JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UTAMADUNI WA KUSHANGAZA: WATOTO(MIAKA 9 & 6) WANAODAIWA KUZALIWA NA MENO, WAOANA

- Baada ya ndoa, Watoto hao walipatiwa nyumba ya kitamaduni kuishi

- Tukio hilo limetoka katika Kijiji cha Nakapyata, Wilayani Buyende nchini Uganda

Zaidi, soma https://jamii.app/WatotoWaonaUG
MAREKANI: BUNGE LAPIGA KURA KUHUSU MISAADA YA KIVITA YEMEN

> Bunge limepiga kura ya kusimamisha ushiriki wa nchi hiyo kwenye vita vya Yemen

> Wabunge 247 walipiga kura kuunga mkono na Wabunge 175 walipinga kusimamisha msaada wa kijeshi

Soma - https://jamii.app/USAidsYemen
RAIS WA UFARANSA AAMURU UCHUNGUZI JUU YA MAUAJI YA KIMBARI

> Rais Emmanuel Macron ameteua tume itakayofanya uchunguzi ili kubaini iwapo Ufaransa ilihusika katika mauaji ya Kimbari yaliyotokea nchini Rwanda kati ya mwaka 1990 na 1994

> Ni kutokana na tuhuma za Serikali ya Rwanda kwamba Ufaransa kwa sehemu fulani ilihusika na mauaji hayo

Soma - https://jamii.app/FranceKimbariGenocides
JOHN PALLANGYO KUIWAKILISHA CCM ARUMERU MASHARIKI

- Mwenyekiti huyo wa Umoja wa Wazazi(CCM) mkoani Arusha, ameshinda kura za maoni ndani ya CCM kwa kura 470 kati ya 690

- Uchaguzi wa Ubunge katika jimbo hilo unatarajiwa kufanyika Mei 19, 2019

Zaidi, soma https://jamii.app/PallangyoArumeruCCM
WANACHAMA WA 'TANGANYIKA LAW SOCIETY' WAPIGA KURA KUMCHAGUA RAIS

- Wanapiga kura kumchagua Rais Mpya wa chama atakayechukua nafasi ya Mwanasheria Fatma Karume anayemaliza muda wake

- Uchaguzi huo unafanyika leo Aprili 06, jijini Arusha

Zaidi, soma https://jamii.app/UchaguziTLS-2019
MEYA WA ARUSHA(CHADEMA) AMUOMBA RAIS MAGUFULI AFIKE KUPOKEA SHUKRANI ZA WANA-ARUSHA

- Kalisti Lazaro amemuomba RC wa Arusha amualike Rais Magufuli jijini humo ili akapokee Shukrani na pongezi badala ya malalamiko kama aliyopata huko Mtwara

Zaidi, soma https://jamii.app/MeyaAR-AmwalikaRais
BASHE: KODI KUKUSANYWA NA WASIO NA UJUZI MOJA YA SABABU SOKO LA KARIAKOO KUFA

- Mbunge wa Nzega(CCM), Hussein Bashe amesema kumeanzishwa 'taskforce' ya kukusanya kodi yenye Polisi na TAKUKURU

- Amesema watu hao hawana ujuzi wa kukusanya kodi

Zaidi, soma https://jamii.app/BasheKodiKariakoo
KLABU BINGWA AFRIKA: SIMBA YALAZIMISHWA SARE NA TP MAZEMBE

- Klabu ya Simba ikiwa nyumbani katika dimba la Taifa jijini Dar imetoka suluhu ya 0-0 dhidi ya klabu ya TP Mazembe

- Mchezo wa marudiano wa hatua hii ya robo fainali utachezwa DR Congo mnamo Aprili 13, 2019

#JFLeo
KLABU BINGWA AFRIKA: AL AHLY YAPIGWA 5 NA MAMELODI SUNDOWS

- Klabu ya Al Ahly kutoka Misri ikiwa ugenini nchini Afrika Kusini imekumbana na kipigo cha goli 5-0 kutoka kwa klabu ya Mamelodi Sundowns

- Mchezo wa marudiano katika hatua hii ya robo fainali utachezwa Misri mnamo Aprili 13, 2019

#JFLeo
DKT. NSHALA AWA RAIS WA CHAMA CHA WANASHERIA WA TANGANYIKA

- Aliyekuwa Makamu wa TLS wakati wa uongozi wa Fatma Karume, Dkt. Rugemeleza Nshala amechaguliwa kuwa Rais kwa mwaka 2019/20

- Amewashinda wenzake wanne kwa kupata kura 629 kati ya 1162

Zaidi, soma https://jamii.app/NshalaTLS-2018-19
CAG: NASHUTUMIWA BILA MAKOSA, NAICHUKULIA HATUA YA BUNGE KWA UTULIVU

- Prof. Mussa Assad amesema hajui sababu zilizosababisha Bunge lifikie uamuzi wa kutoshirikiana naye

- Asema matumizi ya neno ‘udhaifu’ katika lugha ya ukaguzi ni kawaida

Zaidi, soma https://jamii.app/AssadKuhusuBungeKazi
> Leo April 7, 2019 inatimia miaka 47 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar, Hayati Sheikh Abeid Amani Karume aliyezaliwa 1905 na kufariki 7/4/1972, kwa kupigwa risasi

> Aliiongoza Zanzibar kuanzia 1964 baada ya Mapinduzi
> Mchezaji Lionel Messi wa Barcelona, amekuwa mchezaji anayeongoza kushinda mechi nyingi kwenye Ligi Kuu ya Uhispania baada ya jana Barca kumfunga A. Madrid 2-0

> Ameshinda mechi 335 na kuvunja rekodi ya Iker Casillas aliyeshida mechi 334 akiwa R. Madrid

#JFLeo #JFMichezo
MAELFU WAANDAMANA WAKITAKA RAIS JUAN ORLANDO HERNANDEZ AJIUZULU

- Ni ktk mitaa ya Mji Mkuu wa Honduras wakitaka ajiuzulu na yeye na familia yake wachunguzwe

- Adaiwa kuwa na uhusiano na watuhumiwa wa rushwa na usafirishaji wa #DawaZaKulevya

Zaidi, soma https://jamii.app/OppProtestsHNDR
WAASI RWANDA: HAKUNA NJIA NYINGINE ZAIDI YA KUPIGANA NA KAGAME

- Msemaji wa NLF, Meja Sankara amesema Rais Kagame ni Muuaji na Dikteta hivyo watapigana naye ili kuikomboa Rwanda

- Waasi wanashikilia barabara ya Kigali hadi Ruzizi

Soma https://jamii.app/WaasiVsKagame
UPINZANI KUANDAMANA KUSHINIKIZA BUNGE KUFANYA KAZI NA CAG

- Vijana wa ACT-Wazalendo, NCCR Mageuzi, CHAUMA, UPDP na Vyama vingine vitatu kuandamana Jijini Dodoma Aprili 9, 2019

- Wamwomba Spika wa Bunge au Naibu Spika ayapokee maandamano yao Bungeni

Soma https://jamii.app/MaandamanoDOMCAG
SPIKA NDUGAI: LISSU AMESHALIPWA MADAI YAKE YOTE

- Spika amesema, Lissu ameshalipwa madai yake yote na kama kuna madai mengine awasiliane na mamlaka husika na si kuandika kwenye Mitandao ya Jamii

- Amisisitiza yeye hawezi kuzuia haki ya mtu

Soma https://jamii.app/MalipoyaLissuYamekamilika
- Waziri wa Mambo ya ndani, Kangi Lugola amemsimamisha kazi Mkuu wa Upelelezi wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Mbogwe, Geita.

- Aidha, Waziri Lugola amemsimamisha kazi Mkaguzi wa Jeshi Wilayani humo, kwa tuhuma za kupokea rushwa

Soma https://jamii.app/MkuuUpeleleziMbogwe
MICHEZO: Klabu ya Arsenal ya Uingereza imekula kipigo cha goli 1-0 kutoka kwa Klabu ya Everton

- Arsenal inabaki na alama 63 sawa na Chelsea na alama 1 nyuma ya Tottenham
WAVAMIA OFISI ZA TRA NA KUIBA NYARAKA, LAPTOP NA PESA

- Wezi wavamia ofisi iliyopo Kahama, Shinyanga na kuondoka na kompyuta mpakato moja, baadhi ya nyaraka za kodi na Shilingi milioni 2

- Uchunguzi unaendelea kubaini wahusika na lengo lao

Zaidi, soma https://jamii.app/WiziTRAKahama