JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
BIASHARA YA VYUMA CHAKAVU YASITISHWA

> Serikali imezuia biashara ya kuingiza na kusafirisha nje ya nchi taka zenye madhara ikiwemo vyuma chakavu na taka za eletroniki

> Wanaojihusisha watakiwa kujiandikisha upya Baraza la Taifa la Hifadhi

Soma - https://jamii.app/VyumaChakavuYasitishwa
#JFLeo
BODI ZA MAZAO ZATAKIWA KUJISAJILI MSIMBOMILIA

> Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amezitaka bodi za chai, korosho, kahawa, pamba na sukari nchini kujisajili kwenye alama za msimbomilia inayosimamiwa na GS1 Tanzania ili wakulima wanufaike na uuzwaji wa bidhaa hizo nje ya nchi

Soma - https://jamii.app/BodiMazaoMsimbomilia
#JFLeo
UCHUKUE HATUA GANI IWAPO UNASHIKILIWA BILA YA KUWAPO KWA LALAMIKO LA JINAI DHIDI YAKO?

> Kama hakuna lalamiko la kosa la jinai, lakini unaendelea kushikiliwa ni ukiukwaji wa sheria

> Inaitwa kushikiliwa kinyume cha sheria

Zaidi, soma => https://jamii.app/Mambo101Polisi

#JFCivicSpace
TANZIA: MWANAHABARI CHARLES NGEREZA AFARIKI

> Aliyekuwa Mwandishi wa habari wa Redio One, ITV, Idhaa ya kiswahili ya Dw na Makamu Mwenyekiti wa Arusha Press Club, Charles Ngereza amefariki leo asubuhi Machi 23, 2019 katika hospitali ya Mtakatifu Elizabeth Jijini Arusha

> Msiba uko nyumbani kwake, eneo la Kwa Mrefu na taratibu za mazishi zitatangazwa baadaye
#JFLeo
MJADALA WA KIPINDI CHA URAIS KUONGEZWA WAFUNGWA

> Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru amesema mjadala wa muda wa Rais kukaa madarakani kwa miaka 7 badala ya 5 ya sasa ulioanzishwa na Mbunge Juma Nkamia umefungwa na amemtaka Mbunge huyo kutoiendeleza hoja hiyo

Soma - https://jamii.app/MjadalaMudaRais
#JFLeo
VIJANA 10 WAKAMATWA KWA KUWAPA WANAFUNZI MIMBA

> Vijana 10 kutoka maeneo mbalimbali Wilayani Nkasi wanashikiliwa na Polisi kwa tuhuma ya kuwapa ujauzito wanafunzi wa shule mbalimbali za msingi na Sekondari katika kipindi cha Januari hadi Machi mwaka huu

> Kwa miezi miwili, wanafunzi 15 wamepata ujauzito

Soma - https://jamii.app/10MbaroniMimba
#JFLeo
AL-SHABAAB WAUA NAIBU WAZIRI SOMALIA

- Wavamia jengo la Serikali Jijini Mogadishu na kuua takribani watu 15 akiwemo Naibu Waziri wa Ajira

- Tukio hilo lililojeruhi 10 limetokea karibu sana na Makao Makuu ya Intelijensia ya nchi hiyo

Zaidi, soma https://jamii.app/AlShabaabKillMinister
BOTSWANA: SERIKALI KUTOA CHAI KWA WANAFUNZI

> Ni kwa wanafunzi wa shule za awali na shule za msingi kuanzia Aprili 1, 2019

> Vinavyotarajiwa kutolewa ni pamoja na Mkate, Maziwa, Mayai, Uji na upande wa matunda ni machungwa na tofaa(Apple)

Zaidi, soma https://jamii.app/BotswanaChaiShuleni
MALI: WAFUGAJI 134 WAUAWA, AL-QAEDA WAHUSISHWA

- Waliouawa ni kutoka kabila la Fulani miongoni mwao wakiwemo watoto, wanawake na wazee

- Vikundi vya kigaidi vyenye uhusiano na Al-Qaeda vyadaiwa kuchochea mapigano ya wenyewe kwa wenyewe

Soma https://jamii.app/FulaniHerdersKilledMali

#JFLeo
MICHEZO: TFF YATOA UFAFANUZI KUHUSU JEZI ZINAZOSAMBAA MITANDAONI

> Imekana kuhusika na jezi hizo na kwamba ile sio sare inayotumiwa na timu ya Taifa

> Wanaoendelea kuuza jezi hizo watakiwa kuacha mara moja kabla hatua kali hazijachukuliwa

Zaidi, soma https://jamii.app/TFFvsJeziFeki
TANZIA: BEHEWA SEMBWANA AFARIKI DUNIA

> Kiungo wa Kagera Sugar, Behewa Sembwana amefariki dunia leo alfajiri kutokana na maradhi ya tumbo

> Behewa aliwahi kuchezea timu za Njombe Mji na Coastal Union kabla ya kujiunga na Kagera Sugar

Zaidi, soma https://jamii.app/RIPBehewaSembwana
RC RUKWA AAGIZA MSAKO WA WAGANGA WA KIENYEJI

> Amemuagiza RPC Mathias Nyangi kuwakamata waganga wa kienyeji wote wasio na leseni halali

> Ni baada ya mganga mmoja huko Sumbawanga kuua watoto wawili kwa kuwafungia kwenye gari siku 2

Zaidi, soma https://jamii.app/MsakoWagangaRukwa
CANADA: PADRI ASHAMBULIWA AKIWA ANAONGOZA IBADA

> Claude Grou(77) aliyekuwa anaongoza ibada ndani ya Kanisa Katoliki, alivamiwa na mwanaume aliyekuwa amevaa kofia

> Sababu za kuvamiwa bado hazijafahamika, mtuhumiwa anashikiliwa na polisi

Zaidi, soma https://jamii.app/PadreCanadaAshambuliwa
DAR: WAISLAM WAUNGANA KWENYE DUA KUOMBA MVUA

> Dua hiyo kwa ajili ya kuombea mvua inyeshe na ili kuondokana na ukame imefanyika viwanja vya Mnazi Mmoja leo, Machi 24

> Mufti Abubakar amewataka Maimamu nchini kwenye swala ya Ijumaa kuomba Dua ya Kunuti

Zaidi, soma https://jamii.app/WaislamDuaMvua
MICHEZO: Tanzania imefuzu kushiriki Michuano ya Mataifa ya Africa (AFCON) baada ya kuinyuka Uganda goli 3-0

- Matokeo ya Lesotho na Cape Verde ni 0-0 na timu hizo zimeondolewa kwenye mashindano hayo

#afcon2019
TETEMEKO LATIKISA MAENEO YA KENYA, KILIMANJARO & ARUSHA

> Tetemeko la Ardhi lenye ukubwa wa 4.8 kwa kipimo cha Richa limeyakumba maeneo kadhaa ya Kenya & Kilimanjaro na Arusha kwa Tanzania

> Athari za tetemeko hilo hazijajulikana

Soma jamii.app/TetemekoKenya
#earthquake #JFLeo
WALIMU WAANDAMANA NCHINI MOROCCO

- Wameandamana hapo jana katika mitaa ya Rabat wakitaka kuboreshwa kwa mazingira ya kazi

- Wengi ni vijana wanaotaka ajira ya kudumu kwa kuwa wakistaafu hawapati haki sawa na wenye mikataba ya kudumu

Zaidi, soma https://jamii.app/MoroccoTeachersProtest1
RAIS MAGUFULI KUKUTANA NA TAIFA STARS NA BONDIA MWAKINYO

- Rais atakutana na Wanamichezo hao leo Ikulu jijini Dar ili kuwapongeza na kula nao chakula cha mchana

- Pia katika msafara huo atakutana na Viongozi wa TFF na Kamati ya uhamasishaji

Zaidi, soma https://jamii.app/MagufuliWanamichezoIkulu-Machi2019
MWALIMU KUTOKA KENYA ASHINDA TUZO YA MWALIMU BORA DUNIANI

- Mwalimu wa hesabu na fizikia, Peter Tabishi kutoka shule moja ya Sekondari ameshinda tuzo hiyo kwa mwaka 2019

- Amewashinda Walimu wengine 9 kutoka sehemu mbalimbali Ulimwenguni

Zaidi, soma https://jamii.app/MwalimuBoraDuniani-2019