JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
RUVUMA: MWANAFUNZI APORWA BAISKELI NA KISHA KUUAWA

- Tariq Mohamed(16) wa darasa la 6 ameporwa baiskeli kisha kunyongwa hadi kufa katika tukio lililotokea Wilayani Tunduru

- Alifanyiwa unyama huo akitokea shambani alikotumwa kuchukua karanga

Zaidi, soma https://jamii.app/MwanafunziAnyongwaAfarikiRVM
IKULU, DAR: RAIS MAGUFULI AWATUNUKU KAMISHENI MAAFISA WANAFUNZI WA JWTZ

- Amewatunuku Maafisa Wanafunzi 146 kuwa na cheo cha Luteni Usu, Wanaume wakiwa 140 na Wanawake 6

- Walipata mafunzo katika Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi mkoani Arusha

Zaidi, soma https://jamii.app/MagufuliAtunukuKamisheni-Machi2019
IRINGA: WANAOKOPESHA FEDHA MITAANI WATAKIWA KUJISALIMISHA TRA

- RC Ally Hapi ameagiza wanaofanya biashara hizo mitaabi bila leseni kujisalimisha TRA ili wakadiriwe kodi

- Asema amebaini kuwa kuna watu wanafanya biashara hiyo kwa riba kubwa

Zaidi, soma https://jamii.app/WakopeshajiWatakiwaTRA-IRNG
MOSHI: MIUNDOMBINU YAHARIBIKA KUTOKANA NA MVUA KUBWA ILIYONYESHA

- Miti imeanguka katika barabara za Shanty Town, International School na Shule ya Sekondari Mawenzi

- Sehemu nyingine nguzo za umeme zimeanguka na kuharibu miundombinu ya umeme

Zaidi, soma https://jamii.app/MvuaMiundombinuMSH
SHINYANGA: WAGANGA WA JADI 19 MBARONI KWA KUPIGA RAMLI CHONGANISHI

- Ramli hizo zinadaiwa kusababisha mauaji ya Wananchi kutokana na imani potofu za kishirikina

- Pia wamekamatwa na nyara za Serikali ikiwemo mikia ya nyumbu na ngozi ya kenge

Zaidi, soma https://jamii.app/WagangaMbaroniJadiSHY
MICHEZO: Mchezo mmoja wa Ligi Kuu nchini England umemalizika ambapo Manchester City imefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Fulham

- City inayofikisha alama 77 magoli yake yamefungwa na Bernardo Silva dakika ya 5 na Sergio Aguero dakika ya 21

- Michezo inayofuata katika Ligi hiyo kwa siku ya leo ni kama inayoonekana pichani

#JFLeo
GAZA: TAKRIBANI WAPALESTINA 33 WAMEJERUHIWA NA JESHI LA ISRAEL

- Wapalestina hao waliokuwa miongoni mwa Waandamanaji wamejeruhiwa katika vurugu zilizozuka kati yao na Jeshi la Israel

- Inaelezwa baadhi walijeruhiwa kwa risasi za moto na baadhi kwa makopo ya gesi ya kutoa machozi

Zaidi, soma https://jamii.app/MaandamaniMwaka1Gaza
MATOKEO-EPL: HUDDERSFIELD YASHUKA DARAJA, MANCHESTER UNITED YASHINDA

- Imekuwa timu ya pili kushuka daraja kabla ya mwezi Machi kuisha kwenye historia ya Ligi baada ya kufungwa na Crystal Palace goli 2-0

- Man. Utd imefanikiwa kupata ushindi wa goli 2-1 dhidi ya Watford na kuendelea kuweka hai ndoto zake za kumaliza ndani ya nne bora

#JFLeo
KAGERA: POLISI WAKAMATA MALI ZILIVYOPORWA NA MAJAMBAZI

- Mali hizo ni simu za mkononi 9, kompyuta mpakato na chaja yake, begi lenye nguo na pia polisi wamekamata bangi na kisu

- Jeshi la polisi bado linaendelea kuwatafuta majambazi hao

Soma https://jamii.app/PolisiWakamataVituKagera

#JFLeo
RAIS MAGUFULI AMTEUA BW. ADOLF MOHONDELA NDUNGURU KUWA NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO(SERA)

- Rais amefanya uteuzi huu kwa kuwa nafasi hiyo ilikuwa wazi

- Aidha, amemteua Bw. Msafiri Lameck Mbibo kuwa Naibu Kamishna wa TRA

Soma https://jamii.app/MagufuliAmteuaNduguru

#JFLeo
UCHAGUZI ARUMERU MASHARIKI MEI 19, 2019

> Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) yatangaza tarehe ya uchaguzi mdogo wa Ubunge katika Jimbo la Arumeru Mashariki

> Jimbo hilo liko wazi baada ya Joshua Nassari(CHADEMA) kuvuliwa Ubunge kwa utoro

Soma jamii.app/UchaguziArumer
#JFLeo
DC KISARAWE ANENA BAADA YA HARAMBEE YA “TOKOMEZA ZERO”

> Ni ya kuchangia ujenzi wa shule ya mabweni ya wasichana iliyofanyika Machi 30, 2019 Jijini Dar

> Amshukuru Pierre “Mzee wa Liquid” kwa kushiriki kikamilifu na kumuomba msamaha kwa kukwazwa na RC Makonda

Soma https://jamii.app/JokateThanksPierre
#JFLeo
UKRAINE: MCHEKESHAJI ATAJWA KUONGOZA KURA ZA URAIS

> Zelenskiy(41) anaongoza kwa wingi wa kura zinazoendelea kuhesabiwa ktk duru ya kwanza ya Uchaguzi

> Kura za maoni zatabiri atashinda dhidi ya Rais na Waziri Mkuu waliomaliza muda wao

Soma https://jamii.app/ComedianPresUKRN
#JFLeo
CAG AKABIDHI RIPOTI 17 ZA UKAGUZI KWA RAIS

> Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali amekabidhi ripoti hizo za mwaka wa fedha ulioisha Juni 30, 2018

> Ipo ripoti ya Ukaguzi wa Serikali Kuu, Serikali za Mitaa na Miradi ya Maendeleo

Zaidi, soma - https://jamii.app/CAGRipotiRais
MONDULI: MTU MMOJA AFARIKI NA SITA KUJERUHIWA KATIKA MAPIGANO YA ARDHI

- Aliyefariki ni Simeli Oltialulu mkazi wa kijiji cha Lendikinya

- Mgogoro huo umekuwapo kwa muda mrefu ukihusisha vijiji vitatu vya Lendikinya, Emairete na Arkalia

Zaidi, soma https://jamii.app/MapiganoMonduli2
RAIS KUANZA ZIARA YA SIKU MBILI MKOANI MTWARA KESHO

> Rais Magufuli anatarajia kufanya ziara ya kikazi mkoani Mtwara kuanzia Aprili 2 hadi April 4

> Atazindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo upanuzi wa uwanja wa ndege wa Mtwara na ujenzi wa barabara ya Mtwara-Mnivata (Km 50)

Soma https://jamii.app/RaisZiaraMTR
TANZANIA NA MISRI ZARIDHIA UJENZI WA KIWANDA CHA KUCHAKATA NYAMA NCHINI

- Zimesaini hati ya makubaliano ya ujenzi wa kiwanda hicho katika Ranchi ya Ruvu

- Kinatarajiwa kuajiri watu 5000 na kuchinja ng'ombe 1,500 na mbuzi 4,500 kwa siku

Zaidi, soma https://jamii.app/KiwandaNyamaTZ-EGY
ALIYEUA MPENZIWE HOSTELI ZA MABIBO AHUKUMIWA KUNYONGWA

> Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imemhukumu kunyongwa hadi kufa Masamba Musiba (39) kwa hatia ya kumuua mpenzi wake, Betha Mwarabu Juni 2009

> Mshitakiwa pamoja na Betha walikuwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)

Zaidi, soma - https://jamii.app/HukumuKunyongwaMauaji
KUKATIKA UMEME VENEZUELA: SAA ZA KAZI KUPUNGUZWA

- Serikali imetangaza kufunga shule na kupunguza saa za kazi hadi saa 8 mchana kwa ofisi za Umma na binafsi

- Aidha, Rais Nicolas Maduro ametangaza mpango wa siku 30 wa kurejesha nishati hiyo

Zaidi, soma https://jamii.app/SaaKaziKupunguaVENZ
MBEYA: MSIMAMIZI KIWANDA CHA KUCHENJUA DHAHABU KUKAMATWA

- Waziri wa Madini, Dotto Biteko ameagiza kukamatwa kwa msimamizi wa Ntolah Gold Elusion baada ya kubaini utoroshaji wa dhahabu

- Pia, ameamuru Polisi kufunga na kulinda kiwanda hicho

Zaidi, soma https://jamii.app/MsimamiziNtolahKukamatwa