JamiiForums
53K subscribers
34.3K photos
2.42K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
SAKATA LA BREXIT: WAZIRI MKUU THERESA MAY AJIUZULU

> Theresa May atasalia kuwa kiongozi wa chama cha Wahafidhina hadi Juni 7 atakapochaguliwa kiongozi mpya

> Amekuwa akikosolewa kwa kushindwa kuleta mkakati sahihi wa Uingereza kujitoa ndani ya EU

Soma => https://jamii.app/MayAjiuzulu

#MayResigns
ONGEZEKO LA WATALII LACHOCHEA MAPATO SEKTA YA UTALII KUONGEZEKA

> Idadi ya watalii walioingia nchini imeongezeka kutoka 1,327,143 mwaka 2017 hadi kufika watalii 1,505,702 mwaka 2018 na ongezeko hilo limechangia kuongezeka kwa mapato yatokanayo na utalii kutoka dola bilioni 2.2 mwaka 2017 hadi kufikia dola bilioni 2.4 mwaka 2018

Soma - https://jamii.app/OngezekoWataliiMapato
KENYA: MCHUNGAJI AKUTWA AKIFUKUA MAKABURI ILI AUZE SHAMBA

> Polisi katika eneo la Naivasha, Kaunti ya Nakuru wamemkamata Samuel Macharia, baada ya kumfuma akifukua miili ya watu wa familia yake, ili auze shamba

> Alikuwa amefukua miili ya watu watatu kati ya saba iliyopo katika shamba hilo

Soma - https://jamii.app/MchMakaburiShamba
SAKATA LA WATUHUMIWA 17 KUTOROKA GEITA: WAZIRI KANGI LUGOLA AWASIMAMISHA KAZI WAKUU WA POLISI

> Waliosimamishwa kazi ni Mkuu wa Polisi Wilaya ya Geita, Mkuu wa Kituo cha Polisi na Mkuu wa Upelelezi Geita

Soma > https://jamii.app/LugolaPolisiGeita
MAREKANI YAMFUNGULIA MASHTAKA MAPYA JULIAN ASSANGE

> Imemfungilia mashtaka mapya muasisi wa tovuti ya Wikileaks, ikimtuhumu kuiweka Marekani katika kitisho cha kukumbwa na "madhara makubwa" kwa kuchapisha nyaraka mnamo mwaka wa 2010

> Inadai alisaidia katika wizi wa nyaraka za siri na akazichapisha hovyo

Soma - https://jamii.app/USCaseAssange
#JFInternational
NAIROBI, KENYA: MAHAKAMA YAAMUA USHOGA KUENDELEA KUWA KOSA LA JINAI

> Mahakama Kuu imeamua sheria inayozuia mahusiano na ndoa za jinsia moja iendelee kutumika

> Nchini humo wanaokutwa na hatia ya kuwa na makosa hayo wanaweza kufungwa miaka 14

Soma > https://jamii.app/LGBTQVsKenyaJudiciary
WATU MILIONI 3 HUNG'ATWA NA NYOKA KILA MWAKA, LAKI 4 HUPATA ULEMAVU

> Shirika la Afya duniani limezindua mkakati mpya unaolenga kupunguza vifo na majeraha yanayotokana na kung’atwa na nyoka

> Imebainika kati ya watu laki 4, mpaka 4.5 hukumbwa na ulemavu wa kudumu na madhara mengine

Soma - https://jamii.app/WorldSnakeBites
Je, Askari Polisi anatakiwa kukubali kila amri aliyopewa na Waziri, Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya?

> Jibu ni hapana, Askari wa Jeshi la Polisi ni lazima atii amri ikiwa tu ni halali na anaweza akawajibika kwa chochote kibaya atakachokifanya kwa mujibu wa amri atakayokuwa amepewa

Zaidi, soma => https://jamii.app/Mambo101Polisi

#JFCivicSpace
UKRAINE: RAIS APIGA MARUFUKU PICHA YAKE KUWEKWA KWENYE MAOFISI

> Rais mpya wa Ukraine, Volodymyr Oleksandrovych Zelensky amepiga marufuku picha yake kuwekwa kwenye ofisi za umma kwa kile alichodai kuwa Urais sio umaarufu

> Amesema kila mmoja aweke picha ya watoto wake ili awe anaitazama kila anapofanya maamuzi kwa ajili ya nchi hiyo

Soma - https://jamii.app/ZuioPichaRais
MUME WANGU ANAISHI MAISHA DUNI, PESA YOTE INAISHIA KWA NDUGU

> Mdau wa JamiiForums anasema mumewe anamshangaza kwa maisha anayoishi kwani hata akipata mshahara au marupurupu yeye huhangaika kuwasaidia nduguze kijijini hadi anasahau kufanya maendeleo

Soma https://jamii.app/MumeVsNdugu
VENEZUELA: WAFUNGWA 25 WAFARIKI BAADA YA KUZUKA KWA GHASIA GEREZANI

> Ghasia hizo zimetokea katika gereza la Acarigua ambalo lilijengwa kwa ajili ya Wafungwa 250 lakini kwa sasa lina Wafungwa 540

> Katika tukio hilo Askari 20 wamejeruhiwa

Soma > https://jamii.app/VifoGerezaVenezuela
DR CONGO: Rais Felix Tshisekedi amemteua Robert Kidiaba kuwa Waziri wa Michezo

- Robert Kidiaba aliwahi kuwa mlinda mlango wa TP Mazembe na Timu ya Taifa ya DRC

- Januari 2019, Kidiaba alishinda Ubunge wa Jimbo la Katanga

Zaidi, soma > https://jamii.app/KidiabaWaziriDRC

#JFLeo #JFSports
MADIWANI WATAKA MUONGOZO WA KUFUNGUA MADAI YA MALIPO YA KOROSHO

> Wamemtaka Mkuu wa Wilaya ya Masasi, Selemani Mzee, kutoa kauli ya kuwahakikishia ni lini wakulima watalipwa kwa kuwa madiwani hukosa majibu ya uhakika kwenye mikutano ya maendeleo ya kata (WDC), na wanashangazwa kutotekelezwa kwa ahadi ya Serikali ya kuwalipa wenye chini ya kilo 1,500

Soma - https://jamii.app/MadaiMalipoKorosho
UMOJA WA ULAYA: KUJIUZULU KWA MAY HAKUTABADILI MPANGO WA BREXIT

> Umoja wa Ulaya umesema kuwa kujiuzulu kwa Waziri Mkuu wa Uingereza hakutobadili chochote kwenye msimamo wake wa makubaliano yaliyofikiwa kuiwezesha Uingereza kujiondoa kwenye Umoja huo

Soma - https://jamii.app/AUBrexitProceeds
MAMA WA KAMBO AMCHOMA MTOTO KWA MAJI YA MOTO

> Binti mwenye umri wa miaka 16 (jina limehifadhiwa) katika Manispaa ya Bukoba amelazwa katika Hospitali ya rufaa akiuguza majeraha anayodai kuyapata baada ya kuunguzwa kwa maji ya moto na mama yake wa kambo baada ya kumkuta akiwa amepika viazi bila kuambiwa

Soma - https://jamii.app/AchomwaMajiMoto
SERIKALI YATOA MUONGOZO KWA WAKAGUZI WA MIFUKO YA PLASTIKI

> Wakaguzi wameagizwa kutotumia nguvu ikiwemo kuwapiga au kuwabeba watu na kuwaweka ndani

> Haitakiwi kuwasimamisha watu au mtu na kumpekua au kupekua mizigo yake ili kutafuta mifuko ya plastiki

> Wakaguzi wanatakiwa kufanya ukaguzi madukani, magengeni, viwandani, masokoni, mipakani, kwenye maduka makubwa na sio kwenye makazi ya watu au magari

Soma - https://jamii.app/UkaguziMifukoPlastiki
KENYA: ZAIDI YA WAVUVI 100 KUTOKA TANZANIA WANASHIKILIWA KENYA

> Wanashikiliwa ktk Kaunti ya Kilifi kwa tuhuma za kuvuka mipaka ya uvuvi

> Wamekamatwa katika maeneo ya ziwa ya Kilifi, Watamu, Wesa, Ngomeni, Malindi, Uyombo, Mayungu na Kipini

Soma > https://jamii.app/WavuviTzVsKenya
JAFO: SHULE YA ASHIRA ILICHOMWA MOTO KWASABABU ZA HUJUMA

> Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), amesema moto ulioteketeza mabweni mawili ya Sekondari ya Wasichana ya Ashira umesababishwa na hujuma na ameagiza ufanyike uchunguzi wa kina na kwa haraka ili wahusika wachukuliwe hatua za kisheria

Soma - https://jamii.app/HujumaMotoAshiraSec
PAPUA NEW GUINEA: WAZIRI MKUU AJIUZULU

> Peter O’Neill amejiuzulu baada ya kutofautiana na Wabunge wa chama chake wakidai ameshindwa kuongoza vema na kupelekea uchumi kushuka na hali ngumu ya maisha

> Sir Julius Chan atachukua nafasi hiyo

Soma https://jamii.app/PMResignsPNG
MALAWI: MAHAKAMA KUU YAAMURU KURA KUHESABIWA UPYA

> Imeamuru kutotangazwa matokeo ya Urais hadi kura ktk Majimbo 10 zirudiwe kuhesabiwa

> Ni baada ya chama kikuu cha upinzani, Malawi Congress Party(MCP) kwenda kushitaki wakidai kura kuibwa

Soma https://jamii.app/MalawiVoteRecount