JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UCHAGUZI MKUU INDIA: RAIA WAANZA KUPIGA KURA

> Watu milioni 900 wanatarajiwa kupiga kura katika uchaguzi huu katika majimbo 20 ya nchi hiyo yaliyogawanywa na kuzaa majimbo ya uchaguzi 91

> Unatajwa kuwa ndio uchaguzi mkubwa zaidi Duniani

Soma > https://jamii.app/IndianElection
PICHA ZA KWANZA ZA TOBO JEUSI KWENYE SAYARI ZAPATIKANA

> Wanaanga wamefanikiwa kuchukua picha za kwanza ya tobo jeusi (black hole) ambalo linapatikana katika sayari iliyo mbali lenye ukubwa wa Kilomita bilioni 40 kwa upana ikiwa ni mara milioni 3 zaidi ya dunia

> Shimo hilo jeusi lipo umbali wa kilomita milioni 500 na lina uzito mara bilioni 6.5 zaidi ya Jua

Soma - https://jamii.app/1stPicsBlackHole
SUDAN: RAIS BASHIR AACHIA NGAZI NA KUWEKWA CHINI YA ULINZI

- Omar Hassan al-Bashir aliingia madarakani mnamo Juni 30, 1989 akiwa Rais wa 7 wa taifa hilo

- Kwa wakati wote Bashir ameitawala Sudan kupitia Chama cha National Congress Party(NCP)

Soma > https://jamii.app/SudanCoup
UCHAGUZI MKUU INDIA: RAIA WAANZA KUPIGA KURA

> Watu milioni 900 wanatarajiwa kupiga kura katika uchaguzi huu katika majimbo 20 ya nchi hiyo yaliyogawanywa na kuzaa majimbo ya uchaguzi 91

> Unatajwa kuwa ndio uchaguzi mkubwa zaidi Duniani

Soma > https://jamii.app/IndianElection
JULIAN ASSANGE, MWANZILISHI WA MTANDAO WA WIKILEAKS AKAMATWA

> #WikiLeaks ilichapisha taarifa za siri za Serikali mbalimbali mwaka 2010

> 2012 alikimbilia ndani ya Ubalozi wa Ecuador Jijini London baada ya kuanza kusakwa na US & Sweden

Soma > https://jamii.app/AssangeArrested
DIEGO COSTA AFUNGIWA MICHEZO 8 KWA KUMTUSI MAMA WA MUAMUZI

> Mshambuliaji huyo wa Atletico Madrid amekutwa na hatia ya kumtukana Mama wa muamuzi, Jesus Manzano

> Alitolewa kwa kadi nyekundu wakati timu yake ikinyukwa bao 2 - 0 na Barca

Soma > https://jamii.app/CostaBanned
KILIMANJARO: TAKUKURU YAWAKAMATA MAOFISA WA NIDA

> Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoani Kilimanjaro, inawashikilia Maofisa wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wakituhumiwa kushirikiana na matapeli (akiwemo Mwalimu wa Sekondari) kuwauzia wananchi vitambulisho ambavyo kwa kawaida vinapaswa kutolewa bure

Soma - https://jamii.app/MaofisaNIDAMbaroni
UFARANSA YATAKA UCHAGUZI MPYA ILI KUMTOA MACRON

> Christian Jacob, Naibu Mwenyekiti wa chama cha Republican cha mrengo wa kulia amesema kuwa Rais Emmanuel Macron amepoteza heshima na uaminifu kutoka kwa wananchi na hivyo uchaguzi mpya unapaswa kuandaliwa

Soma - https://jamii.app/RepublicanYatakaUchaguzi
INDIA: MWANAFUNZI (MKENYA) AHUKUMIWA JELA MAISHA KWA UBAKAJI

> Mahakama nchini India imemhukumu kifungo cha maisha jela Eric Mulinge Nethuli (26) ambaye ni raia wa Kenya kwa kosa la kumbaka Mkenya mwenzake (22) mnamo mwaka 2016

> Kijana huyo alialikwa kwa ajili ya chakula cha usiku na akaitumia fursa hiyo kumbaka

Soma - https://jamii.app/MkenyaJelaUbakajiIndia
MKURUGENZI WA VODACOM AKIRI MAKOSA

> Hisham Hendi na wenzake 8 wamekiri mashtaka 10 yaliyokuwa yakiwakabili likiwemo la kuongoza genge la uhalifu

> Katika kesi yao wanatuhumiwa kwa kuisababishia Serikali hasara ya shilingi bilioni 5.89

Soma > https://jamii.app/KesiHishamVoda
RWANDA KUSHTAKIWA KWA KUFUNGA MPAKA WAKE NA UGANDA

> Mfanyabiashara wa Uganda amefikisha ombi la kuishtaki Rwanda katika Mahakama ya haki ya Afrika Mashariki kwa tuhuma za kuvunja mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na tayari ombi hilo limewasilishwa rasmi kwa Mkuu wa Sheria wa Rwanda

> Anataka fasiri ya uhalali wa hatua ya Rwanda kuzuia bidhaa na wafanyabiashara wa Uganda tangu Februari 27, 2019

Soma - https://jamii.app/RwandaUgandaMahakamani
MKURUGENZI WA VODACOM AACHIWA HURU

- Hisham Hendi na wenzake 8, wamelipa faini ya Tsh. Bilioni 6.01 baada ya kukiri mashtaka

- Walishtakiwa kwa kuingiza, kutumia, kusimika vifaa vya mawasiliano na kugawa namba za simu bila leseni ya TCRA

Soma https://jamii.app/KesiHishamVoda
KENYA: SHIRIKA LA NDEGE LASITISHA SAFARI ZAKE SUDAN

> Shirika la ndege la nchini Kenya limesimamisha usafiri wa ndege zake kutoka na kwenda nchini Sudan kufuatia kuondolewa madarakani kwa Rais Omar al-Bashir

> Tangazo hilo limetolewa jana usiku kufuatia maandamano ya kisiasa yaliyoleta kuanguka kwa utawala wa Rais Bashir

Soma - https://jamii.app/KenyaAirwaysSudan
SUGU ADAI WASTAAFU WA MAGEREZA NA POLISI BADO WANAISHI KOTA, HAWANA NAULI ZA KURUDI KWAO

> Mbunge huyo wa Mbeya Mjini amedai tangu Rais Magufuli aingie madarakani ni takribani miaka 4 na hajawahi kuongeza mishahara hata kidogo

Zaidi, soma => https://jamii.app/SuguVsMagufuliWatumishi

#JFLeo
KENYA: MAJINA KWENYE CHETI YASABABISHA BABA KUUA MTOTO WAKE

> Polisi mjini Murang'a wamemkamata Paul Njuguna Njogore (25) anayedaiwa kumuua Collins Waweru (5) baada ya mama kukataa kuweka majina ya baba huyo kwenye cheti cha kuzaliwa cha mtoto

> Paul alimuua Collins akiwa usingizini kwa kumkata na panga

Soma - https://jamii.app/BabaAuaMtotoCheti
#JFInternational
SUDAN: WAZIRI WA ULINZI AWA RAIS WA MPITO, MKUU WA MAJESHI MAKAMU WAKE

> Waziri wa Ulinzi wa Sudan Awadh Ibn Auf ameapishwa kuwa Rais wa Baraza la Mpito la kijeshi kwa kipindi cha miaka miwili na Mkuu wa Majeshi Kamal Andel-Marouf ameapishwa kuwa Makamu wa Rais wa Baraza hilo

Soma - https://jamii.app/SudanInterimPresd
#JFInternational
PAKISTAN: WATU 14 WAUAWA KWENYE MLIPUKO WA BOMU

> Mlipuko huo umetokea Kusini Magharibi mwa nchi hiyo katika Soko la Quetta lililopo katika Mji wa Baluchistan

> Baluchistan ni Mkoa wa Pakistan unaokabiliwa na mdororo wa usalama

Zaidi, soma > https://jamii.app/MlipukoPakistan
KENYA: MADAKTARI WAWILI KUTOKA CUBA WATEKWA

> Walitumwa kufanya kazi kwenye Kaunti ya Mandera na wametekwa nyara na washukiwa wa Al-Shabaab mjini hapo

> Mmoja kati ya walinzi wa madaktari hao ameuawa huku mwingine akifanikiwa kutoroka

Soma - https://jamii.app/CubaDoctorsAbductedKE
MWILI WA ALIYEKUWA AFISA WA WIZARA WAFUKULIWA NA KUVULIWA NGUO

> Mary Maramo alizikwa jana huko Pugu. Mwili wake umefukuliwa na watu wasiojulikana usiku wa kuamkia leo

> Uchunguzi unaendelea ili kujua endapo mwili huo umeingiliwa kimwili

Soma > https://jamii.app/MwiliWafukuliwaPugu
WABUNGE WATAKA MADIWANI WAONGEZEWE POSHO

> Imeelezwa kuwa Halmashauri nyingi nchini hazijawalipa posho madiwani kwa zaidi ya miezi sita, badala yake zimekopa fedha zao

> Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia (CCM) amesema Halmashauri ya Chemba inekopa posho za madiwani tangu Oktoba, 2018

Soma - https://jamii.app/MadiwaniMitaaPosho