JamiiForums
52.5K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MAGARI YAENDAYO KASI YATISHIA UWEPO WA DUMA

- Utafiti warekodi ongezeko la vifo vya wanyama hao katika mbuga ya Serengeti kutokana na kugongwa na magari ya watalii yaendayo kasi licha ya faini kuwa kubwa

- Watafiti wahofia kupotea kwao

Zaidi, soma https://jamii.app/VifoDumaMwendokasi
AFYA: UMUHIMU WA KUOTA JUA ASUBUHI

> Watu wengi huwa na upungufu wa vitamini D kwasababu hawapati mwanga wa Jua ambao huchochea uzalishaji wa seli katika ngozi ya mwili

> Vitamini D husaidia kuboresha afya ya mifupa na meno

Zaidi, soma => https://jamii.app/FaidaZaJua

#JFAfya
MUME AMUUA MKEWE BAADA YA KUMFUMANIA

> Julius Rotich amemuua mkewe katika kijiji cha Kaplelach, Kaunti ya Kericho nchini Kenya baada ya kumfumania akishiriki mapenzi na jamaa mwingine chumbani mwao usiku wa kuamkia Aprili 6

> Alimshambulia mkewe kwa panga na kisha kujisalimisha Polisi

Soma - https://jamii.app/KifoMkeFumanizi
SIMBA NA TEMBO WAUA MTU ANAYEDAIWA KUWA JANGILI

> Mtu aliyedhaniwa kuwa jangili wa wanyama aina ya faru amekanyagwa na Tembo na kuliwa na Simba katika Hifadhi ya Taifa ya Kruger, nchini Afrika Kusini

> Fuvu pamoja na suruali yake vilipatikana siku ya Alhamisi

Soma - https://jamii.app/KifoJangiliMbugani
KAMBI YA UPINZANI KUPANGUA BARAZA LA MAWAZIRI VIVULI

> Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe amesema watapangua Baraza la Mawaziri Vivuli na kuwaondoa wabunge wa CUF kutokana na baadhi yao kumuunga mkono Mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba

> Ikitokea hivyo, CUF imesema wataandika barua kwa Spika Ndugai ili kuomba ziwepo kambi mbili za upinzani Bungeni

Soma - https://jamii.app/WaziriKivuliUpinzani
KILIMANJARO: TAKUKURU YABAINI UFISADI WA BILIONI 1.5

> Ufisadi huo umefanyika katika mradi unaoendelea wa ujenzi wa majengo 6 ya Hospitali ya wilaya ya Siha

> Vifaa vilivyonunuliwa kwa ajili ya mradi viko chini ya kiwango

Soma > https://jamii.app/UfisadiSiha
MAREKANI: WAZIRI WA USALAMA WA NDANI AJIUZULU

> Waziri wa Usalama wa Ndani wa Marekani, Kirstjen Nielsen (46), alijiuzulu Jumapili jioni baada ga mkutano aliofanya na Rais Donald Trump Ikulu mjini Washington DC

> Kamishna wa forodha na ulinzi wa mipakani, Kevin McAleenan, atakaimu nafasi iliyoachwa wazi na Nielsen

Soma - https://jamii.app/KujiuzuluWaziriUsalama
RPC DODOMA: ATAKAYEANDAMANA KESHO ATAPIGWA MPAKA ATACHAKAA

> Kamanda Muroto ametoa kauli hiyo baada ya vijana wa ACT-Wazalendo kutangaza maandamano ya kulishinikiza Bunge kufuta azimio lake la kutofanya kazi na CAG, Profesa Assad

Zaidi, soma => https://jamii.app/RPCDodomaVsACT
BABA MBARONI KWA KUMBAKA MTOTO WAKE

> Jeshi la Polisi Mkoani Geita linamshikilia mkazi wa Kata ya Nyankumbu, Selemani Mathis (35), kwa tuhuma za kumbaka binti yake (4)

> Mtoto huyo alikuwa akiishi na baba yake baada ya wazazi wake kutengana

Soma - https://jamii.app/BabaUbakajiMtoto
UZALISHAJI MIFUKO YA PLASTIKI KUSITISHWA JULAI 2019

> Serikali imesema iwapo watakubaliana na taasisi mbalimbali wanazotarajia kukutana nazo wiki hii wanaweza kupiga marufuku matumizi ya mifuko ya plastiki kuanzia Julai mwaka huu

> Kauli hiyo imetolewa leo Aprili 8 Bungeni, na Waziri January Makamba wakati akijibu swali la Mbunge Magdalena Sakaya

Soma - https://jamii.app/ZuioMifukoPlastiki
LUSINDE: 2020 TUFANYE UCHAGUZI WA MADIWANI NA WABUNGE, RAIS AENDELEE

> Mbunge wa Jimbo la Mtera(CCM), Livingstone Lusinde amesema hatua hiyo itasaidia kupunguza gharama kubwa ambazo taifa itazitumia katika uchaguzi huo

Soma > https://jamii.app/KauliLusinde
POLISI WAUA WATU 5 WANAODHANIWA KUWA MAJAMBAZI

> Watu 5 wanaodhaniwa kuwa majambazi wameuawa baada ya kutokea kwa majibizano ya risasi kati yao na Polisi Wilayani Korogwe mkoani Tanga walipofanya jaribio la uporaji kwenye mashamba ya Mkonge

Soma https://jamii.app/PolisiMajambaziKorogwe
MACHAKOS, KENYA: WATUHUMIWA WATATU WA UTEKAJI WA AFISA WA UMOJA WA MATAIFA WAUAWA

> Walikutwa ktk barabara ya Kitui wakijifanya maafisa wa usalama barabarani na kusimamisha magari ndipo walipowekwa chini ya ulinzi na Askari Polisi

Soma > https://jamii.app/WatekajiKenya
MABOMU YARINDIMA SUDAN, ASKARI WA JESHI WATOA HIFADHI KWA RAIA

> Askari wa Jeshi la Sudan wamechukua hatua ya kuwalinda waandamanaji mjini Khartoum baada ya vikosi vya usalama kufyatua mabomu ya gesi ya kutoa machozi ili kuwatawanya

> Wanajeshi hao waliyafukuza magari yaliyokuwa yakifyatua mabomu

Soma - https://jamii.app/SudanCrisis
AFRIKA KUSINI: ALIYEIGIZA TUKIO LA KUFUFULIWA AFARIKI

> Ni Brighton Moyo, aliyepata umaarufu baada ya kuonekana ktk tukio la kufufuliwa na Mchungaji Lukau

> Yaelezwa alikuwa akiishi na VVU. Aidha, Figo na mapafu pia vilishindwa kufanya kazi

Soma https://jamii.app/AliyefufuliwaAfariki
KERO 11 KATI YA 15 KUHUSU MUUNGANO ZIMETATULIWA

> Serikali imeeleza kwamba, changamoto na kero za muungano ambazo zimetatuliwa mpaka sasa ni 11 kati ya 15 zilizowasilishwa

> Changamoto nne zilizobaki zinaendelea kutafutiwa ufumbuzi na hakuna changamoto iliyoshindikana kupatiwa ufumbuzi

Soma - https://jamii.app/UtatuziKeroMuungano
ZIJUE TOFAUTI KATI YA 2G, 3G, 4G NA 5G

> G kwenye tarakimu hizi inawakilisha Generation, yaani kizazi fulani cha teknolojia ya mawasiliano kwa kuangazia zaidi uwezo wa simu

> Kumekuwa na mabadiliko ya teknolojia kuanzia 1G mpaka 5G

Soma > https://jamii.app/TeknolojiaSimu

#JFTeknolojia
UTASA WAPELEKEA AIBE MTOTO WA MIEZI 6

> Jeshi la Polisi Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga linamshikilia mkazi wa Matejoo Mkoani Arusha, Teddy Stephano (26), ambaye anatuhumiwa kuiba mtoto wa kiume anayekadiriwa kuwa na umri wa miezi sita

Soma - https://jamii.app/MbaroniWiziMtoto
WAZUNGU WALIOCHUKULIWA MASHAMBA YAO KULIPWA

> Serikali ya Zimbabwe hivi karibuni itawalipa malipo ya awali waliokuwa wamiliki wa mashamba ya kibiashara kama fidia ya kuchukuliwa ardhi zao katika mageuzi ya ardhi

> Tathmini inafanyika ili kujua kiasi cha fidia itakayolipwa

Soma https://jamii.app/FidiaWazunguArdhi