JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.47K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
VENEZEULA YAONYWA KWA KUMKAMATA ALIYEJITANGAZA RAIS WA MPITO

- Rais wa Colombia, Ivan Duque ameionya Venezuela kwa kumkamata Juan Guaido siku 1 kabla ya kumalizika muda wa kinga yake ya Ubunge

- Amesema hatua hiyo ni uvunjifu wa utaratibu

Zaidi, soma https://jamii.app/Venezuela-Colombia
WAHAMIAJI HARAMU 12 WAKAMATWA NJOMBE

> Ofisi ya Uhamiaji imewakamata wahamiaji haramu 12 wakitokea Dodoma kwa malengo ya kufika Afrika Kusini kutafuta Maisha

> Saba ni raia wa Rwanda, wawili Burundi na watatu kutoka Somalia

Zaidi, soma https://jamii.app/Wahamiaji12wakamatwa
WAANDISHI NA WATETEZI 52 WAMEKAMATWA/KUTEKWA MWAKA 2018

> Ni kwa mujibu wa ripoti ya hali ya watetezi wa haki za binadamu na bango kitita la sheria

> Amri za wakuu wa Mikoa kuwakamata watetezi wa binadamu na raia nazo pia zimeongezeka

Soma - https://jamii.app/RipotiWaandishiKutekwa
SERIKALI KUWASAKA MADALALI WA WAHAMIAJI HARAMU

> Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amempa muda wa mwezi 1 Kamishna wa Idara ya Uhamiaji nchini, kumkabidhi orodha ya mapapa wa biashara ya kuingiza na kusafirisha wahamiaji haramu nchini

Soma - https://jamii.app/MsakoDalaliUhamiaji
KIGOMA: WAKIMBIZI WAOMBA KUHAMISHWA ENEO KUONESHA HAWAHUSIKI NA UHALIFU

- Wakimbizi wa Burundi katika Kambi ya Nduta wanadai kuna wahalifu kutoka Burundi wanaovuruga usalama

- Wahalifu hao wanapelekea Wakimbizi kushutumiwa kwa uhalifu huo

Zaidi, soma https://jamii.app/WakimbiziKigomaUhalifu
KAMANDA MWANDAMIZI WA AL-SHABAB AKAMATWA SOMALIA

> Vikosi vya usalama vya Somalia vimemkamata kamanda mwandamizi wa kundi la Al-Shabab kwenye operesheni ya mtego iliyotekelezwa jana jioni katika eneo la Kusini mwa nchi hiyo

Zaidi, soma https://jamii.app/Al-shababCommanderArrested
RAIS MAGUFULI AANZA ZIARA YA SIKU 6 MKOANI RUVUMA

- Miradi 9 yenye thamani ya Tsh. Bilioni 519.7 itazinduliwa, kuwekewa mawe ya msingi na kukaguliwa

- Atatembelea Wilaya za Tunduru, Namtumbo, Songea, Mbinga na Nyasa

Fuatilia https://jamii.app/ZiaraMagufuliRuvuma
MAREKANI IMEMFUTIA VIZA YA KUINGIA NCHINI HUMO MWENDESHA MASHTAKA WA ICC

- Ni Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu(ICC), Fatou Bensouda aliyetaka Majeshi ya Marekani nchini Afghanistan yachunguzwe juu ya uhalifu wa kivita

Soma https://jamii.app/USRevokesBensoudaViza
UCHUMI WA AFRIKA MASHARIKI KUKUA KWA 5.9% MWAKA 2019

> Ripoti iliyotolewa na benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imesema, ukuaji wa uchumi katika eneo hilo unatarajiwa kukua kwa asilimia 5.9 mwaka huu na asilimia 6.1 kwa mwaka ujao

> Hata hivyo, kuna ukuaji wa kiwango cha madeni kwa nchi ambazo awali zilifaidika kwa kusamehewa madeni yao

Soma - https://jamii.app/OngezekoUchumiEA
MBUNGE ATAKA WABUNGE WAKATWE POSHO KUICHANGIA YANGA. WABUNGE WAGOMA

- Mbunge wa Nkasi Kaskazini(CCM), Ally Keissy ndiye aliyetoa ombi

- Aliomba Wabunge wakatwe Tsh. 100,000 kwenye posho za leo kuichangia klabu ya Yanga iliyokubwa na ukata

Zaidi, soma https://jamii.app/MbungeYangaKuchangia
MTU 1 KATI YA 4 DUNIANI HUFA KWA KUKOSA MLO KAMILI

> Wataalamu wamesema kwamba kifo kimoja kati ya vinne kinatokana na mlo usiotimiza viwango vya lishe bora, na ulaji wa kupindukia wa sukari, chumvi na nyama unasababisha vifo vya mamilioni ya watu kila mwaka

> Takribani watu bilioni moja duniani kote hawapati chakula cha kutosha, huku karibu watu bilioni mbili wanakula kwa kiwango cha kupindukia

Zaidi, soma https://jamii.app/VifoMloHafifu
KENYATTA AWATAKA MATAJIRI KUELEZA VYANZO VYA MALI ZAO

> Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta amesema matajiri wote wakaguliwe mali zao na wataje vyanzo vya utajiri wao na namna wanavyolipa kodi nchini humo kwa kuwa idadi yao ni kubwa lakini haiendani na kiwango cha kodi wanacholipa

Zaidi, soma https://jamii.app/TaarifaMatajiriKE
ASKARI WA ZIMAMOTO AFUKUZWA KAZI KWA KUJIHUSISHA NA RUSHWA

- Joseph Chale mwenye namba US/ZM 2946FC, amefukuzwa kazi kutokana na kuhusika katika vitendo vya rushwa na unyanyasaji kwa wachimbaji wadogo wa madini Wilayani Chunya, mkoani Songwe

Zaidi, soma https://jamii.app/AskariZimamotoRushwa
BRAZIL: WATU 25 WAVAMIA BENKI 2, 11 WAUAWA

> Taarifa iliyotolewa na Polisi inasema watu 25 waliokuwa na silaha walivamia Benki 2 katika Mji wa Sao Paulo kwa malengo ya kuiba na katika makabiliano baina ya Polisi na wezi hao watuhumiwa 11 waliuawa papohapo na wengine 3 wanashikiliwa na Polisi

Zaidi, soma https://jamii.app/25UvamiziBenki
WAZIRI KIVULI WA MAMBO YA NJE WA UINGEREZA AKOSOA SHERIA YA VYAMA VYA SIASA TANZANIA

- Liz Mclnnes ambaye pia ni Mbunge kutoka chama cha Upinzani cha Labour, amesema amesikitishwa na kupitishwa kwa sheria hiyo aliyodai inaminya upinzani

- Amesema sheria hiyo inazuia vikali shughuli za kisiasa kwa kumpa Msajili wa vyama vya siasa mamlaka ya kuvifutia usajili vyama

Zaidi, soma https://jamii.app/SheriaSiasaTZYakosolewa
HALMASHAURI ZATAKIWA KUTOBOMOA NYUMBA ZILIZOPO KWENYE MAKAZI HOLELA

- Halmashauri zote nchini zimetakiwa badala ya kubomoa nyumba za Wananchi zilizopo kwenye makazi holela yasiyopimwa, ziweke utaratibu wa kuwapatia hati miliki wenye nyumba

Zaidi, soma https://jamii.app/MakaziHolelaYasivunjwe
KUFUZU OLIMPIKI 2020: TWIGA STARS YATOKA SULUHU NA DR CONGO

- Timu ya Wanawake ya Tanzania, Twiga Stars imetoka sare ya goli 2-2 na timu ya Wanawake kutoka DR Congo katika dimba la Taifa jijini Dar

- Mchezo wa marudiano utapigwa Aprili 9, 2019 nchini DR Congo