JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.46K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
PWANI: BABA AUA MTOTO KWA KUNYONGA AKIDAI 'AMEBAMBIKIZIWA'

- Polisi inamshikilia Robison Ernest(33) kwa tuhuma za kumuua Modesta Robison(Miezi 6), akidai si mwanae

- Alifanya kitendo hicho Aprili 01, 2019 wakati mama wa mtoto akiwa sokoni

Zaidi, soma https://jamii.app/BabaAuaMtoto-PWN
ICC YAIOMBA MAREKANI KUJIUNGA NA MAHAKAMA HIYO

> Rais wa Mahakama ya Kimataifa ya Kiuhalifu (ICC) ameitolea wito Marekani kujiunga na kusaidia kazi ya Mahakama hiyo

> Chile Eboe-Osuji amesema wahanga wa zamani, wa sasa na wa baadae wa uhalifu dhidi ya binadamu na kivita wanahitaji Marekani kuungana na washirika wake na marafiki

Zaidi, soma https://jamii.app/USOmbiKujiungaICC
SPIKA NDUGAI AMTAKA LEMA KURIPOTI KWENYE KAMATI YA MAADILI YA BUNGE

- Amemtaka Mbunge huyo wa Arusha Mjini, kuripoti kwenye Kamati hiyo kufuatia kauli yake kuwa "Bunge ni dhaifu"

- Lema ametoa kauli hiyo leo Aprili 2, kwenye mkutano wa Bunge

Zaidi, soma https://jamii.app/LemaKamatiMaadili
UCHAGUZI WA KLABU YA YANGA KUFANYIKA MEI 05, 2019

- Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Ally Mchungahela amebainisha hayo

- Ulikuwa ufanyike Aprili 28, 2019 ila siku hiyo kuna fainali za AFCON kwa vijana zitakazofanyika nchini

Zaidi, soma https://jamii.app/UchaguziYangaMei
MOROGORO: ASKARI FEKI WA JWTZ AKAMATWA

- Polisi inamshikilia Fadhil Yahaya(29) aliyekutwa na sare zinazofanana na za JWTZ kwenye kituo cha mabasi, Msamvu

- Polisi waliokuwa doria walimkamata kutokana na taarifa ya Wasamaria wema

Zaidi, soma https://jamii.app/AskariFekiMbaroniMoro
SONGWE: MBIO ZA MWENGE WA UHURU KWA MWAKA 2019 ZAZINDULIWA

- Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan amezindua mbio hizo katika uwanja wa Mlowo

- Amewataka wakimbizaji kuhakikisha miradi inayozinduliwa wakati wa mbio inakuwa na ubora unaotakiwa

Zaidi, soma https://jamii.app/MbioMwenge2019
RAIS WA ALGERIA ATANGAZA KUJIUZULU IFIKAPO APRILI 28

> Rais Abdelaziz Bouteflika ataachia wadhifa wake huo Aprili 28, kabla ya kumalizika kwa muhula wake wa nne baada ya washirika wake wa karibu kujitenga naye

> Kumekuwa na maandamano makubwa ya raia nchini humo ya kumshinikiza kiongozi huyo kung’atuka

Zaidi, soma https://jamii.app/BouteflikaResignsApr28
KENYA: GAVANA WA SAMBURU APATA DHAMANA, KUACHIWA AKIKAMILISHA MASHARTI

- Gavana Moses Lenolkulal ataachiwa kwa dhamani iwapo atakamilisha masharti ya dhamani hiyo

- Anatakiwa kulipa pesa taslim Ksh. Milioni 100 au bondi ya Ksh. Milioni 150

Zaidi, soma https://jamii.app/SamburuGovernorArrestedKE
WATU MILIONI 113 WAANDAMWA NA BAA LA NJAA DUNIANI

> Ni kwa mujibu wa ripoti ya pamoja iliyotolewa na Umoja wa Ulaya na mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa mwaka 2018

> Hali mbaya kabisa ilishuhudiwa nchini Yemen, Jamhuri ya Kidemokasia ya Kongo, Afghanistan, Ethiopia, Syria, Sudan, Sudan Kusini na Kaskazini mwa Nigeria

Soma - https://jamii.app/TakwimuNjaa2018
CAG ASEMA UAMUZI WA BUNGE DHIDI YAKE UNAHITAJI TATHMINI

> Profesa Mussa Assad amesema, Bunge kufikia uamuzi wa kutofanya naye kazi ni jambo zito ambalo linahitaji tathmini na kutazamwa athari zake

> Ametoa rai kuwa mahojiano yake pamoja na Kamati ya Bunge ya Maadili yangewekwa wazi ili kila Mtanzania ajue nini kilichozungumzwa

Soma - https://jamii.app/CAGVsUamuziBunge
RAIS AITAKA TANESCO KUREJESHA MIL 27 ZA MWEKEZAJI MTWARA

> Rais John Magufuli amelitaka shirika la Umeme nchini (TANESCO) kumlipa Tsh milioni 27 mwekezaji wa kiwanda cha kubangua korosho kilichopo Mtwara vijijini mara baada ya kumtaka ajinunulie Transfoma

> Amewataka watendaji wote kuondoa vikwazo kwa ajili ya wawekezaji

Soma - https://jamii.app/RaisTanescoMil27
UEFA YAZIPIGA FAINI KLABU ZA CHELSEA NA MALMO

> Shirikisho la soka Ulaya (UEFA) kimetangaza kuipiga faini ya zaidi ya milioni 33 klabu ya Chelsea kufuatia tukio la mashabiki wao kuingia uwanjani wakati wa mchezo wa UEFA Europa dhidi ya Malmo

> Malmo imepigwa faini ya zaidi ya Tsh milioni 148 kwa makosa ya mashabiki wao kurusha miale ya moto uwanjani wakati mchezo ukiendelea

Soma - https://jamii.app/FainiChelseaMalmo
#JFMichezo
SPIKA NDUGAI AMTOA BUNGENI MBUNGE ESTHER MATIKO

- Amemfukuza ndani ya Ukumbi wa Bunge baada ya Mbunge huyo kupiga kelele kumpinga Spika kutaja deni la Lema

- Spika leo Bungeni amesema Lema ana deni la Milioni 644 tangu aingie Bungeni

Soma https://jamii.app/LemaDeni-SpikaNdugai
SPIKA NDUGAI AMTAKA LEMA KUFIKA KWENYE KAMATI YA MAADILI LEO

- Amemtaka afike saa 8:00 mchana kujibu tuhuma zinazomkabili za kulidharau Bunge

- Pia, amesema huenda Lema ana msongo wa Mawazo kwani ana deni la Milioni 644 tangu aingie Bungeni

Soma https://jamii.app/LemaDeni-SpikaNdugai
JELA MIAKA 30 KWA KUBAKA NA KUMPA UJAUZITO MWANAFUNZI

> Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya, imemhukumu adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela na kuchapwa viboko 12 Anthony Mandawa (58), baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka mwanafunzi wa kidato cha kwanza na kumsababishia ujauzito

> Mandawa alitenda kosa hilo Februari 2018

Soma - https://jamii.app/Jela30VibokoKubaka
MKURUGENZI MKUU MPYA VODACOM-TANZANIA APANDISHWA KIZIMBANI

- Hisham Abdel Hendi na wenzake 8 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka 10

- Yapo mashtaka ya kuongoza mtandao wa kihalifu na kuisababishia Serikali hasara ya Tsh. Bilioni 5.8

Soma https://jamii.app/VodaCEO255Corruption
MBEYA: DEREVA WA BODABODA AUAWA

> Jeshi la Polisi Mbeya, linawasaka watu 2 kwa tuhuma za mauaji ya Aidan Paul Chongola, Mkazi wa Hayanga

> Marehemu alichomwa kwa kitu chenye ncha kali upande wa kulia tumboni, kisha kuibiwa pikipiki yake

Zaidi, soma https://jamii.app/MauajiDerevaPikipiki
VIWANJA VYA AZAM COMPLEX, UWANJA WA TAIFA NA VIWANJA VYA SABASABA VYADAIWA USHURU

- Halmashauri ya Manispaa ya Temeke imetangaza dhamira ya kuvifungia viwanja hivyo kwa kuwa wamiliki hawajawahi kulipa kodi ya ushuru wa huduma

Zaidi, soma https://jamii.app/ViwanjaUshuruKufungwa