JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
RUVUMA: Mhashamu Damian Denis Dallu, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Songea ametoa wito kwa Viongozi mbalimbali wanapostaafu waiache Serikali mpya kufanya kazi kwa uhuru kwani inakuwa tayari ina mipango yao.

Ameyasema hayo katika maadhimisho la Misa Takatifu ya Jubile Kuu ya Ukristo ya Waseminari wa Jimbo Kuu Katoliki Songea, iliyofanyika katika Kanisa Kuu la Kiaskofu la Mtakatifu Matias Mulumba Kalemba Jimbo Kuu Katoliki Songea, Agosti 23, 2025.

Soma https://jamii.app/AskofuDalluWastaafu

#JamiiAfrica #JamiiForums #Governance #JFUtawalaBora
1👍1
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DODOMA: Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa imempitisha aliyekuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Uchaguzi Tanzania (NEC), Dkt. Wilson Mahera Charles kuwa Mgombea Ubunge Jimbo la Butiama katika Uchaguzi Mkuu 2025.

Ikumbukwe, Dkt. Mahera aliteuliwa Oktoba 1, 2019 na Hayati Rais John Pombe Magufuli kuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, baadaye Februari 26, 2023 aliteuliwa na Rais Samia Suluhu kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Soma zaidi https://jamii.app/DktMahera

#JamiiAfrica #JamiiForums  #UchaguziMkuu2025 #Siasa
NIGERIA: Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Mamlaka, Agosti 23, 2025, Jeshi la Anga limewaokoa Watu 76 waliokuwa wametekwa nyara, wakiwemo Wanawake na Watoto, baada ya kufanya shambulio la angani kwa usahihi kwenye ngome ya majambazi katika Jimbo la Katsina Kaskazini Magharibi.

Operesheni hiyo ililenga eneo la Pauwa Hill katika Halmashauri ya Kankara kama sehemu ya msako dhidi ya kiongozi wa genge kwa jina la Babaro, anayetuhumiwa kuhusika na shambulio la msikiti Mjini Malumfashi. Wakati wa uokoaji, Mtoto mmoja alipoteza maisha, ingawa haijabainika kama kulikuwa na vifo vingine vya mateka au wanachama wa genge.

Shambulio hilo linaweza kuashiria hatua muhimu katika jitihada za kuvunja mitandao ya uhalifu kaskazini magharibi mwa #Nigeria, ambako makundi yenye silaha yamekuwa yakiwatisha wakazi wa vijijini kwa miaka mingi.

Soma zaidi https://jamii.app/JeshiNigeria

#JamiiAfrica #JamiiForums #Uwajibikaji #HumanRights
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Sheikh Iddi Abdallah Chaurembo amewaombea wale wote wanaopanga kuleta chuki, kutumia mitandao kudhuru au kuhujumu kura, wapate upofu ili wasifanikiwe katika mipango yao.

Ameyasema hayo leo, Agosti 24, 2025, wakati akishiriki Kongamano la Amani kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025, lililoandaliwa na Umoja wa Maimamu Tanzania (#UMATA) na kufanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, kongamano hilo pia limehudhuriwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

Zaidi soma https://jamii.app/SheikhChauremboUpofu

#JamiiAfrica #JamiiForums #UchaguziMkuu2025 #Demokrasia
Media is too big
VIEW IN TELEGRAM
LINDI: Baadhi ya Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (#CCM) Jimbo la Nachingwea wamerudisha vifaa mbalimbali na kadi za chama huku wakionekana kutoridhishwa na jambo fulani wakati wa kikao kilichohusisha Wananchi mbalimbali.

Akielezea tukio linaloonekana katika video inayosambaa Mtandaoni ikidaiwa limetokea jana Agosti 23, 2025, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nachingwea, Longinus Nambole amesema “Eneo hilo kuna mgogoro wa muda mrefu wa Wakulima na Wafugaji, hivyo inawezekana Wananchi wametumia nafasi hiyo kufikisha ujumbe kuwa hawaridhishwi na maamuzi ya Viongozi.”

Ameongeza “Unajua CCM ndio chama Tawala hivyo kama chenyewe hakifanyi maamuzi sahihi basi Wananchi wanaonesha hisia zao kwa kwa kukiadhibu Chama, lakini nitafuatilia zaidi kujua kilichotokea.”

Soma zaidi https://jamii.app/Nachingwea

#JamiiAfrica #JamiiForums #Siasa #UchaguziMkuu2025 #Demokrasia
1
Wakati Wazazi wao wakiwa ni maarufu kwa makubwa waliyoyafanya kwenye mchezo wa soka, wao wameshindwa kufikia angalau nusu ya mafanikio ya kile ambacho baba zao walikifanya walipokuwa wakicheza.

Enzo Zidane mtoto wa #ZinedineZidane ‘Zizzou’, Romeo Beckham mtoto wa #DavidBeckham na Cristian Totti kijana wa #FrancescoTotti.

Enzo alistaafu kwa sababu aliona hawezi kufika mbali kwenye soka, Romeo sababu Brentford FC haikumpa mkataba mpya kwa kutoridhishwa na kiwango chake wakati Cristian amestaafu kutokana na sababu za kuonekana haoneshi dalili za kufikia mafanikio ya baba yake.

Zaidi soma https://jamii.app/EarlyRetirement

#JFSports #JamiiAfrica #JamiiForums
MICHEZO: Wikiendi inaelekea kumalizika, haya ni baadhi ya matokeo katika Ligi na Michuano mbalimbali Duniani.

Ngazi ya klabu, timu kutoka Jiji la Manchester hazijapata ushindi, moja imepigwa nyingine imepata sare, #Arsenal, #Chelsea, #BayernMunich zote zimepata ushindi mnono.

Tembelea JamiiForums.com kushiriki kwenye mijadala mbalimbali inayohusu Soka.

#JFSports #JamiiForums #JFEPL2025 #JamiiAfrica #CHAN2024 #JFBundesliga2025
Mdau wa JamiiForums.com kutoka Jukwaa la Mahusiano, Mapenzi na Urafiki anaomba ushauri kuhusu changamoto ya mahusiano anayopitia, ameeleza kuwa awali aliwahi kuwa kwenye uhusiano wa mapenzi ya dhati, baadaye alisalitiwa hadi mpenzi wake akapata ujauzito wa mwanaume mwingine.

Anasema kwa sasa ana mwenza mpya na uhusiano wao upo vizuri, lakini bado anapata ugumu kuamini masuala ya ndoa, kwani kila akikumbuka yaliyompata huko nyuma moyo wake unakuwa mgumu.

Kushiriki mjadala soma https://jamii.app/KupendaTena

#JamiiForums #JamiiAfrica #JFMahusiano
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
DAR: Akizungumza leo Agosti 24, 2025 kwa njia ya Mtandao, Mwanasiasa na Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole amesema, “Mungu akituvusha, nashauri Sheria irekebishwe ili Viongozi (Rais) wawajibishwe kwa kushtakiwa kwa makosa waliyoyafanya wakiwa madarakani.”

Soma https://jamii.app/PolepoleTumeuzwa

#JamiiAfrica #JamiiForums #Uwajibikaji #Siasa
👍1