JamiiForums
52.7K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.4K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
ARUSHA: TANI 8 ZA NYAMA YA NG'OMBE NA NGURUWE ZATEKETEZWA

- Serikali imeteketeza nyama hizo zenye viambata vya sumu na zilizokwisha muda wa matumizi

- Zimekamatwa zikiuzwa katika maduka makubwa licha ya kutofaa kwa matumizi ya binadamu

Zaidi, soma https://jamii.app/NyamaZateketezwaArusha
TAKUKURU YAWASHIKILIA VIONGOZI WA CCM KWA TUHUMA ZA RUSHWA

- Ni Katibu CCM tawi la Amana, Jenipher Mushi; Katibu Kata CCM Ilala, Devota Bantulaki na Katibu Hamasa CCM-Dar, Frank Mang'ati

- Waliomba rushwa ya Tsh. Milioni 5 na kupokea Tsh. Milioni 3

Zaidi, soma https://jamii.app/ViongoziCCMIlalaMbaroni
RAIS MAGUFULI AKUTANA NA WACHEZAJI WA TAIFA STARS NA BONDIA MWAKINYO

> Amekutana na Wachezaji wa Taifa Stars, viongozi wa TFF, Kamati ya Uhamasishaji na Bondia Hassan Mwakinyo

> Rais atawapongeza na kula nao chakula cha mchana

Zaidi, soma => https://jamii.app/RaisWanamichezoIkulu
RAIS MAGUFULI AWAPATIA VIWANJA WACHEZAJI WA TAIFA STARS

- Wachezaji hao na Bondia Hassan Mwanyiko na Mwalimu wake watapatiwa viwanja mkoani Dodoma

- Rais amesema hiyo ni zawadi ya Serikali kwa niaba ya Watanzania kama shukrani

Zaidi, soma https://jamii.app/RaisWanamichezoIkulu
RAIS MAGUFULI AMPA MCHEZAJI WA ZAMANI TSH. MILIONI 5

- Aliyepewa ni Peter Tino mchezaji aliyekuwepo kwenye kikosi cha mwaka 1979 kilichofuzu AFCON

- Amempatia wakati alipokutana na Wachezaji wa Taifa Stars na Bondia Mwakinyo

Zaidi, soma https://jamii.app/RaisWanamichezoIkulu
SERIKALI YATOA BILIONI 1 KWA MAANDALIZI YA U-17 AFRICA CUP OF NATIONS

- Rais Magufuli ametoa ahadi hiyo ili kusaidia maandalizi ya michuano hiyo ya chini ya miaka 17 itakayofanyika nchini

- Itafanyika Aprili 14 hadi Aprili 28 mwaka huu ambapo Tanzania inashiriki kwa mara ya pili

Zaidi, soma https://jamii.app/RaisWanamichezoIkulu
KIMBUNGA IDAI: IDADI YA WATU WALIOFARIKI NI ZAIDI YA 750

- Msumbiji idadi ya Watu waliofariki imefikia 446, Zimbabwe imefikia 259 huku Malawi ikiwa ni 56

- Mamlaka inasema kuna uwezekano mkubwa kutokea kwa magonjwa ya Mlipuko

Zaidi, soma https://jamii.app/KimbungaChauaZimbabwe
SERENGETI, MARA: AFUNGWA MIAKA 30 KWA HATIA YA KUMBAKA MAMA YAKE MZAZI

> Mahakama imemkuta na hatia hiyo Choral Samson(28) aliyembaka Bi. Robhi Nyang'ombe(65)

> Kijana huyo ameiomba Mahakama impunguzie adhabu kwani ni kosa lake la kwanza

Soma => https://jamii.app/Miaka30jelaKumbakaMama
MOSHI, KILIMANJARO: VIBAKA WAVAMIA HOSPITALI NA KUIBA

> Vibaka hao wanaoelezwa kuwa walikuwa wawili walivamia Wodi namba 1 katika Hospitali ya Kilimanjaro CRCT

> Katika Wodi hiyo walipora simu, fedha na mikoba ya akina Mama waliolazwa

Soma > https://jamii.app/VibakaHospitali

#JFLeo
KISUTU: MAHAKAMA YAKATAA MDHAMINI WA TUNDU LISSU KUJITOA KWENYE KESI

- Mdhamini Robert Katula katika kesi ya uchochezi aliomba kujitoa akidai kukosa ushirikiano wa Mshtakiwa

- Hakimu amesema Mdhamini hawezi kujitoa mshtakiwa asipokuwepo

Zaidi, soma https://jamii.app/MdhaminiLissuKujitoaKesi
KAMPALA, UGANDA: MAJAJI WA MAHAKAMA KUU WAGOMA, WADAI MASLAHI BORA

> Waamua kusitisha huduma kwenye vituo vya kimahakama 20 kwa maelezo kuwa serikali inapuuza madai yao

> Wanadai ongezeko la marupurupu, fedha za uendeshaji na watumishi

Zaidi, soma https://jamii.app/MajajiWagomaUG
SERIKALI YA NIGERIA YASHINDWA KUTHIBITISHA MADAI DHIDI YA JAJI MKUU

- Jaji Onnoghen alisimamishwa kazi na Rais Buhari akishutumiwa kushindwa kuweka wazi mali alizokuwa nazo kabla ya kuwa Jaji Mkuu

- Serikali yafunga kesi iliyokuwa inamkabili

Zaidi, soma https://jamii.app/SerikaliNGRvJajiMkuu
KENYA: JAJI MWENYE UMRI WA MIAKA 69 APINGA KUSTAAFU

> Jaji wa Mahakama ya Rufani, Erastus Githinji afungua shauri la kupinga muda wake wa kustaafu

> Asema alizaliwa Desemba 30, 1949 hivyo atastaafu Desemba 29, 2019 na si Julai 1, 2019

Soma > https://jamii.app/JajiKenyaKustaafu
DAR: MTOTO WA MIAKA 7 AFARIKI DUNIA BAADA YA KUKANYAGWA UWANJA WA TAIFA

> Mtoto Ibrahim Hassan amefariki dunia baada ya kukanyagwa na kuangukiwa na watu jana

> Inaelezwa kuwa zilitokea ghasia katika geti la kuingilia uwanjani hapo

Zaidi, soma => https://jamii.app/MtotoAfarikiGetiUwanjaTaifa
CHUO CHA URUBANI KUJENGWA NCHINI KWA UFADHILI WA CHINA

- Kitajengwa katika eneo la uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro(KIA)

- Kinajengwa huko kwa ajili ya urahisi wa mazoezi kwani ni karibu na viwanja vya ndege Moshi, Tanga na Arusha

Zaidi, soma https://jamii.app/ChuoUrubaniTanzaniaKujengwa
KENYA: MWANAMKE AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUMNYONYESHA MTOTO HUKU AKIJUA AMEATHIRIKA KWA VVU

> Amefikishwa Mahakamani kwa tuhuma za kumnyonyesha Mtoto wa muajiri wake mwenye miezi 11

> Alikamatwa baada ya kuonekana kwenye Camera za CCTV

Soma > https://jamii.app/VVUAnyonyeshaKE
KAMPENI YAANZISHWA KUSHINIKIZA KUACHIWA KWA WATOTO WALIOKAMATWA KISA PICHA YA RAIS

- Baadhi ya Watumiaji wa mtandao wa Twitter wanasambaza picha za Rais Nkurunzinza wa Burundi zilizochorwa vibaya

- Zinaambatanishwa na hashtag ya FreeOurGirls

Zaidi, soma https://jamii.app/KampeniKuachiwaWatotoBRND
ACT-WAZALENDO YAPEWA SIKU 14 KUJIELEZA KWANINI ISIFUTIWE USAJILI

- Msajili wa Vyama vya Siasa ameeleza kuwa Chama hicho kimevunja sheria kadhaa za vyama vya Siasa

- Ikiwemo viongozi wa chama kutokemea vitendo vya kuchomwa kwa bendera za CUF

Zaidi, soma https://jamii.app/ACTSiku14Kujieleza
TEKNOLOJIA: MAMBO UNAYOWEZA KUFANYA KWA KAMERA YA SIMU

> Kamera ya simu inaweza kufanya kazi nyingi za faida zaidi ya kutumika katika kupiga picha. Baadhi ya kazi hizo ni ku-Scan nyaraka, ukalimani na ku-scan barcodes

Zaidi, soma => https://jamii.app/CameraZaSimu

#JFTeknolojia
MKOA WA DAR KINARA KWA BIASHARA HARAMU YA KUSAFIRISHA BINADAMU

- Waziri Lugola amebainisha hayo na kuwaonya wanaojihusisha na biashara hiyo kuacha

- Aidha, kuanzia Januari-Disemba 2018 Watanzania 147 wahanga wa biashara hiyo wameokolewa

Zaidi, soma https://jamii.app/HumanTraffickingDar