JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
DAR: JESHI LA POLISI LIMEUZUIA MKUTANO WA NDANI WA ACT WAZALENDO

> Askari wa Jeshi la Polisi wamefika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa PR Stadium uliopo karibu na Uwanja wa Taifa na kuwataka Watu waliokuwepo eneo hilo watawanyike

Zaidi, soma => https://jamii.app/PolisiVsMkutanoACT
BIASHARA 5 UNAZOWEZA KUZIANZISHA WAKATI WOWOTE NA ZIKAFANIKIWA

> Biashara ya kuuza mazao ya chakula, kupika na kuuza chakula, huduma za mavazi, ufugaji wa Kuku na Samaki, pamoja na biashara ya kilimo cha mbogamboga na matunda

Zaidi, soma > https://jamii.app/Biashara5

#JFBiashara
KENYA: BAADHI YA WABUNGE WATAKA KUMNG'OA MAKAMU WA RAIS

- Wakiongozwa na Seneta wa Siya, James Orengo wanawaza kumng’oa William Ruto

- Moja ya sababu ni Ruto kudai pesa iliyopotea katika mradi wa mbwawa ni Ksh. Bilioni 7 na si Ksh. Bilioni 21

Zaidi, soma https://jamii.app/RutoImpeachmentMovement
MATANGAZO YA UZAZI WA MPANGO YARUHUSIWA KUTANGAZWA

- Wizara ya Afya imeruhusu matangazo hayo katika redio na runinga baada ya kurekebisha mwongozo wa Vigezo

- Moja ya kigezo kwa sasa ni tangazo kupitiwa na Kamati ya Wizara kabla ya kutangazwa

Zaidi, soma https://jamii.app/MatangazoUzaziMpangoYaruhusiwa
NAMANGA: VURUGU ZAIBUKA MPAKANI MWA TANZANIA NA KENYA

- Wakenya wamechoma matairi barabarani kuzuia Watanzania kuingia nchini mwao

- Wanadai Polisi wa Tanzania jana usiku walivuka mpaka na kumchukua kinguvu Mfanyabiasha wa Kenya akiwa dukani

Zaidi, soma https://jamii.app/VuruguMpakaniNamangaKE-TZ
MAKOSA YA MTANDAO: BOB CHACHA WANGWE ASHINDA KESI DHIDI YA JAMHURI

- Mahakama Kuu imeona hukumu ya kesi ya Jamhuri dhidi ya Wangwe ya kutotii Sheria ya Mtandao haikuwa na mashiko

- Wangwe alilipa faini ya Tsh. Milioni 5 katika kesi hiyo

Zaidi, soma https://jamii.app/WangweAibwagaJamhuri
DAR: POLISI YAZUIA MKUTANO WA ACT-WAZALENDO NA WANAHABARI

- Imezuia mkutano wa Viongozi wa ACT na Wanahabari katika ofisi za chama hicho zilizopo Kijitonyama

- Viongozi walitaka kuongea baada ya mapema leo kuzuiliwa kufanya mkutano wa ndani

Zaidi, soma https://jamii.app/PolisiVsMkutanoACT
WALIOTOROSHA MAKONTENA 329 BANDARINI WAFUNGWA MIAKA 3

- Hukumu hiyo imetolewa katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi

- Watuhumiwa hao watatu wametiwa hatiani katika mashtaka 107 kati ya 110 yaliyokuwa yakiwakabili

Zaidi, soma https://jamii.app/WaliotoroshaMakontenaWafungwa
MEYA WA MANISPAA YA MTWARA MIKINDANI AJIUNGA CCM AKITOKEA CUF

- Meya huyo ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Tandika, Geoffrey Isack Mwachisye ametangaza uamuzi huo leo

- Amesema ameamua kufanya hivyo ili kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli

Zaidi, soma https://jamii.app/MeyaMtwaraAjiungaCCM
MWANZA: WATUHUMIWA WA KESI YA KUTOROSHA MADINI WAKIRI MAKOSA YAO

> Askari wa Polisi wanaotuhumiwa kuomba rushwa na kuwasindikiza wafanyabiashara hao wao wamekana mashtaka dhidi yao

> Serikali imewasilisha ushahidi wake kwenye kesi hiyo

Soma > https://jamii.app/KesiMadiniMwanza

#JFLeo
BURUNDI: WATOTO WALIOKAMATWA KWA KUCHORA VIBAYA PICHA YA RAIS WAACHIWA

- Wameachiwa kwa muda ikiwa ni siku chache tangu baadhi ya watumiaji wa Twitter kuanzisha kampeni ili waachiwe

- Walichora vibaya picha ya Rais Nkurunziza ktk vitabu vyao

Soma https://jamii.app/WatotoPichaRaisWaachiwa
KILIMANJARO: VIJANA WATUMIA SUMU YA PANYA KAMA MBADALA WA DAWA ZA KULEVYA

> Ni baada ya #DawaZaKulevya kuadimika nchini kwa kiasi kikubwa

> Imeelezwa kuwa ni ngumu kudhibiti matumizi ya kemikali hizo kwasababu hutumika kwa mahitaji mengine

Soma > https://jamii.app/KemikaliDawaKulevya
MSUMBIJI: MADHARA YA KIMBUNGA IDAI

> Taarifa zinaeleza kuwa Takribani Watoto 900,000 wameachwa yatima, wametenganishwa na familia zao, wamekosa makazi

> Serikali ya Msumbiji imefanya jitihada za kuwahifadhi kwenye makambi

Zaidi, soma => https://jamii.app/WatotoYatimaIdai
SHERIA ZA MIRATHI: Je, unazifahamu aina ya sheria za Mirathi zilizopo Tanzania?

> Tanzania ina Sheria 3 za Mirathi; Sheria ya Mirathi ya Kimila, Sheria ya Mirathi ya Kiislamu na Sheria ya Serikali ya Mirathi.

Kufahamu matumizi ya Sheria, fungua > https://jamii.app/SheriaMirathi
UTEUZI: RAIS MAGUFULI ATEUA MWENYEKITI WA BODI YA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI

> Aliyeteuliwa ni Dkt. Simbaiga na uteuzi wake ulianza rasmi tarehe 23 Machi 2019

> Kabla ya uteuzi alikuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Idara ya Sosholojia(UDSM)

Soma > https://jamii.app/UteuziSimbaiga
NAMTUMBO: VIONGOZI 11 WA CHAMA CHA USHIRIKA WAKAMATWA KWA KUWAIBIA WAKULIMA

> Ni viongozi wa chama cha Ushirika cha Mjimwema

> Wanatuhumiwa kuchezea mizani na kuwaibia Wakulima tani 10 za Korosho zenye thamani ya Tsh. Milioni 33

Soma > https://jamii.app/ViongoziKoroshoNamtumbo
MICHEZO: KLABU YA BAYERN MUNICH YAMSAJILI BEKI LUCAS HERNANDEZ KWA ADA YA EURO MILIONI 80

> Mfaransa huyo amesaini mkataba wa miaka 5 na atajiunga na Bayern Julai 1, 2019

> Lucas Hernandez anaichezea Atletico Madrid kwa sasa

Soma > https://jamii.app/HernandezBayern

#JFSports
KENYA: MAJAJI WAPENDEKEZA KUPUNGUZWA KWA UMRI WA KUJIHUSISHA NA NGONO

- Wamependekeza umri huo ushushwe kutoka miaka 18 hadi 16

- Wanapingana na adhabu kali wanazopewa Wanaume kwa kushiriki ngono na Wasichana walio/wanaoelekea kubalehe

Zaidi, soma https://jamii.app/UmriNgonoKenya
MALTA: PASIPOTI YA TANZANIA YASHINDA TUZO YA UBORA NA USALAMA

> Nchi zilizotangazwa kushinda ni Tanzania kupitia Pasipoti yake mpya ya Kielektroniki, Kitambulisho cha utaifa cha nchi ya Estonia na Viza mpya ya Umoja wa Ulaya

Zaidi, soma => https://jamii.app/PasipotiTZTuzoUbora
EU YASITISHA KWA MUDA OPERESHENI YA KUKABILIANA NA WAHAMIAJI HARAMU

- Imesitisha operesheni Sophia ya kukabiliana na wahamiaji haramu katika bahari ya Mediterania

- Ni baada ya Mataifa wanachama kushindwa kuafikiana kuhusu operesheni hiyo

Zaidi, soma https://jamii.app/OperesheniSophiaYasitishwa