JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
IMF: UCHUMI WA TANZANIA UNATARAJIWA KUKUA KWA 4% (SERIKALI ILIKADIRIA 7.3%)

> IMF yashusha makadirio yake ya ukuaji wa uchumi nchini kwa mwaka 2019 na 2020

> Uchumi unatarajiwa kukua kwa 4% 2019 na 4.2% kwa 2020. Mwaka 2018 ilikuwa 6.6%

Soma https://jamii.app/IMFVsTzEconomy

#JFUchumi
Nukuu ya Rais Magufuli leo Aprili 10, 2019 akiwa Mkoani Njombe
UTEKELEZAJI WA HUKUMU YA KIFO WAPUNGUA DUNIANI

> Kwa mujibu wa ripoti ya Shirika linalotetea #HakiZaBinadamu la Amnesty International, Takribani nchi 20 zilitekeleza hukumu hiyo kwa watu 690 mwaka 2018, ikiwa chini kwa 31% kutoka kiasi cha watu 993 mwaka 2017

> Upunguaji umeonekana nchini Iraq, Iran, Pakistan na Somalia

Soma - https://jamii.app/TakwimuHukumuKifo
#JFLeo
MUIGIZAJI MKONGWE AIBUKA NA BIDHAA YA BANGI INAYOTULIZA MAUMIVU WAKATI WA HEDHI

> Mtetezi wa matumizi sahihi ya bangi, Whoopi Goldberg(60) amesema amebuni bidhaa hiyo ili kuwaokoa Wanawake kwasababu maumivu ya hedhi sio ya utani

Zaidi, soma => https://jamii.app/BangiKwaHedhi

#JFLeo
KENYA: YAYA ALIYETOROKA NA MTOTO WA MWAJIRI AKAMATWA

> Sharon Chepkoech (24) alikamatwa siku ya Jumatano, Aprili 10, baada ya kutoroka na mtoto wa miezi miwili na kisha kutuma ujumbe wa simu akimtaka mama wa mtoto ampatie pesa kiasi cha Ksh 10,000

> Alitishia kusafiri na mtoto huyo hadi nchini Malawi iwapo hangepewa pesa alizokuwa akizitaka

Soma - https://jamii.app/YayaToroshaMtoto
#JFInternational
BREAKING: Jeshi nchini #Sudan linadaiwa kumwondoa madarakani Rais Omar a-Bashir

> Ikulu inadaiwa kuwa chini ya ulinzi mkali wa Jeshi
> Maafisa wa juu wa Serikali wanashikiliwa
> Uwanja wa Ndege wafungwa

Taarifa zaidi, soma https://jamii.app/SudanCoup
SERIKALI KUAJIRI WATUMISHI 44,807. WENGINE 290,625 KUPANDISHWA VYEO

> Katika mwaka wa fedha 2019/20, miongoni mwa kada zitakazoajiri watumishi wengi ni Elimu (13,526), Afya (9,467), Jeshi la Polisi (3,725)

> Pia watumishi 290,625 watapandishwa vyeo kulingana na maelekezo yatakayotolewa

> Aidha, bodi itafanya utafiti wa hali ya mishahara na maslahi katika vyombo vya ulinzi na usalama ili kushauri namna bora ya kutoa motisha

Soma - https://jamii.app/AjiraVyeoMishahara
TAHADHARI: KUNA MLIPUKO WA UGONJWA WA DENGUE NCHINI

> Kwa mujibu wa taarifa kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jinsia na Watoto Wagojwa 200 wa Dengue wameripotiwa

> Wananchi wametakiwa kufika katika vituo vya afya na kupima endapo wataona mabadiliko katika afya zao

Soma > https://jamii.app/DengueDar
UCHAGUZI MKUU INDIA: RAIA WAANZA KUPIGA KURA

> Watu milioni 900 wanatarajiwa kupiga kura katika uchaguzi huu katika majimbo 20 ya nchi hiyo yaliyogawanywa na kuzaa majimbo ya uchaguzi 91

> Unatajwa kuwa ndio uchaguzi mkubwa zaidi Duniani

Soma > https://jamii.app/IndianElection
PICHA ZA KWANZA ZA TOBO JEUSI KWENYE SAYARI ZAPATIKANA

> Wanaanga wamefanikiwa kuchukua picha za kwanza ya tobo jeusi (black hole) ambalo linapatikana katika sayari iliyo mbali lenye ukubwa wa Kilomita bilioni 40 kwa upana ikiwa ni mara milioni 3 zaidi ya dunia

> Shimo hilo jeusi lipo umbali wa kilomita milioni 500 na lina uzito mara bilioni 6.5 zaidi ya Jua

Soma - https://jamii.app/1stPicsBlackHole
SUDAN: RAIS BASHIR AACHIA NGAZI NA KUWEKWA CHINI YA ULINZI

- Omar Hassan al-Bashir aliingia madarakani mnamo Juni 30, 1989 akiwa Rais wa 7 wa taifa hilo

- Kwa wakati wote Bashir ameitawala Sudan kupitia Chama cha National Congress Party(NCP)

Soma > https://jamii.app/SudanCoup
UCHAGUZI MKUU INDIA: RAIA WAANZA KUPIGA KURA

> Watu milioni 900 wanatarajiwa kupiga kura katika uchaguzi huu katika majimbo 20 ya nchi hiyo yaliyogawanywa na kuzaa majimbo ya uchaguzi 91

> Unatajwa kuwa ndio uchaguzi mkubwa zaidi Duniani

Soma > https://jamii.app/IndianElection
JULIAN ASSANGE, MWANZILISHI WA MTANDAO WA WIKILEAKS AKAMATWA

> #WikiLeaks ilichapisha taarifa za siri za Serikali mbalimbali mwaka 2010

> 2012 alikimbilia ndani ya Ubalozi wa Ecuador Jijini London baada ya kuanza kusakwa na US & Sweden

Soma > https://jamii.app/AssangeArrested
DIEGO COSTA AFUNGIWA MICHEZO 8 KWA KUMTUSI MAMA WA MUAMUZI

> Mshambuliaji huyo wa Atletico Madrid amekutwa na hatia ya kumtukana Mama wa muamuzi, Jesus Manzano

> Alitolewa kwa kadi nyekundu wakati timu yake ikinyukwa bao 2 - 0 na Barca

Soma > https://jamii.app/CostaBanned
KILIMANJARO: TAKUKURU YAWAKAMATA MAOFISA WA NIDA

> Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoani Kilimanjaro, inawashikilia Maofisa wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wakituhumiwa kushirikiana na matapeli (akiwemo Mwalimu wa Sekondari) kuwauzia wananchi vitambulisho ambavyo kwa kawaida vinapaswa kutolewa bure

Soma - https://jamii.app/MaofisaNIDAMbaroni
UFARANSA YATAKA UCHAGUZI MPYA ILI KUMTOA MACRON

> Christian Jacob, Naibu Mwenyekiti wa chama cha Republican cha mrengo wa kulia amesema kuwa Rais Emmanuel Macron amepoteza heshima na uaminifu kutoka kwa wananchi na hivyo uchaguzi mpya unapaswa kuandaliwa

Soma - https://jamii.app/RepublicanYatakaUchaguzi
INDIA: MWANAFUNZI (MKENYA) AHUKUMIWA JELA MAISHA KWA UBAKAJI

> Mahakama nchini India imemhukumu kifungo cha maisha jela Eric Mulinge Nethuli (26) ambaye ni raia wa Kenya kwa kosa la kumbaka Mkenya mwenzake (22) mnamo mwaka 2016

> Kijana huyo alialikwa kwa ajili ya chakula cha usiku na akaitumia fursa hiyo kumbaka

Soma - https://jamii.app/MkenyaJelaUbakajiIndia