JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
VIJANA 10 WAKAMATWA KWA KUWAPA WANAFUNZI MIMBA

> Vijana 10 kutoka maeneo mbalimbali Wilayani Nkasi wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma ya kuwapa ujauzito wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi na Sekondari katika kipindi cha Januari hadi Machi mwaka huu

> Kwa miezi miwili, wanafunzi 15 wamepata ujauzito

Soma - https://jamii.app/10MbaroniMimba
#JFLeo
AL-SHABAAB WAUA NAIBU WAZIRI SOMALIA

- Wavamia jengo la Serikali Jijini Mogadishu na kuua takribani watu 15 akiwemo Naibu Waziri wa Ajira

- Tukio hilo lililojeruhi 10 limetokea karibu sana na Makao Makuu ya Intelijensia ya nchi hiyo

Zaidi, soma https://jamii.app/AlShabaabKillMinister
BOTSWANA: SERIKALI KUTOA CHAI KWA WANAFUNZI

> Ni kwa wanafunzi wa shule za awali na shule za msingi kuanzia Aprili 1, 2019

> Vinavyotarajiwa kutolewa ni pamoja na Mkate, Maziwa, Mayai, Uji na upande wa matunda ni machungwa na tofaa(Apple)

Zaidi, soma https://jamii.app/BotswanaChaiShuleni
MALI: WAFUGAJI 134 WAUAWA, AL-QAEDA WAHUSISHWA

- Waliouawa ni kutoka kabila la Fulani miongoni mwao wakiwemo watoto, wanawake na wazee

- Vikundi vya kigaidi vyenye uhusiano na Al-Qaeda vyadaiwa kuchochea mapigano ya wenyewe kwa wenyewe

Soma https://jamii.app/FulaniHerdersKilledMali

#JFLeo
MICHEZO: TFF YATOA UFAFANUZI KUHUSU JEZI ZINAZOSAMBAA MITANDAONI

> Imekana kuhusika na jezi hizo na kwamba ile sio sare inayotumiwa na timu ya Taifa

> Wanaoendelea kuuza jezi hizo watakiwa kuacha mara moja kabla hatua kali hazijachukuliwa

Zaidi, soma https://jamii.app/TFFvsJeziFeki
TANZIA: BEHEWA SEMBWANA AFARIKI DUNIA

> Kiungo wa Kagera Sugar, Behewa Sembwana amefariki dunia leo alfajiri kutokana na maradhi ya tumbo

> Behewa aliwahi kuchezea timu za Njombe Mji na Coastal Union kabla ya kujiunga na Kagera Sugar

Zaidi, soma https://jamii.app/RIPBehewaSembwana
RC RUKWA AAGIZA MSAKO WA WAGANGA WA KIENYEJI

> Amemuagiza RPC Mathias Nyangi kuwakamata waganga wa kienyeji wote wasio na leseni halali

> Ni baada ya mganga mmoja huko Sumbawanga kuua watoto wawili kwa kuwafungia kwenye gari siku 2

Zaidi, soma https://jamii.app/MsakoWagangaRukwa
CANADA: PADRI ASHAMBULIWA AKIWA ANAONGOZA IBADA

> Claude Grou(77) aliyekuwa anaongoza ibada ndani ya Kanisa Katoliki, alivamiwa na mwanaume aliyekuwa amevaa kofia

> Sababu za kuvamiwa bado hazijafahamika, mtuhumiwa anashikiliwa na polisi

Zaidi, soma https://jamii.app/PadreCanadaAshambuliwa
DAR: WAISLAM WAUNGANA KWENYE DUA KUOMBA MVUA

> Dua hiyo kwa ajili ya kuombea mvua inyeshe na ili kuondokana na ukame imefanyika viwanja vya Mnazi Mmoja leo, Machi 24

> Mufti Abubakar amewataka Maimamu nchini kwenye swala ya Ijumaa kuomba Dua ya Kunuti

Zaidi, soma https://jamii.app/WaislamDuaMvua
MICHEZO: Tanzania imefuzu kushiriki Michuano ya Mataifa ya Africa (AFCON) baada ya kuinyuka Uganda goli 3-0

- Matokeo ya Lesotho na Cape Verde ni 0-0 na timu hizo zimeondolewa kwenye mashindano hayo

#afcon2019
TETEMEKO LATIKISA MAENEO YA KENYA, KILIMANJARO & ARUSHA

> Tetemeko la Ardhi lenye ukubwa wa 4.8 kwa kipimo cha Richa limeyakumba maeneo kadhaa ya Kenya & Kilimanjaro na Arusha kwa Tanzania

> Athari za tetemeko hilo hazijajulikana

Soma jamii.app/TetemekoKenya
#earthquake #JFLeo
WALIMU WAANDAMANA NCHINI MOROCCO

- Wameandamana hapo jana katika mitaa ya Rabat wakitaka kuboreshwa kwa mazingira ya kazi

- Wengi ni vijana wanaotaka ajira ya kudumu kwa kuwa wakistaafu hawapati haki sawa na wenye mikataba ya kudumu

Zaidi, soma https://jamii.app/MoroccoTeachersProtest1
RAIS MAGUFULI KUKUTANA NA TAIFA STARS NA BONDIA MWAKINYO

- Rais atakutana na Wanamichezo hao leo Ikulu jijini Dar ili kuwapongeza na kula nao chakula cha mchana

- Pia katika msafara huo atakutana na Viongozi wa TFF na Kamati ya uhamasishaji

Zaidi, soma https://jamii.app/MagufuliWanamichezoIkulu-Machi2019
MWALIMU KUTOKA KENYA ASHINDA TUZO YA MWALIMU BORA DUNIANI

- Mwalimu wa hesabu na fizikia, Peter Tabishi kutoka shule moja ya Sekondari ameshinda tuzo hiyo kwa mwaka 2019

- Amewashinda Walimu wengine 9 kutoka sehemu mbalimbali Ulimwenguni

Zaidi, soma https://jamii.app/MwalimuBoraDuniani-2019
ARUSHA: TANI 8 ZA NYAMA YA NG'OMBE NA NGURUWE ZATEKETEZWA

- Serikali imeteketeza nyama hizo zenye viambata vya sumu na zilizokwisha muda wa matumizi

- Zimekamatwa zikiuzwa katika maduka makubwa licha ya kutofaa kwa matumizi ya binadamu

Zaidi, soma https://jamii.app/NyamaZateketezwaArusha
TAKUKURU YAWASHIKILIA VIONGOZI WA CCM KWA TUHUMA ZA RUSHWA

- Ni Katibu CCM tawi la Amana, Jenipher Mushi; Katibu Kata CCM Ilala, Devota Bantulaki na Katibu Hamasa CCM-Dar, Frank Mang'ati

- Waliomba rushwa ya Tsh. Milioni 5 na kupokea Tsh. Milioni 3

Zaidi, soma https://jamii.app/ViongoziCCMIlalaMbaroni
RAIS MAGUFULI AKUTANA NA WACHEZAJI WA TAIFA STARS NA BONDIA MWAKINYO

> Amekutana na Wachezaji wa Taifa Stars, viongozi wa TFF, Kamati ya Uhamasishaji na Bondia Hassan Mwakinyo

> Rais atawapongeza na kula nao chakula cha mchana

Zaidi, soma => https://jamii.app/RaisWanamichezoIkulu
RAIS MAGUFULI AWAPATIA VIWANJA WACHEZAJI WA TAIFA STARS

- Wachezaji hao na Bondia Hassan Mwanyiko na Mwalimu wake watapatiwa viwanja mkoani Dodoma

- Rais amesema hiyo ni zawadi ya Serikali kwa niaba ya Watanzania kama shukrani

Zaidi, soma https://jamii.app/RaisWanamichezoIkulu
RAIS MAGUFULI AMPA MCHEZAJI WA ZAMANI TSH. MILIONI 5

- Aliyepewa ni Peter Tino mchezaji aliyekuwepo kwenye kikosi cha mwaka 1979 kilichofuzu AFCON

- Amempatia wakati alipokutana na Wachezaji wa Taifa Stars na Bondia Mwakinyo

Zaidi, soma https://jamii.app/RaisWanamichezoIkulu