JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
SONGWE: MBIO ZA MWENGE WA UHURU KWA MWAKA 2019 ZAZINDULIWA

- Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan amezindua mbio hizo katika uwanja wa Mlowo

- Amewataka wakimbizaji kuhakikisha miradi inayozinduliwa wakati wa mbio inakuwa na ubora unaotakiwa

Zaidi, soma https://jamii.app/MbioMwenge2019
RAIS WA ALGERIA ATANGAZA KUJIUZULU IFIKAPO APRILI 28

> Rais Abdelaziz Bouteflika ataachia wadhifa wake huo Aprili 28, kabla ya kumalizika kwa muhula wake wa nne baada ya washirika wake wa karibu kujitenga naye

> Kumekuwa na maandamano makubwa ya raia nchini humo ya kumshinikiza kiongozi huyo kung’atuka

Zaidi, soma https://jamii.app/BouteflikaResignsApr28
KENYA: GAVANA WA SAMBURU APATA DHAMANA, KUACHIWA AKIKAMILISHA MASHARTI

- Gavana Moses Lenolkulal ataachiwa kwa dhamani iwapo atakamilisha masharti ya dhamani hiyo

- Anatakiwa kulipa pesa taslim Ksh. Milioni 100 au bondi ya Ksh. Milioni 150

Zaidi, soma https://jamii.app/SamburuGovernorArrestedKE
WATU MILIONI 113 WAANDAMWA NA BAA LA NJAA DUNIANI

> Ni kwa mujibu wa ripoti ya pamoja iliyotolewa na Umoja wa Ulaya na mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa mwaka 2018

> Hali mbaya kabisa ilishuhudiwa nchini Yemen, Jamhuri ya Kidemokasia ya Kongo, Afghanistan, Ethiopia, Syria, Sudan, Sudan Kusini na Kaskazini mwa Nigeria

Soma - https://jamii.app/TakwimuNjaa2018
CAG ASEMA UAMUZI WA BUNGE DHIDI YAKE UNAHITAJI TATHMINI

> Profesa Mussa Assad amesema, Bunge kufikia uamuzi wa kutofanya naye kazi ni jambo zito ambalo linahitaji tathmini na kutazamwa athari zake

> Ametoa rai kuwa mahojiano yake pamoja na Kamati ya Bunge ya Maadili yangewekwa wazi ili kila Mtanzania ajue nini kilichozungumzwa

Soma - https://jamii.app/CAGVsUamuziBunge
RAIS AITAKA TANESCO KUREJESHA MIL 27 ZA MWEKEZAJI MTWARA

> Rais John Magufuli amelitaka shirika la Umeme nchini (TANESCO) kumlipa Tsh milioni 27 mwekezaji wa kiwanda cha kubangua korosho kilichopo Mtwara vijijini mara baada ya kumtaka ajinunulie Transfoma

> Amewataka watendaji wote kuondoa vikwazo kwa ajili ya wawekezaji

Soma - https://jamii.app/RaisTanescoMil27
UEFA YAZIPIGA FAINI KLABU ZA CHELSEA NA MALMO

> Shirikisho la soka Ulaya (UEFA) kimetangaza kuipiga faini ya zaidi ya milioni 33 klabu ya Chelsea kufuatia tukio la mashabiki wao kuingia uwanjani wakati wa mchezo wa UEFA Europa dhidi ya Malmo

> Malmo imepigwa faini ya zaidi ya Tsh milioni 148 kwa makosa ya mashabiki wao kurusha miale ya moto uwanjani wakati mchezo ukiendelea

Soma - https://jamii.app/FainiChelseaMalmo
#JFMichezo
SPIKA NDUGAI AMTOA BUNGENI MBUNGE ESTHER MATIKO

- Amemfukuza ndani ya Ukumbi wa Bunge baada ya Mbunge huyo kupiga kelele kumpinga Spika kutaja deni la Lema

- Spika leo Bungeni amesema Lema ana deni la Milioni 644 tangu aingie Bungeni

Soma https://jamii.app/LemaDeni-SpikaNdugai
SPIKA NDUGAI AMTAKA LEMA KUFIKA KWENYE KAMATI YA MAADILI LEO

- Amemtaka afike saa 8:00 mchana kujibu tuhuma zinazomkabili za kulidharau Bunge

- Pia, amesema huenda Lema ana msongo wa Mawazo kwani ana deni la Milioni 644 tangu aingie Bungeni

Soma https://jamii.app/LemaDeni-SpikaNdugai
JELA MIAKA 30 KWA KUBAKA NA KUMPA UJAUZITO MWANAFUNZI

> Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya, imemhukumu adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela na kuchapwa viboko 12 Anthony Mandawa (58), baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka mwanafunzi wa kidato cha kwanza na kumsababishia ujauzito

> Mandawa alitenda kosa hilo Februari 2018

Soma - https://jamii.app/Jela30VibokoKubaka
MKURUGENZI MKUU MPYA VODACOM-TANZANIA APANDISHWA KIZIMBANI

- Hisham Abdel Hendi na wenzake 8 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka 10

- Yapo mashtaka ya kuongoza mtandao wa kihalifu na kuisababishia Serikali hasara ya Tsh. Bilioni 5.8

Soma https://jamii.app/VodaCEO255Corruption
MBEYA: DEREVA WA BODABODA AUAWA

> Jeshi la Polisi Mbeya, linawasaka watu 2 kwa tuhuma za mauaji ya Aidan Paul Chongola, Mkazi wa Hayanga

> Marehemu alichomwa kwa kitu chenye ncha kali upande wa kulia tumboni, kisha kuibiwa pikipiki yake

Zaidi, soma https://jamii.app/MauajiDerevaPikipiki
VIWANJA VYA AZAM COMPLEX, UWANJA WA TAIFA NA VIWANJA VYA SABASABA VYADAIWA USHURU

- Halmashauri ya Manispaa ya Temeke imetangaza dhamira ya kuvifungia viwanja hivyo kwa kuwa wamiliki hawajawahi kulipa kodi ya ushuru wa huduma

Zaidi, soma https://jamii.app/ViwanjaUshuruKufungwa
ASKARI MAGEREZA AKAMATWA NA PEMBE ZA NDOVU

> Cosmas Ndasi (51) anashikiliwa na Jeshi la Polisi baada ya kutengenezewa mtego na akanasa

> Amekutwa na vipande 6, vyenye uzito wa kilogramu 13, sawa na tembo watatu na thamani ya Tsh. Milioni 103.5

Zaidi, soma https://jamii.app/MagerezaMbaroniNdovu
SRI LANKA: WATU 47 WAOMBA KAZI YA KUNYONGA WAFUNGWA

> Nchi hiyo imeanza usahili wa nafasi mbili za kazi ya kunyonga watu baada ya kusitisha adhabu hiyo tangu mwaka 1976

> Adhabu hiyo ni mahususi katika vita dhidi ya #DawaZaKulevya na waajiriwa wapya watapelekwa nje ya nchi kupata mafunzo ya unyongaji

Zaidi, soma https://jamii.app/AjiraKunyongaWahalifu
SERIKALI: HAKUNA TATIZO LA MZUNGUKO MDOGO WA FEDHA KATIKA SOKO

- Naibu Waziri wa Fedha, Dkt. Ashatu Kijaji ameeleza hayo akiwa Bungeni leo

- Amesema katika kutatua changamoto hiyo Serikali ilichukua hatua za kuongeza ukwasi kwenye uchumi

Zaidi, soma https://jamii.app/MzungukoMdogoFedha
UGANDA: ASOMEA SHERIA ILI KURUDISHA ARDHI YA BABA YAKE ILIYOCHUKULIWA

- Jordan Kinyera alikuwa na umri wa miaka 6 wakati Baba yake akipoteza ardhi yao katika kesi

- Ameikomboa ardhi hiyo miaka 23 baadaye baada ya kusoma sheria na kuwa Wakili

Zaidi, soma https://jamii.app/WakiliJordanKinyera
BUNGENI: HATMA YA LEMA BAADA YA KUHOJIWA NA KAMATI YA MAADILI KUJULIKANA LEO

- Kamati hiyo ilitumia takribani dakika 132 kumuhoji Lema hapo jana

- Alihojiwa kutokana na kumnukuu Mbunge wa Kawe(CHADEMA), Halima Mdee kuwa "Bunge ni dhaifu"

Zaidi, soma https://jamii.app/HatmaLemaBungeniAprl04-19