JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
SERIKALI YATOA BILIONI 1 KWA MAANDALIZI YA U-17 AFRICA CUP OF NATIONS

- Rais Magufuli ametoa ahadi hiyo ili kusaidia maandalizi ya michuano hiyo ya chini ya miaka 17 itakayofanyika nchini

- Itafanyika Aprili 14 hadi Aprili 28 mwaka huu ambapo Tanzania inashiriki kwa mara ya pili

Zaidi, soma https://jamii.app/RaisWanamichezoIkulu
KIMBUNGA IDAI: IDADI YA WATU WALIOFARIKI NI ZAIDI YA 750

- Msumbiji idadi ya Watu waliofariki imefikia 446, Zimbabwe imefikia 259 huku Malawi ikiwa ni 56

- Mamlaka inasema kuna uwezekano mkubwa kutokea kwa magonjwa ya Mlipuko

Zaidi, soma https://jamii.app/KimbungaChauaZimbabwe
SERENGETI, MARA: AFUNGWA MIAKA 30 KWA HATIA YA KUMBAKA MAMA YAKE MZAZI

> Mahakama imemkuta na hatia hiyo Choral Samson(28) aliyembaka Bi. Robhi Nyang'ombe(65)

> Kijana huyo ameiomba Mahakama impunguzie adhabu kwani ni kosa lake la kwanza

Soma => https://jamii.app/Miaka30jelaKumbakaMama
MOSHI, KILIMANJARO: VIBAKA WAVAMIA HOSPITALI NA KUIBA

> Vibaka hao wanaoelezwa kuwa walikuwa wawili walivamia Wodi namba 1 katika Hospitali ya Kilimanjaro CRCT

> Katika Wodi hiyo walipora simu, fedha na mikoba ya akina Mama waliolazwa

Soma > https://jamii.app/VibakaHospitali

#JFLeo
KISUTU: MAHAKAMA YAKATAA MDHAMINI WA TUNDU LISSU KUJITOA KWENYE KESI

- Mdhamini Robert Katula katika kesi ya uchochezi aliomba kujitoa akidai kukosa ushirikiano wa Mshtakiwa

- Hakimu amesema Mdhamini hawezi kujitoa mshtakiwa asipokuwepo

Zaidi, soma https://jamii.app/MdhaminiLissuKujitoaKesi
KAMPALA, UGANDA: MAJAJI WA MAHAKAMA KUU WAGOMA, WADAI MASLAHI BORA

> Waamua kusitisha huduma kwenye vituo vya kimahakama 20 kwa maelezo kuwa serikali inapuuza madai yao

> Wanadai ongezeko la marupurupu, fedha za uendeshaji na watumishi

Zaidi, soma https://jamii.app/MajajiWagomaUG
SERIKALI YA NIGERIA YASHINDWA KUTHIBITISHA MADAI DHIDI YA JAJI MKUU

- Jaji Onnoghen alisimamishwa kazi na Rais Buhari akishutumiwa kushindwa kuweka wazi mali alizokuwa nazo kabla ya kuwa Jaji Mkuu

- Serikali yafunga kesi iliyokuwa inamkabili

Zaidi, soma https://jamii.app/SerikaliNGRvJajiMkuu
KENYA: JAJI MWENYE UMRI WA MIAKA 69 APINGA KUSTAAFU

> Jaji wa Mahakama ya Rufani, Erastus Githinji afungua shauri la kupinga muda wake wa kustaafu

> Asema alizaliwa Desemba 30, 1949 hivyo atastaafu Desemba 29, 2019 na si Julai 1, 2019

Soma > https://jamii.app/JajiKenyaKustaafu
DAR: MTOTO WA MIAKA 7 AFARIKI DUNIA BAADA YA KUKANYAGWA UWANJA WA TAIFA

> Mtoto Ibrahim Hassan amefariki dunia baada ya kukanyagwa na kuangukiwa na watu jana

> Inaelezwa kuwa zilitokea ghasia katika geti la kuingilia uwanjani hapo

Zaidi, soma => https://jamii.app/MtotoAfarikiGetiUwanjaTaifa
CHUO CHA URUBANI KUJENGWA NCHINI KWA UFADHILI WA CHINA

- Kitajengwa katika eneo la uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro(KIA)

- Kinajengwa huko kwa ajili ya urahisi wa mazoezi kwani ni karibu na viwanja vya ndege Moshi, Tanga na Arusha

Zaidi, soma https://jamii.app/ChuoUrubaniTanzaniaKujengwa
KENYA: MWANAMKE AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUMNYONYESHA MTOTO HUKU AKIJUA AMEATHIRIKA KWA VVU

> Amefikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kumnyonyesha Mtoto wa muajiri wake mwenye miezi 11

> Alikamatwa baada ya kuonekana kwenye Camera za CCTV

Soma > https://jamii.app/VVUAnyonyeshaKE
KAMPENI YAANZISHWA KUSHINIKIZA KUACHIWA KWA WATOTO WALIOKAMATWA KISA PICHA YA RAIS

- Baadhi ya Watumiaji wa mtandao wa Twitter wanasambaza picha za Rais Nkurunzinza wa Burundi zilizochorwa vibaya

- Zinaambatanishwa na hashtag ya FreeOurGirls

Zaidi, soma https://jamii.app/KampeniKuachiwaWatotoBRND
ACT-WAZALENDO YAPEWA SIKU 14 KUJIELEZA KWANINI ISIFUTIWE USAJILI

- Msajili wa Vyama vya Siasa ameeleza kuwa Chama hicho kimevunja sheria kadhaa za vyama vya Siasa

- Ikiwemo viongozi wa chama kutokemea vitendo vya kuchomwa kwa bendera za CUF

Zaidi, soma https://jamii.app/ACTSiku14Kujieleza
TEKNOLOJIA: MAMBO UNAYOWEZA KUFANYA KWA KAMERA YA SIMU

> Kamera ya simu inaweza kufanya kazi nyingi za faida zaidi ya kutumika katika kupiga picha. Baadhi ya kazi hizo ni ku-Scan nyaraka, ukalimani na ku-scan barcodes

Zaidi, soma => https://jamii.app/CameraZaSimu

#JFTeknolojia
MKOA WA DAR KINARA KWA BIASHARA HARAMU YA KUSAFIRISHA BINADAMU

- Waziri Lugola amebainisha hayo na kuwaonya wanaojihusisha na biashara hiyo kuacha

- Aidha, kuanzia Januari-Disemba 2018 Watanzania 147 wahanga wa biashara hiyo wameokolewa

Zaidi, soma https://jamii.app/HumanTraffickingDar
TAHADHARI YA JOTO KALI NA UKAME YATOLEWA AFRIKA MASHARIKI

- Ni kwa mujibu wa Kituo cha Utabiri wa Hali ya Hewa cha Mamlaka ya Maendeleo Kenya(IGAD)

- Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA) imesema mwaka huu kutakuwa na kipindi kifupi cha mvua

Zaidi, soma https://jamii.app/TahadhariUkameJoto-2019
WATU WATANO WANAODAIWA KUWA MAJAMBAZI WAUAWA KIGOMA

- Polisi imewaua Watu hao wakati wakijiandaa kuteka magari katika pori la Rusohoko barabara ya Kibondo-Kasulu

- Katika tukio hilo, Askari 2 wameheruhiwa na Majambazi wengine kadhaa kukimbia

Zaidi, soma https://jamii.app/MajambaziWauawaKGM
MKURUGENZI MKUU MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE NCHINI(TAA) ATENGULIWA

- Rais Magufuli ametengua uteuzi wa aliyekuwa akishikilia nafasi hiyo Richard Mayongela

- Meneja wa TANROADS-Dar, Mhandisi Julius Ndyamukama ameteuliwa kushika nafasi hiyo

Zaidi, soma https://jamii.app/UteuziMkurugenziTAA-Machi2019
JUMA DUNI HAJI ATEULIWA KUWA NAIBU KIONGOZI ACT-WAZALENDO

- Kiongozi wa chama, Zitto Kabwe amesema Kamati ya Uongozi imeridhia pendekezo lake la kuteua Naibu Kiongozi

- Uteuzi wa Duni aliyejiunga ACT akitokea CUF utaanza rasmi kesho Machi 27

Zaidi, soma https://jamii.app/DuniNaibuKiongoziACT
TAKUKURU YAINGIZA BILIONI 14.9 KWA KUTAIFISHA MALI ZA MAFISADI

> Kisasi hicho kimepatikana baada ya kutaifisha nyumba 7 magari manne kutoka kwa watu wanaoelezwa kuwa ni mafisadi

> Fedha hizo zimepatika kuanzia mwaka 2016 hadi 2019

Soma > https://jamii.app/TAKUKURUBilioni14