JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
UFAHAMU KUHUSU 'PROCESSOR' YA SIMU

> Processor katika simu ni kifaa ambacho huchukua maelezo kutoka kwenye software na kufanya kazi za kimahesabu na kimantiki pamoja na kutoa na kuingiza vitu ili simu yako ifanye kazi kwa ufanisi

> Simu nyingi zinatumia processor aina ya 'arm' na wana aina yao ya processor inayoitwa 'A series' ambayo ndiyo inatumika sana kwenye simu na inajumuisha; cortex A5, A6, A7, A8, A9, A12 na A15

Zaidi, tembelea - https://jamii.app/ProcessorSimu
#JFTeknolojia
LIPUMBA: MAALIM SEIF HAJAHAMA CHAMA BALI ALIFUKUZWA

> Mwenyekiti wa CUF Taifa, Prof. Ibrahim Lipumba amesema kuwa kabla ya Maalim Seif kukihama chama hicho tayari alikuwa ameshafukuzwa kuwa mwanachama wa CUF kwenye mkutano mkuu uliopita, baada ya kubaini hana nia njema na chama na anataka kukidhoofisha

> Amewataka wanaotaka kumfuata Maalim Seif kuchanganya akili zao na kutokurupuka

Soma - https://jamii.app/LipumbaVsMaalimCUF
#JFLeo
VITU VYA KUZINGATIA UNAPOTAKA KUNUNUA KOMPYUTA

> Waranti: Hii itakusaidia wewe mtumiaji kupata msaada pale kifaa kitakapopata matatizo kama hujaiharibu mwenyewe unaweza kubadilishiwa ukapewa nyingine

> Processor: Kuna tofauti kubwa sana kati ya processor za single core kama pentium processors, duo-core, na quad core processors. Kwa mtumiaji wa kawaida processor za intel i3 inamtosha, watumiaji wa kati i5 na kwa wale wakubwa i7 ndio ya kwao

> RAM: Kwa watumiaji wadogo RAM ya 2Gb ni kubwa kutosha matumizi yote ila watumiaji wakubwa hasa wale 'professionals' wanatakiwa kutumia kuanzia 4 - 6 GB

Fahamu zaidi - https://jamii.app/MuongozoKununuaPC
#JFTeknolojia
MTOTO AMUUA MPENZI WA MAMAKE

> Mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika Kijiji cha Deriat kaunti ya Kericho, Kenya amemuua mzee (65) kwa kumchoma kisu kifuani baada ya kumkuta akishiriki tendo la ndoa na mama yake

> Adai huyo si babake na hivyo hana mamlaka ya kulala nyumbani kwao

Soma - https://jamii.app/AuaMpenziMama
#JFInternational
MATUMIZI YA SIMU YACHANGIA DOLA BILIONI 2.5 KATIKA UCHUMI WA TANZANIA

> Simu zimerahisisha huduma za mawasiliano, uzalishaji, na kuchangia kwenye pato la taifa

> Ajira kwa watu milioni 1.5 sawa na 2.6% ya idadi ya Watanzania zimetengenezwa

Soma > https://jamii.app/TzDigitalIndustry

#JFLeo
MTOTO WA MWAKA MMOJA AFIA KWENYE DIMBWI LA MAJI

> Mtoto Alex Fredrick Sanga, mwaka mmoja na miezi saba, Mkazi wa Mapinduzi, Mkoani Mbeya amekutwa amefariki kwenye korongo lenye maji ambalo lipo jirani na nyumbani kwao

> Marehemu alikuwa akicheza na wenzake wakati mama yake akifua na baada ya muda akatoweka

Soma - https://jamii.app/MtotoKifoDimbwi
#JFLeo
MAMA AMCHOMA MTOTO WAKE KWA MAJI MOTO

> Mkazi wa Kijiji cha Ndachi Mkoani Dodoma, Asha Juma anashutumiwa kwa kosa la kumchoma mwanae, Godfrey Banda (13) mikono kwa maji ya moto kwa kile kilichoelezwa kuwa ni udokozi wa nyama

Soma - https://jamii.app/AchomaMtotoMaji
#JFLeo
BUKOBA: BASI LA KAMPUNI YA FRESTER LALIGONGA BASI LA DAR LUX

> Ajali imetokea baada ya basi la Frester lililokuwa likitoka Bukoba kuelekea Mwanza kuligonga basi la Kampuni ya Dar Lux lililokuwa likielekea Dar

> Abiria wachache wamejeruhiwa

Soma > https://jamii.app/FresterVsDarLuxBukoba

#JFLeo
SPIKA WA UINGEREZA AKATAA MPANGO WA BREXIT KUPIGIWA KURA TENA

> Mpango wa Waziri Mkuu, Theresa May kuhusu kujiondoa kutoka Umoja wa Ulaya (EU), maarufu kama Brexit umepata pigo jipya baada ya Spika wa Bunge, John Bercow kutangaza kuwa mpango huo hauwezi kupigiwa tena kura Bungeni, isipokuwa pale utakapofanyiwa marekebisho makubwa

Soma - https://jamii.app/BercowVsTheresaBrexit
#JFInternational
KAMATI YA BUNGE YAISHAURI SERIKALI KUILIPIA TANESCO DENI LA TRILIONI 1.39

> Mashirika ya IPTL, Songas, PAET na TPDC yanaidai TANESCO kiasi cha shilingi bilioni 950 na mabenki ya biashara nayo yanalidai shirika hilo shilingi bilioni 442

Soma => https://jamii.app/PICDeniTANESCO

#JFLeo
MAMBO YA MSINGI KWENYE KUANZISHA BIASHARA YA 'CATERING'

> WAPISHI: Tafuta wapishi wazuri wanaoweza kupika vyakula mbalimbali kwa ufanisi wa hali ya juu

> VIFAA: Unatakiwa kuwa na vifaa muhimu na maalumu vya kuhifadhia na kuandalia vyakula, vitakavyomfanya mlaji afurahie chakula. Unaweza kununua ama kukodi

> BEI: Bei zako inapaswa ziwe zenye kumshawishi mteja kukupa tenda na tengeneza 'menu' yako katika mfumo wa tofauti kwa kuongeza vitu vya ziada ili kukufanya ukae akilini mwa mteja na kukupatia wateja zaidi

Tembelea - https://jamii.app/UjasiriamaliCatering
#JFBiashara
MARA: WATUMISHI 2 WA MUWASA WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA UBADHIRIFU

> Watu 3 wakiwemo watumishi 2 wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Mara(MUWASA) wamefikishwa Mahakani na TAKUKURU

> Wanatuhumiwa kwa kuitia MUWASA hasara ya milioni 613

Soma > https://jamii.app/TakukuruMuwasa

#JFLeo
MIGORI KENYA: MTANZANIA AJIUA KWA KUJINYONGA

> Jeshi la Polisi limeanza uchunguzi wa kifo hicho cha Mtanzania aliyefahamika kwa majina ya Chacha Olupe

> Mwili wake ulikutwa ukiwa unaning'inia juu ya mti siku ya jana(Jumanne)

Zaidi, soma => https://jamii.app/MtanzaniaAjinyongaKenya

#JFLeo
RC SONGWE: MARUFUKU WANACCM KUVAA SARE KWENYE SHEREHE ZA KUWASHA MWENGE

> Brigedia Jeneral Mstaafu, Nicodemus Mwengela amesema kuwa shughuli hiyo si ya chama(CCM)

> Mwenge wa uhuru unatarajiwa kuwashwa Aprili 2 Wilayani Mbozi, Songwe

Soma > https://jamii.app/RCSongweVsCCM

#JFLeo
UGOMVI WA CHAKULA: MWANAMKE AMSHAMBULIA MUMEWE KWA PANGA

> Inaelezwa kuwa Mwanaume huyo alirejea nyumbani kutoka kazini na kuomba apewe chakula

> Hata hivyo ulizuka ugomvi ndipo Mwanamke huyo alichukua panga na kumjeruhi mumewe

Soma > https://jamii.app/MwanamkeAjeruhi

#JFInternational
BAADHI YA DALILI ZA KUTAMBUA KAMA MTOTO ANATUMIKA KINGONO

> Hupata shida wakati wa kukaa au kutembea (miaka 2 -10) na kuwaogopa baadhi ya watu kupita kiasi au sehemu fulani au vitu (miaka 0-5)

> Hupenda kujishika sehemu za siri kiasi cha kujisahau na kukaa chooni muda mrefu au kuhitaji kujisaidia mara kwa mara (miaka 0-5)

> Hushindwa kuzuia haja kubwa (miaka 4-7), kuwa mkimya isivyo kawaida (umri wa balehe) na Msongo wa mawazo (8-17)

Je, unafahamu dalili zingine? Ongezea hapa
Zaidi, soma - https://jamii.app/DaliliMtotoKingono
#JFMalezi
DROO YA HATUA YA ROBO FAINALI YA LIGI YA MABINGWA AFRIKA KUPANGWA LEO

> Klabu ya Simba SC ndiyo timu pekee iliyobakia kutoka ukanda wa Afrika Mashariki

> Kuna uwezekano Simba SC ikapangwa kucheza na Esperance(Tunisia) Wydad Casablanca (Morocco) au TP Mazembe(DRC)

#CAFCLDraw
VIWANGO VYA FURAHA: TANZANIA YASHIKA NAFASI YA 153 KATI YA 156

> Hii ni ripoti ya 7 tangu ripoti hizi zianze kuchapishwa

> Teknolojia ya mawasiliano, utawala na maisha ya jamii yamechangia kwa kiwango kikubwa katika kuandaa ripoto hii

Soma => https://jamii.app/HappinessIndex

#JFLeo
KENYA: POLISI WAKAMATA SANDUKU LENYE NOTI BANDIA BARCLAYS

> Jeshi la Polisi jijini Nairobi linawashikilia watu 6 kwa tuhuma za kumiliki pesa bandia zenye thamani ya Dola milioni 20 (zaidi ya Tsh bilioni 46) zilizopatikana ndani ya chumba cha kuhifadhia fedha cha tawi la Benki ya Barclays

> Kati yao wapo Maafisa wawili wa Benki hiyo

Soma - https://jamii.app/NotiBandiaBarclaysKE
#JFInternational