JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MAREKANI YASITISHA MISAADA AMERIKA YA KUSINI

> Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kusitisha misaada kwa mataifa matatu katika bara la Amerika Kusini ambayo ni Guatemala, Honduras na Salvador

> Mataifa hayo yalishindwa kuwazuia raia wao kuingia nchini Marekani kinyume cha sheria

Soma - https://jamii.app/USCutsAidsCA
#JFInternational
1
2
3
4
Kauli ya Rais Magufuli akiwa Mtwara kuhusu Kangomba wa Korosho (1)
Kauli ya Rais Magufuli akiwa Mtwara kuhusu Kangomba wa Korosho (2)
Kauli ya Rais Magufuli akiwa Mtwara kuhusu Kangomba wa Korosho (3)
KATIBU WA CCM WILAYA YA MOMBA AFARIKI KWENYE SHUGHULI ZA MWENGE

> Fatuma Ngairo aliwahi kuwa Katibu wa UVCCM Arumeru na amefariki kwa ajali alfajiri ya kuamkia leo alipokuwa akifanya mazoezi tayari kwa kuwasha Mwenge katika mji wa Mlowo

> Aidha, vijana wengine zaidi ya 20 wamelazwa katika Hospitali ya Vwawa baada ya kujeruhiwa katika ajali iliyohusisha gari (IT) lililotokea Dar likielekea nchi jirani ya Zambia

Zaidi, soma https://jamii.app/TanziaAjaliMwengeMomba
AU YAOMBA MKUTANO WA UPATANISHI KWA AJILI YA LIBYA

> Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika, Moussa Mahamat amependekeza kufanyika kwa mkutano wa kimataifa wa upatanishi wa Libya ili kusuluhisha msukosuko wa kisiasa nchini humo

> Amekataa hatua za uingiliaji kutoka nje zitakazoufanya msukosuko wa Libya uwe na utatanishi zaidi

Zaidi, soma https://jamii.app/AUUpatanishiLibya
PWANI: BABA AUA MTOTO KWA KUNYONGA AKIDAI 'AMEBAMBIKIZIWA'

- Polisi inamshikilia Robison Ernest(33) kwa tuhuma za kumuua Modesta Robison(Miezi 6), akidai si mwanae

- Alifanya kitendo hicho Aprili 01, 2019 wakati mama wa mtoto akiwa sokoni

Zaidi, soma https://jamii.app/BabaAuaMtoto-PWN
ICC YAIOMBA MAREKANI KUJIUNGA NA MAHAKAMA HIYO

> Rais wa Mahakama ya Kimataifa ya Kiuhalifu (ICC) ameitolea wito Marekani kujiunga na kusaidia kazi ya Mahakama hiyo

> Chile Eboe-Osuji amesema wahanga wa zamani, wa sasa na wa baadae wa uhalifu dhidi ya binadamu na kivita wanahitaji Marekani kuungana na washirika wake na marafiki

Zaidi, soma https://jamii.app/USOmbiKujiungaICC
SPIKA NDUGAI AMTAKA LEMA KURIPOTI KWENYE KAMATI YA MAADILI YA BUNGE

- Amemtaka Mbunge huyo wa Arusha Mjini, kuripoti kwenye Kamati hiyo kufuatia kauli yake kuwa "Bunge ni dhaifu"

- Lema ametoa kauli hiyo leo Aprili 2, kwenye mkutano wa Bunge

Zaidi, soma https://jamii.app/LemaKamatiMaadili
UCHAGUZI WA KLABU YA YANGA KUFANYIKA MEI 05, 2019

- Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF, Ally Mchungahela amebainisha hayo

- Ulikuwa ufanyike Aprili 28, 2019 ila siku hiyo kuna fainali za AFCON kwa vijana zitakazofanyika nchini

Zaidi, soma https://jamii.app/UchaguziYangaMei
MOROGORO: ASKARI FEKI WA JWTZ AKAMATWA

- Polisi inamshikilia Fadhil Yahaya(29) aliyekutwa na sare zinazofanana na za JWTZ kwenye kituo cha mabasi, Msamvu

- Polisi waliokuwa doria walimkamata kutokana na taarifa ya Wasamaria wema

Zaidi, soma https://jamii.app/AskariFekiMbaroniMoro