JamiiForums
52.8K subscribers
34.4K photos
2.45K videos
31.3K links
Official Telegram Channel | Inform x Engage x Empower
Download Telegram
MFANYABIASHARA ALIYEBAMBIKIWA KESI ABAINIKA KUWA MKORA

> Mussa Adam alishawahi kufungwa miaka 20 jela kwa kosa la kubaka, alishaiba mahali na kukimbia na pingu na tukio la mwisho lililomfanya atiwe mbaroni na kubambikwa kesi ya mauaji, ni la wizi wa simu kwenye kituo cha mabasi ambako alipigwa hadi kuvuliwa shati

Soma - https://jamii.app/AliyeachiwaAbainikaMkora
#JFLeo
WANAOTAKA KUNUNUA ARDHI WANASHAURIWA KUFANYA HAYA

> Mjue mtu anayekuuzia na hakikisha unapata taarifa kuhusu umiliki wake, alipataje eneo hilo, ikiwa kuna mgogoro wowote

> Muombe kivuli cha hati (kopi) ili uipeleke ardhi kujiridhisha kuhusu hayo uliyomuuliza hapo juu

> Jiridhishe juu ya uhalisi wa hati miliki (genuineness of certificate of title)

> Baada ya kuafikiana masharti ya mauziano, mnatakiwa kuandika mikataba kwa mujibu wa kifungu cha 64(1) Sheria ya Ardhi, kusainishana, na Wakili kugonga mihuri

Zaidi, tembelea - https://jamii.app/TaratibuUnunuziArdhi
#JFSheria
ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA AFRIKA: SIMBA SC YAPANGWA KUCHEZA NA TP MAZEMBE

> Simba SC ilifuzu hatua hiyo baada ya kujinyakulia alama 9 katika michezo 6 ya kundi lake

> Simba SC ndio timu pekee kutoka ukanda wa Afrika Mashariki inayoshiriki michuano hii

> Timu nyingine zimepangwa kama ifuatavyo; Constantine Vs Esperance, Mamelodi Sundowns Vs Al Ahly na Horoya Vs Wydad Casablanca

#CAFCLDraw
MAHAKAMA KUU YAZUIA UCHAGUZI WA MARUDIO ARUMERU MASHARIKI

> Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma imetoa zuio hilo hadi kesi ya msingi ya kuomba uamuzi wa Spika wa Bunge wa kumfutia Ubunge, Joshua Nassari itakaposikilizwa na kuamuliwa

Zaidi, soma => https://jamii.app/MahakamaKuuVsNassari

#JFLeo
MWANZA: POLISI YAWAKAMATA WAHALIFU 45 WA MAKOSA MBALIMBALI

> Kamanda wa Polisi mkoa huo, amesema wamewakamata wahamiaji haramu 19, waganga wa kienyeji wanaodaiwa kupiga ‘ramli chonganishi’ 15 na watuhumiwa wa #DawaZaKulevya 11

Zaidi, soma > https://jamii.app/WahalifuMWZ

#JFLeo
MACHAKOS, KENYA: KITUO CHA WATOTO WENYE UHITAJI CHAFUNGWA KWA TUHUMA ZA UNAJISI

> Mahakama imetoa amri hiyo baada ya tuhuma za Wavulana 9 kati ya 39 wanaolelewa katika kituo kilicho chini ya Kanisa Katoliki kunajisiwa na mpishi

Zaidi, soma => https://jamii.app/MachakosKituoChafungwaUnajisi

#JFLeo
BASI LA SHULE LATEKWA NA KUCHOMWA MOTO LIKIWA NA WANAFUNZI

> Wanafunzi 51 nchini Italia waliokuwa kwenye gari la shule wamenusurika kifo baada ya gari lao kutekwa na kisha kuteketezwa kwa moto wakiwa ndani ya basi hilo

> Dereva wa gari hilo anadaiwa kuwaelekezea kisu abiria wake na kutoa maneno ya vitisho yanayoilenga Serikali

Soma - https://jamii.app/51StudentsAbducted
#JFInternational
ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUJIDUNGA SINDANO YA MATUNDA

> Mwanamke mmoja (51) nchini China amenusurika kifo baada ya kujidunga yeye mwenyewe sindano iliyosheheni mchanganyiko wa matunda 20 yaliyotengenezwa kwa ajili ya kuimarisha afya

> Alijisababishia madhara kwenye ini, figo, moyo na kuharibu mapafu

Soma - https://jamii.app/KifoSindanoMatunda
#JFInternational
MWANAFUNZI AJINYONGA BAADA YA KAKA KUSHINDWA KUMUHUDUMIA

> Ephria Valeli (15) wa darasa la 7, Shule ya Msingi Ifukutwa Kata ya Mpanda Ndogo Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi amejinyonga kwa kutumia tisheti kwa kile kinachodaiwa kuchoshwa na manyanyaso ya walezi wake walioshindwa kumuhudumia mahitaji yake ya msingi

Soma - https://jamii.app/MwanafunziAjinyongaHuduma
#JFLeo
CHRISTCHURCH, NEW ZEALAND: SILAHA ZA KIVITA ZAPIGWA MARUFUKU KUUZWA KWA RAIA

> Hii ni baada ya kutokea kwa mashambulio katika misikiti miwili na kuua watu 50

> Mtu aliyehusika katika mashambulizi hayo alinunua silaha yake kwa njia halali

Soma => https://jamii.app/NewZealandShooting

#JFLeo
TAHARUKI: TETEMEKO LA ARDHI LAITIKISA MBEYA

> Taarifa kutoka Jiji la Mbeya zinaeleza kuwa tetemeko la ardhi limepita na kuzua taharuki kwa watu. Yaelezwa kuwa limechukua sekunde 5-10

> Lina ukubwa wa kipimo cha 5.1. Athari zake bado hazijafahamika

Zaidi, soma > https://jamii.app/TetemekoMbeya

#JFLeo
DAR: RAIS MAGUFULI AKUTANA NA NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE WA QATAR

> Rais Magufuli ameiomba Qatar ishirikiane na Tanzania katika kutekeleza miradi ya maendeleo kwenye sekta ya nishati umeme, ujenzi wa reli, barabara na madaraja

Zaidi, soma > https://jamii.app/TanzaniaVsQatar

#JFLeo
ASKARI AHUKUMIWA MIAKA MIWILI JELA KWA MAKOSA YA RUSHWA

> Tufike Tumaini aliyekuwa akikabiliwa na mashtaka 13 ya rushwa, amehukumiwa adhabu ya miaka 2 jela, baada ya kutiwa hatiani na Mahakama ya Wilaya ya Same, Mkoani Kilimanjaro kwa kosa la kuomba na kupokea rushwa ya Tsh. 600,000

Soma - https://jamii.app/AskariJelaRushwa
#JFLeo
HISTORIA YA KABILA LA WABENA

> Wabena ni kabila la kibantu linalopatikana katika eneo la Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania Wilaya ya Njombe Mkoa wa Iringa

> Maeneo makuu ya Wabena yamegawanyika katika sehemu tano ndani ya Wilaya ya Njombe ambayo ni Ivanging’ombe, Usovi, Ikilavugi, Nyikolwe na Mfirika

> Kibena ni lugha pana yenye utajiri wa maneno na lahaja kuu tano ila lugha yao ni moja tu ila tofauti ni ndogondogo, zinazotokana na matamshi

Zaidi, tembelea - https://jamii.app/HistoriaKabilaWabena
#JFHistoria
ATHARI ZA TETEMEKO NYANDA ZA JUU KUSINI: MTU MMOJA AFARIKI, NYUMBA NNE ZABOMOKA

> Mkazi Mmoja wa Kijiji cha Iyula(Songwe) amefariki baada ya kuangukiwa na ukuta

> Rukwa: Nyumba 4 na nyingine nyingi zapata nyufa

Soma > https://jamii.app/TetemekoMbeya
#MbeyaEarthQuake #RukwaEarthquake
MASUL, IRAQ: WATU 40 WAMEFARIKI BAADA YA KIVUKO KUZAMA

> Takribani watu 40 wamefariki baada ya kivuko kuzama katika Mto Tigris karibu na eneo la kitalii

> Waliofariki wengi ni Wanawake na Watoto

Zaidi, soma => https://jamii.app/FerrySunkIraq

#JFInternational
TANZANIA KUWASILISHA RIPOTI YA UTEKELEZAJI WA MALENGO YA SDG

> Tanzania itawasilisha kwa mara ya kwanza ripoti ya tathmini kuhusu utekelezaji wa malengo endelevu ya maendeleo (SDG) kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mwaka huu ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa makubaliano ya Umoja wa Mataifa

Soma - https://jamii.app/SDGRipotiTz
#JFLeo
TANZANIA YASHAURIWA KUTATHMINI ONGEZEKO LA WATU

> Benki ya Dunia (WB) imeishauri Tanzania kutathmini mwenendo wa ongezeko la watu, kuwekeza katika elimu kwa kuzingatia mapinduzi ya teknolojia, kuendeleza kilimo na kushirikisha sekta binafsi katika mambo mbalimbali

> Tathimini ya ongezeko la watu na kukua kwa Pato la Taifa vilikuwa ni vitu muhimu ili kufikia uchumi wa kati

Soma - https://jamii.app/WBUchumiTanzania
#JFLeo