JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
2
AFRIKA KUSINI: ADUKUA MTANDAO WA SERIKALI NA KUJIAJIRI

- Bright Chabola alidukua Mtandao wa Serikali kwenye sekta ya Afya na kujiajiri kama Msimamizi wa Mfumo

- Alijilipa shilingi 1,100,000 kuanzia Juni, 2018 na hakuwa akienda kazini

- Kwa sasa anatafutwa na polisi

Soma https://jamii.app/ZAMdukuzi
MICHEZO: Timu ya Vijana chini ya miaka 17 ya Tanzania(Serengeti Boys) imecheza na timu ya Nigeria katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

> Mchezo huo umekamilika kwa Serengeti Boys kufunga 4 na Nigeria kufunga 5
Ligi Kuu ya England: Mpira ni Mapumziko na Matokeo ni Liverpool 0-0 Chelsea
TABORA: MWANAMKE AUA WATOTO 6 NA KUJERUHI WENGINE WANNE

- Mkazi wa Kijiji cha Luzuko, Kata ya Mizibaziba Wilayani Nzega, Nana Maganga anadaiwa kuua watoto wake watano na mmoja wa kaka yake

- Hata hivyo, Mwanamke huyo naye alifariki katika mazingira ya kutatanisha ambapo inadaiwa aliuawa

Zaidi, soma https://jamii.app/AuaWatoto6TBR
SUDAN KUMSHTAKI BASHIR ILA HAITAMPELEKA ICC

- Kamati ya Kijeshi ya Mpito inayoongoza Sudan kwa sasa imebainisha

- Bashir anakabiliwa na mashtaka 5 ya Kiuhalifu dhidi ya binadamu na mawili ya uhalifu wa kivita katika Mahakama ya ICC

Zaidi, soma https://jamii.app/BashirHapelekwiICC
TIGER WOODS ASHINDA TAJI KUBWA BAADA YA MIAKA 11

- Mchezaji huyo wa golf ameibuka mshindi katika mashindano ya 'Masters' na kutwaa taji maarufu la 'Koti la Kijani'

- Mara ya mwisho alishinda taji kubwa mwaka 2008 aliposhinda taji la ‘U.S Open’

Zaidi, soma https://jamii.app/WoodsWinsMastersAftr11yrs
SERIKALI KULETA MABEHEWA NA VICHWA VYA TRENI YA UMEME 1,400

- Msemaji wa Serikali, Dkt. Hassan Abbas amebainisha kupitia ukurasa wake wa Twitter

- Aidha, Julai mwaka huu, kichwa cha treni ya umeme kitaletwa kwa majaribio kwenye SGR

Zaidi, soma https://jamii.app/VichwaTreni1400
DODOMA: BUNGE LIMEAHIRISHWA KWA DHARURA

> Naibu Spika, Dkt. Tulia Ackson alikuwa akiongoza kikao hicho na kutangaza kuwa Wabunge watakutana tena saa 11:00 jioni

> Zipo taarifa kuwa mchana wa leo, Wabunge wa CCM watakutana na Rais Magufuli

#JFLeo
KENYA: MWANAFUNZI WA CHUO ANUSURIKA KUUAWA NA MPENZI WA ZAMANI

- Ni Naomi Chepkemboi, Mwanafunzi wa mwaka wa 3 katika Chuo Kikuu Pwani katika Kaunti ya Kilifi

- Inaelezwa aliyemvamia ni Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Kenyatta, Henry Kipkoech

Zaidi, soma https://jamii.app/StudentStabbedKE
MBEYA: MTOTO ALIYETEKWA ANYONGWA HADI KUFA

> Mtekaji alimtaka Baba wa Mtoto, Junior Bakari Siame atume Tsh. Milioni 10 ili asimdhuru mtoto

> Baba wa Mtoto alijitahidi na kumtumia Mtekaji shilingi elfu 30 lakini akaambiwa hela haitoshi atume nyingine

Soma > https://jamii.app/UtekajiMbeya
MIAKA 30 TANGU MASHABIKI 96 WA LIVERPOOL WAFARIKI UWANJANI

- Ni Aprili 15, 1989 ambapo wengine 766 walijeruhiwa baada ya jukwaa kuanguka

- Tukio lilitokea katika uwanja wa Hillsborough wakati wa mchezo kati ya Liverpool na Nottingham Forest

Zaidi, soma https://jamii.app/Remember96Liverpool
TIMU 4 ZA TANZANIA KUSHIRIKI MICHUANO YA CAF 2020/21

- Timu 2 zitashiriki Klabu Bingwa na 2 zitashiriki michuano ya Shirikisho

- Ni baada ya Tanzania kuwa ya 12 katika viwango vya CAF kutokana na Simba kufika robo fainali ya Klabu Bingwa

Zaidi, soma https://jamii.app/Timu4CAF-TZ
CHAD: SHAMBULIO LA BOKO HARAM LAUA WANAJESHI 7

> Katika shambulio hilo lililotokea katika Jimbo la Ziwa Chad, Askari wengine 15 wa Jeshi la nchi hiyo wamejeruhiwa

> Chambulio hili limefanyika usiku katika Kituo cha Jeshi cha Bohama

Soma => https://jamii.app/BokoShambulioChad
VYAMA VYA UPINZANI VYATAKA SPIKA WA BUNGE KUJISHUSHA

- Vyama vya siasa vya upinzani nchini vimemtaka Spika wa Bunge, Job Ndugai kujishusha kufuatia sakata baina ya Bunge na CAG

- Vimedai sakata hilo limesababisha mgongano baina ya Mamlaka

Zaidi, soma https://jamii.app/UpinzaniSpikaAjiuzulu
UCHUMI: TRA YAKUSANYA TRILIONI 11.96 KWA MIEZI TISA

> Makusanyo hayo ni kuanzia Julai 2018 - Machi 2019

> Mchanganuo wa miezo 3 ya mwaka 2019. Trillioni 1.30 Januari, Trillioni 1.23 Februari na Trillioni 1.43 Machi

Soma > https://jamii.app/TRAMakusanyo
MAREKANI: Mbunge Ilhan Omar mwenye asili ya Somalia amemlaumu Rais Trump kwa kuchochea vitisho vya yeye kuuawa

> Muwakilishi huyo wa Jimbo la Minnesota aliilaumu Marekani kwa kuwazuia Wakimbizi kutoka mataifa ya kiarabu kuingia nchini humo

Soma > https://jamii.app/IlhamVsTrump
BEIJING, CHINA: WATU 10 WAFARIKI BAADA KIWANDA CHA DAWA KULIPUKA

> Wamefariki baada ya kukosa hewa kutokana na moshi uliosababishwa na moto huo

> Wakati huo huo, Wafanyakazi 12 wa kikosi cha zima moto wakijeruhiwa wakati wakizima moto huo

#JFInternational
UFARANSA: KANISA LA KIHISTORIA LATEKETEA KWA MOTO

> Kanisa la Notre Dame lenye umri wa miaka 850 limewaka moto jioni ya leo

> Moto huo umesababisha sehemu ya kanisa hilo kuanguka

> Rais Macron amelazimika kuahirisha hotuba yake

Soma > https://jamii.app/NotreDame