JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KENYA: AMUUA MWENZAKE KWA MADAI KUWA NI MPENZI WA MKE WAKE WA ZAMANI

- Simon Gitari(40) anadaiwa kumuua kwa kumchoma kisu Simon Muriithi(45) katika Kaunti ya Kirinyaga

- Gitari anatafutwa na Polisi kwani anadaiwa kukimbia baada ya tukio

Zaidi, soma https://jamii.app/AuaMpenziMkeKE
RAIA WA MALAWI WAISHIO AFRIKA KUSINI WAOMBA KURUDI NYUMBANI

> Ni aada ya kushambuliwa na raia wa Afrika Kusini na kusababisha Wamalawi wapatao 300 kuyakimbia makaazi yao

> Mpaka sasa watu watatu tayari wameshapoteza maisha

Zaidi, soma https://jamii.app/DurbanCrisis
LEMA KUFUNGIWA MIKUTANO 3. WABUNGE WA UPINZANI WASUSIA KIKAO

- Kamati ya Maadili imeazimia kumpa Mbunge huyo wa Arusha Mjini adhabu hiyo kuanzia leo kwa kuliita Bunge ‘dhaifu’

- Baada ya ripoti kusomwa, Wabunge wa upinzani wametoka nje ya Kikao

Zaidi,soma https://jamii.app/HatmaLemaBungeniAprl04-19
Wabunge hao ni wale waliotoka nje ya Ukumbi wa Bunge mapema leo baada ya Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kutoa ripoti iliyoazimia Mbunge Godbless Lema kuzuiwa kuhudhuria mikutano mitatu ya Bunge
RAIS MAGUFULI AZINDUA KITUO CHA AFYA MBONDE

- Akiwa anaendelea na ziara yake mkoani Mtwara leo yupo Wilayani Masasi alipozindua Kituo hicho

- Kituo hicho kinawakilisha uzinduzi wa vituo vyote 352 vilivyojengwa hapa nchini

#JFLeo
KENYA: MUUZA MAZIWA AHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA KWA ULAWITI

> Hezbon Mogare (25) amehukumiwa kifungo cha maisha baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti mvulana wa miaka 8 mwaka 2017

> Mtuhumiwa anadaiwa kuwa alimfungia mvulana huyo kwenye nyumba yake kwa siku tatu

Zaidi, soma https://jamii.app/JelaMaishaUlawiti
SHINYANGA: POLISI AJIUA AKIDAI SABABU NI KUKOSA MTOTO

> Gideon Clement(30) wa Kituo Kikuu cha Polisi Mjini Kahama, amejiua kwa kujipiga risasi leo asubuhi akiwa lindoni

> Ameacha ujumbe akieleza sababu ya kujiua ni kutokana na kukosa mtoto

Zaidi, soma https://jamii.app/AskariKifoMtoto
BRUNEI: WAPENZI WA JINSIA MOJA KUPIGWA MAWE HADI KUFA

> Nchi hiyo imeanzisha sheria mpya kali zinazoyafanya mapenzi ya jinsia moja kuwa kosa na zimeanza kutekelezwa jana Aprili 03, 2019

> Pia, zinajumuisha uhalifu mwingine ikiwemo kuadhibiwa kwa kukatwa mikono kwa kosa la wizi

Zaidi, soma https://jamii.app/AntGayismLaw
NDUGAI: BUNGE LIMEKATAA KUFANYA KAZI NA PROF. ASSAD SIO OFISI YA CAG

- Amesema hakuna wakati Bunge limekataa kufanya kazi na Taasisi ambayo ni ofisi ya CAG

- Azimio hili la Bunge limekuja baada ya Prof. Assad kusema maneno “huo ni udhaifu wa Bunge” alipokuwa anahojiwa

Zaidi, soma https://jamii.app/Ufafanuzi-Bunge-Assad
KIONGOZI WA MWENGE AGOMA KUZINDUA MRADI WA ZAHANATI

> Mkonge Ally amegoma kuzindua mradi wa kwanza wa ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Igunda kutokana na mgongano wa taarifa

> Taarifa iliyosomwa na Mkuu wa Mkoa wa Songwe haikuonesha kama kuna pesa za Mwenge ambazo zimegharamia miradi ya Mkoa

Zaidi, soma https://jamii.app/MwengeUzinduziZahanati
UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA: WAGOMBEA WATAKIWA KUWA NA VIPATO VYAO

> Uchaguzi wa Serikali za mitaa unatarajiwa kufanyika mwezi Oktoba 2019 na moja ya vigezo kwa wagombea ni lazima wawe na shughuli halali inayoingiza kipato badala ya kutegemea posho zinazotolewa na Halmashauri

> Posho za Wenyeviti wa mitaa hulipwa kulingana na makusanyo ya mapato ya ndani ya Halmashauri husika

Soma - https://jamii.app/UchaguziSerikaliMitaa
NDEGE YA ETHIOPIA ILITAKA KUANGUKA MARA KADHAA KABLA YA AJALI

- Waziri wa Uchukuzi wa Ethiopia, amesema Marubani walifuata maagizo ya Boeing lakini hawakuweza kuidhibiti

- Alikuwa akizungumzia matokeo ya uchunguzi wa awali wa ajali hiyo

Zaidi, soma https://jamii.app/MarubaniNdegeEthiopia
TAIFA STARS YAPANDA NAFASI 6 KATIKA VIWANGO VYA TIMU BORA ZA FIFA

- Tanzania imeshika nafasi ya 131 katika orodha mpya iliyotolewa leo na FIFA

- Uganda(79) ni ya kwanza kwa Afrika Mashariki ikifuatiwa na Kenya(108), Tanzania(131), Burundi(136) kisha Rwanda(138)

#JFLeo
HISTORIA: DARAJA LA SALENDA JIJINI DAR

- Selander Bridge(Daraja la Salenda) lililopo barabara ya Ali Hassan Mwinyi lilijengwa mwaka 1929

- Jina lake linamuenzi Mkurugenzi wa kwanza wa Jamii na Kazi wa Tanganyika, John Einar Selander

Zaidi, soma https://jamii.app/DarajaSalendaDar
VENEZEULA YAONYWA KWA KUMKAMATA ALIYEJITANGAZA RAIS WA MPITO

- Rais wa Colombia, Ivan Duque ameionya Venezuela kwa kumkamata Juan Guaido siku 1 kabla ya kumalizika muda wa kinga yake ya Ubunge

- Amesema hatua hiyo ni uvunjifu wa utaratibu

Zaidi, soma https://jamii.app/Venezuela-Colombia
WAHAMIAJI HARAMU 12 WAKAMATWA NJOMBE

> Ofisi ya Uhamiaji imewakamata wahamiaji haramu 12 wakitokea Dodoma kwa malengo ya kufika Afrika Kusini kutafuta Maisha

> Saba ni raia wa Rwanda, wawili Burundi na watatu kutoka Somalia

Zaidi, soma https://jamii.app/Wahamiaji12wakamatwa
WAANDISHI NA WATETEZI 52 WAMEKAMATWA/KUTEKWA MWAKA 2018

> Ni kwa mujibu wa ripoti ya hali ya watetezi wa haki za binadamu na bango kitita la sheria

> Amri za wakuu wa Mikoa kuwakamata watetezi wa binadamu na raia nazo pia zimeongezeka

Soma - https://jamii.app/RipotiWaandishiKutekwa
SERIKALI KUWASAKA MADALALI WA WAHAMIAJI HARAMU

> Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amempa muda wa mwezi 1 Kamishna wa Idara ya Uhamiaji nchini, kumkabidhi orodha ya mapapa wa biashara ya kuingiza na kusafirisha wahamiaji haramu nchini

Soma - https://jamii.app/MsakoDalaliUhamiaji
KIGOMA: WAKIMBIZI WAOMBA KUHAMISHWA ENEO KUONESHA HAWAHUSIKI NA UHALIFU

- Wakimbizi wa Burundi katika Kambi ya Nduta wanadai kuna wahalifu kutoka Burundi wanaovuruga usalama

- Wahalifu hao wanapelekea Wakimbizi kushutumiwa kwa uhalifu huo

Zaidi, soma https://jamii.app/WakimbiziKigomaUhalifu