JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
AFYA: MADHARA YA KUTUMIA DAWA BILA YA USHAURI WA DAKTARI

> Matumizi holela ya dawa yanaweza kusababisha kifo, kuharibu baadhi ya seli za mwili na kuzifanya kugeuka kuwa seli za saratani, usugu wa maradhi na tatizo la mzio(Allegy)

Zaidi, soma => https://jamii.app/MadharaYaDawa
WALIOCHOMA BENDERA ZA CUF KUFIKISHWA MAHAKAMANI

- CUF imefungua kesi dhidi ya watu walioshiriki kuchoma bendera na kubadilisha rangi za ofisi za chama hicho

- Kesi imefunguliwa jana katika Mahakama ya Vuga iliyopo Mjini Unguja, Zanzibar

Zaidi, soma https://jamii.app/WaliochomaBenderaCUF
JE, NIFANYAJE IWAPO POLISI HATAKI KUNISAIDA AU ANAVUNJA HAKI ZANGU?

> Iwapo Askari Polisi hana msaada au amevunja haki yako, unaweza kulalamika kwa afisa wa Polisi wa ngazi ya juu kwa kupeleka malalamiko kwa barua

Kwa elimu zaidi, fungua https://jamii.app/Mambo101Polisi

#JFCivicSpace
ACT-WAZALENDO YAZUNGUMZIA BARUA YA MSAJILI KUTAKA KUKIFUTA CHAMA HICHO

- Yasema madai ya kutowasilisha hesabu za mwaka 2013/14 si ukweli

- Kuhusu kuchomwa bendera za CUF, imesema msajili anaonesha hana uhakika waliofanya hivyo ni akina nani

Zaidi, soma https://jamii.app/ACTWazalendo-MsajiliVyama
SAMATTA AITAKA TFF IMKUMBUKE SHOMARI KAPOMBE KATIKA ZAWADI

- Kapombe hakuweza kuendelea kuwa katika Kikosi cha Taifa Stars baada ya kupata majeraha ktk maandalizi ya mchezo wa kuwania kufuzu AFCON kati ya Taifa Stars dhidi ya Lesotho

Soma > https://jamii.app/SamattaShomariTFF
BRAZIL: RAIS WA ZAMANI AACHIWA BAADA YA KUKAMATWA KWA TUHUMA ZA RUSHWA

- Michel Temer aliachiwa huru jana baada ya kuwa kizuizini tangu Alhamisi wiki iliyopita

- Mahakama imesema Wapelelezi hawajaeleza umuhimu wa kumuweka kizuizini Rais huyo

Soma https://jamii.app/ExPresidentArrested
KIGOMA: NYUMBA YA TEMBE ILIYOUNGANISHIWA UMEME YAZINDULIWA NA WAZIRI

> Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani ameizindua nyumba ya Rose Kagoma iliyounganishiwa umeme wa REA katika Kijiji cha Ruganga Wilayani Kibondo

Zaidi, soma => https://jamii.app/NyumbeTembeUmeme

#JFLeo
MFANYABIASHARA ALIYETUHUMIWA KUTAKA KUWAUA WANAODAIWA KUWA WANAUSALAMA APEWA DHAMANA

> MARA: Ndugu, Peter Zakaria alikamatwa na kushikiliwa tangu Julai 5, 2018 kwa tuhuma za kujaribu kuwaua kwa kuwapiga risasi Ahmed Segule na Isaac Bwire

Soma > https://jamii.app/PeterZakariaDhamana
ALGERIA: MKUU WA MAJESHI ATAKA RAIS WA NCHI ATANGAZWE KUPOTEZA SIFA YA KUONGOZA

- Ahmed Salah ametaka hivyo kufuatia maandamano kadhaa dhidi Rais Abdelaziz Bouteflika

- Anataka kuanzisha mchakato wa Kikatiba utakaomtangaza Rais kupoteza sifa

Zaidi, soma https://jamii.app/ArmyChief-BouteflikaALG
TANZANIA MBIONI KUISHIWA DAWA ZA KUTULIZA MAUMIVU MAKALI

> Taarifa hii ni kwa mujibu wa tovuti ya 'The East African' imeelezwa kuwa taasisi ya Wagonjwa wa Saratani ya Ocean Road ilitoa taarifa za tishio la kuisha kwa dawa hizo tangu 2018

Soma => https://jamii.app/DawaMaumivu
MPENZI WANGU ANAUZA MAJENEZA, HAMU IMENIISHA

> Mdau wa JamiiForums anaeleza kuwa amekuwa kwenye mahusiano na huyo Mwanamke kwa muda wa miezi 6 sasa

> Anasema walikutana Kariakoo kwenye duka la simu la Mwanamke huyo lakini hakujua kama anamiliki duka la majeneza

Zaidi, soma => https://jamii.app/MpenziMajeneza
DPP KENYA ASEMA UFISADI UNAIMALIZA NCHI HIYO

- Noordi Haji amesema nchini hiyo kiuchumi inaelekea kufa kutokana na kukithiri kwa ufisadi usioelezeka

- Kutokana na Ufisadi, tangu Aprili 2018 hadi Januari 2019 Kenya imepoteza Ksh. Bilioni 16.8

Soma https://jamii.app/UfisadiWakithiriKenya
MAREKANI: SENETA APENDEKEZA WATU KUOA NA KUZAA ILI KUDHIBITI MABADILIKO YA HALI YA HEWA

> Seneta wa Utah, Mike Lee amesema tatizo hilo litatatuliwa na ongezeko la watu watakaoleta ubunifu na soko la bidhaa za utunzaji wa mazingira litakuwepo

Soma > https://jamii.app/SenetaMikeLee
MTUHUMIWA ATOROKA, TAKUKURU KUTAIFISHA MALI ZAKE

- TAKUKURU inamtafuta Magreth Kobelo Gonzaga anayetuhumiwa kutakatisha fedha na kujipatia mali visivyo halali

- Imeeleza kuwa wakati uchunguzi ukiendelea mtuhumiwa huyo alitoroka nchini

Zadi, soma https://jamii.app/TakukuruYamsakaKobelo
MACHAKOS, KENYA: WATU 15 WAFARIKI NA WENGINE KUJERUHIWA KATIKA AJALI

- Imetoka leo alfajiri huko Matuu baada ya basi la abiria kugonga lori lililokuwa limesimama barabarani

- Inadaiwa chanzo ni kutokuwepo kwa alama kuonesha lori limesimama

Zaidi, soma https://jamii.app/AccidentMatuu15Dead
DAR: JESHI LA POLISI LIMEUZUIA MKUTANO WA NDANI WA ACT WAZALENDO

> Askari wa Jeshi la Polisi wamefika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa PR Stadium uliopo karibu na Uwanja wa Taifa na kuwataka Watu waliokuwepo eneo hilo watawanyike

Zaidi, soma => https://jamii.app/PolisiVsMkutanoACT
BIASHARA 5 UNAZOWEZA KUZIANZISHA WAKATI WOWOTE NA ZIKAFANIKIWA

> Biashara ya kuuza mazao ya chakula, kupika na kuuza chakula, huduma za mavazi, ufugaji wa Kuku na Samaki, pamoja na biashara ya kilimo cha mbogamboga na matunda

Zaidi, soma > https://jamii.app/Biashara5

#JFBiashara
KENYA: BAADHI YA WABUNGE WATAKA KUMNG'OA MAKAMU WA RAIS

- Wakiongozwa na Seneta wa Siya, James Orengo wanawaza kumng’oa William Ruto

- Moja ya sababu ni Ruto kudai pesa iliyopotea katika mradi wa mbwawa ni Ksh. Bilioni 7 na si Ksh. Bilioni 21

Zaidi, soma https://jamii.app/RutoImpeachmentMovement
MATANGAZO YA UZAZI WA MPANGO YARUHUSIWA KUTANGAZWA

- Wizara ya Afya imeruhusu matangazo hayo katika redio na runinga baada ya kurekebisha mwongozo wa Vigezo

- Moja ya kigezo kwa sasa ni tangazo kupitiwa na Kamati ya Wizara kabla ya kutangazwa

Zaidi, soma https://jamii.app/MatangazoUzaziMpangoYaruhusiwa
NAMANGA: VURUGU ZAIBUKA MPAKANI MWA TANZANIA NA KENYA

- Wakenya wamechoma matairi barabarani kuzuia Watanzania kuingia nchini mwao

- Wanadai Polisi wa Tanzania jana usiku walivuka mpaka na kumchukua kinguvu Mfanyabiasha wa Kenya akiwa dukani

Zaidi, soma https://jamii.app/VuruguMpakaniNamangaKE-TZ