JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
WAFUNGWA WAKUTWA NA DAWA ZA KULEVYA, ASKARI KUSIMAMISHWA KAZI

> Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Hamad Masauni amemuagiza Kamishna Jenerali wa Magereza kuwasimamisha kazi askari 4 wa Gereza kuu la Luanda jijini Mbeya baada ya kuwakuta wafungwa wakiwa na #DawaZaKulevya na simu za mkononi

Soma - https://jamii.app/GerezaniDawaKulevya
#JFLeo
KENYA: MAHAKAMA YATOA RUHUSA YA KUSAJILIWA KWA CHAMA CHA MASHOGA

> Majaji wa Mahakama ya Rufani wakiongozwa na Jaji Philip Waki, wamesema si sawa kuwazuia watu kuishi watakavyo

> Taasisi za kuwatetea ruska kusajiliwa nchini humo

Zaidi, soma => https://jamii.app/UshogaRuksaKenya

#JFLeo
MICHEZO: CRISTIANO RONALDO APIGWA FAINI KWA UTOVU WA NIDHAMU

> Bodi ya Maadili ya Shirikisho la Soka Barani Ulaya imemtoza faini ya zaidi shilingi za kitanzania milioni 52

> Yaelezwa kuwa ushangiliaji wake si wa kiungwana

Zaidi, soma => https://jamii.app/CristianoRonaldoFaini

#JFSports
CUF YATANGAZA KUJITOA UKAWA

> Katibu Mkuu mpya wa Chama Cha Wananchi CUF, Khalifa Suleiman Khalifa, amesema wao kama chama cha Wananchi wameshajitoa kwenye mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi 'UKAWA' kwa madai upo hoi na hauna msaada kwao

Soma https://jamii.app/CUFYatokaUKAWA
#JFLeo
BOMET, KENYA: MBARONI KWA KUWAUA WATOTO WAKE WATATU

> Mkazi wa Kijiji cha Mabuteek anashikiliwa na Polisi kwa tuhuma za kuwaua Watoto wake na kisha kutoroka

> Alijaribu kujinyonga lakini kamba ilikatika

Soma > https://jamii.app/MauajiBometKE

#JFLeo
AHUKUMIWA MIAKA 30 KWA KUBAKA NA KUMPA MIMBA MWANAFUNZI

> Mahakama ya Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu, imemhukumu Sunzu Mpangala (27) kifungo cha miaka 30 kwa kumbaka na kumpa mimba mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Maswa

> Mtuhumiwa alitenda kosa hilo Juni 12, 2018 wakati akimfundisha mwanafunzi huyo kipindi cha likizo

Soma - https://jamii.app/KifungoUbakajiMimba
#JFLeo
HANDENI, TANGA: MADINI YA DHAHABU YAKAMATWA YAKITOROSHWA

> Madini hayo yana uzito wa gramu 180, yamekamatwa yakiwa yanasafirishwa kwenda nje ya wilaya hiyo kinyume na utaratibu

> Dhahabu hiyo ilichimbwa Mgodi wa Magambazi

Zaidi, soma => https://jamii.app/DhahabuHandeniTanga

#JFLeo
KASULU, KIGOMA: MVUA YA MAWE YAHARIBU MAJENGO YA SHULE NA MASHAMBA

> Majengo ya vyumba 4 vya madarasa katika Shule za Msingi Nyaruhande na Bugaga yabomoka

> Zaidi ya ekari 100 za shamba la mbegu la Wakala wa Mbegu za Kilimo limeharibiwa

Soma > https://jamii.app/MvuaKasulu

#JFLeo
RAIS MAGUFULI ASAINI MUSWADA WA VYAMA VYA SIASA KUWA SHERIA, CHADEMA WATOA NENO

> Baada ya Rais Magufuli kutia saini muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa, CHADEMA watoa tamko na kusema watafungua shauri la kupinga

Zaidi, soma > https://jamii.app/CHADEMAVsMuswadaVyama

#JFLeo
USHAURI: JINSI YA KUDHIBITI CHUNUSI ZISIENEE NA KUACHA MADOA

> Pata ushauri kwa mtaalam ili kujua kama chunusi zako zimesababishwa na bakteria au kitu kingine na usipasue/kutumbua chunusi

> Tumia face wash/facial cleanser au sabuni za kusaidia kuondoa uchafu na vijidudu pamoja na poda kwa ajili ya kukausha mafuta

> Punguza kiasi cha mafuta na viungo unavyokula na Pambana na msongo (Stress)

> Changia kuhusu njia nyingine unayoifahamu ya kusaidia kwenye tatizo hili
#JFUrembo
SENGEREMA: NDUGU WAPIGWA RADI WAKATI WAKIPOKEA MAHARI

> Waliojeruhiwa ni Thomas Ngoshiwabhanya(Baba), Rejina Kube(Mama), Jerina Majige na Neth Thomas

> Majeruhi hao wamelazwa katika Hospitali teule ya Wilaya wakiendelea na matibabu

Zaidi, soma > https://jamii.app/WajeruhiwaRadiSengerema

#JFLeo
BOKO HARAM WAUA WANAJESHI 23 WA CHAD

> Wamefanya mauaji hayo muda wa usiku, mauaji yanayotajwa kuwa makubwa zaidi kwa Wanajeshi wa Chad

> Boko Haram wamekuwa kwenye harakati za kujitenga na taifa la Nigeria kwa takribani miaka 10

Zaidi, soma => https://jamii.app/BokoHaramVsChad

#JFLeo
TANZANIA YASITISHA MKATABA WA UWEKEZAJI BAINA YAKE NA UHOLANZI

> Kuanzia tarehe 1 Aprili 2019 wawekezaji wapya kutoka Uholanzi watakaokuja nchini na wawekezaji wa Kitanzania watakaoenda Uholanzi hawatafanya kazi chini ya mkataba huo

Zaidi, soma > https://jamii.app/TzVsUholanziMkataba

#JFLeo
KENYA: MWANAUME WA MIAKA 60 AKAMATWA KWA MAUAJI YA SHEMEJI YAKE

> Polisi katika Kaunti ndogo ya Rarieda wanamshikilia Elijah Ogutu kwa tuhuma za mauaji ya Susan Omolo kwa madai kuwa anataka kuolewa na mtu asiye sahihi

Zaidi, soma => https://jamii.app/MauajiRariedaKenya

#JFInternational
KENYA: MWANAUME WA MIAKA 60 AKAMATWA KWA MAUAJI YA SHEMEJI YAKE

> Polisi katika Kaunti ndogo ya Rarieda wanamshikilia Elijah Ogutu kwa tuhuma za mauaji ya Susan Omolo kwa madai kuwa anataka kuolewa na mtu asiye sahihi

Zaidi, soma => https://jamii.app/MauajiRariedaKenya

#JFInternational
BIASHARA YA VYUMA CHAKAVU YASITISHWA

> Serikali imezuia biashara ya kuingiza na kusafirisha nje ya nchi taka zenye madhara ikiwemo vyuma chakavu na taka za eletroniki

> Wanaojihusisha watakiwa kujiandikisha upya Baraza la Taifa la Hifadhi

Soma - https://jamii.app/VyumaChakavuYasitishwa
#JFLeo
BODI ZA MAZAO ZATAKIWA KUJISAJILI MSIMBOMILIA

> Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amezitaka bodi za chai, korosho, kahawa, pamba na sukari nchini kujisajili kwenye alama za msimbomilia inayosimamiwa na GS1 Tanzania ili wakulima wanufaike na uuzwaji wa bidhaa hizo nje ya nchi

Soma - https://jamii.app/BodiMazaoMsimbomilia
#JFLeo
UCHUKUE HATUA GANI IWAPO UNASHIKILIWA BILA YA KUWAPO KWA LALAMIKO LA JINAI DHIDI YAKO?

> Kama hakuna lalamiko la kosa la jinai, lakini unaendelea kushikiliwa ni ukiukwaji wa sheria

> Inaitwa kushikiliwa kinyume cha sheria

Zaidi, soma => https://jamii.app/Mambo101Polisi

#JFCivicSpace
TANZIA: MWANAHABARI CHARLES NGEREZA AFARIKI

> Aliyekuwa Mwandishi wa habari wa Redio One, ITV, Idhaa ya kiswahili ya Dw na Makamu Mwenyekiti wa Arusha Press Club, Charles Ngereza amefariki leo asubuhi Machi 23, 2019 katika hospitali ya Mtakatifu Elizabeth Jijini Arusha

> Msiba uko nyumbani kwake, eneo la Kwa Mrefu na taratibu za mazishi zitatangazwa baadaye
#JFLeo
MJADALA WA KIPINDI CHA URAIS KUONGEZWA WAFUNGWA

> Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru amesema mjadala wa muda wa Rais kukaa madarakani kwa miaka 7 badala ya 5 ya sasa ulioanzishwa na Mbunge Juma Nkamia umefungwa na amemtaka Mbunge huyo kutoiendeleza hoja hiyo

Soma - https://jamii.app/MjadalaMudaRais
#JFLeo