JamiiForums
52.6K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
POLISI YAUA WATU WATATU WANAODAIWA KUWA MAJAMBAZI

> Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma katika tukio hilo limefanikiwa pia kukamata risasi 42

> Katika kurushiana risasi Askari mmoja, James Mwita(37) na raia, Sophia Dicksoni(60) walijeruhiwa na wanaendelea na matibabu katika Hospitali ya Kibondo

Zaidi, soma https://jamii.app/PolisiKifoMajambazi
AZAKI: TUNASHUHUDIA HAKI ZA KIDEMOKRASIA, UHURU WA KUJUMUIKA VIKIZIDI KUZOROTA

- Asasi za Kiraia 65 zimetoa Tamko leo Aprili 01, 2019 zikielezea kuguswa na mwenendo wa demokrasia, haki ya kujumuika na uhuru wa kujiunga na vyama nchini

- Pia, Asasi zimemshauri Rais Magufuli kuona umuhimu wa kukutana na vyama vya upinzani nchini na kuzungumza navyo

Zaidi, soma https://jamii.app/TamkoAzaki2019
WAFANYAKAZI OFISI YA MADINI CHUNYA WASIMAMISHWA KAZI

- Waziri Biteko ameagiza wasimamishwe kwa tuhuma za kushirikiana na wachenjuaji kutorosha dhahabu

- Mapema leo aliagiza kukamatwa kwa msimamizi wa kiwanda cha kuchenjua dhahabu cha Ntolah

Zaidi, soma https://jamii.app/MsimamiziNtolahKukamatwa
PERU: WATU 20 WAPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI YA BASI KUUNGUA

> Watu 20 wamepoteza maisha baada ya basi la abiria walilokuwa wakisafiria kushika moto karibu na mji mkuu wa Peru, Lima

> Lilikuwa likielekea katika moja ya miji ya Kaskazini mwa nchi hiyo na inasemekana halikuwa na vifaa vya kuzima moto

Zaidi, soma https://jamii.app/Vifo20BasiMoto
SERIKALI: KANUNI MPYA KWA AJILI YA KUBADILI FEDHA ZA KIGENI ZAANDALIWA

- Waziri wa Fedha, Dkt. Mpango amesema kanuni zitaeleza namna ya kuomba leseni za uendeshaji wa maduka ya kubadili fedha

- Zinalenga kuweka mazingira mazuri ya biashara

Zaidi, soma https://jamii.app/KanuniMadukaFedha-TZ
SERIKALI YAKABIDHI NDEGE YAKE KWA ATCL

- Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi amekabidhi ndege hiyo katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar

- Ndege hiyo ilitolewa na Rais Magufuli ili ikasaidie kubeba abira wa Shirika la ndege la ATCL

#JFLeo
IKULU: NAIBU KATIBU WIZARA YA FEDHA NA NAIBU KAMISHNA TRA WAAPISHWA

- Rais Magufuli leo amemuapisha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha atakayeshughulikia sera, Adolf Hyasinth Ndunguru pamoja na Naibu Kamishna Mkuu wa TRA, Msafiri Lameck Mbibo

- Amewataka viongozi hao kwenda kushughulikia dosari zilizopo katika ofisi zao

Zaidi, soma https://jamii.app/UapishajiIkuluApril2019
AFRIKA KUSINI: WAGENI WAKESHA VITUO VYA POLISI KUKWEPA KUUAWA

> Watu 3 wameuawa huku takribani wengine 50 wakitafuta hifadhi kwenye vituo vya Polisi katika mji wa Durban kufuatia mashambulizi yaliyofanywa na baadhi ya raia wa Afrika Kusini, wanaopinga uwepo wa wageni nchini humo wakidai wanamaliza ajira

> Tukio hilo limetokea leo, Aprili 1

Zaidi, soma https://jamii.app/NativesVsForeignersSA
This media is not supported in your browser
VIEW IN TELEGRAM
RAIS MAGUFULI AFIKA KUMPA POLE MBUNGE WA IRINGA MJINI KWA KUFIWA

- Akiwa na Mke wake, Janeth Magufuli wametoa mkono wa pole kwa familia na heshima za mwisho kwa mwili wa Tryphosa Sanga aliyekuwa dada wa Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa

Zaidi, soma https://jamii.app/MagufuliMsibaDadaMsigwa
FAHAMU KUHUSU MAUMIVU YA KIUNO, MGONGO NA NYONGA

> Tatizo hili huweza kumpata mtu yeyote na huweza kusababishwa na namna mbaya ya kulala/godoro, Kubeba mizigo kwa kuinama, Kulala kwa muda mrefu na matumizi mabaya ya Mto, UTI sugu na Umri-kuzeeka

> Ukipuuza maumivu haya hupelekea kushindwa kufanya tendo la ndoa, kupooza kwa baadhi ya viungo na unaweza kushindwa kutembea au kunyanyuka endapo umekaa au umelala

Tembelea - https://jamii.app/MaumivuKiunoNyonga
#JFAfya
MUUAJI WA KIM JONG NAM KUACHIWA MEI BAADA YA KUKAA MAHABUSU MIAKA 2

> Mwanamke mmoja (30) raia wa Vietnam anayetuhumiwa kuhusika na mauaji ya Kim Jong-Nam ambaye ni kaka wa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un, amehukumiwa kifungo cha zaidi ya miaka 3 gerezani na ataachiwa mwezi ujao, baada ya kukaa rumande kwa zaidi ya miaka miwili

Soma - https://jamii.app/KimNamMurderTrial
#JFInternational
JamiiForums pinned a video
MADUKA 82 KATI YA 87 YA KUBADILI FEDHA JIJINI DAR YALIKUWA NA VIASHIRIA VYA KUTAKATISHA FEDHA

- Hayo yamebinishwa na Gavana wa BoT, Prof. Florens Luoga aliyeongeza kuwa Maduka hayo yalibainika katika uchunguzi ambao unaendelea bado nchini kote

Zaidi, soma https://jamii.app/MadukaFedha82KiukaSheria
KENYA: GAVANA WA SAMBURU AMEKAMATWA NA TUME YA KUPAMBANA NA RUSHWA

- Gavana Moses Lenolkulal amekamatwa na Tume hiyo na kuzuiliwa katika katika Makao Makuu ya Tume

- Inaelezwa ni kwasababu ya sakata la kifisadi la mafuta lililogharimu Ksh. Milioni 84(Tsh. 1,680,000,000)

Zaidi, soma https://jamii.app/SamburuGovernorArrestedKE
KIFO CHA MSANII NIPSEY HUSSLE: LAPD YADAI KUMUONA MSHTAKIWA NA INAMTAFUTA

- Aliyempiga risasi anahusishwa na makundi ya kihuni(gang)

- Nipsey alikuwa anaandaa makala inayomuhusu Dr. Sebi, wengine wanaamini inaweza kuwa sababu ya kifo chake

Zaidi, soma https://jamii.app/NipseyDeath
REA YAPEWA SIKU 28 KUFIKISHA NA KUWASHA UMEME KYELA

> Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ametoa siku 28 kwa Wakala wa Usambazaji Umeme Vijijini(REA) kwa kushirikiana na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kukamilisha ujenzi wa njia ya umeme(Km 20) na kuwashwa kwenye Kata za Nkokwa na Ipande

Zaidi, soma https://jamii.app/REAUmemeKyela
RAIS MAGUFULI KUWASILI MKOANI MTWARA KATIKA ZIARA YA SIKU 2

- Anatarajiwa kuwasili mkoani humo leo Aprili 02 majira ya asubuhi kwa ziara ya kikazi

- Ataweka jiwe la msingi la upanuzi wa Uwanja wa ndege na kuzungumza na Wananchi

Zaidi, soma https://jamii.app/ZiaraMagufuliMtwara
KAMATI YA BUNGE YA MAADILI IMEMTIA HATIANI CAG

- Mwenyekiti wa Kamati, Emmanuel Mwakasaka amesema Prof. Mussa Assad ametiwa hatiani kuhusu kauli yake ya 'udhaifu wa Bunge'

- Alitoa kauli hiyo wakati akihojiwa na Idhaa ya Kiswahili ya UN

Zaidi, soma https://jamii.app/CAGAtiwaHatiani
GARI LA MAFUNDI WA UMEME LAPATA AJALI

> Takribani watu 3 wanasadikiwa kupoteza maisha na wengine 30 kujeruhiwa ktk ajali ya gari la mafundi wa mradi wa kuzalisha umeme Mto Kagera eneo la Rusumo Wilayani Ngara

> Umeme huo ni kwa ajili ya Tanzania, Rwanda na Burundi