIMBA SC YAKABIDHIWA KOMBE LAKE LA LIGI KUU BARA

- Imekabidhiwa kombe hilo na Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola katika Uwanja wa Jamhuri mkoani Morogoro

- Imefanikiwa kumaliza ligi ikiwa na alama 93 baada ya leo kutoka suluhu ya goli 0-0 dhidi ya Mtibwa Sugar
KENYA: GAVANA ATOA SIKU 30 MAJENGO YA NAIROBI YAKARABATIWE NA KUPAKWA RANGI

> Gavana Mike Sonko amesema uongozi wake utawachukulia hatua watu wote watakaokiuka agizo hilo

> Amesema Nairobi ni Jiji la biashara hivyo ni lazima liwe safi

Zaidi, soma => https://jamii.app/SonkoNairobiBuildings
BENKI YA DUNIA: MAZINGIRA YA BIASHARA TANZANIA YAMEZIDI KUWA MABAYA

> Afisa wa WB, Yutaka Yoshino amesema mazingira ya biashara yameshuka kwa nafasi 12 ndani ya miaka 2 iliyopita

> 89% ya bidhaa za viwandani na 97% ya ajira nazo zinatokana na sekta binafsi

Soma > https://jamii.app/WBVsTanzaniaEconomy
MICHEZO: Klabu ya Kagera Sugar pamoja na Klabu ya African Lyon zashuka daraja baada ya kuvurunda katika michezo ya ligi

> Watanzania watazikosa timu hizo kwenye msimu ujao wa Ligi Kuu Tanzania bara

#JFSports
NAMANGA MPAKANI: ZAIDI YA MAGARI YA MIZIGO 100 YAKWAMA TRA, YABEBESHWA LAWAMA

> Inadaiwa TRA na Mawakala wa Forodha wameshindwa kukubaliana juu ya tafsiri ya sheria katika utozwaji kodi

> TRA ilikubali kutumia utaratibu wa zamani wakati ufumbuzi ukitafutwa

Soma > https://jamii.app/TRAVsForodhaNamanga
JAPAN: WAWILI WAFARIKI NA 17 KUJERUHIWA KATIKA SHAMBULIO LA KISU

- Waliofariki ni mwanafunzi wa Kike mwenye miaka 11 na Mzazi mwenye miaka 39

- Mshambuliaji huyo mwenye miaka 50, aliwalenga wanafunzi wa shule waliokuwa wakisubiri basi

Zaidi, soma https://jamii.app/ShambulioKisuJapan-Mei2019
GENNARO GATTUSO AJIUZULU KUIFUNDISHA AC MILAN

- Amejiuzulu baada ya klabu hiyo kushindwa kufuzu kushiriki michuano ya Klabu Bingwa Ulaya kwa msimu ujao wa 2019/20

- Amekuwa kocha wa timu hiyo kwa miezi 18 na anaondoka akiwa amebakiza miaka miwili katika mkataba wake