JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
NDUGAI: BUNGE LIMEKATAA KUFANYA KAZI NA PROF. ASSAD SIO OFISI YA CAG

- Amesema hakuna wakati Bunge limekataa kufanya kazi na Taasisi ambayo ni ofisi ya CAG

- Azimio hili la Bunge limekuja baada ya Prof. Assad kusema maneno “huo ni udhaifu wa Bunge” alipokuwa anahojiwa

Zaidi, soma https://jamii.app/Ufafanuzi-Bunge-Assad
KIONGOZI WA MWENGE AGOMA KUZINDUA MRADI WA ZAHANATI

> Mkonge Ally amegoma kuzindua mradi wa kwanza wa ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Igunda kutokana na mgongano wa taarifa

> Taarifa iliyosomwa na Mkuu wa Mkoa wa Songwe haikuonesha kama kuna pesa za Mwenge ambazo zimegharamia miradi ya Mkoa

Zaidi, soma https://jamii.app/MwengeUzinduziZahanati
UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA: WAGOMBEA WATAKIWA KUWA NA VIPATO VYAO

> Uchaguzi wa Serikali za mitaa unatarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 2019 na moja ya vigezo kwa wagombea ni lazima wawe na shughuli halali inayoingiza kipato badala ya kutegemea posho zinazotolewa na Halmashauri

> Posho za Wenyeviti wa mitaa hulipwa kulingana na makusanyo ya mapato ya ndani ya Halmashauri husika

Soma - https://jamii.app/UchaguziSerikaliMitaa
NDEGE YA ETHIOPIA ILITAKA KUANGUKA MARA KADHAA KABLA YA AJALI

- Waziri wa Uchukuzi wa Ethiopia, amesema Marubani walifuata maagizo ya Boeing lakini hawakuweza kuidhibiti

- Alikuwa akizungumzia matokeo ya uchunguzi wa awali wa ajali hiyo

Zaidi, soma https://jamii.app/MarubaniNdegeEthiopia
TAIFA STARS YAPANDA NAFASI 6 KATIKA VIWANGO VYA TIMU BORA ZA FIFA

- Tanzania imeshika nafasi ya 131 katika orodha mpya iliyotolewa leo na FIFA

- Uganda(79) ni ya kwanza kwa Afrika Mashariki ikifuatiwa na Kenya(108), Tanzania(131), Burundi(136) kisha Rwanda(138)

#JFLeo
HISTORIA: DARAJA LA SALENDA JIJINI DAR

- Selander Bridge(Daraja la Salenda) lililopo barabara ya Ali Hassan Mwinyi lilijengwa mwaka 1929

- Jina lake linamuenzi Mkurugenzi wa kwanza wa Jamii na Kazi wa Tanganyika, John Einar Selander

Zaidi, soma https://jamii.app/DarajaSalendaDar
VENEZEULA YAONYWA KWA KUMKAMATA ALIYEJITANGAZA RAIS WA MPITO

- Rais wa Colombia, Ivan Duque ameionya Venezuela kwa kumkamata Juan Guaido siku 1 kabla ya kumalizika muda wa kinga yake ya Ubunge

- Amesema hatua hiyo ni uvunjifu wa utaratibu

Zaidi, soma https://jamii.app/Venezuela-Colombia
WAHAMIAJI HARAMU 12 WAKAMATWA NJOMBE

> Ofisi ya Uhamiaji imewakamata wahamiaji haramu 12 wakitokea Dodoma kwa malengo ya kufika Afrika Kusini kutafuta Maisha

> Saba ni raia wa Rwanda, wawili Burundi na watatu kutoka Somalia

Zaidi, soma https://jamii.app/Wahamiaji12wakamatwa
WAANDISHI NA WATETEZI 52 WAMEKAMATWA/KUTEKWA MWAKA 2018

> Ni kwa mujibu wa ripoti ya hali ya watetezi wa haki za binadamu na bango kitita la sheria

> Amri za wakuu wa Mikoa kuwakamata watetezi wa binadamu na raia nazo pia zimeongezeka

Soma - https://jamii.app/RipotiWaandishiKutekwa
SERIKALI KUWASAKA MADALALI WA WAHAMIAJI HARAMU

> Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amempa muda wa mwezi 1 Kamishna wa Idara ya Uhamiaji nchini, kumkabidhi orodha ya mapapa wa biashara ya kuingiza na kusafirisha wahamiaji haramu nchini

Soma - https://jamii.app/MsakoDalaliUhamiaji
KIGOMA: WAKIMBIZI WAOMBA KUHAMISHWA ENEO KUONESHA HAWAHUSIKI NA UHALIFU

- Wakimbizi wa Burundi katika Kambi ya Nduta wanadai kuna wahalifu kutoka Burundi wanaovuruga usalama

- Wahalifu hao wanapelekea Wakimbizi kushutumiwa kwa uhalifu huo

Zaidi, soma https://jamii.app/WakimbiziKigomaUhalifu
KAMANDA MWANDAMIZI WA AL-SHABAB AKAMATWA SOMALIA

> Vikosi vya usalama vya Somalia vimemkamata kamanda mwandamizi wa kundi la Al-Shabab kwenye operesheni ya mtego iliyotekelezwa jana jioni katika eneo la Kusini mwa nchi hiyo

Zaidi, soma https://jamii.app/Al-shababCommanderArrested
RAIS MAGUFULI AANZA ZIARA YA SIKU 6 MKOANI RUVUMA

- Miradi 9 yenye thamani ya Tsh. Bilioni 519.7 itazinduliwa, kuwekewa mawe ya msingi na kukaguliwa

- Atatembelea Wilaya za Tunduru, Namtumbo, Songea, Mbinga na Nyasa

Fuatilia https://jamii.app/ZiaraMagufuliRuvuma
MAREKANI IMEMFUTIA VIZA YA KUINGIA NCHINI HUMO MWENDESHA MASHTAKA WA ICC

- Ni Mwendesha Mashtaka wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu(ICC), Fatou Bensouda aliyetaka Majeshi ya Marekani nchini Afghanistan yachunguzwe juu ya uhalifu wa kivita

Soma https://jamii.app/USRevokesBensoudaViza
UCHUMI WA AFRIKA MASHARIKI KUKUA KWA 5.9% MWAKA 2019

> Ripoti iliyotolewa na benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imesema, ukuaji wa uchumi katika eneo hilo unatarajiwa kukua kwa asilimia 5.9 mwaka huu na asilimia 6.1 kwa mwaka ujao

> Hata hivyo, kuna ukuaji wa kiwango cha madeni kwa nchi ambazo awali zilifaidika kwa kusamehewa madeni yao

Soma - https://jamii.app/OngezekoUchumiEA
MBUNGE ATAKA WABUNGE WAKATWE POSHO KUICHANGIA YANGA. WABUNGE WAGOMA

- Mbunge wa Nkasi Kaskazini(CCM), Ally Keissy ndiye aliyetoa ombi

- Aliomba Wabunge wakatwe Tsh. 100,000 kwenye posho za leo kuichangia klabu ya Yanga iliyokubwa na ukata

Zaidi, soma https://jamii.app/MbungeYangaKuchangia
MTU 1 KATI YA 4 DUNIANI HUFA KWA KUKOSA MLO KAMILI

> Wataalamu wamesema kwamba kifo kimoja kati ya vinne kinatokana na mlo usiotimiza viwango vya lishe bora, na ulaji wa kupindukia wa sukari, chumvi na nyama unasababisha vifo vya mamilioni ya watu kila mwaka

> Takribani watu bilioni moja duniani kote hawapati chakula cha kutosha, huku karibu watu bilioni mbili wanakula kwa kiwango cha kupindukia

Zaidi, soma https://jamii.app/VifoMloHafifu