JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
KILOSA, MOROGORO: ASKARI MAGEREZA ADAIWA KUMUUA RAIA

- Lepeli Mandero(20) anadaiwa kuuawa na Askari Magereza baada ya kuingiza mifugo kwenye shamba la gereza la Mbigiri

- Baba wa Marehemu amegoma kumzika mwanae hadi uchunguzi utakapofanyika

Zaidi, soma https://jamii.app/AskariAdaiwaKuua-Kilosa
MABARAZA NA BODI ZA MITIHANI AFRIKA MASHARIKI YAUNGANA

- Waanzisha umoja wa nchi za Afrika Mashariki katika tathmini ya elimu

- Katibu Mkuu wa NECTA, Dkt. Charles Msonde ameteuliwa kuwa Rais wa Umoja huo huku Katibu akitokea Uganda

Zaidi, soma https://jamii.app/MabarazaEAYaungana
KENYA: AKIRI KULAWITI MTOTO MMOJA KATI YA 9 ALIOKUWA ANATUHUMIWA

- Mtuhumiwa David Mutuku Katuku alikiri hayo mbele ya Mahakama ya Kaunti ya Machakos

- Anatuhumiwa kunyanyasa kijinsia Watoto katika kituo cha kulea watoto cha ‘Martyrs of Uganda’

Zaidi, soma https://jamii.app/MwaumeAmlawitiMtoto-KE
KIGOGO PCCB MBARONI

Mkurugenzi wa Mipango wa TAKUKURU, Kulthum A. Mansoor anayetuhumiwa kuwadhulumu viwanja wafanyakazi wa taasisi hiyo, amekamatwa na kufikishwa Kituo cha Polisi Oysterbay

> Sept 2018, Rais Magufuli aliagiza ashughulikiwe

Zaidi, soma https://jamii.app/KigogoPCCB
COMORO: KIONGOZI WA UPINZANI AKAMATWA, RISASI ZARINDIMA KATIKA KAMBI YA JESHI

> Ni saa chache baada ya wagombea wa upinzani kuunda Baraza la Mpito na kupanga kumtoa Rais Assoumani madarakani wakidai hajashinda kwa haki katika Uchaguzi wa Machi 24

Zaidi, soma https://jamii.app/KiongoziUpinzaniAkamatwaCMR
OMBI LA NASSARI KUFUNGUA KESI DHIDI YA SPIKA LAKATALIWA

- Mahakama Kuu Dodoma yakubali mapingamizi ya Serikali na kukataa ombi lake la kufungua kesi ya msingi dhidi ya Spika wa Bunge na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya kupinga kuvuliwa Ubunge

Zaidi, soma https://jamii.app/NassariAshindwaKesiUbunge
LUGOLA: WALIOPANGA KUVURUGA AMANI ZANZIBAR WATAKAMATWA KAMA KUKU

- Asema kuna watu wanaoaminika ni Vyama vya Siasa kumbe ni magenge ya wanasiasa wanaotaka kuvuruga amani

- Asisitiza watakamatwa mmoja mmoja kabla mipango yao haijatekelezwa

Zaidi, soma https://jamii.app/WaletaVuruguKukamatwaZNZ
WANAFUNZI WALIOMALIZA KIDATO CHA NNE 2018 KUCHAGUA UPYA TAHASUSI

- Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo ameeleza kuwa licha ya kutoa fursa ya kubadili Tahasusi(Combination) pia wanaweza kubadili kozi za vyuo kulingana na ufaulu wao

Zaidi, soma https://jamii.app/WachaguaUpyaTahasusi
ALIYEKUWA MKURUGENZI WA MIPANGO TAKUKURU APANDISHWA KIZIMBANI

- Kulthum Mansoor amesomewa mashtaka 8 likiwemo la utakatishaji fedha wa Tsh. 1,447,243,000 katika Mahakama ya Kisutu

- Amekosa dhamana kwani Mahakama hiyo haina mamlaka ya kumpatia

Zaidi, soma https://jamii.app/KigogoPCCB
SERIKALI KUKATA RUFAA UAMUZI KUHUSU SHERIA YA HUDUMA YA HABARI

> Ni baada ya Mahakama ya Afrika Mashariki kuitaka kuhakikisha vifungu vinaendana na Mkataba wa Jumuiya Ya Afrika Mashariki

> Yasema Mahakama inaunga mkono uhuru usio na mipaka

Zaidi, soma https://jamii.app/RufaaSheriaHabari
SERIKALI YATAIFISHA KILO 343 ZA DHAHABU TANGU APRILI 2018 HADI SASA

- Mwaka 2018, ilitaifisha Kilo 24 huku Kilo 319 zikitaifishwa juzi jijini Mwanza

- Kwa kipindi hicho pia imetaifisha Tani 75 na Kilo 25 za madini ya vito ikiwamo tanzanite

Zaidi, soma https://jamii.app/Kilo343DahabuYataifishwa
VIONGOZI WA KANISA KATOLIKI ROMBO WAFUNGA KUOMBEA ULEVI

> Kufunga kwa siku 9 kumuomba Mungu aiepushe jamii yao na ulevi uliopindukia hususani kwa vijana

> Inasemekana vijana wengi wanashindwa kuoa kwa sababu ya ulevi

Zaidi, soma https://jamii.app/MfungoUleviRMB
MICHEZO: GONZALO HIGUAIN ATANGAZA KUSTAAFU KUCHEZA TIMU YA TAIFA

- Mshambuliaji huyo wa Argentina amestaafu kuichezea timu ya Taifa baada ya kuifungia magoli 31 katika michezo 75

- Amesema "Kwa furaha ya wengi, sasa nitakuwa naangalia tu timu ikicheza nikiwa nje”

#JFLeo
BURUNDI: SERIKALI YAZUIA MATANGAZO YA BBC NA VOA

- Matangazo ya Shirika la habari la Uingereza(BBC) na Shirika la Habari la Marekani(VOA) yamezuiwa kwa muda usiojulikana

- Mashirika hayo yanashutumiwa kwa kutokuwa na weledi na kukiuka sheria

Zaidi, soma https://jamii.app/BBC-VOAvsBurundi
INDIA YADAIWA KUITUNGUA HELKOPTA YAKE IKIJARIBU KUTUNGUA NDEGE YA PAKISTANI

- Inaelezwa helkopta hiyo ilianguka muda mfupi baada ya kombora kurushwa

- Wanajeshi 6 waliokuwemo kwenye helkopta na raia mmoja aliyeangukiwa na mabaki, wamefariki

Zaidi, soma https://jamii.app/IndiaYalipuaNdegeYake
CHAD: MAHAKAMA YAENDELEA KUBARIKI KUFUNGIWA MITANDAO

> Mahakama imetupilia mbali ombi la Wanasheria la kuitaka kuamuru Serikali kuruhusu matumizi ya mitandao ya kijamii iliyofungiwa tangu Machi, 2018

> Mitandao hiyo yadaiwa kuhatarisha usalama wa nchi

Zaidi, soma https://jamii.app/InternetBanChad
ARUSHA: AFISA USALAMA AUNGANISHWA KWENYE KESI YA MKURUGENZI WA OBC

- Afisa huyo wa Wilaya ya Ngorongoro, Issa Selfu Ng’itu ameunganishwa kwenye kesi ya uhujumu uchumi ya Mkurugenzi wa OBC, Isaya Mollel(59) na kusomewa jumla ya mashtaka 15

Zaidi, soma https://jamii.app/AfisaUsalamaKesiOBC
MAREKANI: WIZARA YA ULINZI YAIDHINISHA UJENZI WA UKUTA

- ‘The Pentagon' imeidhinisha kuhamishiwa kwa Dola Bilioni 1 kwenda akaunti ya Wahandisi wa Jeshi kwa ajili ya ujenzi wa ukuta wa mpaka baina ya nchini hiyo na Mexico

Zaidi, soma https://jamii.app/UjenziWaidhinishwaKujengwaUSA
VATICAN: SHERIA MPYA KUHUSU UNYANYASAJI WA KINGONO YATANGAZWA

- Wafanyakazi wote katika Makao Makuu ya Kanisa Katoliki na Wanadiplomasia wanaomwakilisha Papa duniani kote wanatakiwa kutoa taarifa haraka juu ya madai ya unyanyasaji wa kingono

Zaidi, soma https://jamii.app/KatolikiSheriaNgono
RUKWA: RADI YAANGUSHA UKUTA WA NYUMBA NA KUUA MMOJA

- Mtu mmoja mkazi wa Kata ya Mkoe, Wilayani Kalambo, Girubat Lungwa(34) amefariki baada ya radi kubomoa ukuta wa nyumba yake kisha kuingia ndani na kusabisha kifo chake papo hapo

Zaidi, soma https://jamii.app/RadiYauaRukwa